
Licha ya kuongoza kura za Maoni katika Mchakato wa Uchaguzi wa Ubunge, Jimbo la Isimani (Mkoa wa Iringa), Kamati Kuu ya CCM, imemuweka kando Mfanyabiashara Fred Ngajiro maarufu kama @fred_vunjabei na kumteua Emmanuela Kaganda Mtafikolo kuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani Mkoani Iringa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Katibu Wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Laban Kihongosi, imesema kuwa kwa kuzingatia mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 105 (7)(f) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la Julai 2025, Kamati Kuu imefanya uteuzi wa mgombea waCCM kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Isimani, lililopo wilaya ya Iringa Vijijini ambapo Mgombea aliyeteuliwa ni Emmanuela Kaganda MTAFIKOLO. #KitengeUpdates





















