Hilda Newton@HildaNewton21
‼️NDULI IDD AMIN MAMA AMESHIKWA PABAYA‼️
Tangu Nduli Idd Amin Mama auwe kwa risasi Watanganyika wenzetu zaidi ya elfu kumi Oktoba 29, 2025 anahangaika sana kutafuta namna ya kujisafisha huko kwa wale aliowaita “WHO ARE YOU”
Awali mara baada ya Oktoba 29, walipoona Bunge la Ulaya limeazimia kuiwekea Tanzania vikwazo ikiwemo kuikatia Tanzania misaada yote, na kule Marekani nako Hali ikawa ivo ivo, Nduli Idd Amin Mama alimtumia Lazaro Nyalandu wakatafuta makampuni kibao huko Ulaya kwa ajili ya kumsaidia kufanya Lobbying kwa lengo la kumsafisha huko kwenye International Community ambapo alitumia mabilioni ya pesa na bado mpango wao ukafeli.
Baada ya kuona mpango wake wa kwanza umefeli, akaja na mpango wa pili akamtuma Jakaya Kikwete, Waziri wa Mambo ya Njee Mahmoud Kombo, Profesa Kabudi na Lazaro Nyalandu wakazunguka Dunia nzima kujaribu kusafisha mikono ya Nduli iliyojaa damu za Watanganyika zaidi ya elfu kumi aliowauwa kwa risasi lakin hata huo mpango nao ukafa kifo cha mende.
Baada ya Mzee Kikwete na wenzake kushindwa kumsafisha huko kwa “Who are you” ndo akaja mpango wake wa tatu ambao ni Report ya Mchongo ya Tume ya Jaji Chande ambayo aliandikiwa na Kabudi, sasa pale ndo ikawa kama amejipaka damu mwili mzima yani ni kama mtu mzima kujiharishia mbele za watu.
Hata hiyo Report ya mchongo ya Jaji Chande na yenyewe haikutosha kumsafisha ndo mambo yakazidi kuwa mabaya, ndipo akaamua kumtumia Bashite kumleta Drogba na Reo Ferdinand lakin kwa mara nyingine tena hata huo mpango ukafeli na ukazidi kumexpose hata ambao walikuwa hawajui kilichotokea Oktoba 29, wakajua kupitia Reo Ferdinand.
Baada ya kuona kila njia alizojaribu kuzitumia ili kujisafisha huko kwenye International Community zimefeli ni kama amechanganyikiwa, sasa ameamua kukimbilia kwa wapopo (Wanaigeria) kaokota Mwandishi wa Blog kama Habibu Mchange kampa mamilioni ya pesa ili amsaidie kutengeneza Documentary ya kumsafisha dhidi ya Documentary ya BBC, CNN, Al jazeera na DW.
Huyu Blogger wa Nigeria aliyempa hiyo kazi anaitwa David Hundeyin (Huyu kwenye hii picha niliyopost) David ni mtu ambae Watawala wa Africa ambao wanateka na kuuwa wananchi wao, huwa wanamtumia kuwatengenezea Documentary za kuwasafisha hata Yoweri Mseveni baada ya kuteka, kuumiza na kuuwa Waganda waliokuwa wanampinga alimtumia huyu huyu David kujisafisha.
Kwenye hiyo Documentary ya kumsafisha Nduli Idd Amin Mama, kwa hapa Tanzania David Blogger ameshirikiana na Mwandishi anaitwa Deodatus Balile, kwa msiomfahamu Balile ni mtu ambae anatumiwa na mfumo kwa miaka mingi sasa na yeye ndo alitumika kutoa Report za uwongo kuhusu Wamaasai wa Ngorongoro ili ionekane uamuzi wa Serikali kuwafukuza Wamaasai Ngorongoro ulikuwa sahihi.
Kwenye hiyo Documentary ambayo Blogger David anatarajia kuiachia hivi karibuni, amewashambulia Wananchi wa Tanganyika waliondamana, ameshambulia Viongozi wa CHADEMA na Wanaharakati kwa kutumia kauli ya Nduli Idd Amin Mama kwamba watu walilipwa ili Waandamane na katika ushahidi wake kaokota ile Tweet ya Madenge ambayo aliwashambulia Ford Foundation japo Madenge mwenyewe alifuta hiyo tweet baada ya kugundua kwamba katoa boko.
Kwenye hiyo Documentary blogger David anapiga propaganda kwamba Idadi ya watu waliouwawa ambayo tunaitaja yani Watanganyika zaidi ya elfu kumi ni ya uwongo na kwamba hakuna makaburi ya halaiki
Na katika propaganda zake anasema kwamba kilichotokea Oktoba 29, 20205 ni mkakati wa Mabeberu kuivuruga Tanzania, kwa ambao huwa mnamfuatilia Siasa za Tanzania hii ni kauli ya Mwigulu na amekuwa akiirudia mara kwa mara.
Maudhui yaliyopo kwenye hiyo Documentary ya Blogger David hayana tofauti na report ya mchongo ya Jaji Chande hii ni kwasababu Mwandishi wa script zote 2 ni Kabudi so hata kwenye hii keshafeli.
Jambo moja ambalo Nduli Idd Amin Mama na vibaraka wake wanapaswa kujua ni kwamba hakuna Documentary, Report wala vitisho ambavyo vinaweza kumsaidia kumsafisha kwenye issue ya Mauaji ya Watanganyika zaidi ya elfu kumi aliyofanya Oktoba 29, 2025.