AyoTV retweetledi

Ndege ya Shirika la Ndege la Air Canada imegongana na Gari la Kikosi cha Zimamoto katika Uwanja wa Ndege wa LaGuardia, New York Nchini Marekani usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya Marubani wote wawili huku Watu wengine kadhaa wakijeruhiwa.
Wakati huu Mamlaka zikisema zinachunguza chanzo cha ajali hiyo, taarifa za Mashuhuda zimesema kuwa Ndege hiyo ilikuwa ikikimbia kwa kasi ya takribani maili 130 kwa saa kabla ya kugonga gari hilo ambapo mawasiliano ya mnara wa kuongozea Ndege yameonesha kuwa gari hilo lilikuwa limepewa ruhusa kuvuka barabara ya Ndege.
Baada ya tukio hilo, shughuli zote za Uwanja wa Ndege zimesimamishwa kwa muda ili kuruhusu huduma za dharura na uchunguzi kufanyika huku Mamlaka ya Anga ya Marekani (FAA) na National Transportation Safety Board wakianza uchunguzi kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo.
#MillardAyoUPDATES

Indonesia














