
Nimezindua Hatifungani ya Samia ya Miundombinu (Samia Infrastucture Bond) ambayo inalenga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 150 ili kuiwezesha TARURA kuongeza mtandao wa barabara za vijijini na mijini.
Hatifungani hii itaweza kuwashirikisha wawekezaji wa ndani katika ugharamiaji wa miradi ya miundombinu, kukuza ushirikiano na Sekta Binafsi na kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa barabara zinazosimamiwa na TARURA, unafanyika kwa wakati ili barabara hizo ziweze kutumika katika kipindi chote cha mwaka.
Vilevile, Hatifungani hii itasaidia kukabiliana na mahitaji ya dharura ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu,unaosababishwa na uharibifu wa mvua kubwa na mafuriko.
Naipongeza Ofisi ya Rais - TAMISEMI, TARURA, Kamati ya Samia Infrastructure Bond, Bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB kwa ubunifu na jitihada zao katika kufanikisha uanzishwaji wa Hatifungani hii. Kadhalika, natoa pongezi za dhati kwa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Benki Kuu ya Tanzania na Wizara ya Fedha kwa kuhakikisha Hatifungani hii inakidhi vigezo na kuiwezesha kuingia sokoni.




Indonesia



























































