Purity Magesa
3.1K posts

Purity Magesa retweetet
Purity Magesa retweetet
Purity Magesa retweetet
Purity Magesa retweetet

SERIKALI YATEKELEZA UJENZI WA KM 206.33 ZA BARABARA ZA LAMI NA MIRADI 76 YA MADARAJA
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
@SuluhuSamia kupitia Wizara ya Ujenzi inaendelea kuimarisha miundombinu ya barabara na madaraja nchini kwa lengo la kurahisisha usafiri, kukuza biashara na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.
Hadi kufikia Februari 2026, Wizara ya Ujenzi imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa kilomita 206.33 za barabara kwa kiwango cha lami, hatua inayochangia kuimarisha mtandao wa barabara na kuboresha mawasiliano kati ya maeneo mbalimbali ya nchi.
Aidha, wizara imekamilisha miradi 76 kati ya 81 ya dharura ya ujenzi wa madaraja yaliyoharibiwa na mvua kubwa za El-Niño pamoja na Kimbunga Hidaya katika mikoa 22 nchini, huku miradi mitano (5) iliyobaki ikiwa katika hatua za mwisho za kukamilishwa.
Kwa upande wa maendeleo ya ujenzi wa madaraja makubwa yanayoendelea kujengwa nchini, utekelezaji wa miradi hiyo umefikia hatua mbalimbali ambapo Daraja la Pangani limefikia asilimia 70, Jangwani asilimia 26, Mbambe asilimia 44, Sukuma asilimia 76, Simiyu asilimia 73, Mirumba asilimia 50, na Mitomoni asilimia 85 ya utekelezaji.
Hatua hizi zinaendelea kuonyesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuimarisha miundombinu ya usafiri nchini, kurahisisha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo ya wananchi.
@ikulumawasliano
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia


Indonesia
Purity Magesa retweetet
Purity Magesa retweetet
Purity Magesa retweetet
Purity Magesa retweetet
Purity Magesa retweetet
Purity Magesa retweetet

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia akizungumza kwenye hafla ya kupokea Taarifa za Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Ameeleza kuwa kutokana na umuhimu mkubwa wa eneo la Ngorongoro, kuna mchanganyiko wa masuala mbalimbali yanayohitaji kuzingatiwa, ikiwemo uwepo wa wananchi na mifugo yao pamoja na wajibu wa kulinda urithi wa dunia uliopo katika eneo hilo.
Ameeleza kuwa hali hiyo imekuwa ikiibua swali muhimu la namna bora ya kukabiliana na mahitaji hayo yote; kwa upande mmoja watu na mifugo yao ni sehemu ya jamii ya nchi, na kwa upande mwingine Ngorongoro ni rasilimali muhimu inayopaswa kulindwa kwa manufaa ya taifa na dunia kwa ujumla.
Rais Samia amesema tume imefanya kazi kubwa na kutoa mapendekezo muhimu ambayo Serikali itayafanyia kazi kwa umakini ili kupata suluhisho endelevu kwa masuala ya eneo hilo.
Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wenyeviti pamoja na wajumbe wa tume hizo kwa kukubali kubeba jukumu hilo kubwa na nyeti kwa maslahi ya taifa. Ameeleza kuwa kazi waliyopewa haikuwa rahisi kutokana na wingi wa masuala yaliyohitaji kujadiliwa, mikutano mingi waliyofanya pamoja na maoni tofauti kutoka kwa wadau mbalimbali waliokutana nao.
Rais Samia amewapongeza kwa kazi yao kubwa ya kizalendo waliyoifanya kwa bidii, uadilifu na weledi mkubwa ili kutimiza kwa mafanikio jukumu walilokabidhiwa kwa manufaa ya nchi.
@ikulumawasliano
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Indonesia
Purity Magesa retweetet

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia akizungumza kwenye hafla ya kupokea Taarifa za Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma
Ameeleza kuwa katika miaka ya nyuma kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu suala la Ngorongoro, ukiambatana na taarifa mbalimbali katika mitandao ya kijamii, malalamiko ya wakazi wa eneo hilo, pamoja na mashtaka yaliyowasilishwa katika taasisi tofauti za kimataifa.
Rais Samia amesema hali hiyo ilimfanya mwezi Desemba mwaka 2024 kutafuta nafasi ya kukutana na viongozi wa kimila wa kabila la Wamasai pamoja na wazee wa jamii ya Ngorongoro ili kuzungumza nao moja kwa moja na kusikiliza kwa kina changamoto zinazowakabili.
Amesema katika mazungumzo hayo, viongozi hao walieleza changamoto zao hususan zinazohusiana na matumizi ya ardhi, uhifadhi wa mazingira pamoja na utekelezaji wa zoezi la uhamaji wa hiari kutoka ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda maeneo yaliyotengwa na Serikali.
Rais Samia amefafanua kuwa zoezi la uhamaji wa hiari lilianzishwa na Serikali kwa lengo la kutoa fursa kwa wakazi wa eneo la hifadhi waliokuwa tayari kuhama, kwa kuwapatia maeneo mbadala ya makazi pamoja na mazingira bora ya kuendeleza shughuli zao za kijamii na kiuchumi.
@ikulumawasliano
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Indonesia
Purity Magesa retweetet
Purity Magesa retweetet
Purity Magesa retweetet

SERIKALI YATOA RUZUKU YA SHILINGI BILIONI 1.63 KUTEKELEZA MRADI WA UMEME WA MAJI IJANGALA NJOMBE
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
@SuluhuSamia kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 1.63 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Maji wa Ijangala uliopo wilayani Makete, mkoani Njombe.
Mradi huo wa Ijangala Mini Hydropower Plant wenye uwezo wa kuzalisha kilowati 360 tayari umeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji na uimara wa nishati ya umeme hususan katika maeneo ya vijijini.
Kupitia ruzuku hiyo, miundombinu muhimu ya mradi imejengwa ikiwemo transfoma chochezi yenye uwezo wa KVA 500 pamoja na njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolt 33 yenye urefu wa kilomita 0.6 inayounganisha mradi huo na Gridi ya Taifa.
Aidha, mradi huo ulipata mkopo nafuu wa shilingi milioni 922 kupitia programu ya Tanzania Rural Electrification Expansion Program (TREEP) inayosimamiwa na REA, uliosaidia kugharamia baadhi ya shughuli za utekelezaji wa mradi.
Mradi huu unatekelezwa na Dayosisi ya Kusini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia Kituo cha Udiakonia cha Tandala, kwa kushirikiana na Serikali katika kukuza uwekezaji kwenye nishati jadidifu na kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo ya vijijini.
@ikulumawasliano
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia


Indonesia
Purity Magesa retweetet
Purity Magesa retweetet




















