پن کیا گیا ٹویٹ

*DK. SAMIA MZIKI MNENE*
Na Mwandishi Wetu
Siku chache baada ya kufikisha siku 100 ikulu, katika kipindi cha pili cha awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Tanzania inaendelea kushuhudia kasi mpya ya maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Fuatilia mfululizo huu wa makala za kazi inaendelea na Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuleta Tabasamu la Taifa.
MIUNDOMBINU
Serikali imeongeza kasi ya ujenzi wa barabara, madaraja makubwa na reli ya kisasa, hatua inayorahisisha usafirishaji na kukuza biashara za ndani na nje ya nchi.
Maboresho ya bandari na viwanja vya ndege yameongeza ushindani wa taifa katika uchumi wa kikanda.
UMEME
Miradi mikubwa ya uzalishaji umeme imekamilishwa na mingine kuimarishwa, hali iliyoongeza upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa viwanda, biashara na makazi ya wananchi. Umeme umefika katika maeneo mengi zaidi vijijini, ukichochea shughuli za uzalishaji.
MAJI
Ujenzi na upanuzi wa miradi ya maji safi na salama umeboresha huduma kwa wananchi wa mijini na vijijini.
Wananchi wengi sasa wanapata maji karibu na makazi yao, kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kuyatafuta.
AFYA
Kuanzishwa kwa Bima ya Afya kwa Wote kumeleta matumaini mapya kwa wananchi, huku hospitali zikiboreshwa kwa vifaa tiba na wataalamu zaidi.
Upatikanaji wa dawa na huduma za msingi umeimarika katika maeneo mengi.
ELIMU
Sera ya elimu bila malipo imeendelea kuimarishwa kuanzia msingi hadi sekondari.
Mabadiliko ya mitaala yamelenga kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kisasa, ubunifu na stadi za maisha zinazoendana na mahitaji ya soko la ajira.
KILIMO
Sekta ya kilimo imepewa kipaumbele kupitia ruzuku za pembejeo, mikopo nafuu na juhudi za kufungua masoko ya uhakika kwa mazao ya wakulima, hatua inayoongeza tija na kipato chao.
MADINI
Mageuzi katika sekta ya madini yameongeza uwazi na mapato ya taifa, huku wachimbaji wadogo wakipewa msaada wa kitaalamu na masoko bora.
Uongezaji thamani ndani ya nchi umeanza kuimarika.
UTALII
Kupitia kampeni za kimataifa na maboresho ya miundombinu, sekta ya utalii imeendelea kukua, kuongeza mapato ya fedha za kigeni na ajira kwa vijana.
AJIRA
Fursa za ajira zimeongezeka kupitia miradi ya maendeleo, ukuaji wa sekta binafsi na uwekezaji mpya unaoendelea kuvutiwa nchini.
SAPOTI KWA WAJASIRIAMALI
Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara kwa kurahisisha usajili na upatikanaji wa mikopo kwa vijana na wanawake, hatua inayochochea ukuaji wa biashara ndogo na za kati.
UHUSIANO WA KIMATAIFA
Diplomasia ya uchumi imeimarisha mahusiano ya Tanzania na mataifa mbalimbali, kufungua milango ya uwekezaji, mikataba ya maendeleo na ushirikiano wa kibiashara.
MAONI YA WANANCHI
Wananchi wengi wanaeleza kuiona kasi ya maendeleo katika maeneo yao, wakisema maboresho ya miundombinu, afya, elimu na ajira yanaonekana kwa vitendo na kuongeza matumaini ya maisha bora zaidi.
Kaa tayari kupata uchambuzi wa sekta kwa sekta, mkoa kwa mkoa na taasisi kwa taasisi katika mfululizo wa makala maalum za Kazi inaendelea na Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuleta Tabasamu kwa Taifa.
Makala hizo zitaletwa kwenu kupitia magazeti ya JAMVI MEDIA GROUP na vyombo vingine katika njia za mtandao, magazeti, redio na Tv.

Indonesia




















