Jamii Check

4.2K posts

Jamii Check banner
Jamii Check

Jamii Check

@JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering Misinformation and Disinformation Online and Offline by JamiiAfrica

Tanzania Присоединился Eylül 2010
67 Подписки4.9K Подписчики
Закреплённый твит
Jamii Check
Jamii Check@JamiiCheck·
Jukwaa la #JamiiCheck hufanya kazi ya Kuhakiki Taarifa zinazopatikana ndani na nje ya Mtandao ili kubaini kama zina Ukweli, Uzushi au Nadharia Jukwaa hili huwa na 'Logo' yenye rangi 4 ambazo ni Njano ikimaanisha Taarifa mpya inayosubiri kuhakikiwa, Kijani ikimaanisha Taarifa iliyohakikiwa na kukutwa na Ukweli, Nyekundu ikimaanisha Taarifa iliyohakikiwa na kukutwa haina Ukweli pamoja na Kijivu ikiwakilisha Taarifa iliyohakikiwa na kukutwa ni Nadharia Tunapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhakiki wa Taarifa, hakikisha unatumia Jukwaa hili uwe sehemu ya Watu wanaopambana na Usambazaji wa #TaarifaPotofu Mtandaoni Kufikia Jukwaa, bofya JamiiCheck.com #FactCheckingDay #FactsMatter #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
Jamii Check tweet media
Filipino
1
8
36
10.5K
Jamii Check
Jamii Check@JamiiCheck·
Ufuatiliaji umejiridhisha kuwa video hii iliyodaiwa kuwa ni ya Mtawala wa Mongolia alipotembelea utawala wa Ming nchini China kwa mara ya kwanza 1440, ni #Potoshi. Video hiyo imehaririwa kwa kuondolewa rangi kutoka katika video halisi ya mtayarishaji wa maudhui Youtube, Darren Jason Watkins Jr (#IShowSpeed) alipotembelea China mwaka 2025, na kuichapisha katika chaneli yake ya Youtube. Soma Zaidi jamii.app/BlackKhanInChi… #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking
Indonesia
0
1
5
143
Jamii Check
Jamii Check@JamiiCheck·
Taarifa inayodai kuwa Kocha wa timu ya taifa ya Senegal, Pape Thiaw amepeleka kombe la AFCON kwenye kambi ya Jeshi kwa ajili ya ulinzi, kama hatua inayoonesha msimamo wa nchi hiyo kutoliachia taji hilo kwa Morocco, na kwamba kwasasa kombe hilo linalindwa na Vikosi vya Jeshi saa 24 ili Shirikisho la Soka Barani Afrika (#CAF) lisiweze kulipata si za Kweli. Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia nyenzo za Kidigitali umethibitisha kuwa Video hii si ya sasa, haihusiani na hukumu ya Kamati ya Rufaa ya CAF na imekuwepo Mtandaoni tangu Februari 8, 2026 wakati timu hiyo ilipokwenda kwenye mojawapo ya Kambi za jeshi kufurahia ushindi wao Soma jamii.app/KombeLaAFCONJe… #JamiiCheck #HakikiTaarifa #Misinformation #Disinformation #FactsMatter
Indonesia
2
2
4
245
Jamii Check
Jamii Check@JamiiCheck·
Kwa kutumia nyenzo za kidigitali, JamiiCheck imejiridhisha kuwa video hiyo imetengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde (#AI) Vilevile mapungufu yanayoonekana katika video hiyo ikiwemo hali ya mawe madogo kuganda hewani, maandishi yasiyosomeka sehemu ya usajili wa Pikipiki yanadhihirisha kuwa video ni ya kutengenezwa. Zaidi soma jamii.app/VideoJengo #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking
Jamii Check tweet mediaJamii Check tweet mediaJamii Check tweet media
Indonesia
0
1
1
103
Jamii Check
Jamii Check@JamiiCheck·
Waandishi wa habari 25 kutoka vyombo mbalimbali mkoani Mtwara wamepatiwa mafunzo ya Uhakiki na Uthibitishaji wa Taarifa, hatua inayolenga kuimarisha mapambano dhidi ya #TaarifaPotoshi kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia. Mafunzo hayo yaliyotolewa na JamiiCheck Machi 17, 2026, yaliwapa washiriki fursa ya kujifunza kwa vitendo Mbinu na Nyenzo za Kidijitali za Kuhakiki na Kuthibitisha Taarifa, pamoja na matumizi sahihi ya Akili Unde (#AI). Washiriki wameahidi kutumia ujuzi walioupata kuilinda Jamii dhidi ya Upotoshaji ndani na nje ya mtandao kwa kuwapatia Taarifa Sahihi. #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking
Jamii Check tweet media
Indonesia
1
1
2
30
Jamii Check
Jamii Check@JamiiCheck·
Digital verification by JamiiCheck found the same video on Facebook, where it was described as showing an NRM supporter who allegedly attempted to breach President Museveni’s security and was forcefully handled by security guards at Kololo. It was established that the video has been misrepresented by linking it to the Member of Parliament for the Adjumani West Constituency Gen. Moses Ali, as he is not the person shown in the footage.​ Read more jamii.app/OldManVideo #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking
English
2
4
5
154
Jamii Check
Jamii Check@JamiiCheck·
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa ukurasa ulionukuliwa kuwa umetoa taarifa ya kifo cha Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, si ukurasa rasmi wa Jeshi la Marekani, ambalo halijawahi kuchapisha taarifa hiyo. Aidha, ukurasa huo umetengenezwa mwezi Machi 2026, tofauti na ukurasa rasmi ambao umekuwepo katika mtandao wa X tangu Septemba 2007. Zaidi soma jamii.app/UkurasaJeshiMa… #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking
Jamii Check tweet mediaJamii Check tweet media
Indonesia
0
0
1
128
Jamii Check
Jamii Check@JamiiCheck·
Shimo hilo linalojulikana kama 'Darvaza Gas Crater' linapatikana Jangwa la Karakum nchini Turkmenistan. Eneo la kipekee duniani linalovutia maelfu ya watu kutokana na mwonekano wake wa moto mkali usiozima, unaoweza kuonekana kwa kilomita kadhaa nyakati za usiku. Moto huo ulianza mwaka 1971 baada ya ardhi kuporomoka wakati wa uchimbaji wa gesi uliofanywa na wataalamu wa Kisovieti. Ili kuzuia kuenea kwa gesi hatari ya Methane, wataalamu hao waliamua kuuwasha moto wakiamini ungeisha ndani ya siku chache. Hata hivyo, moto huo umeendelea kuwaka mfululizo kwa zaidi ya miaka 50 sasa, ukigeuka kuwa moja ya maajabu yanayotisha na kuvutia zaidi duniani. Zaidi soma jamii.app/DarvazaGasCrat… #JamiiCheck #HakikiTaarifa #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck
Indonesia
0
0
4
100
Jamii Check
Jamii Check@JamiiCheck·
Wataalamu wa Hali ya Hewa wanaeleza kuwa tafiti zilizopo zinaonesha hakuna uhusiano wowote kati ya rangi ya nguo na uwezekano wa kupigwa na radi. Wilbert Kikwasi kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (#TMA) anasisitiza kuwa hakuna uthibitisho wa kisayansi unaoonesha rangi nyekundu kuvutia radi. Ili kujikinga na radi, inashauriwa kuepuka kutumia mwamvuli eneo litakalokufanya kuwa kitu kirefu kupita vingine, kuepuka kunawa mikono na kuepuka kuwa karibu na vifaa vya umeme. Soma jamii.app/NguoNyekunduRa… #JamiiCheck #HakikiTaarifa #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck
Jamii Check tweet media
Indonesia
0
1
3
113
Jamii Check
Jamii Check@JamiiCheck·
Waandishi wa habari 40 kutoka vyombo mbalimbali jijini Dar es Salaam wamepatiwa mafunzo ya Uhakiki na Uthibitishaji wa Taarifa, hatua inayolenga kuimarisha mapambano dhidi ya #TaarifaPotoshi katika zama hizi za Kidijitali. Mafunzo hayo yaliyotolewa na JamiiCheck Machi 9, 2026, yaliwapa washiriki fursa ya kujifunza kwa vitendo Mbinu na Nyenzo za Kidijitali za Kuhakiki na Kuthibitisha Taarifa, pamoja na matumizi sahihi ya Akili Unde (#AI). Baada ya mafunzo hayo, Washiriki waliahidi kutumia kikamilifu ujuzi walioupata ili kusaidia kuhakikisha Wananchi wanapata Taarifa Sahihi zitakazowawezesha kufanya Uamuzi Sahihi kuhusu masuala mbalimbali katika Jamii. #VisitJamiiCheck #FactsCheck #HakikiTaarifa #FactsChecking
Jamii Check tweet media
Indonesia
1
2
4
62