KWAHERI UJAMBAZINI....!
Basi siku hiyo ya Ijumaa ya 20 September 2024 ndiyo siku niliyotolewa ujambazini na kupelekwa upande maalum (special wing) wanakoishi mahabusu ambao ni watoto chini ya umri wa miaka 18 ,mahabusu na Wafungwa wengine.
Huko special wing tupo jumla ya wafungwa na mabahusu kama 67. Kati ya hao, mahabusu watoto ni kama 12 tu. Selo yangu namba mbili palikuwa na mahabusu 4 na wafungwa 3 jumla tulikuwa tunaishi watu 7.
Kwanini wanaita special wing? Ni swali kila mtu anajiuliza ndani ya gereza na nje ya gereza lakini hakuna mwenye majibu kamili. Kwa sababu siku hizi hata Ujambazini kuna TV zenye ving'amuzi vya DSTV na AZAM kila Jengo.
Ujambazini kula chakula cha gerezani (ugali maharage umejitakia tu) sababu watu wa Ujambazini wanaruhusiwa kuweka order ya chakula cha canteen.
Ujambazini maji ya kuoga ni uhakika wakati wote. Ujambazini pia wanaishi mahabusu wazungu na mahabusu wa mataifa mbalimbali kama Nigeria, Ethiopia, na Uganda.
Special Wing na ujambazini tofauti kubwa ya haraka ni idadi ya watu wanaoishi Jela hizo, kwa mfano selo zote 10 za ujambazini wanalala watu idadi ya wanaokadiriwa ni 600 wakati Selo 5 za Special wing zinakadiriwa kuwa na watu 60
Wakati ujambazini kuna selo inabeba watu 200 kwa pamoja, special wing selo kubwa ilikuwa ina watu 17 na inabeba hadi watu 23 tu. Selo ndogo kama niliyokuwa nalala mimi kule special wing inabeba watu 7 hadi 11.
Kuhusu nani anatakiwa kuishi ujambazini na nani anatakiwa kuishi special wing ni swali hakuna mwenye majibu kwa kuwa vigezo vya nani awa wapi havipo wazi sana.
Ujambazini kuna wazungu kama Robert Maitland rafiki yangu yeye ana miaka 14 Ujambazini, Segerea na cha ajabu analalamika yupo Jela miaka 10 bila kifungo wala hakuna kesi inayomkabili wala hajui atatoka lini.
Duh! inatisha eeeh.. kua uyaone ndiyo hii sasa, nitakupa hii stori siku nyingine kwa kirefu zaidi. Ujambazini wameshawahi kuishi watu maarufu na matajiri kwa muda mrefu na maisha yakaenda sawa tu.
Ndiyo sababu baadhi ya huduma kama za TV na ving'amuzi kuwepo ujambazini, ni baada ya mahabusu na wafungwa wakishua kupelekwa kule na kujinunulia mahitaji hayo au kuboresha sehemu zao za kuishi kama vile tiles vyooni na kadhalika.
Basi shangwe. Upendo na heshima kutoka kwa mahabusu wa ujambazini ulifanya niondolewe ujambazini na kupelekwa kwenda kuishi special wing ndani ya selo namba 2.
Washikaji wa Ujambazini wakawa wananifuata bado kuja kunipa hadithi za kesi zao na mambo mablimbali ambayo walikuwa wanahisi ningeweza kuwasaidia
Hata hivyo baadae gereza likaweka ulinzi mkali wa askari zaidi ya watatu katika geti la kuingia special wing ili watu wa ujambazini wasikutane na mimi na mimi nilipigwa mkwara hakuna kutoka nje ya geti la special wing kwenda ujambazini bila ruhusa ya askari Magereza.
Nilikuwa nikitoka special wing kwenda popote lazima niwe chini ya escort ya Askari au nyapara, yote kunizuia kukutana na watu wangu wa ujambazini
SELO NAMBA 2, SPECIAL WING
Kwa historia naambiwa alikuwa anaishi Mzee Rugemarila hata umaridadi wa kuweka wavu wa kuzuia mbu (mosquito net) na maboresho ya tiles choo cha selo namba 2 ni jitihada za Mzee Rugemarila kwa fedha zake binafsi.
Ukienda selo namba nne special wing utaambiwa alikuwa anaishi Habinder Seth na Selo namba tano ni maarufu kama selo ya Freeman Mbowe.
Selo namba mbili ndani tulikuwa na watu saba. Wanne wafungwa (Chi, Lee, Aboubakar na Sam na Watatu ni mahabusu Mimi, Reu na Kimaro, familia hii ya selo namba 2 nimeishi nayo kwa muda mfupi lakini nitaikumbuka daima kwa maisha yale ya furaha, upendo na faraja.
Chi na Lee ni wafungwa tena manyapara lakini ni raia wa china. Lee anaongea kingereza na kiswahili kwa taabu sana, ni mtu mzima anajua mambo mengi sana na kila muda selo tulikuwa tunamskiliza kuhusu stori zake na masomo mbalimbali kuhusu,maisha,biashara na habari za fursa Duniani.huyu ni rafiki ambaye namsubiri kwa hamu nje akimaliza kifungo chake 2027
Wakati Chi ni mchina pia lakini kwa sasa anaongea kiswahili kama mndengereko wa Chumbi au Mzaramo wa Samvu la Chole au Homboza. Kwa mara ya kwanza nilikutana na Chi nilipopelekwa gereza la Keko kwa wiki 3 mwaka 2014 wakati nilkiwa na kesi Kisutu ambayo hata hivyo kesi hiyo ilikuja kufutwa baadae
Mimi na Chi tulikuwa tunaishi wote special wing, Gereza la Keko, wakati huo alikuwa hajui Kiswahili kabisa. Miaka 10 baadae tumekutana tena Gereza la Segerea. Safari hii yeye ndiye alinikumbuka na kuniambia tulikuwa wote Keko.
Chi anasema hakunikumbuka kwa Jina wala sura yangu, anasema amenikumba kwa stori ndani ya gereza. Mtu anayeweza kukusanya kiringi cha wafungwa na mahabusu gerezani akaanza kupiga nao stori kama anafahamiana nao au kuishi nao miaka 20 iliyopita.
Hadi watu ndani ya Jela wanasahau kwenda kula sababu ya stori, akawaza ashawahi kuonana na mtu kama mimi Keko kisha akaniuliza kama ndiye mimi, nikamjibu ndiyo nilikuwa ni mimi na washtakiwa wenzangu Sabula na Mramba lakini mimi ndiyo nilikuwa mtengeneza genge la hadithi na stori maarufu pale special wing ya Keko 2014.
Ndani ya Selo namba 2, special wing sikuwahi kuwa na huzuni, majuto au upweke.Tuliishi kwa amani na furaha sana kama ndugu wa damu.
Ingekuwa inaruhusiwa kisheria kurudi gerezani basi ningeweka ratiba angalau kwa mwaka niende mwezi mmoja au miwili niishi na wale watu wangu wa nguvu. Mungu wetu awatunze sana.
10 Years Ago
Ukipata Nafasi ya Kumtia mtu moyo fanya hivyo ungali hai....ukipata Nafasi ya kumshukuru Mtu ama Kumu appreciate mtu fanya hivyo hujui nani atatangulia...utatamani kuandika akiwa ameondoka then kwake haina maana sana inawezekana ungemwambia akiwa hai ungemtia moyo.
Maeneo muhimu ya Kibajeti.
1. Matumizi Ya Internet Katika ku download magazeti
2. Gharama za fedha Kwa ajili ya kuimarisha Mahusiano na Makapuni ya Uchapaji magazeti
3. Tozo mpya za Kuwasomea watu magazeti ili yanunuliwe
4. Bajeti ya kuajiri Graduates Political Analysts.
Enzi hizo zamani mkorofi mkorofi marafiki zake Baba walikuwa Wananiita "Kijana wa Sasali" hawakutaka kabisa kujihusianiasha na Mimi Ila siku hz wananiita "Kijana Wetu"
#Andika Jina Lako Vizuri...