Siasa, na mpira wa miguu yalikuwa maisha yangu tokea utotoni kama mfatiliaji tu..kwenye fani ya uchambuzi wa michezo nilianza nikiwa secondary kwa kuwaeleza watu timu niliyoishabikia kwa nini ilishinda au kufungwa... Ipo siku nitageukia siasa Kwa sababu niliipenda zaidi ya mpira
Kutokujua Kiingereza sio tatizo sana, shida ni maswali yasiyo na maana yanayoulizwa. Waandishi wa habari tuulize maswali ya maana kwa Kiswahili na kuwa na mtu wa kutafsiri. Mfano, tuachane na maswali ya safari ilikuwaje,.. mwisho KAMA MWANDISHI HAUJUI KINGEREZA UMEKWISHA
Waliofeli shule nakufanikiwa kimaisha, wanaomba waliofaulu shuleni wafeli kimaisha wawacheke pia wawaajiri kwa pesa kidogo na masimango juu, tuwaombee wasomi wafanikiwe kimaisha ili wawe chachu kwa watoto wanaokuja kupenda shule
.....Sio mbaya siumeamua kuchaguaa
Moyo wako kumpa yule
Ila kaa ukitambua kwamba mi bila wewe ni sawa na bure
Au labda kuna kitu kipya ulikipata kutoka kwenye mwili wake yule
Na ukaniona mi mshamba na vyeo vyote ukamvika yeye....
"Aliyetangulia duniani ni mwanaume, yeye ndiye anajua chakula kinapatikana wapi , Siku mwanamke alipoleta chakula nyumbani walifukuzwa busitanini, money will put limit in your house - pastor Tony Kapora"
Kama hauna angalau milioni 5 kwenye akaunti yako ya benki, usione aibu kupokea simu za watu. Kila simu inaweza kuwa fursa ya kujifunza au kufungua mlango wa mafanikio....
Walipoomba mkopo, walisema wao ni yatima hawana baba wala mama. Lakini kwenye graduation wameenda na baba, mama, na wenza wao na watoto wao . Kwanza wamekuwa waongo , na pili wametumia pesa ya serikali kuoa 😂.
Ukiona anazidisha sana mapenzi tofauti na mwanzo,,,, weka akilini kuna kitu anahitaji kutoka kwako au TAYARI AMEKUACHA ( amempata mwingine au amerudi kwa yule wa zamani) ,,,ANAKUDANDANYA HUYO.
Kama nilimpenda mtu asiye sahii kwa kiwango hicho, je huyo aliye sahii nitampendaje? 🤔 Ni kama wingu zito la maswali moyoni mwangu, na ninafanya jitihada kuchunguza hisia hizi mpya, napambana ili aje kufurahi pia apate sehemu maalum katika moyo wangu.