Daffy retweetledi
Daffy
1.3K posts

Daffy
@Daffy255
@LFC @realmadrid
Dar es Salaam, Tanzania Katılım Ağustos 2021
681 Takip Edilen1.4K Takipçiler
Daffy retweetledi
Daffy retweetledi
Daffy retweetledi

Daffy retweetledi

Kauli ya Samia Suluhu Hassan ya kutaja taasis kuwa ni aibu kama adhabu ni udhaifu mkubwa mbele ya uzito wa tatizo. Hasara ya mabilioni ya fedha za umma si kosa la kuoneana aibu ni kosa la kuwajibika kisheria.
Tazama tofauti ya mifumo, CANADA, CEO wa Air Canada ameingia kwenye shinikizo kubwa na kuondoka kazini baada ya kufanya mawasiliano ya umma kwa lugha ya Kiingereza pekee huku akisahau Kifaransa. Lugha zote mbili ni rasmi nchini Canada. Hilo lilionekana kukiuka misingi ya uongozi. Na sasa amejiuzulu. Sasa linganisha na Tanzania. Mabilioni yanapotea na utendaji mbaya unaendelea kuimarika lakini adhabu zinabaki kuwa aibu.
Hapa ndipo tatizo lilipo. Taasisi kama Public Procurement Regulatory Authority PPRA na Prevention and Combating of Corruption Bureau TAKUKURU hazikuundwa kutengeneza orodha ya wanaoaibika. Zipo kulinda fedha za umma kwa hatua uchunguzi kesi na adhabu.
Ukiharibu mali ya umma adhabu haiwezi kuwa jina lako kusomwa kwenye ripoti. Lazima iwe hatua inayoonekana.
Bila hivyo aibu inabaki mzaha na mfumo unaendelea kuzalisha uzembe ule ule.
Aibu kubwa ndio hii hapa sasa. Tanzania inaumizwa sana.
Indonesia
Daffy retweetledi
Daffy retweetledi

SAKATA LA WAMAASAI KUFUKUZWA NGORONGORO.
Disemba 23, 2024 Nduli Idd Amin Mama aliunda Tume 2 moja ilikuwa kwa ajili ya kuchunguza Utekelezaji kuhamisha Wamaasai kutoka Ngorongoro kwenda Msomera- Handeni Tanga.
Tume nyingine ilikuwa kwa ajili ya kuchunguza maswala ya ardhi ambayo yanalalamikiwa na Wakati wa eneo la Ngorongoro.
Sasa juzi kati Tume zote mbili zilikabidhi Report zao kwa Idd Amin Mama.
Leo tuanze na Report ya Tume ambayo ilikuwa inachunguza Uhamishwaji wa Wamaasai kutoka Ngorongoro kwenda Msomera Tanga.
Tume hii ilikuwa inaongozwa na Musa Iyombe ambae alikuwa Katibu mkuu TAMISEMI
Kwenye Report ambayo Tume yake imewasilisha.
Wamekiri kwamba katika zoezi la kuhamisha Wamaasai kutoka Ngorongoro kwenda Msomera Tanga kulikuwa na ukiukwaji mkubwa sana wa Haki za binadamu pamoja na udhalilishaji/Kutweza UTU wa Wamaasai.
Serikali ilitumia nguvu kubwa kushawishi Wamaasai kuhama badala kuwashirikisha ili wakubali kuhama kwa hiyari.
Katika zoezi la kuwahamisha Wamaasai Ngorongoro Serikali iliwanyima huduma zote za Kijamii lengo likiwa ni kuwakomoa ili walazimike kukubali kuachia ardhi yao na kwenda Msomera.
Serikali iliondoa fedha za kujenga madarasa vyoo na majengo chakavu kwa shule, hospitali, zahanati na vituo vya afya.
Hadi leo Wakazi wa Ngorongoro wamekatiwa huduma ya maji lakini kwenye Mahotel ambayo yapo ndani ya Ngorongoro wanaendelea kupata huduma ya maji kama kawaida.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliandika barua kwenda kwa wamiliki wa Mahotel ambayo yapo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kuwataka wawafukuze kazi Wamaasai wote wa Ngorongoro.
Wamaasai waliokuwa wameajiriwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro walihamishwa kihuni na kupelekwa taasisi zingine kama TAWA
Mchengerwa akiwa Waziri wa Tamisemi alifuta vijiji vyote vya Ngorongoro kisha Tume ya Uchaguzi ikaondoa vituo vyote vya kupigia kura Ngorongoro na kuwahamisha Wamaasai kwenye mfumo wa daftari la kupigia kura na kuwapeleka Msomera.
Tume imekiri kwamba baada ya mateso Wamaasai waliokubali kwenda Msomera walichoahidiwa na Serikali na walichokikuta huko ni vitu viwili tofauti.
Lakin wakati wa kuhama hakukuwa na tathimini ili kuwafidia wanaohama so watu wengi hawakulipwa fidia.
Awali waliambiwa ardhi ya Msomera haina watu lakin walipofika wakakutana na malalamiko kutoka kwa wenyeji ambao Serikali iliwapora ardhi na kuwapa Wamaasai bila kuwashirikisha wamiliki wa ardhi hiyo so kuna mgogoro mkubwa unaendelea kati ya wageni kutoka Ngorongoro na wakazi wa Msomera na kuna baadhi ya Wamaasai wamefunguliwa kesi ya uvamizi wa ardhi.
Tume inasema hadi inakabidhi Report yake, kule Msomera kuna nyumba zaidi ya 1500 zipo tupu hazina watu na mpaka sasa Serikali tayari imetumia zaidi ya Bilioni 100 kuhamisha Wamaasai Ngorongoro na zoezi lenyewe la uhamishaji limefeli so pesa zimepigwa.
Kibaya zaidi Tume walielezwa na Wamaasai kuhusu mifugo yao kupewa chumvi yenye sumu na serikali naona hiyo wameogopa kuisema wamemute wakati ni jambo limethibitisha na maabara kadhaa akiwemo Mkemia Mkuu wa Serikali, TBS, Maabara ya Mifugo na Chuo Kikuu cha Sokoine.
Pia haijasema kuhusu Serikali kuzuia ndege ya Medical Flying Services hii ni ndege ilikuwa ikifanya huduma ya chanjo na uokozi katika sehemu ambazo hazifikiki sababu ya kutokuwa na miundo mbinu Ngorongoro.
Mwaka 2022 swala la kufukuza Wamaasai Ngorongoro lilipoanza wakazuia hiyo ndege kuruka, mtu ambae alihusika kuzuia ndege hiyo ni Hamza Johari Mwanasheria Mkuu wa Serikali kipindi hicho akiwa TCAA.
Pamoja na madudu yote hayo ambayo Tume ya Iyombe imeyabainisha kwenye report yao bado inapendekeza kwamba zoezi la kuhamisha Wamaasai Ngorongoro liendelee.
Tume ya Iyombe haijasema Chochote kuhusu hatua gani zichukuliwe dhidi ya Viongozi wa Serikali ambao waliendesha zoezi hili wakiongozwa na Kassim Majawaliwa
Waliowaumiza na kuwabagua Wamaasai, waliowanyima Waamasai huduma zote za kijamii, walioiingiza Serikali hasara ya Mabilioni ya pesa kwa kujenga nyumba zaidi ya 1500 huko Msomera ambazo hadi leo ziko tupu?

Indonesia
Daffy retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_MGAWANYO_MALI_ZA_CHADEMA
Part 8
Anasimama Wakili Hekima Mwasipu kutoka upande wa waleta maombi.
Anasema kuhusu haki ya kusikilizwa tunaomba kusema kwamba respondents baada ya Jebra kujiondoa hawakuambiwa chochote.
Descretion tunasema inapaswa kuzingatia haki na Katiba ya nchi sasa alichokifanya Jaji Mwanga ni kuendelea na kesi kinyume na Matakwa ya kuexercise judiciously hiyo descretion.
Anasimama Dr. Nshala Ruge anasema sisi tulisema cause of action ilianza lini na sisi tulisema walianza 2016
Para zote walizosema ukianza na Para ya 7 wanasema wamemaliza kujenga jengo la Chama hawajasema kama kulikuwa na ugomvi.
Wanasema hadi tarehe fulani chama kilikuwa na mali hizi, sasa mgogoro ni nini?
Hakuna mahali walisema walikuwa na migogoro au mgogoro wao ulianza lini? Hawajasema chochote.
Dr. Nshala nina miaka 30 nafanya haya masuala ya sheria ndio nimesikia hizi paragraph ni contexual tu. Sasa hakuna kitu kama hicho.
Hoja yetu ni hizi para zao zinazungumzia mambo ya Kikatiba.
Pia nahisi wenzetu hawasikilizi nilisema S. 22(1) ya Political Party Act Msajili anajukumu la kuhakikisha sheria inatekelezwa. Sect. 4 the function and implemention of this Act amepewa Msajili wa Vyama vya siasa.
Dr. Nshala yuko moto sana.
Anaendelea kuwa huwezi kutoa injuction dhidi ya Chama cha siasa kesi ya Lyatonga Mrema imesema hivyo.
Wakati mwingine unaweza kupata ugonjwa wa moyo ukiwa unafanya hizi kazi.
Jaji sasa Dr. Nshala nikushauri jambo
Dr. Nshala samahani Jaji naomba niache.
Jaji sasa sikiliza nataka kukushauri mimi.
Dr.Nshala sawa Nishauri hakuna shida.
Jaji nataka usubmit hapa Mahakamani ukiwa umerelax ili usipate ugonjwa wa moyo.
Dr. Nshala sawa Ahsante nimepokea.
Watu wanacheka.😂
Dr. Nshala anaendelea
Huyu Marijan amesema conditions za Attilio vs Mbowe hazijawa met hata moja kabisa. Hata ku attach ile petition hawajafanya hivyo. Naweza kutumia maneno mazito lakini naomba niseme hili ni jambo la hovyo sana.
Chama cha siasa kinazuiwa kufanya siasa mwaka wa uchaguzi. Naomba Mahakama ya Rufani ilirudie tena uamuzi wake kuhusu Chama cha siasa hakipaswi kuzuiwa.
Naomba pia Mahakama ya Rufani iseme Jambo fulani juu ya huyu Jaji Mwanga maana mambo aliyofanya ni ya hovyo sana. Naomba mtufungulie hata leo tu.
Jaji sasa tunawashukuru sana.
Tunaenda kutafakari na tutawaambieni ni lini tutawapatieni huo uamuzi. Mtajulishwa. Tunawashukuru sana.
Tunaahirisha hadi kikao kijacho.
Mahakama imehairisha mpaka hapo tutakapoitwa tena kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa Majaji.
Naomba repost yako.
Indonesia
Daffy retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_MGAWANYO_MALI_ZA_CHADEMA
Part 7
Kesi ya Haruni David vs Kangi Lugola Civil appeal No. 36 inasema headings and marginal notes sio sehemu ya sheria.
Sasa temporary injuction inayoongelewa kwenye sub rule 3 ya O.XXXVII hapa tunachokisema trial judge alikuwa sahihi kuitoa na hakuitoa chini ya sub rule 3.
Jaji sasa ulitupeleka kwenye marginal notes ni kama umetuacha tena hiyo sub rule 3 order zinazoweza kutolewa hapo ni zipi?
Anasimama Wakili Mulabuzi anasema s. 105 ya CPC inaipa mamlaka Mahakama kuu inherent power kutoa order hata nje ya sheria
Jaji kwahiyo unataka na sisi tutumie hiyo Section 105 ya CPC?
Wakili ndio muitumie.
Anaendelea hapa Wakili kuwa hakuna single paragraph inayounganisha value ya subject matter lakini hata kama ziko separate ukiangalia aggregate yake inazidi mamlaka za Mahakama za Chini kwahiyo ilikuwa ni lazima ipelekwe Mahakama Kuu.
Jambo la Mwisho la time limit kuhusu cause of action sisi tulisema ilianzia mwaka 2019 hadi 2024 miaka 6 haijazidi.
Nilitaka kurudia hayo mambo mawili na kwa ujumla upande wa Applicant kulikuwa hakuna serious irregularity kuonesha proceedings zilikuwa na shida.
Kama kuna mapungufu basi tunaamini ni madogo sana na tunaomba mwenendo urudishwe mapema mahakama kuu ili tukaendelee na pande zote zipate haki yake. Tunaishia hapo.
Wazee wanaandika hapa, unasubiri maelekezo yao.
Jaji sasa lile suala la kwamba jambo hili lilipaswa kuanzia kwa Msajili wa Vyama vya siasa mnasemaje?
Wakili ukiangalia ukurasa wa 5 kuna juhudi zilifanyika na hazikuzaa matunda na kwenda kwa msajili ni kama unataka kufuta chama sisi wateja wetu walikuwa hawana nia ya kufuta Chama.
Msajili wa Chama asingekuwa na mamlaka ya kutoa nafuu zilizoombwa hapa.
Lakini pia maombi ya kwamba hii kesi ni constitutional au judicial review huko tusingetaka kwenda.
Jaji unasemaje Mpale Mpoki.
Tuna mambo kadhaaa
1. Angalau wamekubali kuwa kesi yao ilikuwa under CPC na wanajua O.VII inasemaje nini kiwepo kwenye proveedings. Mahakama hii ya rufani imesaidiwa kwamba value hawajaweka, hawajesema cause of action imerise lini?
2. Wame admit pia hakuweka value ya subject matter na kuhusu payment nayo hawajasema na Mawakili wanapaswa kujua sheria, akija mteja unapaswa kumwambia gharama za kufungua kesi sasa wao walijiendea.
3. Wameadmit kuhusu hii sio Constitutional case sasa ukisoma hii kesi kila mahali utaona inaitwa ni Public Interest Litigation.
4. Wanaadmit kuwa hii case haijaletwa chini ya Sheria yoyote na reliefs walizoomba ndio zinaelezea aina ya kesi na relief zao ni kesi ya Kikatiba.
Ukiangalia wanachoomba ni kuwalazimisha watu fulani wafanye jambo fulani na hii kwa uelewa wangu ni order ya Mandamus. Isingeweza kuwa Normal Civil Case.
5. Jambo lingine wanasema wako exempted. Ili plaimtif awe exempted under law of limitation anapaswa kusema tuko nje ya muda lakini tuwe exempted ni kwa mujibu O. VII r. 6 sasa hizo grounds za exemption zimetolewa kwa mujibu wa sheria.
Category za exemption lazima ziwe pleaded na useme kwanini hukufungua kesi ndani ya muda mfano nilikuwa naumwa, nilikuwa nimesafiri. Hawajasema lolote kuhusu hayo sasa.
Naomba nimkaribishe Hekima Mwasipu
Part 8 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
Indonesia
Daffy retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_MGAWANYO_MALI_ZA_CHADEMA
Part 6
Anaendelea Wakili wa Said Issa na wenzake
Suala la amri ya zuio inamuhusu nani?
Record yenyewe ya Revision inajieleza nani inamuhusu. Page 153 imewaeleza wanaouzuiwa. Wametajwa bodi ya wadhamini na katibu mkuuu.
O.XXXVII ya CPC inasema kuwa order ya bodi ya wadhamini itawahusu wahusika pekeee. Sasa ukiitaja bodi ya wadhamini maana yake ni Chama chote.
Jaji kwani order inaposema na waliopo chini yake Katibu Mkuu ni chini hadi wapi?
Jaji mwingine anasema walisema kuwa servants na wengine wote wanaofanya kwa niaba sasa je kuna yeyote ambae angeweza kufanya shughuli nyingine?
Wakili naomba niendeleee
Jaji kabla hujaendelea sasa tusaidie mahusiano ya madai ya mali na kufanya shughuli za Chama?
Wakili anajibu waheshimiwa madai hapa sio mgawanyo wa mali lakini kweli mgawanyo wa Mali ni madai ila kitu cha msingi ni kifungu cha 6 cha Political Party Act.
Jaji hebu kisome halafu tuambie kinasemaje na maana yake.
Anakisoma hapa.
Anasema sasa matendo ya viongozi wa Chama yaliwakera wananchi wa Zanzibar.
Jaji wananchi wa wapi?
Wakili Mhe. Jaji namaanisha wakazi wa zanzibar.
Jaji una hakika wakazi wa zanzibar hawakufurahia
Wakili ni wanachama tu.
Jaji unajua kanuni za kutoa interim order hilo zuio?
Jaji mwingine na utuambie nani angepata athari zaidi kwa mfano nyie mmgeshindwa hiyo petition yenu kati yenu na respondents nani angeathirika zaidi?
Wakili sasa waheshimiwa majaji naona kama mnazungumzia kesi ya Attilio vs Mbowe
Bila kuzuia wasitumie hizi property basi wote wasingetumia na zingekuwa salama kwa wote.
Pia kufanya political activities lilikuwa ni zuio la muda tu, zingeachwa zingeendelea kutengeneza friction baina ya members.
Jaji sasa tuambie irreperable loss ni ipi?
Wakili tulisema sera za Chama zinaenda kuwa damaged.
Jaji tena anamuuliza Marijan kwahiyo unasemaje kuhusu kilichoombwa kwenye main case ni kama kilishatolewa kwenye ombi la zuio?
Wakili ni kama vinafanana lakini vinatofautiana.
Jaji huoni amri ya kwenye maombi madogo inaweza kuwafanya waleta maombi wakaona wameshamaliza kesi yao wakaanza kuchelewesha kesi ya msingi au wakaona haina msingi?
Wakili washemiwa nafikiri hakuna mwenye nia ya kupoteza muda kwenye shauri la msingi hivi.
Majaji wanatabasamu na kucheka ki kituristi kidogo halafu wanaandika kwa umakini mkubwa.
Jaji sasa mlisema hii kesi ni ya aina gani?
Wakili sisi tunasema haki zilikuwa infringed
Jaji hizo haki zipo wapi si Article 30?
Wakili ndio ni Article 30.
Jaji sasa kama ni Article 30 ya Katiba ndio zimevunjwa. Swali letu hii ni kesi gani? Ya Kikatiba au sio ya Kikatiba.
Jaji mwingine anasema sasa hapa una address jambo gani hebu tuambie maana kila kitu kina utaratibu wake sasa tueleze.
Anasimama Wakili Kiharuzi kuwa applicants hawahangaiki na haki za kikatiba.
Ila wanachosema ni maombi ambayo yanawaomba ku comply na matakwa ya kisheria hii ni CIVIL Case. Inawalazimisha
Jaji hebu subiri kwanza hoja hapa ni kwamba order ya zuio inaathiri haki zingine za Kikatiba, unasemaje?
Wakili sisi tunasema hayo ndio matokeo ya kosa walilolifanya.
Jaji kwahiyo unasema ni sahihi kuwa constitutional right zimekuwa infringed au vipi? Usituambie mambo ya inawezekana. Tujibu kuwa haki za kikatiba za wanachadema zimenyimwa au hazijanyimwa kwa maoni yako sasa?
Je haki ya kufanya siasa ni haki ya kikatiba au sio? Je mtu akizuiwa ni sahihi?
Sisi hatukufika kwenye Katiba anasema Wakili.
Jaji ndio tunawauliza hii kesi yenu ni Civil Case?
Wakili ndio hii ni Civil Case.
Jaji sasa kwanini hamkuiita Plaint na iwe ni Civil Case.
Jaji mwingine kwahiyo hii mnasema kuwa ni Suit under Civil Procedure na haikuletwa kwa njia ya Plaint? Unasemaje hapa.
Wakili, Mheshimiwa Jaji hii ni Civil Case.
Anakaaa anasimama tena Manywele Waheshimiwa Majaji kuhusu suala amri ya zuio inadumu kwa miezi sita tu.
Part 7 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
Indonesia
Daffy retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_MGAWANYO_MALI_ZA_CHADEMA
Part 5
Anasimama Marijani wakili wa Said Issa na wenzake ana manywele mengi kichwani, anazungumza.. nae anapigwa maswali ya haraka haraka.
Jaji kwahiyo unataka kutuambia kuwa political party act nayo inazuia discrimination
Wakili ndio Mheshimiwa.
Sasa naomba niende kwenye hoja ya kwamba kesi ilifunguliwa nje ya muda.
Kwa mujibu wa Para 7 wa petition inasema chama kilimaliza kununu jengo la Chama na ilikuwa mwaka 2019 hivyo basi kuanzia hii tarehe hii hadi 2024 ilikuwa ni miaka sita tu. Kwahiyo ilikuwa ndani ya muda.
Jaji hebu soma para 10 tuone
Para ya 8 pia inasema kipindi ambacho kipo ndani ya muda.
Jaji kwahiyo tarehe ya kumiliki mali ndio cause of action inaanzia?
Wakili ndio inaanzia hapo kwenye para ya 9 pia imesema.
Jaji sasa uliwasikia wenzako kuhusu O.VII wewe unasemaje?
Wakili hiyo haiapply kabisa.
Jaji lakini Wakili umeelewa kweli hiyo O.VII r.1(e)
Wakili sasa jaji hiyo sasa ipo na ilikuwa stated kwenye petition kwenye paragraph nyingi.
Jaji kwahiyo matakwa ya hiyo O.VII yamezingatiwa na ilikuwa stated direct?
Mheshimiwa hiyo nayo haikuwepo direct lakini.
Kwa mujibu wa Section 18(1) ya Limitation Act
Jaji isome kwanza tusikie.
Anaisoma sasa.
Jaji sasa ina apply kwenye hii kesi?
Wakili ndio.
Anayetaka ku recover ni nani kwahiyo? Anamuuliza Jaji.
Wakili anajibu ni hawa wateja wetu.
Kumbe ni hivyo, haya tuendeleee. 😂
Kuhusu issue ya Locus Stand kwa mujibu wa Para. 6 na page 2 ya records
Jaji anasema hebu subiri wenzenu walisema wajumbe wa bodi kujishitaki wenyewe? Mnasemaje?
Wakili Bodi ya wadhamini inashitakiwa tu.
Jaji sasa walikuwa wanashitaki kwa maslahi ya nani?
Wakili walikuwa wanashitaki kwa maslahi ya Chama.
Jaji sasa wenzio wamesema utaratibu wa bodi ya wadhamini kushitaki ikiwa ni pamoja na kuwashitaki trustee wengine maana maamuzi ya bodi ya wadhamini yanapitishwa kwa kura na yanakuwa maamuzi ya Chama.
Wakili sheria nafikiri haisemi hivyo.
Jaji umemaliza au bado?
Wakili nimemaliza.
Anasimama Wakili mwingine anaitwa GIDO anasema kwenye right to be heard nasema kwamba wenzetu walipewa kabisa haki yao ya kusikilizwa.
Sasa ukisoma Tarehe 10 corum inaonesha mawakili wa pande zote walikuwepo. Jebra na sisi tulikuwepo.
Jebra aliomba shauri liahirishwe hadi siku ya ijumaa, Wakili Mulamuzi alijibu na kupinga ombi hilo na baada ya hapo proceedings ziliendelea na Jaji wa Mahakamu kuu alitoa maamuzi na kusema kesi hii hakuna sababu za msingi za kuahirisha.
Hivyo Waheshimiwa majaji hadi eneo hilo haki ya kusikilizwa walipewa wenzetu.
Mahakama ilisema kuwa sababu alizotoa Jebra kujiondoa basi ajiondoe.
Jaji sasa wateja wamemtuma wakili na yeye amejitoa huyo Wakili. Sasa kajitoa inakuwaje kwa aliyemtuma nae tunamsaidiaje?
Mh. Jaji alisema Mawakili walikuwepo wengi
Jaji sasa sisi tunataka hali ikiwa hivyo tunafanyaje?
Jaji wapili anasema naongezea hapo hukuona kuna umuhimu wa wateja kujulishwa.
Anasema Jaji wa tatu na mimi naongezea tusaidia una authority yoyote katika unayosema?
Hii inaitwa Mbwa Kala Mbwa hawa wazee ni watanzania kweli? 😂 mbona kama leo wamebadilika. Wanapeleka moto sana. Kama hawataki vile.
Wakili anajibu sasa, hata kesi walizoleta ni za Mahakama kuu kuhusu haki ya kusikilizwa haiwalazimishi muifuate.
Jaji sasa wewe yakwako ya Mahakama ya Rufani iko wapi?
Zile sababu Jaji aliziona ni delay tactic.
Jaji sasa hilo lipo wapi kwenye hukumu? Hivi hujawahi kukutana na uamuzi wa Mahakama unaosema makosa ya Wakili hapaswi kuumizwa mteja?
Jaji mwingine tena anasema tena Wakili alijitoa wakati Mahakama ilishasema hapa leo tutaendelea. Sasa huoni kulikuwa na umuhimu wa wateja kuambiwa.
Wakili anajibu anasema Respondent walipewa haki ya kusikilizwa na muwakilishi waliyemtuma hakutaka kuitumia haki hiyo.
Anasimama Marijan anasema naomba ni address inshu zingine.
Part 6 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
Filipino
Daffy retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_MGAWANYO_MALI_ZA_CHADEMA
Part 4.
Mahakama imerejea.
Anasimama Mpale Mpoki na kusema uwakilishi kwa upande wetu ni kama ilivyokuwa awali.
Kwa upande wetu na sisi upande wa waleta maombi uwakilishi uko vile vile.
Alban Fidelis Kairu anasimama na kuanza kusema kwa niaba ya akina Said Issa nitajikita kwenye areas mlizozisema.
Naomba ruling ya Said Issa kuadapt Sect. 4 ya Appellate Jurisdiction naomba kuitumia ruling hiyo katika kujenga hoja zangu.
Hoja ya tukishindwa kuelezea value ya subject matter.
It is proper kwa mujibu wa para 7,8,11, 12 na 14 and 15 ya Petition waliweza ku state value ya subject matter za property ambazo ni mali za Chama.
Pia walisema Chama kilikuwa kina own property zenye thamani ya bilioni 4.
Para 11 ya petition hao petitioners wali allege kuhusu pesa ambazo Chama kilikuwa kinamiliki kwenye Account number za Chama.
Ukiangalia kwenye reply yao walipinga mambo hayo sasa kwa vile wao walipinga basi halikuwa pure point of law.
Jaji anamuuliza kwani uamuzi wa Jaji ulikuwaje kuhusu suala hilo la value ya subject matter?
Ilisema kuwa monetary value haikuwa issue kwasababu hawakudai masuala ya mgawanyo wa pesa.
Jaji sasa tuambie value ilikuwa shilingi ngapi?
Mheshimiwa jaji para ya 7 inasema hivyo.
Jaji tuambie sasa mliandika wapi kwenye petition yenu value ya subject matter.
Mhe. Jaji sasa hapa
Hivi soma CPC kuhusu value ya subject matter inasemaje?
Jaji amemwambia asome sheria inasema kuwa lazima kuwe na statement inayoonesha value ya subject matter.
Expressely haipo lakini impliedly ipo, inasema huyu Bwana mdogo.😂
Jaji hebu sema sasa hiyo Para. 25 unayoase.a inasemaje? Au ndio hiyo ina statememt?
Haya uamuzi wa Jaji umesemaje kuhusu suala hilo maana naona kama ndio unajibu leo haya mambo.
Mheshimiwa Jaji value hazikuunganishwa.
Jaji anamuuliza kwahiyo hiyo ipo kwa mujibu wa O.VII?
Jamaaa amechanganyikiwa hawa wazee wanapiga sana maswali.
Majaji wa Mahakamaa ya Rufani ni kama wao ndio Mawakili aiseee.😂
Alban Fidelis Kairu anaendelea kuhusu Court fees hilo ni suala la Mahakama halikuwa suala letu.
Uamuzi wa Mahakama kuu uliotolewa ni kweli haikuwa Kesi ya Kikatiba. Na Appllicants walikuwa wanalalamikia under Political Party Act.
Jaji sasa kama haikuwa Constitutional case ilikuwa ni kesi gani?
Wakili wa akina Said Issa hii kesi yetu ilikuwa ni Petition. Inaanzia ukurasa wa kwanza.
Jaji wa Mahakama ya Rufani isome kama ilivyo.
Wakili anasema imeandikwa CIVIL CAUSE.
Jaji na huko chini imeandikwaje?
Wakili amasema imeandikwa Petition.
Jaji: Sasa hapo nini ni nini?
Mheshimiwa haya mambo magumu lakini ndio yako hivyo. 😂
Jaji sasa katika suit kuna civil case, constitutional case. Hii ni ipi?
It is suit under political parties Act anajibu wakili wa serikali.
Jaji labda tuendelee na wenzako pengine watakusaidia. Haya endelea tu.
Naomba niwasomee uamuzi wa Mahakama kuu ulivyosema. Anausoma hapa.
Kwa kifupi huyu jamaa anayeitwa Wakili anayoongea hata Majaji hawamuelewi. Wanangonga maswali yakutosha. Kwanza sauti yake imeisha kabisa sasa hivi hatumsikii. Ananong'oneza tu kule mbele. 😂
Waheshimiwa Majaji ukurasa wa 720
Jaji sasa hiyo si ni ile barua?
Wakili anajibu ndio.
Jaji sasa hiyo barua inaelezea ruling na ruling ndio inapingwa wewe hatukuelewi hapa unasema nini?
Wakili mimi nasema Jaji alikuwa sahihi tu.
Jaji sasa yale madai yenu yana affect constitutional right wewe unasemaje?
Wakili anasema hizo rights tulizosema tuna refer kwenye Political Party Act.
Jaji unataka nikukumbushe kila walichosema ili uweze kujibu? Wewe hukuwasikia?
Waheshimiwa walitaja Article 12 na 30 hazihusiani na kesi iliyopo Mahakamani. Hakuna constitutional demand iliyopo.
Jaji kwahiyo unasema ulikuwa una demand nini?
Sisi tunademand kuvunjwa kwa Katiba ya Chadema na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa.
Part 5 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
Filipino
Daffy retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_MGAWANYO_MALI_ZA_CHADEMA
Part 2
Anaendelea Dr. @rugemeleza
Uamuzi huo wa Jaji aliutoa bila kuelewa trustees zinavyofanya kazi.
Wakifungua Trustee yao ni watu wamoja na kama itatokea mgongano mmoja anafungua kesi basi anashitaki wenzake kwa nafsi zao.
Kifungu cha 14 cha Trustees Incoporation Act, kinasema all trustees inco. under this Act, they should be answerable in their acts as if there is no such trustee incorporation.....
Sasa kwahiyo tuna incompetent suit hawa 2nd and 3rd ni trustee na kwa mujibu wa sheria walipaswa kuwashitaki other trustee kwa majina yao wenyewe na sio kuishitaki Trustee.
Jaji wa Mahakama kuu alipaswa kuifuta na kuifukuza hii kesi kwa mujibu wa vifungu vya Sheria.
Logic behind ni kwamba trustees wana fiduciary relationship to each other ni lazima useme wenzangu wamekosea nini?
Madai mbele yenu kulikuwa na makosa ya Mahakama kuu na hakukuwa na competent suit before the Court of Law.
Kwenye hoja ya Jurisdiction ni kwamba nani ana mamlaka na Vyama vya siasa?
Kama unasema kumekuwa na ukiukwaji na Sheria ya Vyama vya siasa madai kama hayo yanaenda kwa Msajili ndo maana Msajili wa Vyama vya siasa amepewa mamlaka hata ya kufuta Chama cha siasa kama Chama husika hakijatekeleza matakwa ya Sheria ya Vyama vya siasa.
Jaji sasa katika kuamua jambo hilo alisema sio suala la ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, hilo ni suala la kisheria.
Kesi ya Mbeya Rukwa Mahakama ya Rufani ilisema jambo ambalo mamlaka fulani au taasisi ya kiserikali imepewa mamlaka ya kulishughulikia.
Basi Mahakama isiingilie kabla mamlaka hiyo husika haijafanya maamuzi.
Dr. Nshala anasema amemaliza sasa anaomba Wakili Hekima Mwasipu nae aendeleee.
Anaendelea Mwasipu
Ni ukweli kwamba Order 10/06/2025 ilitolewa bila Respondent kuwepo Mahakamani.
Kilichotokea ni kwamba maombi ya Revision yalikuja kusikilizwa lakini wakati wa kuanza kusikilizwa Wakili Jebra Kambole aliomba kesi iahirishwe aende kumsindikiza Wakili mwenzake kuzika.
Mahakama ikamkatalia na ikaendelea na kusikiliza maombi husika.
Pia Wakili Jebra Kambole akaomba kwenda kuhudhuria msiba wa Dada yake Hekima Mwasipu.
Jaji akakataaa tena.
Jebra Kambole alisema naomba kuondoa instructions yangu kwasababu sitaweza kuwawakilisha wateja wangu vizuri.
Wakili wa waleta maombi alisema tunaomba kuendelea exparte kwasababu respondents hawapo.
Sasa sisi hoja yetu ni kwamba je ni utaratibu gani unapaswa kufuatwa wakili anapoondoa instruction kwa wateja.
Kesi ya Abdala Chuga vs Halima Ismail ni kesi ya Mahakama kuu haiwabani waheshimiwa Majaji wa Mahakama kuu katika uamuzi huu ambao hauwabani lakini tunaomba kuwashawishi muukubali na kuutumia.
Mahakama Kuu ilisema baada ya Wakili kujiondoa katika kesi basi Mahakama kuu inapaswa kuwatumia summons wateja wa wakili husika na kumpa taarifa.
Kesi ya Andrew Gwande Sule Vs Republic nayo pia inasema ni lazima respondents ni lazima mteja apewe notice lakini jambo hili halikufanyika.
Implication yake ni nini?
Respondents hawakupewa ni ibara ya 13(6)(a) ya Katiba inasema linapoamuliwa suala lolote kuhusu haki yake ni lazima sasa mtu huyo apewe haki ya kusikilizwa.
Kesi ya Mbeya Rukwa inasema Natural right ni haki ya Kikatiba na sio suala ambalo tumelipokea kama mapokeo tu bali ni takwa la Sheria zetu.
Sasa remedy ya mambo haya ni nini?
Kesi ya Ntagazwa ni reported na Mahakama ya Rufani ilisema kuwanyima haki ya kusikilizwa maana yake proceedings zote ni haramu na ziondolewe.
Na sisi ndio ombi letu kuwa proceedings zote baada ya Wakili Kambole kujiondoa basi Mahakama inapaswa kufuta yote yaliyoendelea baada ya hapo.
Naomba niende kwenye hoja nyingine.
Kwa mujibu wa CPC inasema ukitoka kutoa amri ya zuio isizidi miezi 6 kama itatokea jambo hilo bado lipo Mahakamani basi atatakiwa kwenda kuomba kuongezewa muda.
Part 3 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
Indonesia
Daffy retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_MGAWANYO_MALI_ZA_CHADEMA
Part 1
Mahakama imeanza!
Mawakili wa pande zote mbili wapo.
Anaanza Wakili wa upande wa waleta maombi Mzee Mpale Kaba Mpoki @MpaleMpoki
Kuhusu hoja ya Cause of action ilianza lini yani madai ya akina Said Issa na wenzake yalianza lini wao wanasema ni mwaka 2016.
Kwa Mujibu wa Sheria ya Law Limitation Act kipindi cha mwisho kwa kesi ambazo hazijaelezwa na sheria itakuwa ni miaka 6 lakini wao wameleta kesi hii baada ya miaka 9.
Na jambo hili hawajalisema kwenye kesi yao ya msingi hata hiyo ya kuwa cause action ilianza mwaka 2016.
Wamekuja kuisema baadae kwenye pingamizi lao kuwa Mwenyekiti wa Chama asiunganishwe kwenye maombi yao ya msingi.
Sasa sisi tunasema kwenye shauri/maombi ya msingi hawakusema cause of action ilianza lini lakini hata hili la 2016 walilolisema liko nje ya muda.
Labda ingekuwa kesi ya Kikatiba wangeweza kuruhusiwa maana hakuna limitation of time.
Lakini hii kesi yao sio ya Kikatiba kwasababu kwanza imesikilizwa na Jaji mmoja na hakuna kesi ya Kikatiba inasikilizwa na Jaji mmoja.
Sasa Effect ya kutokuweka Cause of Action O. VI r.11 ya Civil Procedure Code katika hali ya kawaida hii kesi ilipaswa kuwa rejected na Court kwasababu haikuonesha ni lini Cause of action arouse.
Eneo lingine ni Failure to raise the value of the property. Takwa la ku disclose cause of action pia iko O. VII r. 1(i) ya CPC. The value of the subject matter of the Suit is of paramount importance for the case to be admitted.
Sheria inasema tunaweka value ya subject matter ili kuonesha pecuniary jurisdiction lakini kuisaidia mahakama kujua inacharge kiasi gani ili kuilipia gharama za kusajili kesi husika.
Sasa Ukurasa wa tano wa bando tulilowapa. Mara nyingi tungeona wamesema value ya subject matter lakini hawajasema.
Madai yao yaliyopo ukurasa wa nne wanadai distribution un even distribution of party asserts na pia paragraph 7 inasema tuna nyumba mikocheni yenye thamani ya milioni 726, landed property zenye thamani ya bilioni 2 na usheee, kulikuwa na magari 8 yenye thamani ya 576 milioni, Pikipiki 478.
Sasa hawajasema thamani ya wanachokidai ni shilingi ngapi?
Tumeangalia kwenye filing system imelipiwa kama fees ya shilingi elfu 50.
Sasa naomba niwapeleke kwenye GN. No. 247/2018 Court Fees Rules ambayo inasema inazidi kiwango cha juu zaidi inapaswa kulipiwa milioni 5.
Receipt ambayo tumeiona ni ya elfu 50, mtu ambae anaamua walipe shilingi ngapi angesema walipe milioni 5 na sio elfu 50.
A case has been deemed proper filed once the proper fess has been paid accordingly and as it is required by the law. Sasa ni wasilisho letu ni kwamba order ya injuction haikuwa sahihi kutokana na hakukuwa na kesi iliyofailiwa Mahakamani. Na tunaona lilikuwa ni pungufu kubwa sana.
Sasa naomba Dr. Rugemeleza Nshala aendeleee.
Dr. @rugemeleza anaanza. Nawashukuru sana kwa nafasi.
Naomba nizungumze hoja moja kwanza ukurasa wa 4 wa petition yao. Kwenye hoja ya Kikatiba.
Anasoma maneno yao ambayo wanasema viongozi wakuu wamekuwa wakisema maneno dhidi ya Zanzibar ambayo yanatishia Muungano na utendaji kazi wao kama wazanzibari.
Sasa Maneno haya yanaonesha madai yao ni ya Kikatiba. Na kesi hii ilipaswa kuwa ya Kikatiba. Lakini kesi hii imesikilizwa na Jaji mmoja na haikuwa kabisa kesi ya Kikatiba.
Jaji alipelekewa suala hili akasema mambo ya Kikatiba tuachane nayo. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana. Ilikuwa ni hatari sana kwa Jaji mmoja kujivika madaraka ambayo hana.
Kesi za Kikatiba yanaletwa chini ya BRADEA au kwa mujibu wa ibara ya 108 ya Katiba. Hawajafanya hivyo.
Haya Madai yao yana UVUNDO sina Lugha nyingine ya kutumia Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Sasa Dr. Nshala anaendelea hapa.
Wafungua maombi wa 2 na 3 wamesema wao ni member wa Board of Trustees ya Chama.
Sasa sisi tunasema hawawezi kufanya hivyo kwasababu wanapingana na Trustee Incorparation Act.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
Filipino
Daffy retweetledi
Daffy retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 225
Mhe. Lissu anaendelea hapa.
Kama mtakumbuka nilisema ninavyoishi Ukonga, siruhusiwi kuonana na Mawakili wangu in private.
Mnaruhusiwa kutembelea Magereza naomba mliangalie na hili kama itawapendeza inawapa Mamlaka ya kutoa mapendekezo na mamlaka za Magereza kurekebisha masuala yanayohusu wafungwa kama haya niliyosema.
Ni muhimu kwamba kuwasiliana na washauri wangu wa kisheria ilindwe kama sheria inavyosema bila kusikilizwa na maafisa wa Magereza.
Ni hayo tu Waheshimiwa
Mhe. Tundu Lissu amemaliza na amekaa sasa.
Majaji wanaandika hapa.
Anasimama Renatus Mkude kuwa tutampatia hizi nyaraka ndani ya siku 14 tutampatia.
Hili la masuala ya utawala wa mambo ya magereza kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha National Prosecution Act na sisi ofisi ya DPP tutatembelea ili kuhakisha kunakuwa na fair trial.
Wameombwa Majaji anasema DPP ataenda eti huko Magereza kuangalia haki za Mtuhumiwa. Uongo uongo uongo. Hawana hata aibu hawa jamaa.
Majaji wanaandika baada ya kusikia hayo kutoka kwa Wakili wa Serikali, Renatus Mkude.
Majaji wanajadili pale.
Yuko Jaji muda wote yeye huwa anacheka anafurahi tu sijui huwa anatabasamu jambo gani? Wanaofika hapa Mahakamani wanamfahamu vizuri.
Jaji Ndunguru: Tumesikia hoja za Jamhuri na Hoja za Mshitakiwa nae kama ambavyo mshitakiwa ameturahisishia kuwa mikono yetu imefungwa kwamba yapo hayo maombi ya marejeo Mahakama ya Rufani.
Sasa shauri hili linasimama hadi pale Mahakama ya Rufani itakapotoa uamuzi.
Suala la Gerezani wakili wa Serikali amesema na sisi pia tumelichukua.
Mwenendo wa shauri hili unasimama hadi pale mambo ya Court of Appeal yatakapoisha.
So kesi hii imeahirishwa hadi hapo itakapoitwa tena.
Naomba Repost yako.
Indonesia
Daffy retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 224
Majaji wameingia muda huu saa nane Kamili Mchana.
Wanaandika pale juu.
Mheshimiwa Lissu ameingia na kuteta jambo na Dr. Nshala tunamsikia anasema waende kokote watakapotaka kwenda tutakutana nao huko. Sasa sijui ni wapi anamaanisha.
Anasimama Renatus Mkude Wakili wa Serikali kwa niaba ya jopo la Mawakili wa Serikali tunaomba radhi kwani tulifikiri tungetumia lisaa limoja.
Mchana huu nipo na Ajuaye, Thawabu Issa na Cathbert Mbiringe. Kwa wote tunawakilisha jamhuri na Mshitakiwa yupo.
Shauri lilipangwa kuendelea na mashahidi. Lakini tumetafakari na tunaitafsiri kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha Appellate Jurisdiction Act na kanuni ya 65(1) ya kanuni za Mahakama ya Rufani.
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) anatoa taarifa ya kuwasilisha taarifa ya mapitio (revision)
Hapa kwanza anakosea Mapitio ni Review alipaswa kusema Marejeo ndio Revision sijui kasoma wapi nae huyu jamaa.😂😂😂
Anaendelea hapa Renatus Mkude, kuwa Notice of motion hiyo imeambatanishwa na kiapo cha Cathbert Mbiringe Wakili wa Serikali ambayo taarifa hii ya kutoa notice kwenda Mahakama ya Rufani imesainiwa leo Tar. 24/02/2026.
Na kupokelewa kwa mifumo ya kielektroniki inayotambulika na Mahakama na kusajili kama. CRIMINAL REVISION NO. 7203216/2026 imepokelewa na Mahakama ya Rufani Tanzania hapa Dar es salaam.
Ambalo chimbuko lake ni Criminal Sessions No. 19605/2025 ambayo iko mbele yenu Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu. (Ndunguru, Karyemaha, Kiwonde)
Kwa kuwa shahidi wetu aliyekuwa anafuata ACP Mahamba tuliyemuombea notice additional substamce of evidence na ikakataliwa.
Ni Rai yetu kwamba kwa kuwa shauri hili limeshapokelewa Mahakama ya Rufani haiwezi kusimama ili kuweza kutoa nafasi kwa shauri husika huko Mahakama ya Rufani kuweza kuamuliwa.
Ni hayo tu kwa sasa.
Tunamsubiri Mh. Lissu atajibu nini?
Mhe. Lissu anaanza.
Baada ya kuzikiliza wasilisho la upande wa Mashitaka nina haya ya kusema.
1. Kwa vile mimi nipo gerezani na wanajua nataka wanipatie hiyo nakala ya Notice of Motion waliyofile niweze kuiona.
2. Ninafahamu na ninatumaini na wao wanajua kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 8(2)(d) cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa ambacho wamekitaja (Appellate Jurisdiction Act) wanafahamu kwamba hakiruhusu rufaa wala mapitio wala marejeo ya maamuzi ya Mahakama ambayo hayamalizi shauri la msingi. (Interlocutory decisions) sina shaka na wao wanalifahamu hilo.
3. Waheshimiwa Majaji siwaombi mtoe uamuzi wowote kuhusu hili ninalolisema.
Nataka iwe kwenye record kwamba nafahamu na naamini upande wa mashitaka wanafahamu lengo la kupeleka ombi la marejeo Mahakama ya rufani na wanafahamu hairuhusiwi ni kurefusha mashauri haya ili niendelee kukaa Gerezani. Ni hilo tu.
Kwamba tupeleke Mahakama ya Rufani ili huyu mbaya wao ambae ni mimi aendelee kukaa Gerezani.
Kwa vile wananipeleka kwe ye Mahakama ya Rufani nataka niwaeleze kuwa nitawafuata huko huko naenda kuwashughulikia huko huko.
Kama ambavyo kesi yao is dead on arrival najua hata hii revision yao pia imeshakufa.
Tutarudi hapa yakiisha huko ya Mahakama ya rufani tutarejea hapa na nitawashughulikia tukirudi.
Jambo la Mwisho Mawakili wangu wametaka kunipa nyaraka hapa lakini siwezi kupewa hadi nyie mseme.
Sijui wanaogopa nini watu wa magereza nisipewe huo uamuzi hapo ni makaratasi tu.
Naambiwa ni hukumu kutoka huko Umoja Wa Mataifa lakini Magereza wanaogopa nisipewe.
Tena ni uamuzi unaohusiana na mimi kuwepo Gerezani. Tatizo liko wapi?
Jaji anasema uko wapi? Umepelekwa wameuona wamesema wape Mawakili wa Serikali.
Wako wanasoma hapa Mawakili wa Serikali huo uamuzi.
Anasimama Renatus Mkude anasema mimi ni member wa working group za UN Human Rights Council.
Jaji: Tumesema apewe au asipewe?
Renatus Mkude: Apewe tu.
Part 225 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Indonesia
Daffy retweetledi
Daffy retweetledi

#UPDATES_KUTOKA_MAHAKAMA_KUU
Majira ya saa nane kasoro tano, wameingia Mawakili wengine wa Serikali.
Ananitonya Wakili mmoja hapa kwamba amechungulia nyaraka aliyonayo Renatus Mkude ni Notice of Motion kwenda Mahakama ya Rufani nafikiri wanaenda kufanya Revision ya uamuzi uliofanywa leo na Majaji wa Mahakama kuu leo kuhusu ile notice ya kuongeza ushahidi wa Amin Mahamba.
Huku ni kupoteza muda wa shauri hili.
Kwa kifupi kisheria tunaambiwa kukata rufaa au kupeleka maombi ya kufanya marejeo mahakama ya rufani haizuii kesi kuendelea.
Mahakama inayo mamlaka pia kukataa maombi yoyote ya Jamhuri ya kutaka kuahirisha kesi hii ikiona wanachotaka kulifanya Jamhuri ni kupoteza muda na kukiuka haki za msingi za Mshitakiwa.
Muda mfupi ujao tutajua ukweli wa mambo.
Kwa sasa tunajaribu kuchokonoa kidogokidogo kinachoendelea.
Tuendelee kuwa pamoja.✊
Indonesia
Daffy retweetledi

#UPDATES_KUTOKA_MAHAKAMA_KUU
Muda huu saa nane kasoro mchana.
Ameingia Wakili wa Serikali Renatus Mkude, tunasubiri Majaji nao waingie, amekuja peke yake akiwa na kikaratasi kimoja kinachosadikika kuwa ni kiapo fulani ambacho wameshakifile Mahakamani.
Hatujui kinahusiana na kufuta mashitaka, kukata rufaa au jambo gani lakin amekuja peke yake na hako ka nyaraka kake.
Muda mfupi ujao tutajua nini ni nini? Au nini kinaendelea..
Indonesia






