CHAUMMA Tanzania

938 posts

CHAUMMA Tanzania banner
CHAUMMA Tanzania

CHAUMMA Tanzania

@ChaummaT

Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) advocating for democracy, the rule of law, accountability, and respect for human rights for the advancement of Tanzania.

Dar es Salaam, Tanzania Katılım Ağustos 2020
7 Takip Edilen1.3K Takipçiler
CHAUMMA Tanzania retweetledi
Jambo TV
Jambo TV@Jambotv_·
Karibu kuungana nasi kwenye kipindi cha 'Jambo Asubuhi' kinachorushwa mubashara na Jambo TV kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 03:00 hadi 05:00 Asubuhi, Alhamisi hii ya Machi 26.2026, tutakuwa na mahojiano maalum na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA @ChaummaT) Tanzania Bara, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Kuandika Katiba Mpya ya chama hicho Benson Kigaila.
Jambo TV tweet media
Indonesia
0
1
7
1.1K
CHAUMMA Tanzania retweetledi
Jambo TV
Jambo TV@Jambotv_·
VIDEO: Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA @ChaummaT) kimeanza rasmi mchakato wa kuandika upya Katiba ya chama hicho, hatua inayotajwa kuchochea chama hicho kwenda sambamba na ukuaji wake huku dhamira ikiwa ni kuwa chama kikubwa zaidi kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Katibu Mkuu wa CHAUMMA Salum Mwalimu leo, Jumanne Machi 24.2026, amezindua rasmi Kamati mahsusi iliyopewa jukumu la kuandika Katiba Mpya ya chama hicho, kamati yenye Wajumbe 11 ikiongozwa na Mwenyekiti wake Benson Kigaila ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kamati hiyo, iliyofanyika kwenye ukumbi wa makao makuu wa CHAUMMA, Kinondoni, Jijini Dar es Salaam, Mwalimu amesema mchakato huo unapaswa kukamilika katika kipindi cha miezi sita (6) ikiwa ni utekelezaji wa vikao halali vya chama hicho kuanzia Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.
Indonesia
24
4
30
16.9K
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
Picha kutoka Kikao cha CHAUMMA na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Parfait Onanga-Anyanga. Katibu Mkuu, Mhe Salum Mwalim, akiambatana na Katibu wa Sekretarieti, Ndugu, Edward Kinabo, waliwakilisha Chama. Chaumma inaamini kwamba "mazungumzo" ndiyo njia sahihi zaidi ya kuliponya na kulikwamua Taifa kutoka kwenye mtanziko wa kisiasa wa tangu na baada ya uchaguzi Mkuu wa 2025 na kuweka misingi madhubuti ya Haki na Demokrasia ya kweli kupitia kuandikwa kwa katiba mpya na kuimarishwa kwa mifumo huru na ya kuaminika ya uchaguzi.
CHAUMMA Tanzania tweet mediaCHAUMMA Tanzania tweet media
Filipino
17
6
37
5.9K
CHAUMMA Tanzania retweetledi
Jambo TV
Jambo TV@Jambotv_·
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimeeleza kuwa malengo yake ya kimkakati yaliyokipeleka katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 yametimia kwa kiasi kikubwa, huku kikijipanga kutumia uwakilishi wake mpya bungeni kusukuma ajenda ya mageuzi ya kikatiba na kisheria nchini. Kulingana na taarifa iliyotolewa Machi 08, 2026 na Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Salum Mwalim, kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichoketi Machi 4, 2026, jijini Dar es Salaam, kimefanya tathmini ya kina na kubainisha kuwa licha ya dosari zilizojitokeza katika mchakato wa uchaguzi, chama hicho kimefanikiwa kupata wabunge na madiwani watakaokuwa sauti ya wananchi. “Kimsingi, malengo yote yaliyoipeleka CHAUMMA katika uchaguzi mkuu wa 2025, kama yalivyotajwa hapo juu, yametimia kwa kadri ilivyowezekana licha ya dosari zote zilizojitokeza katika uchaguzi. CHAUMMA imeweza kupata uwakilishi bungeni na kwenye baadhi ya halmashauri nchini, ikiwemo kupata nafasi adhimu za kuongoza kamati ya bunge ya hesabu za serikali kuu (PAC), ukamishina wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa mwanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kinachoundwa na vyama vyenye uwakilishi bungeni. Mafanikio haya yameijengea CHAUMMA msingi mzuri wa kupigania zaidi haki, demokrasia na maslahi ya wananchi”, imeeleza taarifa hiyo. Kamati Kuu ya chama hicho imeeleza kuwa uzoefu wa uchaguzi wa 2025 umethibitisha kuwa tatizo la uchaguzi nchini si sheria pekee, bali ni kukosekana kwa dhamira ya kutii sheria kutoka kwa baadhi ya wasimamizi. CHAUMMA imelaani matukio ya vifo na uharibifu wa mali yaliyotokea Oktoba 29, 2025, na kutoa pole kwa familia zilizoguswa. “Kamati Kuu imesikitishwa na madhila ya maandamano ya Oktoba 29/2025 ambayo kimsingi hayakufanikiwa kuzuia uchaguzi, lakini yalisababisha ulemavu, vifo na uharibifu wa mali na miundombinu, na kutengeneza “mwanya mbaya” uliokiathiri chama chetu kwa kiwango kikubwa na kutoa mwanya kwa baadhi ya watu kuvuruga uchaguzi kwenye baadhi ya maeneo”, ameeleza. Ili kujiandaa na chaguzi zijazo na uimarishaji wa chama, Kamati Kuu imepitisha Mpango Mkakati wa miaka mitano (2025 -2030) wa Chama, unaotoa mwongozo wa kupigania mageuzi ya kikatiba na kisheria na namna ya kutekeleza shughuli zote za ujenzi na uimarishaji wa Chama, kwa lengo la kuhakikisha Chama kinashinda chaguzi ndogo, uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wa 2029 na uchaguzi mkuu wa 2030. Aidha, Kamati Kuu ya CHAUMMA imepitisha mchakato wa maboresho ya Katiba ya Chama na hatua zake zote, ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Mkutano Mkuu wa Chama wa 2025, na kwamba mchakato wote wa kuboresha katiba ya chama uchukue muda usiozidi miezi sita.
Jambo TV tweet media
Indonesia
17
3
72
8.4K
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
MSIMAMO WA CHAUMMA Maazimio ya Kamati Kuu: "Tutaanza na Mabadiliko Makubwa sana ya Katiba yetu ndani ya Chama" Mhe: Salum Mwalim Katibu Mkuu CHAUMMA
Indonesia
1
3
10
255
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
Yaliyotokea siku ya Uchaguzi mkuu tarehe 29 Octoba, 2025 yalikuwa mambo mabaya sana kwa taifa letu na yalisababisha maafa makubwa sana na hii ilikuwa mara ya pili kwa taifa letu kukumbwa na maafa ya Vifo na uharibifu katika uchaguzi Mkuu baada ya maafa kama hayo kutokea kwenye uchaguzi Mkuu wa Zanzibar mwaka 2001,natoa pole za dhati kwa watanzania wote waliokumbwa na maafa yale hasa kwa familia zilizopoteza wapendwa wao ,waliojeruhiwa na zile familia zilizosababishiwa umaskini kwa mali zao kuporwa na kuharibiwa. Tumeskitishwa matukio hayo; na kwa kuwa kuna Tume ya Rais iliyoundwa na inaendelea na uchunguzi ili kujua nini hasa kilifanyika ,sitapenda sana kujadili yaliyotokea siku hiyo na siku zilizofuata kwani tayari Chama chetu kimeshakutana na Tume hiyo na kuwasilisha maoni yake na hivyo tutaendelea kusubiri majibu/ripoti ya Tume kuhusu uchunguzi wake japo kwa tahadhari kuu. Pamoja na hujuma zote zilizofanyika, Chaumma inaamini kwamba "mazungumzo" ndiyo njia sahihi zaidi ya kuliponya Taifa kutoka kwenye mtanziko wa kisiasa wa tangu na baada ya uchaguzi mkuu wa 2025 na kuweka misingi madhubuti ya upatikanaji wa haki na demokrasia ya kweli nchini. Chama kipo tayari kwa "mazungumzo" kwa maslahi mapana ya Taifa na Tunaendelea kuwashauri wale wote wenye nia njema na taifa letu kuwa tayari kuzungumza kwani ndio mwelekeo sahihi wa kuliponya taifa letu.”Mh.Salum Mwalim
CHAUMMA Tanzania tweet media
Indonesia
23
4
19
5.1K
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
“Tatu,napenda kuwashukuru wadau wetu wote ambao waliweza kutuchangia gharama mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha kufanikish kampeni zetu tangu tulipoanza mpaka tulipomaliza kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Nne,nawapongeza sana wale wote ambao waliweza kushinda nafasi za Ubunge na Udiwani kwani tumeweza kuandika historia mpya ya Chama chetu kuwa na Wabunge na Madiwani kwa mara ya kwanza katika historia yake tangu kilipoasisiwa mwaka 2012. Nafahamu wapo ambao wanatubeza kwa mafanikio hayo wakidhani kuwa ni kidogo ila ukweli wanaujua kuwa mwaka 1994 walipata madiwani 42 wakati sisi tumepata Madiwani 54, walipata Wabunge 4 sisi tumepata Wabunge 3” Mh.Salum Mwalim
CHAUMMA Tanzania tweet media
Indonesia
5
2
6
1K
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
‘’Pili, napenda kuwashukuru sana wagombea wetu wote wa nafasi za Ubunge na Udiwani ambao walijitoa kwa hali na mali katika kipindi chote cha kampeni kwa kutumia rasilimali zao ili kuhakikisha kuwa Chama chetu kinapata ushindi.’’Mh.Salum Mwalim
CHAUMMA Tanzania tweet media
Filipino
0
2
9
704
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
Nawapongeza sana Wanawake wote kwa kujitokeza kwa wingi katika siku hii ambayo ni kumbukumbu yenu ya umuhimu na hakika mmeitendea haki na mmependeza sana kwa unadhifu wenu, hongereni kwa kuendelea kuwa wabunifu na hakika mnaendelea kuonyesha njia na kuwa mafano wa kuigwa.Kwa kuwa leo ndio siku yangu ya kwanza kujitokeza mbele ya wanachama na viongozi wenzangu tangu tulipomaliza kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, nitaomba kusema machache kuhusu kampeni zile na uchaguzi kwa ujumla. Mosi, nawashukunı sana viongozi wenzangu wa Chama pamoja na wanachama kwa kuniamini mimi na Makamu wangu kuwa tupeperushe bendera ya chama, aidha nawashukuru sana watanzania wote kwa kutupokea na kutuunga mkono kipindi chote cha kampeni na kutupigia kura siku ya uchaguzi Mkuu.
CHAUMMA Tanzania tweet media
Filipino
1
3
8
484
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
“Yaliyotokea Octoba 29 ,yalituumiza na kutuhuzunisha, ni mara ya pili taifa letu lilitumbukia kwenye machafuko ya uchaguzi mkuu baada ya maafanya mwaka 2001 kule Zanzibar . Tunatoa pole za dhati kwa watanzania wote waliopoteza wapendwa wao na walioharibiwa mali zao na tunasubiri ripoti ya Tume ya Uchunguzi kwa tahadhari kubwa”Mh.Salum Mwalim
CHAUMMA Tanzania tweet media
Indonesia
7
3
10
4.1K
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
“Waheshimiwa wenzangu hayo Ndio yalikuwa maadhimio ya Kamati Kuu , Wabunge wetu na Madiwani wetu hamna kibali cha kwenda kuungana na Serikali kazi yenu ni kwenda kupigania haki Za watanzani, hatutosita kukuchukulia hatua Za kinidhamu ukishindwa kupigania haki Za watanzania”Mh.Salum Mwalim Katibu Mkuu wa CHAUMMA
CHAUMMA Tanzania tweet media
Indonesia
0
2
8
1.7K
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
“Tunajivunia kuwa na Mwenyekiti wa Chama Ambae yupo tayari kupokea mawazo ya watu wengine mara nyingi anatuagiza kwa kusema nendeni kwa kujenga chama” Mh.Salum Mwalim
CHAUMMA Tanzania tweet mediaCHAUMMA Tanzania tweet mediaCHAUMMA Tanzania tweet mediaCHAUMMA Tanzania tweet media
Indonesia
4
4
16
2K
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
“Ndugu zangu mengi yamesemwa na mengi yataendelea kusemwa kwa sasa CHAUMMA ni tishio” Mh.Salum Mwalim
CHAUMMA Tanzania tweet media
Indonesia
31
6
24
4.1K
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
Leo hii tarehe 08/03/2026 Chaumma kupitia kitengo cha wanawake *Kiwacha* wakinaadhimisha siku ya wanawake Dunia katika viwanja vya UBUNGO PLAZA 📍
Indonesia
3
2
13
537
CHAUMMA Tanzania
CHAUMMA Tanzania@ChaummaT·
Mwenyekiti wa Chama Taifa Wakili Msomi Hashim Spunda Rungwe akiambatana na Viongozi wa Chama Taifa wakiingia Ukumbini tayari kutoa mwelekeo wa Chama. Leo tar 8 March 2026
Indonesia
4
3
12
1.3K