
Mwananzengo
73.5K posts

Mwananzengo
@SpotiMasta
Mwanazengo Investiment







DK. SAMIA MWENDO MDUNDO Anachanja Mbuga Kanda ya Ziwa, Bukombe Yatingisha kwa 'MASHINE' Biteko Na Mwandishi Wetu – Geita Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuchanja mbuga katika mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu. Katika mwendelezo wa ziara zake Kanda ya Ziwa, Dkt. Samia amepokelewa kwa shangwe na maelfu ya wananchi waliomiminika kumshuhudia na kusikiliza sera za maendeleo anazoendelea kuzisemea kwa nguvu. Akizungumza jana katika mikutano mikubwa wa kampeni iliofanyika Ushirombo, Runzewe - Bukombe, na ule wa awali uliofanyika Mbogwe mkoani Geita, Dkt. Samia aliwapigia wananchi saluti kwa umoja wao na kuwashukuru kwa kumwamini yeye pamoja na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayoleta matokeo halisi kwa wananchi. Katika mkutano hiyo iliofurika wananchi, Rais Samia alimsifia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, akimwelezea kama “MASHINE” iliyothibitisha uwezo wake kwa vitendo. “Nataka niwaambie, mmeniletea MASHINE. Mmeniletea kijana ambaye nilimuamini kumfanya awe Naibu Waziri Mkuu, kijana ambaye anatusaidia sana kazi zetu. Na kwa sababu ya hiyo, nanyi mkamuheshimu — hakuna mwingine aliyejitokeza,” alisema Dkt. Samia huku akishangiliwa kwa nguvu na wananchi wa Bukombe. Kanda ya Ziwa yaendelea kung’aa kwa miradi mikubwa Ziara ya Dkt. Samia Kanda ya Ziwa imekuwa sio tu ya kisiasa, bali ni onyesho la matokeo ya kazi kubwa iliyotekelezwa na serikali yake katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Kanda hii imekuwa kinara wa miradi mikubwa ya kimkakati katika sekta za miundombinu, maji, nishati, kilimo na madini. Miongoni mwa miradi hiyo ni Daraja la Busisi lenye urefu wa zaidi ya kilomita 3.2 linalounganisha mikoa ya Mwanza na Geita, mradi ambao ukikamilika utarahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa kutoka maeneo ya uzalishaji hadi masoko, hususan sekta ya uvuvi, kilimo na madini. Vilevile, serikali imetekeleza kwa kasi miradi ya maji vijijini na mijini kupitia mamlaka mbalimbali za maji na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), ambapo maelfu ya wananchi wa maeneo ya Geita, Chato, Misungwi, Sengerema na Bukombe sasa wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao — hatua iliyopunguza adha kubwa kwa wanawake na watoto. Katika sekta ya kilimo, Rais Samia ameongeza bajeti ya pembejeo kwa wakulima wa pamba, mpunga, na mahindi, huku ruzuku ya mbolea na mbegu bora ikiimarisha uzalishaji na kipato cha wakulima. Serikali imewezesha pia upanuzi wa skimu za umwagiliaji katika maeneo ya Magu, Nyang’hwale, na Shinyanga, hatua inayosaidia kilimo cha uhakika hata katika vipindi vya ukame. Sekta ya madini nayo imepiga hatua kubwa. Kanda ya Ziwa sasa imekuwa injini ya uchumi wa madini nchini, huku shughuli za uchimbaji zikisukumwa na sera rafiki kwa wachimbaji wadogo, na ujenzi wa vituo vya ukusanyaji na uchenjuaji madini ukiendelea kwa kasi katika Geita, Chunya na Kahama. Bukombe, wilaya inayong’ara leo kwenye kampeni, imepata pia neema ya miradi mipya ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Uwanja wa mpira wa Ushirombo, unaotarajiwa kufungua fursa za kiuchumi, utalii na biashara kwa mkoa mzima wa Geita kwa timu mbalimbali kuutumia utakapokamilika. Hamasa ya ushindi yazidi kupanda Wachambuzi wa siasa wanasema kampeni za Dkt. Samia Kanda ya Ziwa zimekuwa zenye mwamko mkubwa kuliko kipindi chochote, zikionekana kama sherehe za kutathmini matunda ya uongozi wake. Maelfu ya wananchi wamejitokeza katika kila eneo, wakiwa na mabango na ujumbe wa kumpongeza kwa utekelezaji wa miradi inayogusa maisha yao moja kwa moja. Kwa wengi, Kanda ya Ziwa imekuwa kielelezo cha “maendeleo yanayoonekana” chini ya uongozi wa Dkt. Samia — maendeleo yanayojengwa juu ya dira ya umoja, utulivu na kazi. #Samia2025 #MwendoMdundo #Bukombe #MASHINE #KandaYaZiwa #CCM #KaziInaendelea #TanzaniaMpya
















