Mr. Magnifico
27.2K posts

Mr. Magnifico
@FelicianROM
MNMA ALUMNI 🧑🎓 (2021) Still hunting for big bags💰. A @ManUtd fan

"The LORD regretted that he had made human beings on the earth, and his heart was deeply troubled." Genesis 6:6




#TANZANIA: CHADEMA KUANZISHA KAMPENI NZITO KUSHINIKIZA LISSU KUACHIWA HURU, "TUTAANDAA MAANDAMANO MAKUBWA, HATUTAPIGA MAGOTI" Makamu Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Bara, @HecheJohn leo Aprili 09, 2026 wakati wa mjadala maalum ulioendeshwa kwa njia ya mtandao ambapo @TunduALissu anatimiza mwaka mmoja (siku 365) akiwa gerezani ametoa wito kwa Watanzania walio ndani na nje ya nchi hususani Vijana kuanzisha kampeni maalum ya kuzishinikiza Mamlaka kumuachia huru Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu akisema Lissu hajatenda kosa bali amebambikiwa kesi. “Jambo langu kwako wewe Kijana unayetuona, unayedai kwamba unatuunga mkono sio kusemea chinichini, tunapaswa kuanzisha kampeni kubwa wamuachie Tundu Lissu kwasababu Lissu amekamatwa kwa ajili yetu, kwasababu wote tunajua na wote tunaamini Lissu hana kosa, ni Mtu mwema anayetupigania, ili asikate tamaa ili asiwe na baridi kule aliko anafikiri kwamba nimekamatwa na Watu niliokuwa nawapigania wamerudi nyuma, tunapaswa kuanzisha kuanzia leo kampeni kubwa kwenye kila platform Instagram, Facebook, TikTok, Twitter ya kumdai Tundu Lissu” - Heche “Watu wetu wa Diaspora mfanye kama waliofanya Watu wa Diaspora waliokuwepo wa Afrika Kusini wakati ule , Vijana wetu mlioko ndani ya nchi tuandike vipeperushi visambae kwenye masoko, kwenye nguzo za umeme zikiwa na picha ya Lissu na ujumbe wa kutaka Lissu aachiwe” - John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara. Zaidi: youtu.be/V87WaO-2oPY




















