RICKIE retweetledi
RICKIE
47.8K posts

RICKIE
@Rickmsodoki
Football addicted Saini ya mtaa @manchester united fan Office machine maintance
Dar es Salaam, Tanzania Katılım Temmuz 2021
240 Takip Edilen422 Takipçiler
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi

Kuna hii page huko duniani imelitambua goli la chama , hiyo 238K ni watu walioona kupitia hii page
Tazama hao walioifollow hiyo page😀
Fabrizio Romano
David ornstein
Hao ni waandishi wakubwa sana duniani. Huenda na wenyewe wameliona hilo goli kupitia hiyo page na wanapanga muda wao watalipost😀 (Roho mbaya mshindwe)
Fabrizio ndio gwiji wa habari za usajiri duniani anatokea Italy.
David ornsten ni mwandishi mkubwa kutoka Uingereza.


Filipino
RICKIE retweetledi

Ratiba ya kufuzu kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika 2027 imetangazwa rasmi michezo ya kwanza ikiwa imepangwa kuanza kutimua Septemba 21, 2026.
Michuano hiyo mikubwa ya bara la Afrika itafanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 17, 2027, ambapo itahudhuriwa na mataifa 24, huku Kenya, Tanzania na Uganda wakiwa wenyeji wa pamoja.Droo ya kupanga makundi inatarajiwa kufanyika Mei 19, 2026.
Katika kanda ya CECAFA, timu zinazoshiriki hatua ya makundi ni Kenya, Tanzania, Uganda, Sudan, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Sudan Kusini, Eritrea na Somalia, baada ya baadhi ya timu hizo kufuzu kutoka hatua ya awali.
Ratiba ya michezo ya kufuzu imegawanywa katika vipindi vitatu vya FIFA:
•Mechi za 1 na 2: Septemba 21 – Oktoba 6, 2026
•Mechi za 3 na 4: Novemba 9 – 17, 2026
•Mechi za 5 na 6: Machi 22 – 30, 2027
Mashindano haya yanatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na mfumo mpya wa makundi na ongezeko la idadi ya timu zinazoshiriki.
#KitengeSports

Indonesia
RICKIE retweetledi

TAARIFA KWA UMMA
Msimamo wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juu ya Hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi na hotuba ya Samia Suluhu iliyofuata juu kile kilichoitwa Ghasia na Vurugu za Oktoba 29. 2025
1. Mnamo tarehe 28-29 Aprili 2026 Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ilikutana kwa mara ya kwanza kutokea kuondolewa kwa zuio haramu na batili lililokuwa limewekwa dhidi ya CHADEMA na Jaji Hamidu Mwanga kupitia Kesi Ndogo Namba 8960 ya 2025 iliyofunguliwa na Saidi Issa Mohamed, Ahmed Rashid na Maulidah Anna Komu. Wakati ikiendelea na Kikao chake mnamo usiku wa tarehe 28 Aprili 2026 Kamati Kuu ilipokea Taarifa ya kufariki kwa Maulidah Anna Komu na hivyo kuifanya kesi hiyo kubakia na walalamikaji wawili. Zuio hilo haramu lilisababisha CHADEMA kushindwa kufanya kazi kwa siku 309 hadi lilipoondolewa na Mahakama ya Rufaa kupitia Kesi ya Mapitio Namba, 1, 2, 3, na 4 za 2026.
2. Zuio hilo liliwekwa kwa makusudi kabisa ili kuizuia CHADEMA isifanye shughuli za kisiasa katika Mwaka wa Uchaguzi Mkuu na huu ulikuwa ni mkakati uliosukwa na kutekelezwa kwa ushirikiano mkubwa wa hao walioitwa walalamikaji, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, na Mahakama. Ni aibu na fedheha kubwa kuwa hata baada ya zuio hilo haramu kutolewa mnamo tarehe 14 Julai 2025 Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam aliandika barua Kumb Na. Shauri Dogo Na. 8960/2025 ikionyesha kuwa amri hiyo iliwagusa na kuwabana viongozi na wanachama wote wa CHADEMA.
3. Matokeo yake mamilioni ya Watanzania ambao ni wanachama, wafuasi na wapenzi wa Chadema, ambacho ni chama kikuu cha siasa nchini, walinyimwa haki ya kufanya siasa ambayo ni haki yao ya Kikatiba kwa mujibu wa Ibara ya 20, 21, 29(1)-(2) na (5) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
4. Kabla ya hapo mnamo tarehe 9 Aprili 2025 Mwenyekiti wa chama, Ndugu Tundu Anthipas Mughwai Lissu, alikamatwa huko Mbinga, Ruvuma. Siku iliyofuata, tarehe 10 Aprili 2025, alifunguliwa kesi mbili za jinai ikiwa ni pamoja na kesi kubwa kushinda zote katika nchi yetu ya uhaini. Hadi Kamati Kuu inakutana Ndugu Lissu amekuwa nguvuni katika Gereza Kuu la Ukonga kwa mwaka mmoja na siku 22.
5. Kamati Kuu inasema kuwa Kitendo cha Tume ya Chande kutaja vyanzo vya matukio ya Oktoba 29, 2025 kuwa ni: madai ya muda mrefu ya katiba mpya na mifumo mibovu ya demokrasia (uchaguzi),ukosefu wa ajira,utekaji na utendaji usioridhisha wa taasisi za umma na baada ya kutaja vyanzo hivyo ikaachana navyo na ikajikita kuongelea vile ilivyoviita vichocheo ni ushahidi wa kukosa kabisa umakini kwani vyanzo hivyo ndivyo msingi mkuu wa madai ya wananchi kwa zaidi ya miaka thelathini na minne na ulipofika muda wa uchaguzi viligeuka kuwa vichocheo kwa wananchi. Waliopuuza madai hayo kwa kila aina ya mbinu, katika kipindi chote hicho, ndio waliosababisha madhara yaliyotokea.
6. Kamati Kuu inaona kuwa vichocheo halisi vya mgogoro vilikuwa ni kasoro za msingi katika mfumo wa uchaguzi, zikiwemo madai ya uporaji wa kura, ukosefu wa uwazi katika usimamizi wa uchaguzi, pamoja na matumizi ya nguvu kupita kiasi na vyombo vya dola dhidi ya wananchi waliokuwa wakidai haki zao kwa amani. Katika mazingira haya, kaulimbiu za kisiasa zilikuwa ni dalili ya tatizo, si chanzo chake.
7. Kamati Kuu inasema kuwa sababu kuu ya mauaji makubwa katika historia ya Tanzania ni Serikali ya mabavu na haramu ya Samia Suluhu Hassan na Chama Cha Mapinduzi. Samia na CCM walikataa kwa makusudi, wakiwa wamejaa ghiliba, kejeli, dharau, na ulevi wa madaraka, kukubali kufanywa kwa mabadiliko muhimu katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na sheria zote zinazohusu uchaguzi ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inafanya chaguzi zilizo huru na haki. CHADEMA ilikutana na Samia tarehe 22 Mei 2022 na kumueleza kasoro kubwa katika mfumo mzima wa uchaguzi wa nchi yetu na hii ni kutokana na chaguzi haramu za mwaka 2019 na 2020 ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tamisemi ziliwaengua wagombea karibu wote wa upinzani. Ikamueleza wazi kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 wagombea wengi wa vyama shindani, ikiwemo CHADEMA walienguliwa na kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Polisi na Usalama wa Taifa walishirikiana na CCM kupora uchaguzi.
8. Wakati wa majadiliano hayo Samia Suluhu Hassan, aliyeingia madarakani kwa mujibu wa Katiba, baada ya kifo cha John Magufuli, aliagiza iundwe kamati ya watu kumi kutoka CCM na CHADEMA ili wajadiliane na kutoa mapendekezo ya kina ambayo yatafanyiwa kazi. CHADEMA ilitekeleza wajibu wake na kuwasilisha kwa kina uchambuzi makini wa mabadiliko ya Katiba na sheria za uchaguzi ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki. Lakini CCM na Serikali yake walikataa mapendekezo hayo na kusema mabadiliko yasubiri uchaguzi wa 2025!
9. Badala yake Serikali, Samia ikapeleka miswada ya sheria za uchaguzi na kuleta mabadiliko ya urembo (cosmetic) ikiwa ni pamoja na kubadilisha jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuiita eti ‘Tume “Huru” ya Taifa ya Uchaguzi. Ajabu yake, wajumbe wa Tume hiyo isiyo huru na isiyofuata wala kuzingatia haki, usawa, na ukweli wakiongozwa na Jacobs Mwambegele na Mbarouk Salim Mbarouk na wajumbe wengine akiwemo aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Omari Ramadhani Mapuri, wao walikuwa hawaguswi na matakwa ya sheria hiyo juu ya uteuzi wao. Kwani sheria hiyo ilisema wataendelea kutumikia nyadhifa zao hadi pale muda wao utakafikishia mwisho!
10. Mnamo mwaka 2024 Novemba, CCM na Samia Suluhu Hassani wakiwa wamejaa kiburi na jeuri kubwa waliendesha uchaguzi wa Serikali za mitaa kama ambavyo walifanya mwaka 2019 na waliwaengua karibu asilimia 90 ya wagombea wa vyama vya ushindani ikiwemo Chadema. CCM, kupitia Tamisemi, iliyokuwa ikiongozwa na Mohamed Mchengerwa ambaye ni mkwe wa Samia Suluhu Hassani, ilijitangazia ushindi wa asilimia 99.1!
11. Ikumbukwe kuwa kwa muda wote tokea mwaka 1992 hadi 2025 serikali ya CCM imekuwa ikikwepa kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba na sheria za uchaguzi kama ambavyo ilipendekezwa na Tume ya Jaji Francis Nyalali, Tume ya Jaji Robert Kisanga, na Tume ya Jaji Joseph Sinde Warioba. Tume hizi zote tatu zilichambua kwa makini Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na sheria za uchaguzi pamoja na za vyombo vya ulinzi na usalama na kupendekeza mabadiliko ambayo yatahakikisha kuwa Tanzania inauishi na kuufuata kwa dhati mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Serikali zote za CCM za kuanzia wakati huo zimekataa kwa visingizio mbali mbali na kikubwa zaidi kikiwa ufupi wa muda kuelekea Uchaguzi Mkuu. Ukweli ni kuwa CCM haijawahi kuukubali mfumo huu wa vyama vingi kwa dhati na imekuwa ikifanya kila aina ya udanganyifu na upotoshaji wenye lengo la kukataa kufanywa kwa mabadiliko ya kweli ya Katiba ya nchi yetu na sheria zake za uchaguzi ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
12. Watanzania wakumbuke kuwa Septemba 7, 2017, Ndugu Tundu Lissu, aliyekuwa Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alipigwa risasi 16 mwilini mwake na kulazimika kukimbizwa Hospitali Kuu ya Dodoma, Hospitali ya Nairobi Kenya, na baadaye Hospitali ya Leuven Ubelgiji. Hadi leo Serikali ya CCM imekataa kufanya uchunguzi huru wa wale waliohusika na unyama huo pamoja na vitendo vinavyokiuka kabisa Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
13. Pale Serikali inapokataa kufanya uchunguzi dhidi ya tishio la uhai wa mtu, inakuwa imekiuka msingi mkuu wa watu kukaa katika nchi moja (social compact). Inaamaanisha Serikali inaona uhai wa watu fulani ni bora zaidi kuliko wa wengine na kuwa uhai wa wale wanaoikosoa si wa muhimu.
14. Mnamo mwaka 2018 na 2019 kauli za ajabu na kutisha zilitolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally na Rais John Magufuli. Bashiru Ally alinukuliwa na akisema kuwa CCM itatumia “dola kubaki na dola” kwani haipo tayari kugeuka kama vyama vya KANU ya Kenya na UNIP ya Zambia ambavyo vilipoteza madaraka na kushindwa na vyama vya upinzani. Aidha, kati ya mwaka huo 2018 na 2019 Rais Magufuli alitamka kuwa Wakurugenzi wa Wilaya, ambao pia ni Wasimamizi wa Uchaguzi, watakaomtangaza mpinzani kushinda watatenguliwa!
15. Kana kwamba hiyo haitoshi, makada mbali mbali wa CCM na wakuu wa wilaya walijitokeza hadharani na kutoa kauli zinazothibitisha mikakati na mipango ya matendo maovu ya kuvuruga uchaguzi, kuwateka na kuwaua wapinzani yanayofanywa na CCM. Kule Ngara, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera mwaka 2023 alinukuliwa akisema “Jeshi la Polisi, Tukiwapoteza Wanaomtukana Raisi Msiwatafute.” Aidha, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Loliondo, Arusha, Marco Henry Ngúmbi aliwahutubia madiwani wa wilaya ya Longido na kuwaeleza wazi kuwa madiwani hao wote walishinda mwaka 2020 kutokana na nguvu ya Serikali na si kampeni zao. Vivyo hivyo Nape Nnauye ambaye mwaka 2014 alizungumzia kushinda uchaguzi kwa “goli la mkono” mwaka 2024 alisikika akiwa Bukoba kuwa kuna namna nyingi za kushinda uchaguzi kwa njia halali na haramu na kuwa ukitumia njia haramu baadaye unaenda kutubu! Kule Arusha, Kiongozi mmoja wa UVCCM alisikika akijinasibu katika Mkutano wa CCM Mkoa huo wa Arusha kuwa yeye ndiye alikuwa Kiongozi wa chinjachinja dhidi ya wapinzani!
16. Aidha, Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa haramu wa Mkoa wa Dar es Salaam alinukuliwa akisema kuwa:
“nimesoma kwenye mitandao wapo vijana wenzetu makada wa vyama vya siasa wanasema tarehe 29 mwezi wa kumi,Siku ya Uchaguzi wataandamana, watafanya fujo, wengine wamesema wataenda kuchoma sijui vituo vya mafuta, mimi naomba niwaeleze ukweli Ndugu zangu wana Kongowe kuwa mji wenu huu wa Dar es Salaam uko salama sana, wala msije mkaogopa kitu chochote hata kama wewe ndiwe unayetaka kufanya, hata wewe wala usiogope, wewe kama unataka kufanya wala usiogope wala mtu asikutishie kwamba bwana wewe acha wale wewe nenda tu, ukajaribu kile unachotaka kufanya, “nakuthibitishia”! “nakuthibitishia”! yaani kabla hujapeleka mguu wako mbele lazima utakuwa umesali sala ya Baba Yetu mara tano. Kwa sababu hii mambo ya mizaha tumekwisha kuchekeana sana”
17. Si hapo tu mara baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wassira amenukuliwa akisema kuwa “CCM itatawala milele hadi Yesu atakaporudi.” Kauli hizo pamoja na kauli za kutisha zilizotolewa na wagombea wa CCM ikiwemo Samia Suluhu Hassan aliyesikika mwaka 2020 akisema kuwa “Askari wao hawakosei shabaha, wakilenga risasi moja haimkosi mtu” na baadaye alipokuwa Kiongozi wa Serikali alisema kuwa “kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake, ila wao wanakula mpaka wanavimbiwa.” Hiyo haikutosha ikaja kashfa ya kugawa bandari za nchi yetu kwa DP World, kampeni ya kuwahamisha Wamaasai kwa nguvu kutoka Loliondo na Ngorongoro.
18. Wakati wa kampeni za 2025, Samia na CCM waliendesha kampeni zilizojaa rushwa ya wazi wazi ikiwa ni pamoja na ugawaji wa pikipiki na baiskeli zilizoandikwa SSH na za majina ya wagombea ubunge na udiwani wa CCM. Na alisikika akisema kuwa “tumejipanga vyema kuilinda nchi hii. Kwa hiyo hakutakuwa na nywinywi wala nywinywinywi. Naomba watu tokeni, amshaneni mkapige kura.” Tarehe 22 Oktoba 2025 pale Leaders Club, Dar es Salam, alisema kuwa “Nataka niwaambie, maandamano yatakayokuwepo ni ya watu kwenda vituoni kupiga kura, hakuna maandamano mengine. Hakuna tishio la usalama litakalokuwepo. Anayesema ni Amiri Jeshi Mkuu.” Hii inaendana na kauli yake aliyoitoa Mwezi Januari 22 2024 alipokuwa akihutubia Mkutano wa Saba wa Mkuu wa Majeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Makamanda kwa mwaka 2024 alisema:
"Tuko wengi, ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi, vyenye nia tofauti...hatuoni kama kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, kwa hiyo ni vyema mkajiweka tayari kwa chochote kile kitakachojitokeza,"
19. Ni katika muktadha huo, Kamati Kuu ya CHADEMA iliijadili Hotuba ya Mwenyekiti wa ile iliyoitwa Tume ya Raisi ya Kuchunguza matukio ya ghasia na uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2025 aliyoiwasilisha mnamo tarehe 23 Aprili 2026 kwa Samia Suluhu ambaye ni mtawala wa mabavu asiyechaguliwa na wananchi wa Tanzania.
20. Kamati Kuu inakumbusha kuwa kuanzia miaka ya 2021, mara tu baada ya Samia kuingia madarakani, vitendo vya utekaji na ubambikiaji wa kesi za jinai kwa wanaharakati na wanasiasa wa vyama shindani ulianza kwa nguvu ikiwemo kushikwa na kushitakiwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, kushikwa na kupotezwa kwa Deusdedit Soka na wenzake wawili, kutekwa na kuuawa kwa Mzee Ali Kibao, kutekwa na kuteswa na kutupwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa Ndugu Edgar Mwakabela (Sativa); kutekwa na kupotezwa kwa Ndugu Mdude Nyagali, Ndugu Shadrack Chaula, Ndugu Juma Kaswahili, na kutekwa na kupotezwa kwa Balozi Humphrey Polepole n.k.
21. Matendo hayo machafu yalifanywa hata kuelekea Siku ya Kimataifa ya Vijana Agosti 12, 2024 ambayo CHADEMA ilipanga kuyaadhimisha Mkoani Mbeya. Siku moja kabla ya siku hiyo viongozi wa CHADEMA walivamiwa, kupigwa na kuumizwa vibaya na kuondolewa mkoani Mbeya kwa nguvu. Hapakuwa na hata kosa waliloambiwa kufanya ila kisingizio kisicho kwisha cha “Taarifa za kiintelejensia.” Uovu huo uliendelea mara baada ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Athipas Lissu mnamo tarehe 9 Aprili 2025 kule Mbinga mkoani Ruvuma. Jeshi la Polisi na kwa kushirikiana na uongozi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bila sababu yoyote ile ya msingi, ila kwa lengo la kufanya uovu mkubwa, kuanzia tarehe 24 Aprili 2025 waliwazuia wananchi kuhudhuria kesi ya Lissu na wakataka kuendesha kesi zake mbili za jinai kwa njia ya mtandao.
22. Wanachama na viongozi wa CHADEMA waliofika mahakamani hapo walishikwa na kupigwa, kuumizwa vibaya sana na wengine walifanyiwa matendo ya udhalilishaji wa kingono. Aidha, wana harakati kutoka Kenya na Uganda, Boniface Mwangi na Agather Atuhaire walichukuliwa kutoka vyumbani mwao katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam na kupelekwa Kituo cha Kati (Kikuu) cha Dar es Salaam na baadaye walifanyiwa matendo ya kinyama ikiwa ni pamoja na kulawitiwa na kuingiliwa kinyume cha maumbile na baadaye kutupwa mpakani mwa nchi zao na Tanzania.
23. Kwa kutimiza nia yao ovu, mnamo tarehe 12 Aprili 2025, Mkurugenzi Uchaguzi wa ile iitwayo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani, alitangaza kuwa CHADEMA haitashiri katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa vile haikusaini fomu za Kanuni za Maadili ya Uchaguzi ambazo Tume hizo ilitaka zisainiwe na vyama vyote tarehe hiyo licha ya ukweli kuwa Kanuni hizo zilikuwa zinaanza kutumika siku moja kabla ya tarehe ya uteuzi wa wagombea ambayo ilikuwa ni mara baada ya Bunge kuvunjwa mwezi wa Nane 2025!
24. Kamati Kuu imetilia maanani na inapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa mnamo tarehe 30 Aprili 2025, Padri Dkt. Charles Kitima, Katibu Mtendaji wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, alivamiwa, kupigwa na kuumizwa vibaya sana akiwa ameenda uani katika Ofisi za Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) Kurasini, Dar es Salaam. Polisi bila haya wala soni wakasema kuwa alikuwa amepata kinywaji. Hadi leo hii hawajachunguza uharamia huo.
25. Si hapo tu mnamo mwezi Septemba Padri Jordan Kibiki wa Jimbo Katoliki Mafinga alitekwa na baadaye Jeshi la Polisi lilisema kuwa alijiteka kwa kuwa alikuwa na madeni. Ukweli ni kuwa alitekwa na kufanyiwa vitendo vya kinyama sana na baadaye kutupwa Mbalizi Mbeya ambako eti ndipo alipokutwa!
26. Aidha, Padri Camillus Nikata alitekwa na kuteswa vibaya sana katika Mkoa wa Ruvuma. Alipatikana kwa jitihada kubwa za Kanisa Katoliki Jimbo la Songea, TEC, na wasamaria wema. Jeshi la Polisi halikuona shida kusema kuwa lilipomuhoji alikuwa akikabiliwa na msongo wa mawazo na madeni. Aidha mtawa mtarajiwa (Kandidati), Vestina Shikawe, naye alitekwa na kufanyiwa udhalilishaji kule Mwanza na hadi hivi sasa hakuna uchunguzi wowote uliofanywa zaidi ya kukejeliwa na Jeshi la Polisi.
27. Hiyo yote haikutosha kwani mnamo tarehe 2 Juni 2025 Msajili wa Vyama vya Hiari na Kiraia katika Wizara ya Mambo ya Ndani, alitangaza kufuta usajili wa “Glory of Christ Tanzania Church”maarufu kama Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima. Askofu Gwajima, aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, alikuwa ametoa hotuba kama raia akipinga utekwaji na upotezwaji wa watu. Badala ya kupongezwa kwa kupinga vitendo hivyo,Kanisa lake lilifungiwa na jitihada za kupata utatuzi mahakamani zilikwama kwani kesi yake ilifanyiwa kila aina ya danadana ili kumkomoa yeye na waumini wake!
28. Tarehe 5 Agosti 2025, Luhaga Joelson Mpina, aliyekuwa Mbunge wa CCM Kisesa, alihamia ACT-Wazalendo na kupendekezwa na chama hicho kuwa mgombea wake wa uraisi. Aliwekewa kila aina ya vikwazo na licha ya kushinda kesi Mahakama Kuu bado alizuiwa kushiriki na Tume isiyo huru ya Uchaguzi kutokana na pingamizi la Mwanasheria Mkuu ambaye ni mteule wa Samia Suluhu Hassan! Alipokwenda Mahakama Kuu tena jitihada zake zikagonga mwamba na alikataa rufaa kabla ya uchaguzi huo hadi leo hii rufani yake haijapangwa wala kusikilizwa
29. Aidha, Kamati Kuu inasema uovu huu ulienda sambamba na kuiwekea zuio CHADEMA mnamo Juni 10, 2025 ndipo Chadema ikafungiwa na kunyimwa haki yake ya kufanya siasa. Licha ya uharamu wa amri hiyo viongozi na wanachama wa CHADEMA waliitii na kusitisha shughuli zao zote za kisiasa na kuelekeza nguvu zao katika kesi hizo na kesi ya Mwenyekiti Tundu Lissu. Hiyo haikulizuia Jeshi la Polisi mnamo tarehe 22 Oktoba 2025 kumkamata na kumshikilia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tanzania Bara Mhe John Heche kwa siku 21. Hiyo iliendana na kuwashika kuwaweka na mahabusu viongozi na wafuasi wengi wa CHADEMA katika sehemu mbali mbali za Tanzania.
30. Kamati Kuu inasema mlolongo huu wa vitendo hivyo haramu vilivyotajwa hapo juu ambavyo vilitekelezwa na CCM chini ya John Pombe Magufuli na Samia Suluhu Hassan unaonyesha wazi kwa mtu mwenye akili nzuri na timamu kuwa tatizo hapa ni Samia Suluhu, CCM, Polisi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mahakama, Msajili wa Vyama vya Siasa, TAKUKURU, Uhamiaji, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na vyombo vya habari huru na binafsi ambavyo viliamua kushirikiana kuhakikisha kuwa Samia na CCM wanabakia madarakani kwa namna yoyote ile.
31. Matendo hayo yote maovu ya CCM na Samia yasingeweza kuachwa na Tume makini na yenye uweledi na nia ya dhati ya kufahamu chanzo cha kweli cha mauaji hayo haramu ya kabla, mnamo, na baada ya tarehe 29 Oktoba 2025 kuwa ndiyo chanzo kikuu cha maandamano ya vijana hao wazalendo.
32. Kamati Kuu inasisitiza kuwa pale haki za kidemokrasia na njia zote za kujieleza na kutetea haki za mtu zinapofungwa kunasababisha watu kutokuwa na njia nyingine bali kuingia barabarani na kueleza chuki zao na kudai mabadiliko ya kweli.Kufanywa hivyo hakuwezi Kamwe kuwa sababu ya wao kuuawa na kujeruhiwa kinyama kama ambavyo ilifanywa katika siku hizo mbaya na za majonzi makubwa katika nchi yetu. Kugeuza uchaguzi kuwa mchezo wa kuviziana na wa nani ni mjanja ni kitu cha hatari kabisa. Hakuna anayestahili kuongoza nchi yetu kwa njia nyingine yoyote ile isipokuwa kwa kuchaguliwa na wananchi katika uchaguzi ulio huru na wa haki. Lakini hapa Tanzania haki hiyo haipo.
33. Kwa kipindi chote tangu nchi yetu ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi CCM imekuwa ikipora chaguzi na kutumia mabavu kubakia madarakani. Wananchi wamechoka na hawako tayari kuvumilia uporwaji na utwaaji wa madaraka unaofanywa na genge la watu wachache ambao wamekula yamini ya kubakia madarakani kwa kila mbinu huku wakiisigina na kuinajisi haki ya msingi katika nchi yetu, ambayo ni Jamhuri, kuwa mamlaka yote hutoka kwa wananchi na kuwa viongozi na Serikali watawajibika kwa wananchi.
34. Kamati Kuu inasema kuwa kuwataka wananchi waheshimu sheria za nchi wakati huku genge la watu wachache kupitia CCM na kiongozi wao Samia Suluhu Hassan wakisigina haki zao ni kuwageuza wao kuwa ni mandondocha. Wananchi wana haki ya kukasirika na kuonyesha hasira zao dhidi ya uovu wowote ule unaofanywa na Serikali na genge la watu wasioheshimu demokrasia. Pale mfumo wa uchaguzi na utumishi wa umma unapoharibiwa ni jukumu la wananchi kunyanyuka na kukomesha ukiukwaji huo. Vijana na wote waliouawa mnamo tarehe 29 Oktoba 2025 na wale waliotekwa, kuteswa, na kuuawa kabla na baada ya tarehe hiyo ni Mashujaa wa taifa letu na CHADEMA inawatangaza hivyo.
35. Siku hiyo ya tarehe 29 Oktoba 2025 Kamishina Mkuu wa Polisi, Camillius Wambura, alitangaza amri ya zuio la kutotoka nje kwa wakazi wa Dar es Salaam kuanzia saa 12 jioni. Zuio hilo lilitekelezwa katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu na liliondolewa pale Samia Suluhu Hassan alipotimiza nia yake ya kutwaa madaraka kwa nguvu na kuapishwa huko Dodoma. Kamati Kuu inatamka kwa kauli moja kuwa agizo hilo la Camillius Wambura lilikuwa batili, haramu na kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Ni Raisi pekee aliyechaguliwa na wananchi ambaye ndiye aliyepewa mamlaka ya kutangaza amri ya Hali ya Hatari nchini. Ibara ya 32(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inatamka:
(2) Rais aweza tu kutangaza kuwa kuna hali ya hatari iwapo—
(a) Jamhuri ya Muungano iko katika vita; au
(b) Kuna hatari hasa kwamba Jamhuri ya Muungano inakaribia kuvamiwa na kuingia katika hali ya hatari ya vita; au
(c) kuna hali halisi ya kuvurugika kwa amani ya jamii au kutoweka kwa usalama wa jamii katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote kiasi kwamba ni lazima kuchukua hatua za pekee ili kurejesha amani na usalama; au
(d) kuna hatari Dhahiri na kubwa, kiasi kwamba amani ya jamii itavurugika na usalama wa raia kutoweka katika Jamhuri ya Muungano au Sehemu yake yoyote ambayo haiwezi kuepukika isipokuwa kwa kutumika mamlaka ya pekee; au
(e) karibu kutatokea tukio la hatari au tukio la balaa au baa ya kimazingira ambalo linatishia jamii au Sehemu ya jamii katika Jamhuri ya Muungano; au
(f) kuna aina nyingineyo ya hatari ambayo kwa dhahiri ni tishio kwa nchi.
36. Pindi Raisi anapotangaza amri ya hatari anatakiwa, kwa mujibu wa ibara ya 32(4,) kuwasilisha kwa Spika tangazo hilo na ndani ya siku kumi na nne (14) Mkutano wa Bunge unatakiwa kuitishwa na Spika baada ya kushauriana na Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni. Ibara ya 32(6) inatamka na kutoa masharti ya utekelezaji na mipaka ya utekelezaji wa Hali ya Hatari inaposema:
(6) kwa madhumuni ya kuondoa Mashaka juu ya ufafanuzi au utekelezaji wa masharti ya ibara hii, masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge na ya sheria nyingine yoyote inayohusu utangazaji wa hali ya hatari kama ilivyotajwa katika ibara hii, yatatumika tu katika Sehemu ya Jamhuri ya Muungano ambapo hali hiyo imetangazwa.
37. Kamati Kuu baada ya kupitia ibara hiyo ya Katiba imebaini kuwa hakuna sheria iliyotungwa na Bunge inatoa haki kwa Kamishina Mkuu wa Polisi kutumia sehemu ya madaraka ya Raisi ya kutangaza Hali ya Hatari kama iruhusuvyo ibara ya 32(4) na kuwa Camillus Wambura alitangaza zuio la watu kutoka nje Jijjini Dar es Salaam bila kuwa na madaraka hayo kisheria. Aidha, Kamati Kuu imepata taarifa nyingi kutoka sehemu mbali mbali nchini kuwa amri hiyo ya zuio ilitumika katika sehemu hizo bila kuwepo tangazo maalumu juu ya zuio kuwekwa rasmi katika sehemu hizo. Aidha, Kamati Kuu imebaini kuwa mauaji mengi yalifanywa baada ya kutolewa kwa amri hiyo haramu. Ni polisi, watu wa usalama, askari wa KMKM, na askari waliokuwa wakizungumza lugha ya Kiingereza chenye lafudhi ya lugha za Uganda ndio walikuwa mitaani na wanaodaiwa kufanya mauaji hayo ya kinyama.
38. Kamati Kuu inapenda kukumbusha Watanzania na watu wote kuwa, ilipinga na inapinga kwa nguvu zake zote kuanzishwa kwa tume yoyote ile ya uchunguzi wowote ule na Samia Suluhu na chama chake cha CCM kwani wao ndio watuhumiwa nambari moja wa mauaji ya kinyama na kishetani yaliyofanywa kabla, mnamo, na baada ya tarehe 29 Oktoba 2025.
39. Mara baada ya mauaji hayo na kuapishwa kwa nguvu kwa Samia Suluhu Hassan, katika kambi moja ya Jeshi Mkoani Dodoma, mnamo tarehe 3 Novemba 2025, Kamati Kuu ilipinga uamuzi wa Samia wa kusema ataunda Tume hiyo ya uchunguzi. Alipoiunda, Kamati Kuu ilitoa tamko la kupinga kuundwa kwa tume hiyo. Tume hiyo ilikuwa imeundwa na mtu ambaye yeye mwenyewe ndiye anatakiwa kuchunguzwa. Aidha, Radhia Msuya huyu ni mdogo wake wa damu na Dkt. Asha Rose Mtengeti Migiro, ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM. Bi Stargomena Lawrence Tax, huyu alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia katika utawala wa Samia Suluhu Hassani hadi tarehe 3 Novemba 2025. Mtu kama huyu ambaye Wizara yake inatakiwa kuchunguzwa anawezaje kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchunguzi? Ikumbukwe baada ya Tume kuundwa ilipingwa na wahanga na wadau wengi kwani wengi hawakuiamini na waliiona kuwa ni Tume ya kuficha ukweli na yenye lengo ovu.
40. Ni kanuni isiyohitaji ubishi kuwa mtu hatakiwi kuwa hakimu au muamuzi katika suala linalomuhusu yeye mwenyewe kwa Kilatini “nemo judex in causa sua”na kwa Kiingereza “No one should be a judge in his own cause”. Sasa unapokuwa na Tume ya aina hiyo, je unategemea kupata na kuujua ukweli? Jibu ni Hapana na ndicho ambacho Tume hii haramu ya Jaji Chande imekifanya.

Indonesia
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi

Ndege ya Jean-Pierre Bemba aina ya Boeing 727-100 imetangazwa rasmi kukamatwa nchini Ureno, baada ya mmiliki wake kushindwa kutimiza masharti yaliyowekwa na mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Faro.
Kwa mujibu wa Mamlaka hizo, Bemba ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alipewa siku 60 za kuondoa Ndege hiyo pamoja na kulipa ada ya maegesho iliyokusanywa kwa kipindi cha miaka 19, inayokadiriwa kufikia karibu euro Milioni moja. Hata hivyo, muda huo ulipita bila hatua kuchukuliwa.
Tangu wakati huo, Ndege hiyo imeendelea kubaki hapo, hali ambayo ilionekana kuwa kinyume cha sheria mpya nchini Ureno kuhusu Ndege zilizotelekezwa viwanjani.
Mamlaka za Ureno zinasema kuwa kuendelea kuwepo kwa Ndege hiyo bila matumizi kwa muda mrefu kulikiuka sheria mpya kuhusu Ndege zilizotelekezwa katika viwanja vya Ndege.
Wakati Bemba hajatoa kauli rasmi, watu wa karibu naye wanasema kuwa jukumu la gharama hizo linapaswa kubebwa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai , ambayo ilihusika katika kuzuia mali zake.
Wanaongeza kuwa msimamo huo unatokana na ukweli kwamba aliachiliwa huru mwaka 2018 baada ya kufutwa kwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.
#KitengeUpdates

Indonesia
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi

“Samia Suluhu, she’s a very bad dictator who has blood on her hands and we’re happy that, the @IntlCrimCourt is slowly cornering her..”-; @rigathi
English
RICKIE retweetledi
RICKIE retweetledi

🚨 OFFICIAL: Kylian Mbappe’s camp reacts with a statement to AFP on recent criticism.
“Part of the criticisms are based on an overinterpretation of elements related to a recovery period strictly supervised by the club”.
“This is NOT corresponding to the reality of the commitment and the work that Kylian does daily for the good of the team”.

English















