Sour inc.
2 posts


1. Rais Samia Suluhu Hassan tangu ashike madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 19.03.2021, amefanya safari 59 za kimataifa kama Rais wa Tanzania katika nchi mbalimbali kutoka katika bara la Afrika, Ulaya, Asia na Amerika ya kaskazini.
2. Rais Samia Suluhu Hassan kasafiri mara 38 nchi za Afrika, safari 9 katika nchi za bara Ulaya, safari 9 katika nchi za bara Asia, safari 3 nchi za Amerika kaskazini. Rais Samia Suluhu Hassan hajafanya ziara katika nchi za Amerika Kusini, Australia na Antarctica.
3. Rais Samia Suluhu Hassan katika orodha ya safari na ziara zake 59 za kimataifa nchi ambazo amekwenda mara nyingi ni Uganda (mara 4), Mozambique (mara 3), United States of America (mara 3), United Kingdom (mara 2), United ArabEmirates (mara 2).
4. Pamoja na hivyo, zipo safari ambazo Rais SSH amekaa katika nchi hizo kwa zaidi ya siku mbili. Mfano katika ziara yake nchini Korea Kusini, Rais ameishi Seoul kwa siku takribani sita (6). Alikwenda na watu wengi wakiwepo wasanii wa sanaa za maigizo.
5. Netherlands (Uholanzi), Willem-Alexander King of the Netherlands, hufanya safari (state visit) zisizozidi tatu kwa mwaka mzima. Mfalme amewekewa utaratibu wa kupokea ugeni wa aina hiyo mara tatu kwa mwaka. GDP ya Netherlands ni 1.14 trilioni.
6. GDP ya Tanzania (2024) ni TZS 79.61bilioni. Rais wa Tanzania amefanya ziara 59 katika kipindi cha miaka mitatu. GDP ya Netherlands ni kubwa mara 14 ya GDP ya Tanzania, lakini mfalme amesafiri kutoka Netherlands kwenda nchi 7 katika miaka 3.
7. Rais wa Tanzania anafanya matumizi mengi katika ziara zake kuliko mfalme wa Netherlands, wakati kiwango cha umaskini (poverty rate) Tanzania ni 26% kwa mujibu wa National Bureau of Statistics (NBS). Kiwango cha umaskini Netherlands ni 0.30%.
8. 2022, Netherlands ilituma €10billion (baada ya kukatwa fidia ya kukusanya ushuru wa bidhaa). Mapato kupitia fedha zilizo chini ya usimamizi wa pamoja yalifikia takribani €1.0 bilioni. Ni fedha ambazo Netherlands anachangia bajeti ya Umoja wa Ulaya.
9. Julai 4, 2023 Ikulu, Dodoma, Rais Samia Suluhu Hassan alikutana na Balozi wa EU - Tanzania, Manfredo Fantl. Walishuhudia utiaji saini wa mikataba mitatu ya kusaidia Bajeti ya Tanzania 2013/2024 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) ya thamani ya TZS 455 bilioni.
10. Kwamba, Tanzania ambayo bajeti yake inachangiwa na fedha za Umoja wa Ulaya TZS 455 bilioni (kutoka TZS 33 trilioni za mchango wa Netherlands katika bajeti ya Umoja wa Ulaya, watawala Tanzania wanafanya matumizi makubwa kuliko wahisani wao.
Martin Maranja Masese, MMM • Brigedia Mtikila.

Indonesia