
BENKI YA EQUITY TANZANIA YAZINDUA TAWI JIPYA LA UBUNGO LILILOPO EAST AFRICAN COMMERCIAL LOGISTICS CENTRE (EACLC) JIJINI DAR ES SALAAM.
Benki ya Equity Tanzania imezindua rasmi tawi jipya la Ubungo, lililopo ndani ya EACLC Mall (East African Commercial Logistics Centre),Ghorofa la Kwanza, jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huu ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo wa kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja na kuongeza urahisi wa kupata huduma kwa wakazi wa eneo la Ubungo na maeneo jirani.Tawi hili jipya linatoa huduma kamili za kibenki, ikiwemo kufungua akaunti, kutoa mikopo, kuweka na kutoa fedha, huduma za fedha za kimataifa (money transfer), huduma za biashara, na usaidizi kwa wateja wa benki hiyo.
Kwa kufunguliwa kwa tawi hili, Equity Tanzania inaimarisha mtandao wake wa matawi nchini, unaoendelea kukua kwa lengo la kuwafikia watanzania wengi zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania, Bi. Isabela Maganga, aliyezindua rasmi tawi hilo, alisema kuwa uzinduzi wa tawi la Ubungo ambalo ni tawi la kibiashara ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa benki hiyo kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kifedha karibu na maeneo wanayoishi na kwenye maswala amziam ya kibiashara biashara.
Tunaendelea kuwekeza katika miundombinu ya matawi na teknolojia ili kuhakikisha huduma zetu zinawafikia Watanzania wengi zaidi, hasa wale walio kwenye maeneo yenye shughuli nyingi za kiuchumi.
Ubungo ni kitovu muhimu cha biashara na usafiri, hivyo tawi hili litasaidia kuongeza kasi ya shughuli za kifedha kwa wafanyabiashara na wakazi wote wa eneo hili," alisema Bi. Maganga.
Tawi hili linajumuishwa katika jumla ya matawi 19 ya benki yaliyopo nchini, ambayo yanaendelea kutoa huduma kwa wateja katika mikoa mbalimbali. @TzEquityBank




Filipino







































