Ahmad Issa Michuzi

46.1K posts

Ahmad Issa Michuzi banner
Ahmad Issa Michuzi

Ahmad Issa Michuzi

@MichuziJr

Influencer

Dar es salaam Beigetreten Haziran 2009
1.8K Folgt47K Follower
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
BENKI YA EQUITY TANZANIA YAZINDUA TAWI JIPYA LA UBUNGO LILILOPO EAST AFRICAN COMMERCIAL LOGISTICS CENTRE (EACLC) JIJINI DAR ES SALAAM. Benki ya Equity Tanzania imezindua rasmi tawi jipya la Ubungo, lililopo ndani ya EACLC Mall (East African Commercial Logistics Centre),Ghorofa la Kwanza, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huu ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo wa kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja na kuongeza urahisi wa kupata huduma kwa wakazi wa eneo la Ubungo na maeneo jirani.Tawi hili jipya linatoa huduma kamili za kibenki, ikiwemo kufungua akaunti, kutoa mikopo, kuweka na kutoa fedha, huduma za fedha za kimataifa (money transfer), huduma za biashara, na usaidizi kwa wateja wa benki hiyo. Kwa kufunguliwa kwa tawi hili, Equity Tanzania inaimarisha mtandao wake wa matawi nchini, unaoendelea kukua kwa lengo la kuwafikia watanzania wengi zaidi. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania, Bi. Isabela Maganga, aliyezindua rasmi tawi hilo, alisema kuwa uzinduzi wa tawi la Ubungo ambalo ni tawi la kibiashara ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa benki hiyo kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kifedha karibu na maeneo wanayoishi na kwenye maswala amziam ya kibiashara biashara. Tunaendelea kuwekeza katika miundombinu ya matawi na teknolojia ili kuhakikisha huduma zetu zinawafikia Watanzania wengi zaidi, hasa wale walio kwenye maeneo yenye shughuli nyingi za kiuchumi. Ubungo ni kitovu muhimu cha biashara na usafiri, hivyo tawi hili litasaidia kuongeza kasi ya shughuli za kifedha kwa wafanyabiashara na wakazi wote wa eneo hili," alisema Bi. Maganga. Tawi hili linajumuishwa katika jumla ya matawi 19 ya benki yaliyopo nchini, ambayo yanaendelea kutoa huduma kwa wateja katika mikoa mbalimbali. @TzEquityBank
Ahmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet media
Filipino
0
0
0
41
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (katikati), Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil (mbele kulia), Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza (mbele kushoto) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Tausi Kida (wa tatu kushoto nyuma) wakiwa katika moja ya Mitaa ya Jijini Washington DC nchini Marekani wakielekea Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF kwa ajili ya kushiriki Mikutano mbalimbali ya Majira ya Kipupwe. Tanzania ni nchi mwanachama wa Taasisi hizo kubwa za fedha duniani. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington D.C, Marekani).@mofURT
Ahmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
3
2
23
4.2K
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb)(kushoto), akiwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Biashara - Business Council for International Understanding (BCIU), Bw. Peter Tichansky, baada ya Mkutano wao wa Uwekezaji ulioandaliwa na Baraza la Biashara - Business Council for International Understanding (BCIU), uliofanyika katika Ofisi za BCIU, jijini Washington D.C nchini Marekani, pembezoni mwa Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, ambapo BCIU wameonesha nia kuwekeza nchini katika Bima kwa wakulima, kuzalisha mbegu bora za kisasa, bandari na katika Sekta ya Afya. @mofURT
Ahmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
1
1
2
190
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kulia), ukiwa katika Mkutano wa Uwekezaji ulioandaliwa na Ujumbe Baraza la Biashara - Business Council for International Understanding (BCIU) (kushoto), uliofanyika katika Ofisi za BCIU, jijini Washington D.C nchini Marekani, pembezoni mwa Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, ambapo BCIU wameonesha nia kuwekeza nchini katika Bima kwa wakulima, kuzalisha mbegu bora za kisasa, bandari na katika Sekta ya Afya. @mofURT
Ahmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
1
2
3
184
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
𝗖𝗖𝗠 𝗬𝗔𝗧𝗢𝗔 𝗙𝗨𝗡𝗭𝗢 𝗟𝗔 𝗨𝗪𝗘𝗞𝗘𝗭𝗔𝗝𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗩𝗬𝗔𝗠𝗔 𝗩𝗬𝗔 𝗨𝗣𝗜𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜 "Fremu hizi hazipangishwi kwa wana CCM pekee, bali ni wananchi wote wa vyama vyote CUF, CHAUAMA, ACT, CHADEMA na wengine wote wanaruhusiwa hata wasio na vyama..CCM hakuna ubaguzi tunafanya kazi na watu wote, tunnachoangalia ni maslahi mapana ya Taifa letu na ndicho kipaumbele chetu.." Hayo yameelezwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. 𝗞𝗲𝗻𝗮𝗻𝗶 𝗞𝗶𝗵𝗼𝗻𝗴𝗼𝘀𝗶 leo tarehe 17 Aprili 2026, wakati akizungumza na wananchi alipotembelea na kukagua mradi wa kitega uchumi wa CCM unaojengwa katika eneo la sabasaba Kata ya Kalangalala Wilayani Geita Mjini Mkoani Geita. Akirejea kwenye maazimio ya Mkutano Mkuu wa CCM uliopita, Mwenezi Kenani amebainisha kuwa miongoni mwa maazimio 18 ilikuwa ni jukumu la kuimarisha uchumi wa Chama pamoja na Jumuiya zake huku akitoa pongezi kwa Mkoa wa Geita kutekeleza maazimio hayo kwa vitendo. Mwenezi Kenani amesema utekelezaji wa miradi hiyo ni wazi kuwa CCM imelenga katika kuhakikisha kila mtanzania anakuwa kiuchumi, imelenga kusimamia maslahi na matakwa ya watanzania wote pasipo kujali dini, ukabila wala itikadi za vyama vyao. Akieleza zaidi kuhusiana na mradi huo, Mwenezi Kenani amebainisha kuwa mradi huo umekuwa sehemu ya kuwanufaisha wananchi wa Geita kwakuwa kumekuwa na ajira mbalimbali katika utekelezaji wa mradi huo huku ukifungua fursa kwa wajasiriamali wadogowadogo wakiwemo Mama lishe hali iliyopelekea kuinua sehemu ya uchumi wa wananchi wa Geita wanaozunguka mradi huo. Katika hatua nyingine, Mwenezi Kenani ametoa rai kwa vyama vingine vya siasa nchini kujifunza kupitia CCM namna nzuri ya kukusanya mapato na kuyafanyia matumizi ya uwekezaji yenye tija kwa Chama na Taifa kwa ujumla. "..Ninaamini hata wenzetu ambao wanapenda kuomba michango na kuitafuna wana wajibu wa kuja kujifunza kwenye uwekezaji maana nimeona jana kwenye taarifa kuna bwana mmoja ameposti tunaomba mchango, tunaomba tonetone, yani familia zao zipo Ulaya zinalipwa wanakula maisha na wanataka hela za Watanzania..tushtuke tuone kabisa kwamba kuna makanjanja kwenye siasa.." Alisema Mwenezi Kenani. #KaziNaUtuTunasongaMbele
Indonesia
0
1
1
55
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameitembelea na kuifariji familia ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Marehemu William Vangimembe Lukuvi, katika mkazi yao Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 16 Aprili 2026. Wakati wa Msiba na Mazishi ya Kiongozi huyo, Makamu wa Rais alikuwa nje ya nchi kwa ziara ya kikazi.
Ahmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
1
7
75
10.7K
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
MNEC-SUKI RABIA HAMIDI,KANSELA WA CPC WAFANYA KIKAO KAZI JIJINI DAR Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndg. Rabia Abdalla Hamid, amefanya Kikao kazi na Kansela wa Chama Cha Kikomunisti (CPC), Ubalozi wa China nchini Tanzania Ndg. Xu Sujiang leo tarehe 16.04.2026, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam. Lengo la kikao hicho ni kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha uhusiano na itikadi za vyama hivyo. @ccm_tanzania
Ahmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
0
0
2
93
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
NMB Yatoa Sh Milioni 500 Kusaidia Huduma za Upandikizaji Figo na Uboho BMH. Mgeni Rasmi na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu (wa pili kulia), akipokea hundi mfano kutoka kwa Mkurugenzi wa Mahusiano ya Wawekezaji, Uendelevu na Mawasiliano ya Umma wa Benki ya NMB, Innocent Yonazi (kushoto), wakati wa hafla ya uchangishaji wa Mfuko wa Upandikizaji Figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, hoteli ya Serena Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Prof. Abel Makubi (wa pili kushoto), na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa NHIF, Dk. Raymond Mwenesano (kulia). @nmbtanzania Benki ya NMB imeahidi kutoa Sh milioni 500 ndani ya kipindi cha miaka miwili kwa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), kusaidia upanuzi wa huduma za upandikizaji figo na uboho. Hatua hiyo inaonesha dhamira ya benki hiyo katika kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za afya za kibingwa nchini na kuwafikishia Watanzania huduma muhimu karibu zaidi. Ahadi hiyo ilitangazwa katika hafla ya uchangishaji fedha iliyofanyika Dar es Salaam, ambapo Sh milioni 250 zilikabidhiwa kama sehemu ya utekelezaji wa msaada huo. Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, alisema uwekezaji katika huduma maalumu za matibabu ni muhimu kwa sababu unasaidia kupunguza gharama kubwa ambazo wagonjwa na familia zao hulazimika kubeba wanapotafuta tiba nje ya nchi. Akizungumza kwa niaba ya NMB, Mkurugenzi wa Uhusiano kwa Wawekezaji, Uendelevu na Mawasiliano, Innocent Yonazi, alisema mchango huo unaakisi azma ya benki hiyo ya kuendelea kuunga mkono vipaumbele vya maendeleo ya taifa, hasa katika sekta ya afya. Alieleza kuwa NMB imeendelea kuelekeza sehemu ya faida yake kwenye shughuli za uwajibikaji kwa jamii, huku afya ikiwa miongoni mwa maeneo yake muhimu ya kipaumbele. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Prof. Abeid Makubi, alisema msaada huo utaongeza uwezo wa hospitali kutoa huduma hizo kwa Watanzania wengi zaidi, hususan wale wasioweza kumudu gharama za matibabu ya kibingwa.
Ahmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
0
0
0
130
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Mgore Miraji wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu Dkt. Nchemba amemuomba kutembelea Jimbo la Musoma Mjini kwaajili ya kutafuna mifupa migumu ambayo inakwamisha maendeleo.
Indonesia
1
0
1
192
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
KATIBU MKUU CCM AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA JUMUIYA YA MADOLA Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Asha-Rose Migiro, leo tarehe 15 Aprili 2026 amefanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Lazarus Chakwera, katika Ofisi za CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalijikita katika hali ya kisiasa nchini pamoja na matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Mhe. Chakwera yupo nchini Tanzania kwa ziara maalum katika nafasi yake kama Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Shirley Ayorkor Botchwey. Kikao hicho ni sehemu ya mashauriano yake na wadau mbalimbali wa kitaifa kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu maendeleo ya kisiasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025, pamoja na juhudi zinazoendelea za kuimarisha amani, demokrasia na mshikamano wa kitaifa nchini Tanzania. @ccm_tanzania @AshaRoseMigiro @LAZARUSCHAKWERA
Ahmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
0
0
2
195
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia kitabu kinachoelezea masuala ya Mazingira, Nishati na masuala mbalimbali ya Poland wengine pichani ni Rais wa Kampuni ya Grupa Zenith kutoka nchini Poland, Dkt. Aleksander Joseph Widuchi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Aleksandra Stephania Widuchi, tarehe 14 Aprili, 2026 Ikulu Dar es laam.
Ahmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
0
0
0
103
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
Tusibezi sana kwenye matokeo ya kisiasa, yatatupeleka pabaya,tubezi sana kwenye matokeo ya kufanya kazi ili tupate Taifa bora na si bora Taifa - Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao ndugu Steve Nyerere @stevenyerere2
Indonesia
0
1
0
74
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
KUHUSU HOFU : Ni kweli,wengine hawataki kufanya kazi,lazima tuwe ma Taifa la watu wanaofokasi kwenye maendeleo,Vija wengi wanafokasi kwenye siasa,wanafokasi kwenye kubeti,kwenye mifumo ambayo sio ya kwao"- Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao ndugu Steve Nyerere @SteveNyerere2
Indonesia
1
0
0
161
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
KATIBU MKUU MIGIRO AWASILISHA SALAAM ZA DKT. SAMIA KWA RAIS WA SAHRAWI Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahara (SADR), Mhe. Brahim Ghali. Katika mazungumzo hayo, aliwasilisha salaam za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 9 Aprili 2026 katika makazi rasmi ya Mhe. Ghali, Kambi ya Ausserd, Tindouf, Algeria. Balozi Migiro alisisitiza kuwa msimamo wa Tanzania na CCM wa kuunga mkono haki ya watu wa Saharawi kujitawala ni wa muda mrefu. Alieleza kuwa msingi wake uliwekwa tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Kwa upande wake, Mhe. Ghali alimshukuru Rais Dkt. Samia kwa salaam na kwa kutuma uwakilishi kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya SADR yaliyofanyika tarehe 8 Aprili 2026 katika Kambi ya Ausserd. Pia aliomba salamu zake zifikishwe kwa Rais, CCM na Watanzania. Aliongeza kuwa watu wa Saharawi wanathamini mchango wa Mwalimu Nyerere katika kuhamasisha mshikamano wa Afrika na dunia. Alisema mshikamano huo umeendelea kuimarisha harakati za SADR, chini ya uongozi wa Chama cha Polisario, katika kudai haki ya kujitawala. @ccm_tanzania
Ahmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
0
0
1
103
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
ZAIDI YA WATALII TISINI WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA MKOMAZI KUFUATIA UFUNGUZI WA TAMASHA LA SAME UTALII FESTIVAL. Zaidi ya Watalii 90 wametembela Hifadhi ya Taifa Mkomazi kuvinjari na kufurahia utalii wa ndani leo Aprili 11, 2026 kufuatia ufunguzi wa tamasha la utalii lijulikanalo kama Same Utalii Festival msimu wa Tatu katika viwanja vya stendi wilayani Same, Mkoani Kilimanjaro. Watalii hao walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi ikiwemo Mbula, Kisima na Njiro na kujionea wanyamapori aina ya faru weusi, kivutio kinachowavutia wazawa na wageni lukuki toka nje na ndani ya mipaka ya Same kushuhudia ikolojia ya wanyama hao. Akizindua rasmi tamasha hilo Waziri Mkuu (Mst.) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyelitumikia Taifa kwa kipindi cha Awamu ya Nne kati ya mwaka 1990 hadi 1994 Mhe. John Malecela alisema kuwa matamasha haya ni kichocheo kikubwa cha utalii na hifadhi pia zina nafasi kubwa ya kuibua mazao mapya ya utalii yatakayochagiza kuongeza idadi ya watalii kutembelea hii kwa kuwa na vionyo tofauti. Aidha, Mhe. Malecela aliongeza kuwa utalii wetu uanze na sisi watanzania wenyewe ndani ya vivutio vyetu na hii ni kutokana na gharama nafuu zilizowekwa pamoja na uwezo mkubwa wa kufikia maeneo hayo kwa wepesi tofauti na wale wanaotoka maeneo ya mbali. Naye, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. John Mabula alieleza kuwa idadi ya watalii katika Hifadhi ya Taifa Mkomazi imeongeza kwa kiasi kikubwa kutoka 7800 kwa mwaka na kufikia 11000 kwa mwaka 2022 hadi 2026. Kadhalika alieleza kuwa uwepo wa vivutio na ongezeko la wageni ni fursa kwa wazawa kuweza kujiinua kibiashara na kuongeza kipato katika kaya zao. Kwa, upande wake Mkuu Wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni alieleza kuwa Hifadhi ya Taifa Mkomazi iwape fursa vijana wa bodaboda kwa kutoa elimu ya kuongoza wageni ili wanapowapokea watalii waweze kuwakaribisha na kuwapa miongozo ya awali itakayochangia pato katika majukumu yao. Hifadhi ya Taifa Mkomazi imekuwa moja ya kivutio pendwa katika tamasha hili kwa kuwakutanisha wageni mbalimbali kutoka nje na ndani ya wilaya ya Same kutembelea wanyamapori adimu ikiwemo faru weusi, mbwa mwitu pamoja na uoto wa asili unaoipamba hifadhi hiyo.
Ahmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
1
0
0
106
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
CHAKWERA,TUME YA JAJI CHANDE WATETA MWAKILISHI wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola na Rais Mstaafu wa Malawi, Dk.Lazarus Chakwera, amekutana na kufanya mazungumzo na Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025. Ujumbe huo wa Jumuiya ya Madola ulikutana na Tume hiyo leo Aprili 11,2026 katika Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es Salaam. Rais Chakwela amesema ujumbe wake umekuja Tanzania lengo kuu likiwa ni kutafuta suluhisho la kutafuta Suluhu la Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu. “Ujumbe wangu umekuja Tanzania kwa lengo la kila mmoja kutafuta Suluhu ya yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi hilo ndilo muhimu kwa sasa mengine nitazungumza baada ya kuhitimisha ziara yangu ya Tanzania,” amesema Chakwera. Akizungumzia ziara hiyo, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Othuman Chande, alisema mazungumzo yao yalijikita zaidi kueleza shughuli za Tume hiyo na hadidu za rejea za Tume huku akiwataka waandishi kusubiri taarifa za mjumbe huyo baada ya kukamilisha ziara yake nchini Tanzania. Mjumbe huyo jana alikutana na Msajili wa Vyama vya Siasa na viongozi wa vyama mbalimbali. Bado anaendelea na ziara yake ya kikazi ambayo anataraji kuhitimisha Aprili 16,2026 baada ya kutembelea Zanzibar na Dodoma.
Ahmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
1
0
6
996
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA CHUO KIKUU CHA NASARAWA CHA NIGERIA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan,akishiriki hafla ya kutunukiwa shahada ya heshima na Chuo Kikuu cha Nasarawa nchini Nigeria kupitia njia ya mtandao. Tukio hilo linafanyika leo Jumamosi Aprili 11, 2026 katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Ahmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet media
Filipino
0
0
0
145
Ahmad Issa Michuzi
Ahmad Issa Michuzi@MichuziJr·
Serikali yakutana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola. Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukingozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi, imekutana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na Rais wa zamani wa Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera, na kujadiliana kuhusu namna Tanzania ilivyojidhatiti katika kudumisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania. Kikao hicho kilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) siku ya Alhamisi Aprili 9, 2026 mchana baada ya Mheshimiwa Chakwera kumtembelea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahamoud Thabit Kombo, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa ziara ya Mjumbe huyo Maalum nchini Tanzania. Katika kikao hicho, Mhe. Profesa Kabudi alimueleza kwa kina Mjumbe huyo Maalum, kuhusu hatua mbalimbali zinazoendelea kuchululiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuimarisha demokrasia nchini huku ikiweka msisitizo katika kulinda na kuheshimu utu wa Mtanzania, kuzingatia haki na uwajibikaji, amani na utulivu pamoja na kudumisha umoja wa kitaifa. “Tumekutana na Mheshimiwa Chakwera na tumemueleza mambo mengi kuhusu Tanzania na historia ya nchi hii tangu ipate uhuru mwaka 1961, hali ya siasa na demokrasia nchni, na hatua ambazo serikali inaendelea kuchukua ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa tulivu na kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi jumuishi na kujiletea maendeleo”, ameeleza Waziri Kabudi. Waziri kabudi ameeleza kuwa kikao hicho kimekuwa kizuri na chenye mafanikio kutokana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kupata ufafanuzi wa kutosha juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini hususani katika kudumisha amani, umoja wa kitaifa na ustawi wa Watanzania. Mbali na kukutana na ujumbe wa Serikali, Mheshimiwa Chakwera anatarajiwa kukutana na wadau mbalimbali ambapo jana Aprili 10, 2026 alikutana na Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. Jaji Mstaafu Francis Mutungi pamoja na vyama vya siasa vya ACT–Wazalendo, Chama cha National League for Democracy (NLD), United Democratic Party (UDP), Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Chama cha NCCR Mageuzi, Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Alliance for African Farmers Party (AAFP) na Chama cha ADA-TADEA. Vyama vingine ni pamoja na Democratic Party (DP), Tanzania Labour Party (TLP), Union for Multiparty Democracy (UMD), United People’s Democratic Party (UPDP), Chama cha Kijamii (CCK), Demokrasia Makini, Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Katika ziara yake hii, Mheshimiwa Chakwera anatarajia pia kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa matukio yaliyotokea Oktoba 29, 2025 na baada ya Uchaguzi Mkuu, Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Othman Chande, Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jaji Joseph Warioba, Jumuiya zisizo za Kiserikali, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Mhe. Jaji George Joseph Kazi, Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jaji George Mcheche Masaju, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro. Aidha, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, atakutana pia na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pamoja na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ahmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet mediaAhmad Issa Michuzi tweet media
Indonesia
0
0
3
230