고정된 트윗

Hapa Munich Jua limekuwa kali sana asubuhi ya leo lakini ndio kumekucha na Fainali inapigwa hapo baadae kidogo
Kwenye moja ya mgahawa hapa kwenye Hotel niliyopo nimekutana na gwiji na mwanahabari nguli kweli kweli ambaye ameliteka soko la dunia kwa sasa @FabrizioRomano
Tumepiga stori nyingi lakini nimempenyezea exclusive kuwa Bongo unaweza kulala ukaamka ukakuta habari imechapishwa na watu wanne tofauti lakini inafanana kila kitu cha ajabu amecheka sana, sasa sijui amecheka nini
Naendelea kumshawishi hapa huwenda akaripoti Dabi ya June. 15, Siku ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa nchini Jamhuri ina kiu kubwa ya kutaka kumjua Bingwa wa msimu huu siku hiyo
Bila kupoteza Focus, Nipo Munich kwa Ajili ya Fainali na wakali ni Heineken ambao wamesimamia kila kitu kuhakikisha ripoti zangu zinakufikia mwanzo hadi mwisho wa tukio
Hapo Bongo hakikisha unafika Mlimani City leo @HeinekenTZ wameweka mazingira mazuri kwa ajili yako na hakuna kiingilio

Filipino

















