Simon L. Matiko

62.6K posts

Simon L. Matiko

Simon L. Matiko

@SimonMatiko_

Simba Mnyamaaaaaa 🦁⚽ | Nguvu Moja ndani ya uwanja na nje pia! 🇹🇿 | #NguvuMoja

kahama-Tanzania Beigetreten Kasım 2021
3.7K Folgt10.4K Follower
Angehefteter Tweet
Simon L. Matiko
Simon L. Matiko@SimonMatiko_·
@lifeofmshaba Rais Samia Tunae na Tunatamba nae ni Mzalendo na Mchapakazi Kwa Maslahi Mapana ya Tanzania, Watanzania Tunamkubali na Tunaendelea nae 2025-2030, Kazi na Utu Tunasonga Mbele na Dkt Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Oktoba 2025 ni yeyeeeeh SSH 🇹🇿🖐️✅,
Filipino
10
4
9
4.6K
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Jenga taifa kwa maneno na matendo yako
Filipino
0
4
4
68
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Jenga taifa kwa maneno na matendo yako
Filipino
0
5
5
55
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Tanzania Kupanda katika viwango vya nchi zenye mazingira bora ya uwekezaji Afrika ni ishara ya kuwepo kwa jitihada za maksudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan. Hatua mojawapo ni ya hivi karibuni tu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo kukabidhi hati za ardhi kwa wawekezaji sita katika Mji Maalumu wa Kiuchumi wa Bagamoyo (BEMC SEZ) Prof. Kitila alibainisha kuwa mwaka 2024 Tanzania ilikuwa nafasi ya 11 kwa uwekezaji Afrika na mwaka huu imepanda na kufikia nafasi ya tisa ikiongozwa na Kisiwa cha Shelisheli, Mauritius, Misri, Afrika Kusini, Morocco, Ghana, Algeria na Ivory Coast. Profesa Kitila alisema Serikali ilianzisha programu za vielelezo saba kote nchini ambazo ni utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 na Eneo Maalumu la Kiuchumi la Bagamoyo ni mojawapo. Sambamba na hilo, imesema kwa mwaka 2025 miradi ya uwekezaji iliyosajiliwa imeongezeka na kufikia 915 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 10.95. Aidha, katika eneo hilo lenye ekari 9,800 Serikali inatarajia kujenga Bandari ya Bagamoyo, ukanda maalumu wa ujenzi wa meli na kituo cha usafirishaji, kituo maalumu cha matumizi ya nishati safi na eneo litakojengwa mji mpya wa kisasa. “Sisi ni wa tisa kwa kuwa na mazingira bora ya uwekezaji Afrika, na kabla ya mwaka 2021 Tanzania kwenye orodha ya nchi zinazovutia uwekezaji ilikuwa haionekani sasa hivi tumewazidi majirani,” alisema Profesa Kitila. Prof Kitila amesisitiza kuwa eneo hilo lina maeneo 60 ya uwekezaji na Serikali imeanza na wawekezaji sita watakaowekeza katika ujenzi wa viwanda na chuo, akisisitiza wawekezaji kujitokeza. miradi hiyo itakapotekelezwa, Sh trilioni nane zinatarajiwa kuwekezwa katika eneo hilo ikiwa ni uwekezaji mkubwa kutoka ndani na nje ya nchi.
Mchambuzi tweet media
Indonesia
0
5
5
58
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuimarisha nafasi ya Tanzania katika jukwaa la kimataifa kupitia mfululizo wa mazungumzo ya kimkakati yaliyofanyika kando ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia. Hatua hiyo ya Rais Samia kupanua wigo wa diplomasia ya kiuchumi imetafsiriwa kama pigo kwa wale wasioitakia mema Tanzania. Kwa sasa Tanzania inazidi kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa viongozi wa mataifa mbalimbali barani Afrika kutokana na ushawishi wake unaozidi kukua siku hadi siku. Katika kile kinachoonekana kuwa ni kuimarika kwa mashirikiano ya kiuchumi Rais Samia alifanya mazungumzo na Rais wa Angola João Lourenço ambapo kiongozi huyo amekubali kufanya ziara ya kiserikali nchini Tanzania na kuwa mgeni rasmi katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba mwaka 2026. Makubaliano hayo yanatarajiwa kufungua fursa mpya za uwekezaji katika sekta za nishati madini na viwanda huku viongozi hao wakisisitiza umuhimu wa kuimarisha mahusiano ya kihistoria kwa manufaa ya ustawi wa wananchi wa pande zote mbili. Vilevile Rais Samia alikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Dkt. Abiy Ahmed Ali ambapo walijadili kuimarisha biashara na ushirikiano katika sekta ya usafiri wa anga na usimamizi wa rasilimali za maji. Mazungumzo hayo pia yaligusia mwelekeo wa ukuaji wa uchumi ambapo Tanzania inatarajia kufikia ukuaji wa asilimia 6.5 ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali za kuimarisha maisha ya wananchi wake kupitia mipango madhubuti ya kiuchumi inayopata sifa ndani na nje ya mipaka ya nchi. Mafanikio hayo ya kidiplomasia yalihitimishwa kwa mazungumzo kati ya Rais Samia na Rais wa Comoro Azali Assoumani ambaye ametoa shukrani za dhati kwa mchango wa Tanzania katika kuimarisha huduma za afya na usalama nchini kwake. Rais Assoumani ameonesha nia ya kufanya ziara ya kiserikali nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya kutambua nafasi ya Tanzania kama muhimili wa amani na maendeleo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika hali inayozidi kuwadhalilisha wakosoaji wa uongozi wa Rais Samia wanaoshuhudia nchi hiyo ikipaa kimataifa kuelekea Dira ya Mwaka 2050.
Mchambuzi tweet media
Indonesia
0
4
5
56
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Usiku wa Februari 14, huku zulia jekundu (Red Carpet) katika ukumbi wa The Super Dome Masaki likiwaka moto kwa nakshi na mitindo, ujumbe mmoja mzito ulitawala anga: Filamu za Tanzania sasa ni biashara ya kimataifa, si mradi wa sinema tu, na vijana lazima kujipamnga kuvuna fursa hizo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amewataka wasanii nchini kubadili ‘script’ za kazi zao na kuandika hadithi zitakazoshindana duniani na kuleta fedha za kigeni (Dola), akisisitiza kuwa serikali imeshaweka mazingira ya "High Definition" (HD) kwa ajili yao. Katika kilele cha hotuba yake, Msigwa alibainisha kuwa mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kujenga studio ya kisasa ya Shilingi Bilioni 150 ni ishara tosha kuwa safari ya ushindi katika tasnia ya filamu imeanza. “Tukisimamia ubora na filamu zetu zikafikia viwango vya kimataifa, watengeneza filamu ni mabilionea duniani. Ukifanya kazi kwa mazoea au ‘heya heya’, utaishia kupata milioni mbili, lakini ukizingatia utaalamu, unatafuta mabilioni,” alisema Msigwa huku akishangiliwa na wadau wa tasnia. Katibu Mkuu hakumung’unya maneno kuhusu ushindi wa wasanii wageni na chipukizi waliojitokeza safari hii. Alieleza kuwa siri ya mafanikio yao ni kwenda shule na kufuata maelekezo ya kitaalamu. Alimtaja Profesa Mhando kama mmoja wa wabobezi wanaoandaa maandiko na miongozo ya kitaalamu ili kuwapata wasanii wanaojua misingi ya ubora. “Tusipoandaa wasanii kutekeleza kazi hizi kwa weledi, hata tukiweka miundombinu, itakuwa kazi bure,” alionya. Kujirudia kwa majina ya washindi kulielezwa kuwa ni matokeo ya majaji wabobezi wanaokagua kazi kitaalamu na si kwa hisia. lengo likiwa ni kuhakikisha TAFFA inakuwa na viwango vinavyotambulika nje ya mipaka, ambapo filamu zinazoshindana zinatakiwa kuwa ni kazi za sanaa (Artistic works) na si miradi ya kutafuta pesa ya haraka.
Mchambuzi tweet media
1
5
5
61
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Katika mkakati wa kuhakikisha kunakuwa na utulivu wa kiuchumi na usalama wa ajira kwa vijana, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na taasisi ya Benki ya CRDB (CRDB Bank Foundation), zimetenga Shilingi bilioni 4.6 kwa ajili ya kuwezesha miradi bunifu nchini kupitia ‘Mfuko wa Samia’. Hatua hiyo inatajwa kuwa ni mwendelezo wa juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kutengeneza mazingira wezesha ya ajira, jambo ambalo ni nguzo kuu ya kudumisha amani na utulivu. Fedha hizo ni mchango sawa wa Shilingi bilioni 2.3 kutoka kila upande, zikilenga kugeuza mawazo ya kiteknolojia kuwa biashara halisi zinazozalisha ajira. Akizindua programu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, alisema serikali inatambua kuwa kuwapa wananchi mikopo inayoambatana na maarifa ni chachu ya mabadiliko chanya. Alisisitiza kuwa uwezeshaji huo ni dhamira ya dhati ya kuthaminisha ubunifu wa ndani ili kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi. “Nawaomba COSTECH na CRDB Bank Foundation mhakikishe mnawafikia wabunifu wengi kadri iwezekanavyo. Kwa kutumia ubunifu wa ndani, Tanzania inaweza kutatua changamoto zake bila kuhitaji maarifa kutoka nje,” alisema Wanu, akibainisha kuwa uthubutu huu unalenga kuinua hali ya maisha ya Watanzania kote nchini. Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, alieleza kuwa ushirikiano huo ni ushahidi wa nguvu ya sekta binafsi inapoungana na serikali kuwahudumia wananchi. Alibainisha kuwa mfuko huo ni suluhu ya muda mrefu ya kuondoa changamoto ya ukosefu wa mitaji iliyokuwa ikisababisha mawazo mengi ya vijana kufifia na hivyo kuhatarisha usalama wao wa ajira. Naye Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk. Amos Nungu, aliongeza kuwa Mfuko wa Samia umekuja kusaidia biashara changa kupiga hatua kutoka maabara kuelekea sokoni. Alisema uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuona uwepo wa kizazi cha vijana wenye uwezo mkubwa wa kubadili mwelekeo wa uchumi wa taifa ikiwa wataungwa mkono na mifumo rafiki na mitaji yenye masharti nafuu. Hata hivyo, wadau wa kijamii na kiuchumi wamehusisha uwezeshaji huo na hitaji la kudumisha amani ya nchi. Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Kibaha Mjini, Jabir Makasala, alitoa wito kwa Watanzania kuiombea nchi amani akisisitiza kuwa bila utulivu hakuna maendeleo yanayoweza kufanyika, huku akibainisha kuwa amani ndiyo inayomfanya kila mmoja kuwa huru kutafuta ridhiki yake. Sauti hizo ziliungwa mkono na Alex Msimbe, Naibu Katibu Mkuu wa Soko la Loliondo Kibaha, aliyesema kuwa amani ni mtaji namba moja kwa wafanyabiashara. Aliongeza kuwa mshikamano wa kitaifa ndio utakaowezesha miradi kama hii ya uwezeshaji vijana kufanikiwa na kuleta tija iliyokusudiwa katika kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Hadi kufikia Julai 2025, jumla ya maombi 152 yalikuwa yamepokelewa katika dirisha la mpito la mfuko huo, ikiwa ni ishara ya kiu kubwa ya vijana katika kujiajiri na kuchangia katika uchumi wa kisasa, huku wakitakiwa kuepuka ushawishi wa vurugu na badala yake kulinda utulivu uliopo kwa ajili ya ustawi wa vizazi vya sasa na vijavyo.
Mchambuzi tweet media
Indonesia
0
4
5
78
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Wakati serikali ikiendelea kupata ushindi katika uwekezaji wa sekta za afya, sanaa, na teknolojia, madhehebu ya dini nchini yametakiwa kuwa mstari wa mbele kulinda utulivu uliopo, kwani bila amani hakuna uwekezaji unaoweza kustawi. Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki jijini hapa wakati wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Taasisi ya Fiysabilillah Tabligh Markaz, uliowakutanisha maelfu ya waumini kutoka mataifa ya Tanzania Bara, Zanzibar, Kenya, Uganda, na Malawi. Akizungumza katika mkutano huo, Sheikh wa Mkoa wa Arusha, Shabani Juma, amesema kuwa taasisi za kidini zina wajibu wa kisheria na kimaadili kuishi kwa kuzingatia misingi na malengo ya kuanzishwa kwake, huku ziking'ang'ania umoja na mshikamano kama ngao ya kulinda amani ya nchi. “Tofauti za kimadhehebu ni jambo la kawaida na ni sehemu ya utajiri wa imani yetu ndani ya Uislamu, lakini hazipaswi hata kidogo kuwa chanzo cha migawanyiko. Tunapaswa kushikamana ili nchi yetu iendelee kuwa tulivu, jambo ambalo linafungua milango kwa serikali kuleta maendeleo zaidi,” alisema Sheikh Juma. Alisisitiza kuwa amani si jambo la sadfa, bali ni zao la watu walioamua kuishi kwa kuvumiliana na kuheshimiana. Mkutano huo umefanyika wakati ambapo wadau wa maendeleo nchini wamekuwa wakipongeza ushindi wa serikali katika kuvutia wawekezaji na wataalamu kutoka nje ikiwa ni matokeo ya moja kwa moja ya sifa ya Tanzania kama kisiwa cha amani. Wadau wa mkutano huo waliazimia kuendelea kuwa mabalozi wa amani katika maeneo yao, wakiamini kuwa mshikamano wa kitaifa ndio utambulisho pekee utakaowezesha kizazi cha sasa na kijacho kufurahia matunda ya uwekezaji unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita. Mloganzila Inavyopiga Bao: Uwekezaji wa Tiba Wavuta Madaktari Bingwa Korea Kusini. Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya afya umezidi kutoa matunda baada ya Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kuanza kambi maalumu ya matibabu ya kibingwa, inayodhihirisha kuongezeka kwa imani ya kimataifa kwa wataalamu wa ndani. Kambi hiyo inayolenga kutengeneza na kurekebisha mishipa ya kuchuja damu (Arterio-Venous Fistula Creation) kwa wagonjwa wenye changamoto za figo, ni matokeo ya ushirikiano wa karibu kati ya wataalamu wa Tanzania na jopo la madaktari bingwa kutoka nchini Korea Kusini. Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo kutoka Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Hamis Isaka, amesema kuwa kambi hiyo si tu inatoa matibabu, bali ni jukwaa muhimu la ubadilishanaji wa ujuzi. Uwepo wa wataalamu kutoka Korea Kusini, ambao wamebobea duniani katika teknolojia ya matibabu, unasaidia kuwaongezea ujuzi wa hali ya juu madaktari wazalendo. Hatua hii inathibitisha kuwa uwekezaji katika miundombinu ya tiba nchini unalipa, kwani sasa Tanzania imekuwa kitovu kinachovuta wataalamu kutoka mataifa yaliyoendelea kuja kufanya kazi na kufundisha. Hali hii inapunguza hitaji la wagonjwa kusafiri nje ya nchi kufuata huduma hizo, hivyo kuokoa fedha nyingi za kigeni. Kambi hiyo, ambayo ni sehemu ya mikakati ya hospitali hiyo kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi, inatarajiwa kuhitimishwa Februari 18, 2026. Inakadiriwa kuwa takribani wagonjwa 50 wenye matatizo ya figo watanufaika na huduma hiyo ya kisasa, ikirejesha matumaini ya maisha kwa wahitaji.
Mchambuzi tweet media
Indonesia
0
4
4
51
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Amani na Mshikamano ni Jukumu la kila mmoja wetu.
Indonesia
0
4
4
47
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Mshikamano wa kweli huanzia kwa kila mmoja kuchagua amani kila siku.
Indonesia
0
4
5
46
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Kulinda amani na kudumisha mshikamano ni jukumu la kila Mtanzania.
Filipino
0
4
4
68
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Mshikamano wa kweli huanzia kwa kila mmoja kuchagua amani kila siku.
Indonesia
0
4
4
41
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Taifa lenye umoja hujengwa na wananchi wanaowajibika kwa amani.
Indonesia
0
4
4
49
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Katika historia ya Tanzania, jina la Julius Kambarage Nyerere linasimama kama alama ya uongozi uliotanguliza umoja na amani. Mwalimu Nyerere aliamini kuwa bila amani, hakuna maendeleo ya kweli. Kwa mtazamo wake, amani haikuwa tu kutokuwepo kwa vita, bali ilikuwa msingi wa mshikamano, utu na umoja wa kitaifa. Akizungumza kuhusu mshikamano wa Watanzania, aliwahi kusema, “Amani hailetwi na bunduki; amani hujengwa na moyo wa kuvumiliana na kuheshimiana.” Kauli hii inaonyesha wazi kuwa nguvu ya taifa haipo katika silaha, bali katika umoja wa watu wake. Hata hivyo, katika nyakati hizo wapo watanzania wachache ambao kwa makusudi wamekuwa wakifanya Katika kipindi cha uongozi wake, Tanzania iliendelea kubaki kisiwa cha amani katikati ya migogoro iliyolikumba bara la Afrika. Mwalimu alisisitiza mara kwa mara kuwa tofauti za kikabila, kidini au kisiasa hazipaswi kuwa chanzo cha mifarakano. Alisema, “Tukigombana sisi kwa sisi, tunajidhoofisha wenyewe. Lakini tukisimama pamoja, hakuna linaloshindikana.” Baada yake, Serikali zilizofuata ziliendeleza dhamira hiyo ya kulinda na kuimarisha amani ya taifa. Chini ya uongozi wa Benjamin Mkapa, msisitizo uliwekwa katika utawala wa sheria, uwazi na uwajibikaji kama nguzo za kudumisha utulivu wa nchi. Hayati Mkapa aliwahi kusema, “Amani ni mtaji wa maendeleo; bila amani hakuna uwekezaji, hakuna ajira, hakuna ustawi.” Kauli hiyo ilionyesha wazi uhusiano wa moja kwa moja kati ya amani na ukuaji wa uchumi. Katika Awamu ya Sita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea kusisitiza umuhimu wa amani, maridhiano na umoja wa kitaifa. Mara kadhaa amekumbusha kuwa maendeleo yanayokusudiwa hayawezi kupatikana bila mazingira ya utulivu. Katika moja ya hotuba zake alisisitiza, “Amani na utulivu wa nchi yetu ni tunu ya kipekee; ni wajibu wetu sote kuilinda na kuienzi.” Kauli hiyo imekuwa wito kwa Watanzania kushiriki katika kujenga taifa lenye mshikamano. Aidha, Rais Samia amehimiza siasa za kistaarabu na mazungumzo kama njia ya kutatua tofauti. Amesema, “Tofauti za mawazo si uadui; ni sehemu ya demokrasia. Lakini lazima tuzilinde kwa misingi ya amani na heshima.” Msisitizo wake umeonyesha dhamira ya kuimarisha umoja bila kuacha misingi ya utulivu iliyojengwa tangu enzi za Mwalimu. Leo hii, tunapoangalia changamoto za kijamii na kisiasa zinazoikabili dunia, mafundisho ya viongozi wetu bado yana uzito. Amani inahitaji jitihada za kila mmoja wetu. Inahitaji uvumilivu, mazungumzo na kuheshimu sheria. Ni wajibu wetu kulinda urithi huu. Kama Mwalimu Nyerere alivyotukumbusha, “Bila amani, hatuwezi kujenga; na bila umoja, hatuwezi kudumisha amani.” Maneno haya yanapaswa kuwa mwongozo wetu, leo na kwa vizazi vijavyo.
Mchambuzi tweet media
Indonesia
1
5
5
69
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
SERIKALI ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imetuma salamu nzito kwa watendaji wa umma wanaozembea kutoa haki za wananchi baada ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, kuamuru watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro kuchanga fedha mifukoni mwao kumlipa papo hapo mwananchi aliyekuwa akidai tangu mwaka 2022. Tukio hilo la kushtukiza limetokea jana, Februari 18, 2026, katika mkutano wa hadhara eneo la Ndungu, baada ya mkandarasi mmoja wa kizawa kujitokeza mbele ya Waziri Mkuu na kueleza masahibu yaliyompata kutokana na ucheleweshaji wa malipo yake ya ujenzi wa matundu ya vyoo vya shule. Akizungumza kwa uchungu mbele ya umati wa wananchi, mkandarasi huyo alieleza kuwa deni hilo la Shilingi milioni mbili limemletea athari kubwa za kijamii na kiuchumi. Alibainisha kuwa kutolipwa kwake kulisababisha kupoteza baadhi ya mali zake, mgogoro mkubwa wa ndoa uliotishia familia yake, na kushindwa kuwalipa vibarua waliomsaidia kazi hiyo tangu miaka minne iliyopita. Simulizi hiyo ya kuhuzunisha ilionekana kumgusa Waziri Mkuu ambaye hakusubiri maelezo marefu ya kiofisi, bali aliamua kuchukua hatua ya papo kwa hapo ili kurejesha heshima ya mwananchi huyo na serikali kwa ujumla. Dkt. Mwigulu, kwa sauti ya mamlaka, aliwataka watendaji wa halmashauri hiyo wanaohusika na mchakato wa malipo hayo "kujitathmini" kama wanastahili kuendelea na nafasi zao ikiwa jambo dogo kama hilo linamtesa mwananchi kwa miaka minne. Aliagiza watendaji hao kuchangishana kiasi hicho cha fedha na kumkabidhi mwananchi huyo mbele ya mkutano, akisisitiza kuwa Serikali ya Samia haina urafiki na watendaji wanaovuruga ustawi wa wananchi. "Hatuwezi kuwa na watendaji wanaokaa ofisini huku wananchi wakiteseka kwa madeni ya tangu 2022. Kama fedha zipo na mchakato ulikamilika, kwanini asilipwe? Kama hamuwezi kumlipa kwa taratibu za ofisi mlizozikwamisha, lipeni hapa hapa," kilisikika chanzo kimoja kikikariri msisitizo wa kiongozi huyo. Tukio hili limeibua mijadala mipana miongoni mwa wananchi na wachambuzi wa masuala ya utawala. Wengi wamepongeza hatua hiyo wakisema inarudisha nidhamu ya kazi serikalini. Hata hivyo, baadhi ya wananchi wametoa rai kuwa mifumo ya halmashauri inapaswa kujiendesha kwa ufanisi bila kusubiri ziara za viongozi wa kitaifa. Msimamo huu wa Dkt. Mwigulu ni kielelezo tosha kuwa kaulimbiu ya "Kazi Iendelee" inaambatana na "Haki kwa Wote." Inapeleka ujumbe kwa wakurugenzi, wahasibu, na wahandisi wa wilaya nchi nzima kuwa uzembe, urasimu, na dharau kwa madai ya watoa huduma wadogo hautavumiliwa tena. Baadhi ya wananchi waliokuwepo mkutanoni walionekana kushangilia hatua hiyo wakisema ni "maamuzi ya kiume" na yenye tija. "Huu ndio utaratibu tunaoutaka. Mwananchi amefanya kazi, apewe haki yake. Serikali ya Mama Samia inaonyesha kuwa haiko mbali na watu wa chini," alisema mmoja wa wakazi wa Ndungu. Kwa hatua hii, Serikali imethibitisha kuwa mtendaji yeyote atakayeshindwa kwenda na kasi ya Rais Samia katika kuwahudumia wananchi, hana budi "kukaa pembeni" ili kupisha damu ngeni yenye uchungu na matatizo ya watu.
Mchambuzi tweet media
Indonesia
1
5
5
114
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imetoa wito kwa vijana nchini kuacha kupoteza muda kwenye mitandao ya kijamii kwa kufuatilia mambo ya upuuzi na chuki, badala yake watumie muda huo kutafuta fursa za kiuchumi zinazotolewa na mamlaka hiyo. Wito huo umetolewa jijini Mbeya wakati wa ziara ya mamlaka hiyo katika kiwanda cha vinywaji changamshi cha Mati Dry Gin, kinachomilikiwa na kampuni ya Kitanzania ya Mati Group of Companies Limited iliyopo eneo la Iwambi. Akizungumza katika ziara hiyo, Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa TISEZA, Daudi Riganda, amesisitiza kuwa amani iliyopo nchini ndiyo inayotoa mwanya wa uwekezaji, hivyo vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuilinda badala ya kuitumia mitandao vibaya. Alibainisha kuwa uwekezaji wa ndani una mchango mkubwa katika kutoa ajira na kukuza uchumi, jambo ambalo haliwezi kufikiwa ikiwa jamii itakumbatia chuki na vurugu zinazochochewa kidijitali. Kwa upande wake, Meneja wa Fedha wa Mati Group, Davis Bila, akimwakilisha Mkurugenzi wa kampuni hiyo, alisema kiwanda chao kilianza uzalishaji Februari 2, 2023, kwa mtaji wa shilingi milioni 500 na mpaka sasa kimetoa ajira za moja kwa moja kwa Watanzania 55. Alieleza kuwa usajili wao kupitia TISEZA umewapa manufaa makubwa, ikiwemo unafuu wa ushuru wa forodha kwa asilimia 75 pamoja na urahisi wa kupata nyaraka muhimu za uwekezaji. Serikali imeendelea kuwahimiza Watanzania kuiga mfano wa kampuni ya Mati Group kwa kuwekeza katika sekta za uzalishaji. Ujumbe mkuu unabaki kuwa: amani ni silaha na mtaji, na vijana wanapaswa kutambua kuwa maendeleo ya kweli yanapatikana kwa kufanya kazi na kutumia fursa kama za TISEZA, huku wakidumisha umoja wa kitaifa kwa kauli mbiu ya "Tanzania Kwanza."
Mchambuzi tweet media
Indonesia
1
5
5
97
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito mzito kwa waumini wa dini za Kikristo na Kiislamu nchini, kuitumia msimu huu wa kipekee wa ibada kuliombea Taifa amani, umoja, mshikamano na ustawi wa kijamii. Katika hali ya kipekee ambapo kalenda za kidini zimekutana, Rais Samia Februari 18, 2026, ametuma salamu za heri na baraka kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, akisisitiza umuhimu wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu na kuimarisha uhusiano wa kibinadamu kupitia sala na sadaka. Kwa upande wa waumini wa Kikristo wanaoanza safari ya siku 40 ya Kwaresma , Rais Samia amewatakia mfungo mwema wenye baraka, akiwataka kutumia ibada ya Jumatano ya Majivu kama fursa ya kutafakari na kuimarisha imani yao. “Safari hii muhimu kiimani kwenu mnayoianza leo... iwe fursa ya kutafakari, kuendelea kuimarisha uhusiano na Mwenyezi Mungu; na kudumu katika ibada, kuiombea nchi yetu amani, umoja, mshikamano na ustawi kwa wote,” aliandika Rais Samia. Rais alihitimisha salamu hizo kwa kunukuu Maandiko Matakatifu kutoka kitabu cha Yoeli 2:12-13, kinachosisitiza kurejea kwa Bwana kwa mioyo yote kupitia kufunga na kuomboleza, huku akisisitiza waumini "kurarua mioyo yao na si mavazi yao." Wakati huo huo, Rais Samia amewatakia kheri na mfungo mwema Waislamu wote nchini wanapojiandaa au kuanza kutekeleza nguzo muhimu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Amewasihi waumini hao kusujudu kwa shukrani kwa neema ya kufikia mwezi huo adhimu. “Tunapotekeleza nguzo hii muhimu, tumwombe (Mwenyezi Mungu) atujalie kudumu katika ibada na upendo kwake na jamii na akaipokee funga yetu,” alieleza Rais katika ujumbe wake. Aliwakumbusha Waislamu wajibu wao wa kisheria na kiimani kwa kunukuu aya ya Qur’an Tukufu kutoka Sura Al-Baqara 183, inayosema: “Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.” Rais Samia amehimiza kuwa katika vipindi hivi vya kufunga na kusujudu, waumini wa dini zote wasichoke kuiombea nchi ya Tanzania ili iendelee kubaki katika misingi ya amani na utulivu. Amewaombea wafungaji wote nchini ili Mwenyezi Mungu azipokee funga, sala na sadaka zao, na kuwakirimia mema kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia hadi Taifa kwa ujumla. Tukio hili la dini zote mbili kubwa nchini kuingia katika kipindi cha toba na kufunga kwa wakati mmoja, limeonekana kama ishara ya kiroho ya kuimarisha umoja wa kitaifa, huku kauli ya Rais ikiongeza chachu ya utulivu na uchamungu nchi nzima.
Mchambuzi tweet media
Indonesia
1
5
5
47
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
SERIKALI imewataka wananchi kote nchini kuacha tabia ya kubeza na badala yake kuanza kuwathamini na kuwakumbatia wawekezaji wazawa, ikielezwa kuwa wao ni nguzo muhimu katika kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Dkt. Jafar Seif, alipofanya ziara ya kikazi mkoani Geita kukagua shughuli za maendeleo, ikiwemo uwekezaji unaofanywa na wazalendo katika sekta ya madini. Akizungumza baada ya kutembelea mgodi wa mwekezaji mzawa, King Mapung’o uliopo mkoani hapa, Dkt. Seif alisema kuwa uwekezaji wa ndani una faida kubwa ya kipekee kwani fedha zinazopatikana hubaki ndani ya nchi na kusaidia ujenzi wa miundombinu ya huduma za kijamii. “Tunaposema tuthamini wawekezaji wazawa, tunamaanisha hawa ndio watu ambao wanaguswa moja kwa moja na matatizo ya wananchi wenzetu. Wanapopata faida, hawaipeleki nje ya nchi, bali wanashirikiana na Serikali kujenga shule, zahanati na barabara katika maeneo yenu,” alisema Dkt. Seif. Katika kuonyesha mfano wa kivitendo wa namna mwekezaji mzawa anavyoweza kuisaidia serikali, mwekezaji huyo, King Mapung’o, ametangaza kutoa ufadhili wa Bima ya Afya kwa wananchi 600 wa mkoani Geita. Hatua hiyo imetajwa na Dkt. Seif kuwa ni muendelezo wa kuunga mkono maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akipigania Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata matibabu bila vikwazo vya kifedha. “Huu ni mfano wa kuigwa. Kitendo cha mwekezaji mmoja kulipia bima ya afya watu 600 ni mzigo mkubwa alioutua serikali na ni msaada mkubwa kwa wananchi hawa ambao sasa watapata matibabu bora bila hofu ya gharama. Huu ndio uzalendo tunaoutaka,” alisisitiza Naibu Waziri huyo. Dkt. Seif alibainisha kuwa kuwekeza kwa wazawa kuna faida nyingi, ikiwemo ajira kwa vijana,uhamisho wa ujuzi na utulivu wa kiuchumi. Aidha, Naibu Waziri huyo aliwaasa watendaji wa serikali katika ngazi za mitaa kuacha kuweka vikwazo visivyo na tija kwa wawekezaji wazawa, badala yake wawape ushirikiano wa karibu ili waweze kukua na kutoa mchango mkubwa zaidi. Kwa upande wake, mwekezaji King Mapung’o aliahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kila hatua, akisisitiza kuwa jukumu la kuijenga Tanzania si la serikali pekee, bali ni la kila mdau anayenufaika na rasilimali za nchi.
Mchambuzi tweet media
Indonesia
1
5
5
46
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
DIPLOMASIA ya uchumi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa matunda baada ya Serikali ya India kupitisha bajeti ya kihistoria ya Dola za Marekani Bilioni 1.1 (takriban Shilingi Trilioni 2.7) kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini Tanzania kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Hatua hiyo ni kielelezo tosha cha imani kubwa ambayo mataifa ya nje na washirika wa maendeleo wanayo kwa uongozi wa Rais Samia katika kuimarisha sekta za kijamii na kiuchumi. Akizungumza wilayani Longido mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama katika Kijiji cha Losirwa, Balozi wa India nchini, Bishwadip Dey, alisema kati ya fedha hizo, Dola milioni 600 (Shilingi Bilioni 1.4) tayari zimeshatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya afya, elimu, maji na barabara. Balozi Dey alisisitiza kuwa India haitoi fedha hizo kama wahisani tu, bali kama washirika wanaounga mkono kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia kwa wananchi wake. "Serikali ya India imetenga fedha hizi kumuunga mkono Rais Samia kwa kazi nzuri anayoifanya. Sikuja Longido kama mtalii, nimekuja kama mwanafamilia kukagua miradi yetu," alisema Balozi huyo. Katika ziara hiyo, Balozi Dey alizindua mradi wa maji wa Chemchemi ya Tono uliogharimu Shilingi Milioni 125, mradi utakaonufaisha zaidi ya watu 2,000. Aidha, alipongeza Kampuni ya Dar Solution kwa kutoa vifaa vya TEHAMA vya Shilingi Milioni 15 na kuchangia Shilingi Milioni 30 katika ujenzi wa shule shikizi. Balozi aliahidi kuwa India itaendelea kufanyia kazi changamoto za elimu wilayani humo ili kuwapunguzia watoto adha ya kutembea umbali mrefu kufuata shule. Naye Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Longido, Dkt. Steven Kiruswa, alimshukuru Balozi huyo na kueleza kuwa ushirikiano huo ni matokeo ya mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na Rais Samia. Alisema nguvu za wananchi na wadau wa India zimesaidia kufikisha mabomba na matanki ya maji katika vitongoji vya Kisambi na Olomuki. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Longido, Salumu Kally, aliwataka wananchi kuitunza miradi hiyo kama mboni ya jicho ili kuwajengea imani wahisani waweze kuleta miradi mingi zaidi.
Mchambuzi tweet media
Indonesia
1
5
5
74
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
SERIKALI imetangaza mkakati mzito wa kuhakikisha huduma zote za umma zinahamia katika mifumo ya kidijitali iliyo salama na jumuishi, lengo likiwa ni kufikia asilimia 80 ya huduma hizo ifikapo mwaka 2050. Hatua hiyo imebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Benedict Ndomba, wakati wa ufunguzi wa Kikaokazi cha Sita cha Serikali Mtandao jijini Arusha. Ndomba amesisitiza kuwa eGA sasa imejikita katika kuimarisha Mtandao wa Mawasiliano Serikalini (GOVNET) ili kuongeza uwazi na uwajibikaji. Ndomba ameeleza kuwa kasi hiyo ya kidijitali si ya kubahatisha, bali ni utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Ilani ya CCM ya 2025 (Ibara ya 46), inayoelekeza kuwa ifikapo mwaka 2030, asilimia 50 ya huduma za serikali ziwe zinapatikana kiganjani. "Tumeimarisha Vituo vya Serikali vya Kuhifadhi Data (Data Centers). Hii ina maana taarifa za serikali na wananchi sasa ziko salama zaidi, na gharama za uendeshaji zimepungua kwa sababu taasisi hazihitaji kujenga miundombinu ya pekee yao," alisema Ndomba. 📦 BOKSI: AMANI NI NGAO YA MAENDELEO Wakati serikali ikiboresha mifumo, wananchi kutoka sekta mbalimbali wametoa rai kuwa maendeleo yote hayo ya kidijitali na kiuchumi hayawezi kuwepo bila Amani na Utulivu. Frimatus Mtenga (Fundi Magari, Kibaha): "Wazazi wafundisheni watoto kutunza amani. Amani ndiyo ngao yetu inayotufanya tufanye shughuli zetu za maendeleo bila hofu." Amina Mwinyimvua (Soko la Loliondo): "Mambo ya vurugu hatujayazoea. Tunahitaji mshikamano tuliojengewa na viongozi wetu. Amani haina mbadala." Malugu Nkwabi (Bariadi, Simiyu): "Amani ni kila kitu. Tuliona wakati wa misukosuko ya uchaguzi, tulilazimika kufunga biashara mapema. Yale yalikuwa maisha magumu yasiyohitajika tena." Naye Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu, Mululi Mahendeka, amebainisha kuwa Serikali Mtandao ni nyenzo muhimu ya utawala bora. Katika dunia ya sasa ya mabadiliko ya kasi ya teknolojia, mifumo ya kidijitali inasaidia kuziba mianya ya rushwa na kuwafanya wananchi wapate huduma kwa haraka bila urasimu. Mwenyekiti wa Bodi ya eGA, Dkt. Mussa Kissaka, ameongeza kuwa mafanikio ya ajenda hii yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuweka mikakati ya pamoja ya usalama wa mtandao (Cybersecurity). Mseto huu wa teknolijia salama kutoka eGA na kilio cha amani kutoka kwa wananchi wa hali ya chini, unatoa picha moja: Tanzania ya kidijitali inajengwa juu ya misingi ya utulivu. Bila amani, hata mifumo bora ya kompyuta haiwezi kutoa huduma.
Mchambuzi tweet media
Indonesia
1
5
5
48
Simon L. Matiko retweetet
Mchambuzi
Mchambuzi@Baraza_Kuu·
Usalama ni Jukumu letu sote tukishirikiana Amani itadumu
Indonesia
1
6
7
54