Britanicca

6.5K posts

Britanicca banner
Britanicca

Britanicca

@Britanicca0

whistle-blower living in Vladivostok Russia , CCM Member Since 2002, Defending People.

Vladivostok, Russia Tham gia Nisan 2021
81 Đang theo dõi6.6K Người theo dõi
Tweet ghim
Britanicca
Britanicca@Britanicca0·
Kigogo hawa watu watafanya niwe active Tena hapa tuna kaa kimya kuficha aibu ndogo ndogo za chama Chetu sasa watu wasifanye nifungulie moto kama wakati wa Meko! Watu wanaleta masiala kwenye mambo nyeti dadeki hawa machawa Vipi kaka ?
Kigogo Media@kigogo2014

Hawajui haya mambo !...

Indonesia
5
5
42
20.2K
Britanicca đã retweet
Kigogo Media
Kigogo Media@kigogo2014·
KWA HAPA TULIPOFIKA TUME YA JAJI CHANDE IWE MAKINI SANA.📌 Kwa hali tuliyofika sasa tume ya Jaji Chande inapaswa kuwa makini sana na mambo yake inayoyofanya!.. Ni rahisi sana kwa tume hii kupoteza credibility ya kile watakachokuja kukisema wamechunguza kwa hii tabia yao ya kusogeza muda mbele kila siku na kuomba kuongezewa muda.! Tafsiri ya jambo hili ni nyepesi sana na ni kwamba tume inabadikisha na kumoderate findings zake ili kukidhi matakwa mahsusi ya wahusika maalumu ambao wameguswa na huu uchunguzi. 🚨Suala la kuongezewa muda mara mbili kwa tume hii ya Jaji Chande haliwezi kuwa ni muda hauwatoshi kwa kuwa tunaijua ToR/ hadidu za rejea zao na hazionyeshi kuwa tume imeelemewa na kazi mpaka watake muda kuongezwa kiasi hiki. 🚨Mambo pekee yanayoweza kufanya tume hii iongezewe muda marq mbili nje ya muda wa awaki ni yafuatayo; 👉 ripoti ina mambo magumu sana ambayo watawala wanajisikia kupaliwa na wanakosa pumzi ya kuhimili yakiende public 👉kuna watu wametajwa kwenye ripoti (akina Kizigha) ambao kwa haki yoyote ile wangependa walindwe na kutoonekana kwenye ripoti 👉kuna wahusika wakuu ametajwa na ripoti na kutakwa kwao kutavuruga uwepo wa serikali na CCM na dola 👉kuna watu na wahusika ambao wamekataa kutokewa sadaka na kufa peke yao badala yake wanataka jumba lote lianguke na lizame na wote waliohusika 👉kuna mapendekezo ya tume hayajafurahisha wakubwa na wahusika hicyo tume inalazimika kufumuafumua findings zake ili mapendekezo yawe na sukari kufurahisha wakubwa. 🚨Haiingii akilili kabisa kwa ToR hizi ziko 6 tu halafu tume ya Jaji Chande inaongeza muda mara mbili kutoa hii ripoti.! Kivipi yaani? Kwamba mambo bi mengi au? 🚨Kwa hali hii hapa hakuna ripoti ya maana itatolewa na kwa hali hii ni wazi kabisa sasa ni uchunguzi huru tu na wa nje ndiyo utatoa majibu ya nini kilifanyika kwenye ile shughuli ya 29 Oktoba 2025 kwa usahihi bila chenga chenga hizi ya Jaji Chande na tume yake!. 🚨Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kungoja hii ripoti ambayo tayari imeshaleta mashaka makubwa kiasi hiki na kuamini ina jambo la maana kuja kusemwa!.. WE NEED TO FIX THIS COUNTRY NOW... BEFORE IT IS TOO LATE.. #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media tweet mediaKigogo Media tweet media
Indonesia
0
18
121
21.6K
Britanicca đã retweet
Kigogo Media
Kigogo Media@kigogo2014·
UCHUMI WA TANZANIA UKO KUZIMU..TUACHE KUDANGANYA WATANZANIA KUWA UNAKUA📌 WATANZANIA wanaweza wakawa hawana maarifa ya kusoma na kuelewa takwimu za kiuchumi na kuzichambua lakini hawawezi kushindwa kusoma na kuelewa mambo tunayowaambia kwa urahisi na ulaini kama uji... UCHUMI wa Tanzania uko kuzimu na ni suala la muda tu tutakuwa tunaongea lugha moja na kukubaliana kuwa kwa miaka minne tokea 2021 Tanzania imekuwa inashauriwa vibaya kwenye tabia yake ya kukopakopa tukidhani kufanya hivyo ndiyo kukuza uchumi TUMESIKIA nyimbo za kuwa uchumi unakua kwa 6% lakini watanzania wanatoa macho tu kwa kuwa hawaoni huo ukuaji kwenye maisha yao ya kila siku na kwenye maisha yao na familia zao. Unapokuwa na uchumi wa hivi na kudanganya watu kuwa unakua ni wazi kuwa hujui unaongea nini na kama unaongea basi unajua unaongea na watoto wadogo wasiojua mambo haya.. Watanzania lazima waelewe kuwa ushauri wa hovyo wa aliyekuwa waziri wa fedha na sasa Waziri Mkuu Bwana Mwigulu ndiyo chanzo cha serikali ya Rais Samia kufanya maamuzi mabovu ya kuingiza nchi kwenye matatizo makubwa sana ya kiuchumi na leo tuko hapa tulipo mpaka tunaogopa kuchambua takwimu zetu wenyewe kwa kuwa zinaogopesha. TUNAPOWAAMBIA kuwa kukua kwa uchumi na kukusanya mapato kunakovuka malengo na TRA ni bosheni maana yake ni hii ifuatayo; KUHUDUMIA DENI LA TAIFA/ DEBT SERVICING 🚨 Deni la Tanzania kwa sasa tunalipa riba na deni ni 14.5% ya mapato ya taifa ( 14.5% of government revenue) 🚨 Kiwango cha juu kabisa cha kimataifa cha pato la taifa kulipia madeni na riba hakipaswi kuwa 18% ya mapato ya taifa ( dept servicing ceiling MUST NOT exceeds 18% of govt revenue) 👉🏼Kwenye awamu hii ya bwana Mwigulu kama waziri wa fedha ameifikisha Tanzania kwenye kulipa madeni kwa kutumia 14.5% ya mapato yake na kiwango cha kimataifa kinachoruhusiwa ni 18% ya mapato 👉🏼 Kwa takwimu hizi maana yake deni walilokopa kinyemela Dec 2025 na halijakuwa captured litaipeleka Tanzania kwenye limit ya mwisho kabisa ya ukomo wa 18% ya pato la taifa kulipa madeni na mikopo. 👉🏼 Kwa takwimu hizi za BoT na serikali yenyewe maana yake tumebakiza 3.5% buffer ya kufika 18% ya ukomo wa kutumia pato la taifa kulipa mikopo na madeni.. Sasa kwa hali hii nataka tujiulize uchumi gani unakua na tunawezaje kujipiga kifua kuwa tunakuza uchumi? Uchumi unaokuwa kwa ajili ya kulipa madeni una faida gani kwa watanzania? TRA wanapokusanya mihela na kuvuka malengo kila siku lakini zinakwenda kulipa madeni kuna faida gani kwa watanzania? Mimi napenda sana kuangalia namba na takwimu kwa sababu hizi ndizo zinaonyesha tofauti ya uelewa wa mambo kati ya wenye huruma na nchi hii na waliopo kwa ajili ya kupiga mapambio tu. Huwezi kuwa na nchi ina uchumi unaokuwa na una manufaa kwa watanzania kama; 🚨uwiano wa deni na ukuaji wa uchumi ni 48.2% huku kiwango kinachoruhusiwa ni 55% ( tuna only 5-6% buffer kufika kiwango cha mwisho cha kimataifa) 🚨gharama ya kulipa deni na mikopo iko kwenye 14.5% ya pato kuu la taifa huku kiwango cha kinachoruhusiwa ni 18%( tuna 3% buffer kufika kiwango hatarishi ) 🚨unakuwa na ongezeka la deni kwa miaka minne tu (2021-2025) kufikia $6.2b kwa mwaka na kufanya deni kuwa ni $53.3tr ( na kwa ongezeko la mkopo fulani wa Disemba 2025 ni 130trilion TZS) 🚨Ongezeka la deni la taifa kwa kipindi cha 2021-2025 ni kubwa kuliko mikopo yote toka 1961 yaani Tanzania toka ipate uhuru na kimahesabu ni ongezeka la 26,650%( yaani deni limekuwa kwa pasenti elfu ishirini na sitamia sita na hamsini) Kwa hali hii tunamdanganya nani kuwa uchumi unakua? Tunamficha nani na takwimu ziko uchi kiasi hiki?Haya sisi tungeweza kukaa kimya kama tulivyokuwa tunakaa kimya kwenye mauozo mengi sana ya serikali lakini hii ni maisha ya watanzania na tunakopa sana na hela zinaibiwa na majizi kama akina Anjela Kizigha.. LAZIMA tufike mahalii tukubali kuwa Mwigulu amechangia kuuwa uchumi wa hii nchi na tukiri kuwa serikali hii imeuwa uchumi na imetumbukiza nchi shimoni. WE NEED TO FIX THIS COUNTRY📌 #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media tweet media
Indonesia
0
3
37
3.1K
Kipanga
Kipanga@Kipanga1986·
Kwamba muda waliopewa haukutodha au vip, kuna mchezo gani unachezwa hapa? Sawa siku21 sio nyingi sana
Kipanga tweet media
Indonesia
3
2
6
502
Britanicca
Britanicca@Britanicca0·
Heshima uliyojijengea kwa miaka zaidi ya 50, usiiharibu kwa vipande 30 vya fedha
Indonesia
0
3
8
747
Britanicca
Britanicca@Britanicca0·
Report Inaweza isisomwe kama ya wizi wa Mali za CCM maana kuna Sehemu pameguswa ni wakubwa sana
Indonesia
2
4
29
8.5K
Britanicca
Britanicca@Britanicca0·
Sawa walikuwa na mapungufu ila Ma kizigha kizigha couldn’t even dare to touch state house
Britanicca tweet media
Indonesia
8
10
213
13.7K
Britanicca đã retweet
Dr Lwaitama
Dr Lwaitama@lwaitama1·
Magufuli ndiye mwasisi wa mauaji ya 29/10.Wa TZ wengi hawawezi kulijua kwa sababu elimu yetu imefanya nchi iwe na mass ignorance.Hata Samia ni product ya Magufuli,kwa akili nilikuwa naona kabisa kuwa kumfanya Samia awe ''president in waiting''lilikuwa ni jambo la hatari sana.
Indonesia
36
42
229
8K
Britanicca đã retweet
Kigogo Media
Kigogo Media@kigogo2014·
UTEUZI WA ANJELA KIZIGHA UMEIDHALILISHA SANA IKULU📌 IKULU ni sehemu adilifu sana na takatifu sana kuliko ofisi zote za nchi na ni mahali ambapo panapaswa kuwa na integrity ya hali ya juu sana kwa kuwa ndipo ilipo ofisi ya juu kuliko zote ndani ya nchi. IKULU ni sehemu takatifu sana na haipaswi kuwa ni sehemu inayonyooshewa vidole kwa mambo ya hovyo hovyo na machafu kwa kuwa inapaswa kuwa na uadilifu wa haki ya juu sana. IKULU siyo sehemu ya kuingiaingia wezi na wahuni na mafisadi na kuigeuza ni sehemu yao ya kwenda kutembea au kuigeuza kama ni sebuleni kwao wanakwenda tu kupumzika au kunywa pombe wakitaka! IKULU yetu imegeuka kuwa sehemu isiyo na heshima na usafi wowote kwa aina ya mambo yanayofanyika ndani yake ikiwemo la Anjela Kizigha kuteuliwa kuwa mbunge wa bunge la Tanzania huku akiwa mbunge wa EALA na wanaomteua wakijua wamekiuka katiba ya Tanzania ambayo waliacha kuiheshimu na kuifuata muda mrefu sana na wamevunja treaty iliyoanzisha EA community. Tunapokuwa tumefika hatua tuliyoko sasa ya teuzi zinafanywa na kuvunja taratibu na katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa na tunaona sawa tu basi tukae tukijua ofisi hii kuu ya nchi imeshaharibiwa sana na imetekwa iko mikononi mwa watu ambao hawajali lolote zaidi ya maslahi yao na siyo watanzania. Unamteuaje Anjela Kizigha kuwa mbunge? Kwanza ana kashfa nyingi za wizi, ufisadi na anatajwa kuhusika kwenye kupanga mauaji ya watu 29 Oktoba 2025 akiwa ndani ya Ikulu yetu huku cheo chake kikiwa hakijulikani anafanya kazi gani. Mtu anayetajwa kwenye lundo la kashfa za mikataba ya wizi ndani ya nchi hii na kutumia nafasi yake na uswahiba wake na wakazi wa Ikulu kufanya mambo ya kutisha kiasi kile anateuliwaje kuwa mbunge? Anateuliwa kupewa zawadi au shukrani ya kuhusika na kuuwa watu? Anapewa cheo kama zawadi ya kuhusika na wizi wa hela za watanzania? Anapewa cheo kumpa zawadi kwa kuwa sehemu ya kampeni za uchaguzi ule? Anapewa cheo kama zawadi ya kusaidi kutumia makampuni yake kupitishia hela za wizi? Anapewa cheo cha nini hasa? Maswali ni mengi lakini mwisho wa siku jibu ni moja tu kuwa amepewa cheo kama ishara ya kumshukuru kwa aliyoyafanya akiwa Ikulu na ndiyo maana hatujali ana uchafu kiasi gani au ana kashfa kiasi gani anapewa cheo na watanzania mkiongea mtajiju yaani!.. Anjela Kizigha kitaaluma na kimaarifa hana uwezo huo wa kuwa ni mtanzania exceptional sana wa kulazimika kuvunjwa kwa katiba ili ateuliwe. Ameteuliwa ili kumuondoka Ikulu ambako alikuwa ni king'ang'a kama luba huku tukisahau kuwa uteuzi wake ni wa hovyo na unavunja katiba. Tunapofika mahali IKULU ya nchi inafanya mambo kwa mtindo huu basi ni wazi kuwa tumepoteza sifa ya IKULU kuwa sehemu safi na ofisi ya juu kabisa ya nchi!..Ikulu imegeuka kuwa kijiwe cha watu kupeana vyeo kwa matakwa ya kirafiki na undugu na kuacha misingi ya teuzi za watu kuzingatia sifa na uwezo na taaluma zao!.. Anjela Kizigha ana tuhuma za kuhusika kwenye kampuni yake kuingiza silaha nchini zilizotumika kwenye shughuli pevu ya 29 Oktoba 2025. Iwe ni kweli au uongo hiyo tu ilitosha kungoja tume ya Jaji Chande ije kusema nani na silaha gani zilitumika kwenye ile shughuli. Kama tunampenda sana kulikuwa na shida gani kungoja asafishwe na tume ndiyo teuzi hizi za ki nepotism ziendelee? Kulikuwa na haraka gani yaani? Mwanasheri Mkuu wa serikali Bwana Hamza Johari amekuwa anapotosha IKULU kwenye teuzi nyingi sana na amekuwa anafanya hivyo kwa kuwa yeye mwenyewe uteuzi wake una mashaka na ulivunja katiba! Hakuwa na sifa za kuwa hapo alipo! Kwa hiyo unapokuwa na AG hana sifa haya ndiyo matokeo yake. Na shida zaidi utakuja kuiona kwenye aina ya mikataba ya madiki inayosainiwa na serikali na kupitia kwake!. Aina hii ya AG ndiyo ilifanya watu wamepiga hela yote ya SGR kule Tabora , wamepiga hela yote ya mradi wa maji kule Same na hakuna kitu wamefanywa!.. MWISHO ni kuwa uteuzi wa Anjela Kizigha ni wa hovyo na umedhalilisha IKULU na kuifanya kuwa sehemu isiyo na uzito wowote kwa kuwa inavunja sheria kila siku. #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media tweet mediaKigogo Media tweet media
Indonesia
1
6
56
7.4K
Britanicca
Britanicca@Britanicca0·
Tanzania
Britanicca tweet media
Español
2
9
60
4.1K
Britanicca
Britanicca@Britanicca0·
Inasikitisha sana kuona nchi imetekwa na wanyang'anyi na maharamia; na bado tumelala tu. Ma-cartel wamejimilikisha uchumi wa nchi yetu, kampuni moja ina ubia na watu walioko serikalini ilipewa tenda kuagiza mafuta na kusimamia bei
Indonesia
0
5
26
631
Britanicca
Britanicca@Britanicca0·
Kusogezwa sogezwa kwa Tarehe ya Kusoma Report nanusa kitu hapa ili editing ifanyike vema
Britanicca tweet media
HT
11
17
171
6.3K
Britanicca
Britanicca@Britanicca0·
Madilu Bwana 😆 na huyu ana mahitaji maalumu? Sanaa
Britanicca tweet media
Indonesia
35
13
285
34.7K
Britanicca đã retweet
African Hub
African Hub@AfricanHub_·
Tanzania 🇹🇿 government officials struggling to go through a road
English
8
46
191
15.6K
Britanicca đã retweet
millardayo
millardayo@millardayo·
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amehoji kupanda kwa ghafla kwa bei ya mafuta Nchini, akitaka ufafanuzi kuhusu uhalali wa ongezeko hilo licha ya uwepo wa hifadhi ya mafuta iliyotangazwa na Serikali. Heche ametoa kauli hiyo leo, Aprili 6, 2026, akirejelea taarifa ya awali ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt, James Mataragio. Kwa mujibu wa Heche, Katibu Mkuu huyo aliwahakikishia Watanzania kuwa Nchi ina akiba ya mafuta inayoweza kutumika kwa takribani miezi mitatu. Hata hivyo, amesema inashangaza kuona Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ikitangaza ongezeko la bei ya mafuta siku chache baadaye, hali inayozua maswali kuhusu uhalisia wa hifadhi hiyo na namna bei zinavyopangwa. Aidha, ameeleza kuwa kihistoria, Tanzania iliweka miundombinu ya kuhifadhi mafuta tangu baada ya Vita vya Kagera mwaka 1979, ambapo hayati Mwalimu Julius Nyerere alianzisha matenki ya kuhifadhia mafuta katika eneo la Kigamboni ili kujikinga na athari za dharura za kiuchumi na kiusalama. Kwa msingi huo, Heche amehoji mantiki ya kupanda kwa bei wakati mafuta yaliyopo yalipaswa kuwa sehemu ya akiba hiyo ya ndani. "Tutakumbuka Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, anayeitwa Bw. Mataragio, alitoka na akawaambia Watanzania kwamba bado tuna hifadhi ya mafuta ya kutumia kwa miezi mitatu. Na kama mnavyokumbuka, tangu baada ya vita ya Uganda na Tanzania mwaka 1979, Mwalimu Nyerere alijenga matenki ya kuhifadhia mafuta ya TIPER ambayo yapo Kigamboni, baada ya kujifunza kwamba kunaweza kutokea dharura na nchi ikaingia kwenye matatizo." Na matenki haya yamekuwa yakihifadhi mafuta ya ndani ya Nchi na mafuta ambayo yanasafirishwa kwenda kwenye Nchi zinazotumia Bandari yetu. Ndiyo maana Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati alituambia kwamba kuna mafuta ya miezi mitatu. Sasa kama tuna mafuta ya miezi mitatu ambayo, huu mgogoro ulipoanza, yalikuwa tayari yako ndani ya Nchi, inakuwaje hayo mafuta yapande bei ghafla kabla ya kuingizwa kwa mafuta mapya ambayo yameingia Nchini?" amesema Heche. #MillardAyoUPDATES.
Indonesia
12
25
228
9K
Britanicca đã retweet
3AM….SWAG🃏🏴‍☠️
🚨 JUST IN: Nigerian business mogul and UBA CEO Tony elumelu has reportedly divorced his wife after a DNA test shows his 7 children doesn't belong to him.
3AM….SWAG🃏🏴‍☠️ tweet media3AM….SWAG🃏🏴‍☠️ tweet media
English
2.5K
718
5.9K
959.4K
Britanicca
Britanicca@Britanicca0·
Hii ni project nzuri ya kugawia watu fulani pesa. Tunajua from the beginning kwamba hakuna namna ambayo taxpayers wa Tanzania watanufaika na matokeo ya kazi ya tume
Maulid Kitenge@mshambuliaji

MAMLAKA ya Uteuzi imeridhia maombi ya muda wa ziada kwa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 hivyo imeiongezea tena muda wa siku ishirini na moja (21) na kuitaka ikamilishe kazi kabla au ifikapo Aprili 24, 2026. Mamlaka hiyo imeeleza sababu za kuongeza muda huo kwa Tume ni pamoja na kuiwezesha Tume kukamilisha uchambuzi wa ushahidi, taarifa na maoni yaliyopokelewa, kutoa fursa kwa wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi kufanyia kazi baadhi ya vielelezo vipya vilivyowasilishwa. Sababu nyingine ni kuiwezesha Tume kukamilisha maandalizi ya Ripoti itakayowasilishwa kwa Rais na kutoa fursa kwa Tume kuandaa tafsiri ya Ripoti hiyo. Tume hiyo ilianza kutekeleza majukumu yake Novemba 20, 2025 na kutarajiwa kukamilisha kazi yake ndani ya kipindi cha siku 90. Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali, Tume iliongezewa muda wa kukamilisha kazi na kutakiwa kuwasilisha Ripoti kwa Rais kabla au ifikapo April 3, 2026. Hivyo, kufuatia nyongeza ya muda, wananchi waliendelea kujitokeza kwa wingi tofauti na matarajio ya Tume. Hivyo, Tume iliendelea kupokea ushahidi, taarifa na maoni zaidi. Kwa sababu hiyo, Tume haikuweza kukamilisha kazi yake ndani ya muda wa nyongeza uliotolewa na hivyo kulazimika kuomba muda wa ziada ili kukamilisha kazi yake. Tume inaendelea kuwashukuru wananchi na wadau wote waliotoa ushirikiano kwa Tume wakati wa kufanya uchunguzi, ikiwemo wale waliofika mbele ya Tume kutoa ushahidi, taarifa na maoni, waliopiga simu na kutuma ujumbe, waliotuma ushahidi, taarifa na maoni kwa maandishi na waliowasiliana na Tume kwa njia za mitandao ya kijamii. #KitengeUpdates

Filipino
0
0
0
392