Mutashobya
4.1K posts

Mutashobya
@DenisMuta
Think-Tank | Mathematician | Scientist | Mkulima | IT |CHADEMA | Yanga| Catholic |
Bukoba Katılım Temmuz 2014
4.5K Takip Edilen1.3K Takipçiler

Mwambe anadai alikua anaenda Nairobi kwa matibabu. Ni matibabu ambayo yalishindikana bongo.
Anayo barua ya rufaa na appointment ya daktari. Anafika mpakani Namanga anazuiwa kuvuka. Ananyang'anywa passport na kuamriwa kurudi.
Anaona kaonewa. Anaamua kufungua kesi Mahakamani ili arudishiwe passport yake, na apate haki ya kusafiri kwenda kitibiwa.
Mahakama inapanga tarehe ya kesi, idara ya uhamiji wanaitwa, lakini hawatokei mahakamani. Kumbuka anayefanyiwa hivi sio Mkulima wa Kamachumu wala Mwalimu wa Kyabakari-Ni Waziri mstaafu.
Hii ina maanisha nini?? 🤷♂️
TUTAKUWEPO🫵😎

Indonesia

M/Kiti Tundu Lissu wewe ni SAUTI ya HAKI na Mzalendo.
Historia uwakumbuka waliosimama imara wakitetea ukweli.
Uongozi wa kweli haupimwi kwa UHURU wa mwili bali upimwa kwa uhuru wa mawazo na misimamo.
Sauti inaweza kuzimwa kwa nguvu, lakini ukweli hauwezi kufutwa. #LissuSioMhaini

Filipino

“Amin nawaambia, msipogeuka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Yeyote ajinyenyekeze kama mtoto huyu, ndiye mkubwa katika ufalme wa mbinguni.” — [Mathayo 18:3–4]
//
“Truly, I say to you, unless you turn and become like children, you will never enter the kingdom of heaven. Whoever humbles himself like this child is the greatest in the kingdom of heaven.” — [Matthew 18:3–4]

Filipino
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 12
Anaendelea Mhe. Lissu
Tatu. Mahakama ya Rufaa kwenye kesi ya Dodoli Kapufi ilisema nini kuhusu kifungu cha 183?
Jaji Chande alisema in essence that section is deal with trial not deal with Committal. Section inayodeal na committal ni S. 261.
Nimemaliza na hiyo niendeleee na kesi yao nyingine.
Hii nayo imeletwa bure kabisa.😂
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba nishughulike na JOB MREMA.
Huyu Katuga nimemaliza nae.
Anasimama Katuga anasema kifungu cha 187 hajakisemea.
Mhe. Lissu anasema nawashukuru sana Katuga. Ngoja nije hapo.
Hicho cha 187 trial at a place where act done.
Hii section is about trial na section about committal is 262, 263 hadi 265.
Hivyo basi kama ambavyo sect. 183 ilivyo irrelevant basi hata section 187 nayo ni hivyo hivyo haihusiki hapa tunazungumzia committal. Tofautisha Committal na trial.
Sasa nirejee kwenye suala la Mashahidi. Nalo lilizunguzwa na Mrema na nimesema naanza kushughulika nae.
Suala la Mashahidi wangu kutokuandikwa. Walilizungumza.
Katuga anasema hawakuitwa na kuandikwa wanaweza kuandikwa baadae hakuna tatizo. There is no prejudice.
Wakili Mrema pia alisema Mshitakiwa alishauriwa kuwa majina ya mashahidi atakuja kuwasema mahakama kuu. That one was premature kwahiyo hamna shida.
Waheshimiwa majaji naomba niwaonyeshe jinsi ambayo hii nayo ni shida kubwa.
Mashahidi kutokuandikwa kwenye commitall proceedings.
Ipo hivi Waheshimiwa majaji, Mshitakiwa ana haki ya kutamka majina na anuani ya mashahidi wake wakati wa committal maana asipoitumia inabaki fadhila ya mahakama.
Kwenye committal nilikuwa na haki ya kusema mashahidi wangu na anuani zao. Kwenye mahakama hii ni descretion yenu sio haki yangu tena.
Mnaweza kuamua au msiamue sasa niwapeleke kwenye sheria.
Kifungu cha 264 cha CPA ndo kinatoa haki kwa mshitakiwa kutaja majina ya mashahidi wake wote.
Nikisema nina mashahidi wewe Hakimu KISWAGA huwezi sema nitawasemea mahakama kuu, unapaswa kuandika.
Hilo halikufanyika.
Mawakili wa serikali wanasema ni premature, unaweza kuita baadae, sasa hiyo baadae iko kifungu cha 281 na 314 ya CPA. (Kumbukeni CPA ni Criminal Procedure Act - Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai)
S. 281 inasema hivi msajili wa mahakama kuu ataandaa wito kwa mashahidi wote ambao orodha yao ipo. Registrar/ msajili anatoa summons/wito kwa hao uliowataja. Kinasema hivyo.
Sasa kama hujataja nini kinapaswa kufanyika ndio S. 314 inaingia hapo. Kinasema hivyo mtuhumiwa hawezi kuwa na haki ya kuita mashahidi wake ambao hawakuwa kwenye orodha yake labda mahakama ijiridhishe kuwa kuna umuhimu wa mashahidi hao kuitwa.
Sasa hii ni fadhira ya majaji haki yangu nimesema ilikuwa Kisutu.
The accused person shall not be entitled to call witness without approval au consent ya majaji sasa kuna prejudice kubwa kuliko hiyo kunyang'anywa mashahidi wangu.
Haya maneno ya kwamba naweza kuwaita baadae ni maneno ya watu wenye nia mbaya sana na mimi.
Wanasema mambo ambayo sheria haiyatambui na kuyakubali, naomba waheshimiwa majaji msikubali jambo hili.
Sasa Job Mrema alisema majaji mnapaswa mjiulize hili pingamizi kama liko sawasawa mbele ya mahakama hii.
Na alilisema jambo hili kwa mbewembwe kabisa.
George Abdon Kilinga na wenzake vs Anna na wenzake ni mashauri ambayo aliyaleta hapa.
Kwanza hii ni kesi ya mirathi ilianzia mahakama ya mwanzo, ikaenda mahakama ya wilaya ya Babati ambayo iliamua kwamba wadaaawa wataamua watumie sheria gani? Mahakama kuu rufaa ya pili sasa Madam Justice alisema parties can not by agreement confer jurisdiction to a Court.
Wadaawa hawawezi jiamulia kuipa mamlaka mahakama hii kwasababu suala la jurisdiction (mamlaka) ni suala la Jaji.
Kwenye kesi yangu sasa Mshitakiwa anasema alikuwa committed na mahakama ambayo haikuwa na mamlaka.
Part 13 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 11
Anaendelea Mhe. Lissu
Walinipa uamuzi wa kesi ya Ishengoma na wenzake sita.
Kesi ya Mahakama ya Rufani hiyo Kesi ya Donatus Ishengoma ukurasa wa 15 umecite kesi ya Mbogo niliyoitaja hapo awali.
Anasoma hiyo kesi hapa ilichosema. Maelezo marefu hapa.....
Waheshimiwa majaji nani anauwezo kuwa na ubishi na hili, Mimi sina.
Sina ubishi na superior Court can do on interference to surbodinate court.
Kifungu cha 265 hakina descretion kihivyo wanavyodhani. Its only partially decretion. Naomba nikisome hicho kifungu.
Anakisoma sasa hicho kifungu hapa.
Descretion nimeambiwa hapa kwamba ni kumpeleka mtuhumiwa gerezani. Hiyo ni 265(1).
Ukianza kusoma vifungu vingine ikitaka kuahirisha iandike sababu za hayo maahirisho.
Mamlaka haina option ya kutokuandika sababu na haina option ya kutokutoa reason hizo.
Naomba niendleee hiyo kesi ya ishengoma imeenda kwa kiwango hicho.
Naendelea na kesi zao zingine.
Waheshimiwa majaji wakili Kasuga aahhh samahani Katuga aliuliza a very rhetorical question kwamba sasa turudi kisutu?
Hili nitalijibia lamwisho.
Twende kwenye improper dating kubadilisha proceedings na kubadilisha tarehe za matukio mahakamani.
Tuliambia hiyo ni amere sleeping of the pen na tukapewa Kesi ya Baraka Mashaka Kesi ya Mahakama kuu PC Civil appeal/2023.
Hoja yangu ni kwamba kukiwa na kosa moja au mawili kwenye kurasa 101 unaweza kusema ni sleep of a pen.
Sasa ukiwa na makosa mia kwenye nyaraka hiyo hilo la kukosea tarehe haliwi kosa dogo kabisa lazima yaangaliwe kwa uzito.
They are part of the designing kwangu mimi na naomba hayo makosa ya kuteleza kwa mkono naomba yachukuliwe kuwa sio kuteleza kwa mkono yachukuliwe kama sehemu ya uchafu mwingi uliopo humu na niliousema toka siku ya kwanza.
Kwenye hiyo kesi hiyo mshitakiwa alihukumiwa maisha kwa kumfanya kinyume na maumbile mtoto lakini mahakama ikamfunga kwa kosa la armed robbery.
Mahakama ya rufaa ilisema kwa vile adhabu ni ileile kwa makosa hayo basi ni sleep if a pen.
Sasa huwezi kuleta kesi ya namna hii itumike kwenye hoja za kesi tuliyonayo leo hapa.
Kuna kitu amekisema sana Katuga kwamba malalamiko yangu ni kutaka huruma amekisema toka kisutu.
Sympathy..!! Ilianzia Kisutu imekuja hadi mahakama hii.
Pamoja na kwamba sidhani kama itaamua one way to other naomba niweke for the record kupata huruma unapoonewa sio jambo baya.
Kuomba huruma unapokuwa kwenye matatizo sio jambo baya.
Kama anadhani ukipata matatizo unahitaji huruma.
Sasa la msingi ni nini? Siwaombi Majaji chochote mtakachoamua msiamue kwa huruma. Muamue yote kwa haki na kwa mujibu wa viapo vyenu. Msinihurumie na sihitaji huruma yenu nahitaji muamue kwa haki.
Nayasema haya for the record nimeona Katuga anayarudia rudia sana.
Kuna hoja ilitolewa na Katuga na imerudiwa na Mrema kuhusu kifungu cha 183 cha CPA.
Job Mrema anasema inapaswa kusomwa na 187 pia za CPA izo zote zinazungumzia mamlaka ya mahakama.
Mahakama ya Kisutu. CPA ni sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
S. 183 inazungumzia general authority of Court in Tanzania. Kwamba mahakama yoyote ina mamlaka ya kuamrisha mtu kwenda mahakamani ndani eneo la mahakama hiyo kama mtu huyo amefanya kosa ndani ya eneo la utawala wa mahakama hiyo.
Sasa wameleta hii ili waseme kwamba uliletwa kisutu kwasababu ulifanyia kosa Dar es salaam hicho kifungu walichotaja cha 183 kinazungumzia tayari ameshashtakiwa kinaipa mamlaka amri aletwe kwenye mahakama husika.
Mimi nilikamatwa Mbinga na wakati nakamatwa sikuwa mshitakiwa.
Mimi nimekuwa mshitakiwa baada ya kupelekwa Kisutu na kusomewa mashtaka.
Sababu ya pili ni kwamba kwani nilipelekwa Kisutu kwasababu mahakama iliamua nipelekwe kisutu? Hakukuwa na order hiyo.
Kwahiyo S. 183 haiwezi ku apply kabisa.
Part 12 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 11, 2025
Jana tuliishia Part 9 so leo tunaendelea na
Part 10
Hali ya hewa ya mahakama ni nzuri na imetulia.
Askari magereza wameingia hawa wawili watatu ambao wamekuwa wakivaa haya madude usoni ingawa wengi wao siku hizi hawajifichi sura zao kama walivokuwa wanajificha wakati tupo Kisutu.
Imesikika sauti ndogo ya askari High Courtttttttttt.
Kinyonge sana ni kama jamaa hajapata breakfast.😂
Majaji wanaingia na watu wote wamesimama.
Mheshimiwa Lissu ameingia na style yake mpya anakunja ngumi na kuizungusha kwa vibe sana kama kwenye ile video mliyoiona juzi.
Majaji wanaandika andika muda huu.
Wameingia kwa tabasamu kubwa sana leo Majaji wote watatu.
Wamevaa haya magauni yao mekundu na hivi vitai vyeupe shingoni kwao.
Jaji Nduguru kiongozi wa jopo anateta jambo na Kalani wa mahakama.
Sasa Jaji anataka kuongea hapa huku anamuangalia Mh. Tundu Lissu.
Karani anaita kesi Criminal Case No. 19605/2025.
Jaji: Jamhuri Karibuni.
Katuga: Nipo na Misieh Kahima, Thawabu Issa, Harrison Lukosi, Cathbert Mbirnge hawa wote ni Mawakili wa Serikali ambao ni 6 tunaiwakilisha Jamhuri katika shauri hili na mshitakiwa yupo Mheshimiwa Jaji.
Katuga: Tunaendeela na usikilizaji wa mapingamizi na mwenzetu mshitakiwa kama yupo tayari aendeleee. Sisi hatuna shida.
Jaji: anaandika. Anamuuliza Mh. Lissu vipi uko tayari.
Mhe. Lissu: Niko tayari na imara kabisa.
Jaji: anaandika na kuteta kidogo na wenzake.
Sasa unaweza kuendelea ndugu Lissu.
Mhe. Lissu Waheshimiwa Majaji nimefurahi kuwaona na niwapongeze kwa kazi kubwa mliyofanya toka jumatatu.
Lissu anaendelea sasa.
Jana niliomba ahirisho ili nikasome kesi walizonipa hawa jamhuri naomba niseme hiyo kazi nimeifanya vizuri sana.
Niwashukuru mawakili wa serikali kuleta hizo kesi kwasababu zitanisaidia sana kuja kusema nitakachosema siku ya leo.
Ni kesi wamezileta wenyewe sio mimi.
Wakili wa serikali Katuga na Mrema walitoa hizo kesi wenyewe kwahiyo nitaonesha namna hizo kesi kama ni relevant au sio relevant kwa kesi tuliyonayo.
Kwa kuanzia naomba nizungumzie kauli ambayo ilitolewa juzi na wakili wa serikali Mkuu Katuga kwamba committal proceedings lengo lake ni kuhakikisha fair trial.
Hiyo position ipo kwenye maamuzi mengi ambayo yametajwa toka jumatatu mimi nakubaliana na msimamo huo ni kuhakikisha kuna fair trial katika kesi zinazosikilizwa mahakama kuu. Na kesi hizo ni kesi kubwa.
Kama lengo ni kuhakikisha fair trial/hearing hivyo basi committal Court is responsible to make sure the accused person is given full opportunity
Huwezi kumpa nyaraka nusunusu mtuhumiwa kwenye kesi yake, huwezi kuacha makosa mengi yote kama yaliyopo.
Ni lazima mshitakiwa apewe nafasi ya kusema maelezo yake yote. Apewe hiyo fursa na ipo hoja ya whether nilipewa fursa ya kutoa maelezo yangu kwenye committal Court (mahakama ya ukabidhi)
Mahakama ya ukabidhi ilipaswa pia kunipa nyaraka zote zilizopatikana kwenye committal processes.
Hayo yote yakitimizwa kutakuwa na fair trial na yasipotimizwa hayo hakutakuwa na fair trial kabisa.
Waheshimiwa Majaji Wakili wa Serikali Kiswaga watu wanacheka.😂😂😂
Anasema Waheshimiwa huyu Kiswaga amenikaa sana kichwani. Samahani ni Katuga.
Sasa anasema lengo la niliyosema ni kuupotosha umma na nyie majaji kwa hayo ambayo nimeyasema tangu jumatatu mimi binafsi siamini kama kuna chochote nimesema cha kuipotosha mahakama.
Nafikiri nimewezesha mahakama hii na umma kuwaleeza mambo mengi ambayo yalikuwa yamefichwa.
Katuga anasema kuhusu S. 265(1) of CPA anasema hayo mamlaka ya kuahirisha kesi na kutoa sababu za msingi za kuahirisha na kuandika sababu hizo alisema all that is descretion..
A superior court like this should not interfere that power.
Nikapewa kesi ya MBOGO and ANOTHER 1993 kwamba inaunga mkono msimamo wao huo.
Waheshimiwa majaji hiyo kesi ya Mbogo vs Shah sina library yangu ningeipata hiyo kesi yote.
Part 11 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 14
Anaendelea Mhe. Lissu
Swali je mfanyaje?
Mahakama ifanye nini?
Turudi Kisutu?
Ndio Swali lililoulizwa tangu juzi. Turudi Kisutu?
Mnakumbuka wakati namalizia hoja yangu nilisema futeni haya mashauri nirudi nyumbani kwangu nikalale niliwaambia.
On the bases of the law of this country you have no option than setting me free.
Kama mahakama ya kisutu haikuwa na mamlaka basi maana yake tunaendaje kisutu?
Kuna kesi gani sasa kama mmefuta committal?
Mkiamuru turudi Kisutu ndio Kisutu itakuwa na jurisdiction kwa kuwa mmesema kwasababu Kisutu haina mamlaka Kisheria.
Pia hoja ya Mrema kunirudisha nikaanze mwanzo pale Kisutu.
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Mahakama ikifuta kesi imefuta proceedings anaendeleaje kukaa gerezani mshitakiwa?
My submission is that decision was made per incurium na maana yake ni kwamba mahakama imefanya uamuzi kwa kusahau sheria kwa ambao hamjui kilatini. Maana yake ni hiyo.
Watu wanacheka hapa 🤣🤣
Decision made per incurium hatusemi majaji hawajui sheria tunasema wamesahau.
Wahesimiwa majaji hii sio kesi rahisi na kufanya maamuzi ninayotaka mfanye sio maamuzi rahisi pia.
Mnapaswa kufanya maamuzi bila kuogopa chochote.
Msimame kwa miguu yenu.
Mjiamini na mquash this proceedings, yaondoeni haya mashtika.
Swali linabaki kuwa what about Mbinga?
Mpaka hapa tulipo mkinipeleka Mbinga naenda kufanya nini? Labda niende kumsalimia Dada angu Songea na sio mimi kwenda Mbinga.
Mkifuta kesi siendi ukonga Prison tena. Naenda nyumbani kwahiyo majibu ya hilo swala la Mbinga ndio hilo.
Nawaombeni individually and collectively. Each one of you will have to write ruling.
Ameanza kuzungumzia kanuni za kuteua majaji watatu mamlaka hayo anayo CJ ZIMETUNGWA juzi hapa tarehe 05/09.
Nimemaliza Waheshimiwa majaji, nimemaliza mimi.
Nawashukuru sana.
Sasa uamuzi wa watu waliosahau sheria hauwezi kunirudisha gerezani nikifutiwa mashitaka yangu narudi nyumbani. I walk home free.
Mhe Lissu kamaliza kuwasilisha hoja zake hapa.
Sema nini hapa mwisho Mhe. Lissu kaongea kwa hisia mpaka tumachozi tumenitoka, si unajua sisi Wanawake tukogo emotional sana.🥹
Tuendelee
Baada ya Mhe. Lissu kumaliza
Watu wanateta na sauti zinazosikika nyingi sana ni watu wanasema KIMEUMANA😂
Majaji wanaandika jambo hapa na kuteta pamoja.
Mhe Lissu anakusanya vitabu vyake vingi vya sheria na makaratasi yake kibao aliyonayo.
Sijui kwanini ameanza mapema kuyakusanya si angesubiri mahakama iahirishwe ndio aanze kuyakusanya na hawa magereza tumsalimie hata kidogo juu kwa juu.😂😂😂😂
Watu waliokuja mahakamani badala wasilitike kwa hii kesi lakini sura zao zinaonekana zina amani na bashasha sana. Watu wamefurahia show za Mh. Lissu.
Tulikuwa tunafuatilia kesi ambayo mwisho wake mtu anaweza hukumiwa kunyongwa lakini wafuatiliaji tunaenjoy utadhani tunaangalia movie tuipendayo.
Au kama mtu aliyeshinda bingo
Nimewasikia waliokaa huko gorofani wanasema taratibu Utatoa hutoi?
Sijui wanamwambia nani maana hawakawii kuwa wanataka kumwambia Job Mrema hayo mambo.😂😂😂😂
Sasa Jaji anahangaika kuwasha kipaza sauti hapa tusikie ataahirisha kesi au watasema wanasoma ruling Leo leo.
Maana hapa ni either watupe tarehe au watuambie watasoma ruling mchana wa leo.
Sidhani kama kwa ubishani hili suala litaisha leo leo lazima wapate muda wakuandika na kutafakari kama sio maelekezo kutoka juu kama yatakuwepo ingawa juzi hapa Jaji Mkuu alisema maelezo kutoka juu yasiwepo.😂😂😂
Sasa Jaji Ndunguru anaongea.
Nawashukuru sana pande zote.
Mmewasilisha mambo mengi sana toka jumatatu. Mmetoa authorities nyingi kurejea hoja zenu na kufanya uchambuzi wa vifungu nbalimbali vya sheria.
Na sisi tunahitajika kwenda kuandaa uamuzi wetu.
Tukasome na kuvipitia kwahiyo tukutane hapa siku ya Jumatatu tarehe 15/09/2025 saa tatu asubuhi kwa ajili ya ruling (uamuzi mdogo). Ahsanteni sana.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 13
Anaendelea Mhe. Lissu
Upande wa mashitaka unalazimisha kuipa mamlaka Kisutu ambayo haikuwa na hayo mamlaka, wao wanasema inayo mamlaka mimi nasema haina.
George Abdon Kilinga mahakama inasema walikubaliana.Totally wrong. It is distinguishable.
Joseph Mkenda vs Ladislaus...... tulipewa kesi hiyo nyingine....kesi inahusiana na mauziano ya ardhi na mnunuzi aliuziwa ardhi na mtu ambae sio mmiliki kwahiyo mahakama ilishughulika na jambo kama kesi ya mkataba na sio kesi ya ardhi.
Jaji alitoa Obiter dictum kwamba Jurisdiction of the court is the creature of the law.
Obiter dictum maana yake ni maneno yaziada kwenye hukumu sio yanayoamua kesi husika.
Sasa hata ingekuwa sio ibiter dictum mimi sina pingamizi mambo yaliyosemwa hapo na mimi nasema hii kesi inaunga mkono ninachosema nashukuru sana kwa wao kuniletea hii kesi.😂
Kesi ya tatu Commisioner General TRA na wenzake.
What was the issue before the Court of appeal? Whether the High Court has the jurisdiction to assume its revisionary jurisdiction. Ilifanya review ya mambo ya kodi kwenye mgogoro mwingine.
Nani atakayebisha msimamo huo baada ya kusoma aliyosoma? Mimi sibishi.
Hoja ya msingi the question of jurisdiction ambayo kisutu iliendelea na shauri ambalo haina mamlaka kulisikiliza.
Je mnatakiwa kuendelea na hilo kwa mtindo huo. You should not condon such illegality.
Na hii kesi ya Job Mrema nayo pia inaunga mkono hoja yangu ndio maana niliwashukuru kwakweli.
Kuhusu kesi ya Elias John.
Kesi hii ii ilikuwa ndio Climax ya hoja za wakili wa serikali mwandamizi alileta kwa mbwembwe sana.
Kwamba huyu mshitakiwa angejua wala asingeleta haya mambo alisema hivyo.
Hii kesi ilikuwa ni kesi ya mauaji na wakata rufaa Elias , Daniel, Dotto walikuwa convicted of murder and sentenced to hell the committal proceedings were conducted to Chato District Court where they have arrested.
In the High Court ilisema kulikuwa na makosa mengi mahakama ya Committal kule chini.
Mahakama kuu iliona hii committal haikuwa halali ikaifutilia mbali na kuamua committal ifanyike de novo. Ifanyike upya. Hiyo committal denovo haikufanyika.
Mahakama kuu ikaendelea na kesi bila committal kufanyika na mahakama kuu ikaendekea na kesi na kuwahukumu kifo washitakiwa wote wawili.
Kesi ikaenda mahakama ya rufaa mtaona majaji kuanzia ukurasa wa 6 mpaka wa 9 mahakama ya rufani inazungumzia jinsi mahakama kuu ilikosea kuendesha kesi bila committal order.
Mahakama ya rufani kwa kutumia revisionary power ikafutilia mbali proceedings za mahakama kuu na mahakama ya Chato.
Halafu mwisho kabisa mahakama kuu baada ya kuwa imefuta proceedings zote watu wamehukumiwa kifo, ikasema sasa hawa waliohukumiwa kifo waendelee kukaa gerezani meanwhile the Appellant shall remain in custody for afresh new committal.
Ndio maana wakili Job Mrema alikuwa anasema tutarudi Kisutu, tena alikuwa anasema kwa mbwembwe kabisa.
Sasa naomba niseme yafuatayo.
1. On its facts Elias Dotto case is completely distinguishable with the case at hand in other words is completely irrelevant here. Kwenye facts zake. Kesi ilisikilizwa na sentenced to death.
Mimi I'm a mere accused. Charge yangu inahusiana na mambo ya kisiasa tu je inafananaje na convicted murderers.
2. Committal ilifanyika vibaya na mahakama kuu ikaifuta na wakaendelea na kesi.
Hapa kwangu bado hamjasema kuwa committal ilikuwa ni mbovu, hoja yangu hapa ni kwamba toka jumatatu nawaambia msiendeleee na kesi hii kutokana na makosa yaliyofayika kisutu.
Sasa hizi kesi zinalinganaje?
Mfanano wake ni upi?
I'm asking the court not to follow in that trap. Msifanye kesi iliyotoka committal Court unlawful inalingajaje na hii?
Hata hii kesi is totally irrerelevant to this case.
Part 14 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 12
Anaendelea Mhe. Lissu
Tatu. Mahakama ya Rufaa kwenye kesi ya Dodoli Kapufi ilisema nini kuhusu kifungu cha 183?
Jaji Chande alisema in essence that section is deal with trial not deal with Committal. Section inayodeal na committal ni S. 261.
Nimemaliza na hiyo niendeleee na kesi yao nyingine.
Hii nayo imeletwa bure kabisa.😂
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba nishughulike na JOB MREMA.
Huyu Katuga nimemaliza nae.
Anasimama Katuga anasema kifungu cha 187 hajakisemea.
Mhe. Lissu anasema nawashukuru sana Katuga. Ngoja nije hapo.
Hicho cha 187 trial at a place where act done.
Hii section is about trial na section about committal is 262, 263 hadi 265.
Hivyo basi kama ambavyo sect. 183 ilivyo irrelevant basi hata section 187 nayo ni hivyo hivyo haihusiki hapa tunazungumzia committal. Tofautisha Committal na trial.
Sasa nirejee kwenye suala la Mashahidi. Nalo lilizunguzwa na Mrema na nimesema naanza kushughulika nae.
Suala la Mashahidi wangu kutokuandikwa. Walilizungumza.
Katuga anasema hawakuitwa na kuandikwa wanaweza kuandikwa baadae hakuna tatizo. There is no prejudice.
Wakili Mrema pia alisema Mshitakiwa alishauriwa kuwa majina ya mashahidi atakuja kuwasema mahakama kuu. That one was premature kwahiyo hamna shida.
Waheshimiwa majaji naomba niwaonyeshe jinsi ambayo hii nayo ni shida kubwa.
Mashahidi kutokuandikwa kwenye commitall proceedings.
Ipo hivi Waheshimiwa majaji, Mshitakiwa ana haki ya kutamka majina na anuani ya mashahidi wake wakati wa committal maana asipoitumia inabaki fadhila ya mahakama.
Kwenye committal nilikuwa na haki ya kusema mashahidi wangu na anuani zao. Kwenye mahakama hii ni descretion yenu sio haki yangu tena.
Mnaweza kuamua au msiamue sasa niwapeleke kwenye sheria.
Kifungu cha 264 cha CPA ndo kinatoa haki kwa mshitakiwa kutaja majina ya mashahidi wake wote.
Nikisema nina mashahidi wewe Hakimu KISWAGA huwezi sema nitawasemea mahakama kuu, unapaswa kuandika.
Hilo halikufanyika.
Mawakili wa serikali wanasema ni premature, unaweza kuita baadae, sasa hiyo baadae iko kifungu cha 281 na 314 ya CPA. (Kumbukeni CPA ni Criminal Procedure Act - Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai)
S. 281 inasema hivi msajili wa mahakama kuu ataandaa wito kwa mashahidi wote ambao orodha yao ipo. Registrar/ msajili anatoa summons/wito kwa hao uliowataja. Kinasema hivyo.
Sasa kama hujataja nini kinapaswa kufanyika ndio S. 314 inaingia hapo. Kinasema hivyo mtuhumiwa hawezi kuwa na haki ya kuita mashahidi wake ambao hawakuwa kwenye orodha yake labda mahakama ijiridhishe kuwa kuna umuhimu wa mashahidi hao kuitwa.
Sasa hii ni fadhira ya majaji haki yangu nimesema ilikuwa Kisutu.
The accused person shall not be entitled to call witness without approval au consent ya majaji sasa kuna prejudice kubwa kuliko hiyo kunyang'anywa mashahidi wangu.
Haya maneno ya kwamba naweza kuwaita baadae ni maneno ya watu wenye nia mbaya sana na mimi.
Wanasema mambo ambayo sheria haiyatambui na kuyakubali, naomba waheshimiwa majaji msikubali jambo hili.
Sasa Job Mrema alisema majaji mnapaswa mjiulize hili pingamizi kama liko sawasawa mbele ya mahakama hii.
Na alilisema jambo hili kwa mbewembwe kabisa.
George Abdon Kilinga na wenzake vs Anna na wenzake ni mashauri ambayo aliyaleta hapa.
Kwanza hii ni kesi ya mirathi ilianzia mahakama ya mwanzo, ikaenda mahakama ya wilaya ya Babati ambayo iliamua kwamba wadaaawa wataamua watumie sheria gani? Mahakama kuu rufaa ya pili sasa Madam Justice alisema parties can not by agreement confer jurisdiction to a Court.
Wadaawa hawawezi jiamulia kuipa mamlaka mahakama hii kwasababu suala la jurisdiction (mamlaka) ni suala la Jaji.
Kwenye kesi yangu sasa Mshitakiwa anasema alikuwa committed na mahakama ambayo haikuwa na mamlaka.
Part 13 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 11
Anaendelea Mhe. Lissu
Walinipa uamuzi wa kesi ya Ishengoma na wenzake sita.
Kesi ya Mahakama ya Rufani hiyo Kesi ya Donatus Ishengoma ukurasa wa 15 umecite kesi ya Mbogo niliyoitaja hapo awali.
Anasoma hiyo kesi hapa ilichosema. Maelezo marefu hapa.....
Waheshimiwa majaji nani anauwezo kuwa na ubishi na hili, Mimi sina.
Sina ubishi na superior Court can do on interference to surbodinate court.
Kifungu cha 265 hakina descretion kihivyo wanavyodhani. Its only partially decretion. Naomba nikisome hicho kifungu.
Anakisoma sasa hicho kifungu hapa.
Descretion nimeambiwa hapa kwamba ni kumpeleka mtuhumiwa gerezani. Hiyo ni 265(1).
Ukianza kusoma vifungu vingine ikitaka kuahirisha iandike sababu za hayo maahirisho.
Mamlaka haina option ya kutokuandika sababu na haina option ya kutokutoa reason hizo.
Naomba niendleee hiyo kesi ya ishengoma imeenda kwa kiwango hicho.
Naendelea na kesi zao zingine.
Waheshimiwa majaji wakili Kasuga aahhh samahani Katuga aliuliza a very rhetorical question kwamba sasa turudi kisutu?
Hili nitalijibia lamwisho.
Twende kwenye improper dating kubadilisha proceedings na kubadilisha tarehe za matukio mahakamani.
Tuliambia hiyo ni amere sleeping of the pen na tukapewa Kesi ya Baraka Mashaka Kesi ya Mahakama kuu PC Civil appeal/2023.
Hoja yangu ni kwamba kukiwa na kosa moja au mawili kwenye kurasa 101 unaweza kusema ni sleep of a pen.
Sasa ukiwa na makosa mia kwenye nyaraka hiyo hilo la kukosea tarehe haliwi kosa dogo kabisa lazima yaangaliwe kwa uzito.
They are part of the designing kwangu mimi na naomba hayo makosa ya kuteleza kwa mkono naomba yachukuliwe kuwa sio kuteleza kwa mkono yachukuliwe kama sehemu ya uchafu mwingi uliopo humu na niliousema toka siku ya kwanza.
Kwenye hiyo kesi hiyo mshitakiwa alihukumiwa maisha kwa kumfanya kinyume na maumbile mtoto lakini mahakama ikamfunga kwa kosa la armed robbery.
Mahakama ya rufaa ilisema kwa vile adhabu ni ileile kwa makosa hayo basi ni sleep if a pen.
Sasa huwezi kuleta kesi ya namna hii itumike kwenye hoja za kesi tuliyonayo leo hapa.
Kuna kitu amekisema sana Katuga kwamba malalamiko yangu ni kutaka huruma amekisema toka kisutu.
Sympathy..!! Ilianzia Kisutu imekuja hadi mahakama hii.
Pamoja na kwamba sidhani kama itaamua one way to other naomba niweke for the record kupata huruma unapoonewa sio jambo baya.
Kuomba huruma unapokuwa kwenye matatizo sio jambo baya.
Kama anadhani ukipata matatizo unahitaji huruma.
Sasa la msingi ni nini? Siwaombi Majaji chochote mtakachoamua msiamue kwa huruma. Muamue yote kwa haki na kwa mujibu wa viapo vyenu. Msinihurumie na sihitaji huruma yenu nahitaji muamue kwa haki.
Nayasema haya for the record nimeona Katuga anayarudia rudia sana.
Kuna hoja ilitolewa na Katuga na imerudiwa na Mrema kuhusu kifungu cha 183 cha CPA.
Job Mrema anasema inapaswa kusomwa na 187 pia za CPA izo zote zinazungumzia mamlaka ya mahakama.
Mahakama ya Kisutu. CPA ni sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
S. 183 inazungumzia general authority of Court in Tanzania. Kwamba mahakama yoyote ina mamlaka ya kuamrisha mtu kwenda mahakamani ndani eneo la mahakama hiyo kama mtu huyo amefanya kosa ndani ya eneo la utawala wa mahakama hiyo.
Sasa wameleta hii ili waseme kwamba uliletwa kisutu kwasababu ulifanyia kosa Dar es salaam hicho kifungu walichotaja cha 183 kinazungumzia tayari ameshashtakiwa kinaipa mamlaka amri aletwe kwenye mahakama husika.
Mimi nilikamatwa Mbinga na wakati nakamatwa sikuwa mshitakiwa.
Mimi nimekuwa mshitakiwa baada ya kupelekwa Kisutu na kusomewa mashtaka.
Sababu ya pili ni kwamba kwani nilipelekwa Kisutu kwasababu mahakama iliamua nipelekwe kisutu? Hakukuwa na order hiyo.
Kwahiyo S. 183 haiwezi ku apply kabisa.
Part 12 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 11, 2025
Jana tuliishia Part 9 so leo tunaendelea na
Part 10
Hali ya hewa ya mahakama ni nzuri na imetulia.
Askari magereza wameingia hawa wawili watatu ambao wamekuwa wakivaa haya madude usoni ingawa wengi wao siku hizi hawajifichi sura zao kama walivokuwa wanajificha wakati tupo Kisutu.
Imesikika sauti ndogo ya askari High Courtttttttttt.
Kinyonge sana ni kama jamaa hajapata breakfast.😂
Majaji wanaingia na watu wote wamesimama.
Mheshimiwa Lissu ameingia na style yake mpya anakunja ngumi na kuizungusha kwa vibe sana kama kwenye ile video mliyoiona juzi.
Majaji wanaandika andika muda huu.
Wameingia kwa tabasamu kubwa sana leo Majaji wote watatu.
Wamevaa haya magauni yao mekundu na hivi vitai vyeupe shingoni kwao.
Jaji Nduguru kiongozi wa jopo anateta jambo na Kalani wa mahakama.
Sasa Jaji anataka kuongea hapa huku anamuangalia Mh. Tundu Lissu.
Karani anaita kesi Criminal Case No. 19605/2025.
Jaji: Jamhuri Karibuni.
Katuga: Nipo na Misieh Kahima, Thawabu Issa, Harrison Lukosi, Cathbert Mbirnge hawa wote ni Mawakili wa Serikali ambao ni 6 tunaiwakilisha Jamhuri katika shauri hili na mshitakiwa yupo Mheshimiwa Jaji.
Katuga: Tunaendeela na usikilizaji wa mapingamizi na mwenzetu mshitakiwa kama yupo tayari aendeleee. Sisi hatuna shida.
Jaji: anaandika. Anamuuliza Mh. Lissu vipi uko tayari.
Mhe. Lissu: Niko tayari na imara kabisa.
Jaji: anaandika na kuteta kidogo na wenzake.
Sasa unaweza kuendelea ndugu Lissu.
Mhe. Lissu Waheshimiwa Majaji nimefurahi kuwaona na niwapongeze kwa kazi kubwa mliyofanya toka jumatatu.
Lissu anaendelea sasa.
Jana niliomba ahirisho ili nikasome kesi walizonipa hawa jamhuri naomba niseme hiyo kazi nimeifanya vizuri sana.
Niwashukuru mawakili wa serikali kuleta hizo kesi kwasababu zitanisaidia sana kuja kusema nitakachosema siku ya leo.
Ni kesi wamezileta wenyewe sio mimi.
Wakili wa serikali Katuga na Mrema walitoa hizo kesi wenyewe kwahiyo nitaonesha namna hizo kesi kama ni relevant au sio relevant kwa kesi tuliyonayo.
Kwa kuanzia naomba nizungumzie kauli ambayo ilitolewa juzi na wakili wa serikali Mkuu Katuga kwamba committal proceedings lengo lake ni kuhakikisha fair trial.
Hiyo position ipo kwenye maamuzi mengi ambayo yametajwa toka jumatatu mimi nakubaliana na msimamo huo ni kuhakikisha kuna fair trial katika kesi zinazosikilizwa mahakama kuu. Na kesi hizo ni kesi kubwa.
Kama lengo ni kuhakikisha fair trial/hearing hivyo basi committal Court is responsible to make sure the accused person is given full opportunity
Huwezi kumpa nyaraka nusunusu mtuhumiwa kwenye kesi yake, huwezi kuacha makosa mengi yote kama yaliyopo.
Ni lazima mshitakiwa apewe nafasi ya kusema maelezo yake yote. Apewe hiyo fursa na ipo hoja ya whether nilipewa fursa ya kutoa maelezo yangu kwenye committal Court (mahakama ya ukabidhi)
Mahakama ya ukabidhi ilipaswa pia kunipa nyaraka zote zilizopatikana kwenye committal processes.
Hayo yote yakitimizwa kutakuwa na fair trial na yasipotimizwa hayo hakutakuwa na fair trial kabisa.
Waheshimiwa Majaji Wakili wa Serikali Kiswaga watu wanacheka.😂😂😂
Anasema Waheshimiwa huyu Kiswaga amenikaa sana kichwani. Samahani ni Katuga.
Sasa anasema lengo la niliyosema ni kuupotosha umma na nyie majaji kwa hayo ambayo nimeyasema tangu jumatatu mimi binafsi siamini kama kuna chochote nimesema cha kuipotosha mahakama.
Nafikiri nimewezesha mahakama hii na umma kuwaleeza mambo mengi ambayo yalikuwa yamefichwa.
Katuga anasema kuhusu S. 265(1) of CPA anasema hayo mamlaka ya kuahirisha kesi na kutoa sababu za msingi za kuahirisha na kuandika sababu hizo alisema all that is descretion..
A superior court like this should not interfere that power.
Nikapewa kesi ya MBOGO and ANOTHER 1993 kwamba inaunga mkono msimamo wao huo.
Waheshimiwa majaji hiyo kesi ya Mbogo vs Shah sina library yangu ningeipata hiyo kesi yote.
Part 11 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 9
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa hoja ni je yanayozungumzwa kwenye hivyo vifungu yanazungumzia confession peke yake?
S. 263(3) of CPA inasema you may say anything that relevant to charge against you and will be written and may be used in evidence at your trial.
Sasa kwenye kifungu hiki kuna admission yoyote?
Kesi ya Dodoli Kapufi mahakama ya kabidhi hairuhusiwi kufanya maamuzi ya maswala ya kisheria 266(6)
Anasoma hapa hiki kifungu....
Anaanza kuelezea hapa kwamba Hakimu alipaswa kuandika maelezo ya Lissu kama yalivyo na sheria imeandika kabisa kuwa inampasa na kumlazimu kuandika maelezo hayo ila mahakama ya kabidhi ilizuia maelezo hayo kuandikwa.
Kwahiyo Waheshimiwa Majaji haya maneno niliotakiwa kusema yalikuwa ushahidi wangu unaopaswa kutumika kwenye mahakama hii.
Wakili Katuga anasema bila kusomewa hayo maelezo Lissu kaathirika vip?Lissu anajibu kuwa maelezo yangu ambayo ni ushahidi hayakuchukuliwa hio ilikuwa kinyume na sheria na kinyume na haki.
Anaendelea hapa anasema twende kwenye mashahidi wangu mtakumbuka mashahidi aliowataja walikuwa Rais, Waziri Mkuu, Makamu Rais.
Ukisema Shahidi yangu Yesu basi atakuuliza nipe anuani yake hiyo ndio gist ya 264 ya CPA.😂
Sio kusema sitaki kuandika.
Presidential affairs Act imesemwa jana na imerudiwa leo hii mahakama hii imeambiwa kuwa hawa wana kinga za kupewa summons za mahakama kuja kitoa ushahidi mahakamani.
Mmesomewa kifungu cha 10 jana kilitajwa cha 9 leo wamerekebisha.
Anasoma kifungu cha 10 cha Presidential Affairs Act. .....
Kwahiyo Rais hawezi pelekewa Summons ya Mahakama kwa maneno hayo niliyosema.
Sheria inasema unatakiwa umuone Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu wa Rais au Katibu Mkuu baada ya kuombwa na mahakama wa kuomba msaada wa kumserve Rais huyo Katibu wa Rais au Katibu Mkuu kiongozi watatoa utaratibu.
Sasa haya ndio yanayotoa zuio? Au wanasoma sheria kwa namna gani?
Walisema kifungu hiki kinawahusu Waziri Mkuu na Makamu wa Rais sasa katika kifungu hiki wapi wamesemwa hawa aliowataja Mrema leo?
Sasa Mheshimiwa Jaji kuna kitu hakisemwi naomba nikiseme mimi.
Sect. 9 ya sheria hiyo ya Sasa. Presidential Affairs Act.
Kinasema immunity of Arrest au kumlazimisha aje mahakamani.
Sasa mimi nimeomba Rais akamatwe? Hakuna nilipoomba.
Kifungu cha 9 kinasema kama yupo mtu atahitaji Rais awe shahidi Mahakama itamnotify Rais kuhusu nia ya mtu huyo.
The court is required to notified the President. Ana kinga ya kutokushitakiwa tu na sio kinga ya kuja kutoa ushahidi.
Mahakama inapaswa kumpelekea Katibu Mkuu kiongozi au katibu wa Rais na hao wanapaswa kuisaidia mahakama kumfikishia Rais sio kwa mujibu wa sheria kuwa jambo hilo limekatazwa. Sio kweli.
Hiyo hoja ni ya bure. 😁😁😁
Naomba sasa nijielekeze kwenda kusoma haya maamuzi waliyonipa ili tuweze kurudi kesho nije kujibu kuhusu hayo.
Jaji anasema Katuga unasemaje.
Katuga anajibu kuwa mimi sina shida. Akasomeee tukutane kesho.
Majaji wanateta hapa kidogo.
Wanaandika wakiwa wameinama chini. Tusubiri maelekezo. Kuna dalili tutakutana kesho hapa.
Jaji anasema kutokana hakuna pingamizi lolote tunaahirisha shauri hili saa tatu asubuhi kesho tutakuja kukusikiliza umalizie
Shauri limeahirishwa hadi kesho asubuhi saa tatu.
Naomba repost kwenye tweet hii.
English
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 8
Anaendelea Mhe. Lissu
Katuga jana anasema mahakama ilikuwa inapewa sababu na mahakama inaamua.
Sasa nimwambie Katuga S. 265 inasema sababu zinazohitajika ni za mahakama na sio za wakili wa serikali.
Alipaswa kutuambia mahakama ilisema nini wakati inaahirisha na sio Katuga aliiomba nini ili mahakama iahirishe.
Ni anakili kuwa mahakama haikuwa inatoa sababu ila sababu zilikuwa ni zake.
Hakuna mahakama imezifanya hizo sababu kuwa zake na kuzitoa yenyewe.
Wakili wa Serikali Mkuu, Katuga anasema utaratibu uliofanywa na Hakimu Kiswaga na yeye kuandika amri zake nje ya amri zilizotolewa na Jaji Mtembwa.
Sasa naomba niseme kwamba kuna ukiukwaji wa sheria hasa kwenye committal proceedings zinajumuisha proceedings za sect. 194 za witness protection measures.
Nilisema mtakumbuka effect ya mahakama kutoa amri ya kuficha mashahidi.
Amri ya Jaji Mtembwa hakikisheni mnaficha utambulisho wa hao mashahidi. Sasa clearly S. 194(2) cha CPA hakikuzingatiwa.
Sasa wao wamenipa nyaraka ambazo zina ninafanya niwafahamu hao mashahidi.
Kanuni ya 8 inasema endapo amri ya ulinzi imetolewa nyaraka zote zinazohusiana na amri ya ulinzi vitaambatanishwa na kupewa mtuhumiwa.
Sasa committal proceedings zilitakiwa kuendeshwa kwa mujibu wa amri ya Jaji Mtembwa na sio amri ya Franco Kiswaga PRM.
Amri ya ulinzi ya Jaji sio ya Franco Kiswaga. Ieleweke hivyo.
Waheshimiwa majaji wakili wa serikali sikuonesha sheria iliyovunjwa?
Sasa nilipaswa kuonyesha nini zaidi ya haya?
Kwa kumalizia hiyo hoja, Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu haikuwa na mamlaka yoyote once the high Court made six orders the commitall Court was duty bound to respect and act in accordance with the High Court directives.
Sasa mahakama kuu itaendeleaje kwa kutumia committal order ambayo haikuzingatia amri ya mahakama kuu.
Magistrate should not in this country have power to vary orders of superior courts.
Wakili Kiswaga sorry Wakili Katuga.
Alisema kwani kulikuwa na shida gani kwa mahakama kufunga live streaming wakati yenyewe ndio iliyotuhusu hiyo live streaming.
Kwahiyo tulipata kwa ufadhili wa mahakama na na imeondoa kwa ufadhili huo.
Rekodi ya tarehe 13 au 18 nilisema pale Kisutu kuwa wayu wa nchi hii wana haki ya kikatiba kuona kinachowahusu. Kesi ya uhaini niliwaambia juzi kuwa they come once every two generation.
Nilisema juzi kuwa kwenye katiba yetu inasema kwamba kosa kubwa kuliko yote ni kosa la uhaini.
Mahakama ya hakimu kisutu iliombwa ikakubali na yakatangazwa karibu miezi miwili.
Anaendelea Mh. Lissu Mahakama kuu haikukataza live streaming, haikukataza publication of the proceedings. Hayo hayakukatazwa.
Yaliyokatazwa nilishasema na anayataja hapa kutoka kichwani amezikalili zozote.
Sasa haya ya kisutu yalitokea wapi? Kiswaga alisema ukisema hata kwenye social media utaenda jela. Sasa wapi Mtembwa alizungumzia watu kupost kwenye mitandao.
Amri ya Kiswaga ilikuwa kinyume na sheria na kinyume na amri ya Mtembwa.
Sasa kila saaa tunasikia hilo tu, hiyo tu. Ndio tufute proceedings yote? Wanasema hivyo.
Sasa naomba tuelewane kuwa tunapaswa kuziangalia hizi irregularities that was very systematic.
If that was the case mahakama kuu haiwezi kuassume hizi records za namna hii.
Waheshimiwa Majaji naomba sasa nizungumzie yale maelelzo ya mtuhumiwa.
Wakili Kiswaga ala samahani sana. Alisema huo utaratibu wa s. 263(4)(5) ya CPA unahusika pale mtuhumiwa anapokiri kosa tu yaani admission au confession.
Kwamba baada ya kukiri asomewe hayo maneno yake ili aongeze hayo maneno ndio anasema hivyo.
Kwa vile mimi sikukiri kosa kwahiyo hakukuwa na sababu ya mimi kupewa nafasi.
Kwa maneno hayo nashukuru upande qa jamhuri wanakubali kuwa hayo masharti hayakufuatwa.
Na hayakufuatwa kwasababu sikukiri kosa.
Part 9 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 7
Anaendelea Mhe. Lissu
Hichi kinachoonekana intended to deceive me.
Sasa niendelee nafikiri hiyo hoja tumeiweka vizuri.
Wakili Kiswaga samahani Wakili Katuga.
Watu wanacheka. 😂
Nimelelewa na one among the best state attorney naomba nisamehewe.
Sio Wakili Kiswaga ni Wakili Katuga. Naomba niendelee ni rafiki zangu hawa.
Ni kama Katuga alisema unalalamika nini wakati sisi ndio tulikuombea.
Kwahiyo huna ulichonisaidia.
It was My own expozeeee🤣 nililiibua mimi sio Katuga. Asijipe umuhimu kwenye hili.
Hoja ya tatu ya Katuga juu ya maahirisho.
Naomba kuna kitu niseme kidogo kwenye forgery zipo proceedings za Tar. 13 hazijawahi kuonekana. Hazipo.
Anasimama Katuga anasema hayo ya Tar 13 hakusema.
Lissu anasema nilisema hayo na mahakama iangalie kama sikusema basi naomba niendelee na nyie angalieni huko.
Sasa nirudi kwenye maaahirisho.
Sasa kwamba sheria kuhusu adjournment haikufuatwa basi ni grievances yaani malalamiko tu na hapa sio mahala pake.
Sasa namjibu kwamba kweli I was aggrieved by the adjournment. Sikufurahishwa nayo kabisa. Hilo la kwanza.
Na my grievances zipo kufungu cha 265(1) cha CPA kinaleeza utaratibu wa kuahirisha kesi wakati wa committal.
So of course I'm aggrieved kwasababu sheria imekiukwa at my expense.
S. 265 ya CPA inasema anaisoma.
Tafsiri yake ni kwamba kila kesi inapoahirishwa wakati wa committal lazima sababu zitolewe.
Na zile kesi za akina Kapufi zilisema mahakama ya ukabidhi lazima ifuate sheria za ukabidhi.
Kwanini sheria inataka sababu za msingi ziwepo na sababu hizo ziandikwe?
Mimi naishi gerezani kwenye maximum security prison. Najua nini maana ya kuishi kule.
Nafikiri Katuga hajui labda amwambie haya maneno naona hayasemi hapa.🤣
Sasa sheria inasema labda sababu za msingi ziwepo pale unapoamua kumpeleka gerezani uwe na sababu za msingi. Na hizo sababu ziandikwe. Hiyo ni sheria inasema sio Katuga.
Katuga anakuna kinywa Kama mtu mwenye mba ule unaochoma choma hasa ukisuka nadhani hapa wadada wenzangu mnanielewa vema, nyie kaka zangu hamuwezi kuelewa hii.😂
Haya tuendelee na Mhe. Lissu
Katika mara 13 ambazo kesi iliahirishwa ni mara tatu tu ndio ilitoa sababu mara 10 walikaa kimya.
Kama nilivyoonesha kwenye rekodi ilipigiwa kelele na mawakili wangu na baadae nilipoamua kujitetea mwenyewe. Hatukuacha kupiga kelele.
Na Hakimu Kiswaga ali ignore concern zetu na hata hakuandika sababu za kuahirisha.
So I paid for those adjournments sasa anaposema sijaonesha namna gani nimeathiriwa na maahirisho hayo.
Sasa unahitaji kuwa katili kiasi gani? An innocent man as per Constitution living with condemned prisoners
Halafu anatokea mtu anasema eti ameumiaje?
Amesimama Katuga anasema hakusema kama aliathirikaje kwahiyo asiende huko.
Lissu anasema nilisema Mhe jaji siku kadhaa. Anarudia maneno aliyosema.
Jaji Ndunguru anasema hayo ni kweli ulisema.
Katuga anasema sasa jaji hakusema aliathirika vipi?
Watu wanazomea.😁😁😁😁
Jaji anasema nafikiri alisema Tundu Lissu hebu endelea.
Waheshimiwa majaji wanaoahirisha kesi na wanaotakiwa kutoa sababu ni mahakama ya kisutu na Wakili wa serikali Katuga akiwa hapa Mahakama kuu.
Haya aliyosema wakili wa serikali Katuga yalipaswa yaonekane kwneye rekodi za mahakama. Iseme mahakama yenyewe.
Hakuna mahali kwenye rekodi zinasema tunaahirisha kwasababu mtuhumiwa hayupo. Haipo.
Sasa yeye aliyokuwa anasema kuwa eti kuna siku mtuhumiwa hakuwepo. Hayo tunayapata wapi? Ukurasa wa ngapi? Hajaonesha na haipo.
Nimesema ni mara tatu tu mahakama imewahi kuahirisha kw kutoa sababu na hizo sababu haijawahi kutolewa kuwa ni mtuhumiwa hayupo kwenye hizo mara tatu.
Hili jaribio la to shift the burden with the committal Court wanataka tushare dhambi. Mimi siko tayari. Labda Katuga na Kiswaga ila mimi hapana siko tayari kushare hiyo dhambi.
Part 8 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Filipino
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 7
Jaji anasema sisi tukizonazo kama Majaji zinaonesha colum ya kwanza tar. 10/04/2025. Na anasoma waliokuwepo siku hiyo.
Upande wa utetezi pia anawasoma waliokuwepo.
Jaji anasema au tukupe kwanza ili uendeleee. ?
LISSU anakubali.
Wameenda kuzitafuta huko ili wamleteee aweze kuendelea.
Sijui kwanini walizificha.😂
Ili tuwe fair tunaomba uzipate kwanza halafu useme unazionaje.
Lissu anasema mkinipa hizo nyaraka nitahitaji dakika 30 tu nipitie na nitakuwa na cha kusema.
Anasimama KATUGA anasema busara tumpe muda wakutosha
Leo Katuga amekuwa mtetezi wa Lissu kwa mara ya kwanza. 🤣🤣🤣🤣
Eti upande wetu tunaangalia fair hearing. Watu wanacheka. 🤣🤣🤣🤣
Katunga anasema wao wanaiachia mahakama apate.
Jaji anasema hiyo nusu saa kwani kaomba nani? Si yeye wewe una shida gani?
Lissu ameulizwa amejibu anasema kwa kuwa leo Katuga ameamua kunipenda sana naomba nipewe lisaa limoja.
Jaji anauliza tukirudi saa 10 unahisi tunaweza kuendelea?
Lissu anasema niko tayari mimi labda nyie majaji mseme hamko tayari.
Jaji amesema tukupe lisaa limoja halafu turudi hapa.
Anamuuliza Katuga yeye anasemaje watu wanacheka sana. 😂😂😂
Katuga amesimama tunasubiri sijui atajibu nini?
Katuga amesimama haongei.
Watu humu mahakamani wanasema KATUGA piga simu uuloze kwamba LISSU aruhusiwe kukaa humu ndani ya mahakama ya lisaa limoja au akasomee lockup? 😂😂😂
Maana Mh. Lissu amesema akipewa hizo nyaraka azisomeee humu humu ndani na Mawakili wanaomsaidia research asiende kule lockup.
KATUGA amefikisha dakika kadhaa hajasema kitu.😂😂😂
Jaji anasema utapelekwa sehemu unayostahili na mawakili watakuja huko. Na saa 10:10 tutarudi hapa kwa pamoja.
Tukutane hapa saa 10 ndugu zangu.
Naomba Repost yako kwenye tweet.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 6
Anaendelea Mhe. Lissu
Katuga anasema kifungu cha sheria 266(1) cha CPA kwamba nyaraka nitapewa trial ikianza.
Hoja yangu ni kwamba what is a trial?
Sasa ngoja niwapeleke kwenye Black's Law Disctionary ni likitabu kubwa sana jekundu mtoto wa miaka mitano habebi. Analifungua kwa mizuka.
A trial does two things, examine evidence and adjudicate legal claims. Hiyo ndio trial.
Sasa hapa tuna àdjudicate legal claim. Hatujafika kwenye mashahidi lakini tayari tuko kwenye trial tunajadili masuala ya kisheria.
Sasa kama mahakama hii haiko kwenye trial ipo kwenye nini hapa?
Kwenye kesi zote ambazo mahakama kuu ina original jurisdiction.
Lazima zije hapa kupitia committal proceedings. Iwe ya Kisutu au ya Mbinga.
Sasa kama mahakama ya Kisutu haikuwa na mamlaka maana yake kazi yao ilikuwa ni SUFULI.
Hii ameitamka kama nilivyoandika. Kaitamka kinyaturu kabisa🤣🤣
Anaendelea kwahiyo kinachoendela hapa ni SUFULI pia.
Hatuwezi kuendelea na mambo ya SUFULI. yaani sifuli au zero.
Ndio anamaanisha hapo muelewe.🤣
S. 263 ya CPA aliyoisema Katuga sasa nakala niliyopewa ina kurasa 16 na nilipoanza kusema mambo yako tofauti ndio ikabidi nipewe rekodi za mahakama.
Sasa Katuga alikuwa ana justify anasema utaratibu tuliokuwa tunatumia siku zote ni huo.
Mambo ya practical experience kama ni kweli wamekuwa wanafanya hivyo. Basi naomba niseme huo ni uzoefu katika uvunjaji wa sheria.
Unajisifia uzoefu kuvunja sheria hoja hapa ni sheria inasema nini? Kama wao wamekuwa wanavunja sheria basi mahakama hii isiwakubalie kuendelea uzoefu huo.
Na kuna kifungu naona kama kinawatatiza sana na hawakielewi mawakili wa serikali sasa naomba nikisome ili wakielewe.
Anakisoma hapa. Mhe. Lissu nae anapiga Kingereza fulani ambacho sijui kama hawa Mapolisi angeamua kuwa anaongea nao kingereza huko Polisi wangeweza kumuhoji lolote.😁😁😁
Anaendelea hapa Mhe. Lissu.
S. 263(6) of CPA inasema nyaraka gani napaswa kupewa na mahakama ya ukabidhi na mimi sijapewa hizo nyaraka.
Practical experience itatupeleka kwenye shimo refu sana.
Katuga amehoji kwamba kuna criminality kuhusu nyaraka. Katuga anasema je hizi nyaraka ni za kughushi?
Waheshimiwa majaji naomba niseme Na nitafafanua.
Sio tu kuna ushahidi wa kughushi bali kuna conspiracy to defeat justice.
Anasimama Katuga anasema conspiracy haikuwepo asiende huko.
Lissu anasema siendi subiri sasa.
Waheshimiwa majaji sorry makaratasi yamekuwa mengi.
Kwanini nasema kuna forgery
1. Niliyopewa ina kurasa 16 na iliyopo mahakamani ni 101
2. Scanned berg pia nyaraka ya mahakama lakini ile ya karatasi 18 haikuwa na uthibitisho kuwa ni nyaraka ya mahakama na imeletwa na mahakama na ameitoa Kiswaga. Nikapewa
3. Inaanzia tar. 18 na inaishia siku hiyo hiyo. Document ya mahakama inaanzia tar. 10/04 hadi 18/08
4. Angalia ukurasa wa 1 wa nyaraka niliyoletewa gerezani haina submission kwenye page 1 lakini page ya 86 ya document ya mahakama inaonesha kulikuwa na submission page 86. Mahakama ilitoa uamuzi nyaraka inaonesha.
Aliyetengeneza hizi nyaraka alikuwa na nia gani kama sio kughushi ni nini?
Na Katuga alisema tuangalie kifungu cha 393 kuhusu forgery lengo ni kudanganya.
Hiyo nyaraka ilikuwa na lengo la kunideceive. Inawezekanaje kesi ya miezi mitano inaletwa rekodi ya siku what was the intent if it was not to deceive?
Part 7 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 5
Anaendela Mhe. Lissu
Kama ilivyowezekana if you choose where to arrest you should know which court you need to take the accused
Katuga anasema kwa busara tu ndio maana tuliletwa Kisutu kwasababu kosa lilifanyika huku.
Sasa mimi nasema Tafsiri ya masuala ya kisheria haipaswi kuwa tafsiri ya busara. Hii sio mahakama ya busara ni mahakama ya sheria. Ingekuwa mahakama ya busara msingekuwepo hapa mahakamani leo. Pengine huko mtaani wapo watu wengi wangekuwa majaji na nyie mngekosa kazi hii mliyonayo.
Ila sisemi kwamba hamna busara ila ninachosema ni kwamba nyie ni majaji kwasabbau ya sheria.
Ungekuwa ni mpira ukimuona Messi au Mpanzu anacheza mpira unaweza kuamka kesho asubuhi ukaenda kununua viatu na wewe uwe mcheza mpira.
Ndio hivyo kwenye sheria ukimsikiliza Lissu akionngea sheria unaweza kwenda kununua suti na mafile kesho na wewe uingie mtaani.
Tusomesheni watoto ndugu zangu.😁
Sasa sheria ya mamlaka za mahakimu amezitaja Katuga nashangaa zinahusiana nini na kesi hii.
Katuga ametaja kifungu cha 5 ambacho kiuhalisia kinanibeba mimi kwasababu hicho kifungu kinasema mamlaka ya hakimu kinatakiwa kuzingatiwa sheria zingine mahsusi zinazoelezea mamlaka ya mahakama.
Sasa je sheria gani inahusiana na mambo ya ukabidhi?
Yaani commitall ni MCA? HAPANA.
Ni sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai yaani CPA. Na ndio inasema nipelekwe Mbinga kusomewa sio kisutu ndio nilikokamatiwa.
Kwahiyo Katuga ameleta kifungu cha 5 cha sheria ya mamlaka za mahakimu kunaunga mkono hoja yangu nafikiri amesema mambo ambayo haelewi. Hii sheria imeandikwa kingereza sasa sijui tatizo ni nini?
Anasimama Katuga anasema Mh. Anaenda mbali sana. Section nyingine sikusema.
Mh. Lissu anasema alisema kama hakusema niambieni majaji?
Majaji wansema endelea Lissu.
Lissu anaendelea 😂
Hicho kifungu cha 41 cha MCA kinaleezea kule kwenye schedule yake sheria za ulevi, pombe mambo ya mitaro na maji machafu.
Sasa huyu Katuga analeta mambo haya kwenye hii kesi lakini hii sheria mwisho inasema mahakama hiyo ya wilaya itakuwa na mamlaka kusikiliza kesi zingine kwa mujibu wa sheria zingine.
Kwahiyo hata hii 41(1) ya MCA nayo inaunga mkono hoja yangu entirely kwamba turudi kwenye sheria za committal na sheria za commitall ndio ziansema msomeee shitaka mahali ulipomkamatia mtuhumiwa. Kanuni ni hiyo.
Ananendelea Mh. Lissu
Sasa mawakili wa serikali waliitaja kesi ya Farid Had Mohamed ambayo mimi niliiwasilisha hapa.
Ukurasa wa 9 wa kesi hii unasema s. 243 to 246 ya CPA na kwasasa tunasema ni s. 261 hadi 264 kwa sheria ya sasa.
Mahakama ya rufaa inasema hizo ndio crucial section za committal proceedings.
Sasa tuanzie 264 ambayo inatoa limitations and exceptions. Inayoweka nipaka na utaratibu wa Committal. Tumetumia miezi mitano Kisutu bila mamlaka.
Nimekalishwa gerezani miezi mitano na mahakama ambayo haina mamlaka. Ukweli ndio huo.
Sasa Waheshimiwa Majaji mahakama ya rufaa kwenye Dodoli Kapufi ilisemaje? Na pia hiyo kesi ya Hadi.
Ili mahakama kuu ipokee shauri for trial lilitokea mahakama ya ukabidhi.
Mahakama ya rufaa inasema it should be properly investigated and properly committed. It said duly committed.
Duly committed maana yake it has been committed in accordance of the legal requirement. Then, can any one serious should say kuna kesi imeletwa mahakama kuu? Hayupo.
Katuga alisema sielewi hoja ya mahakama ya kisutu imetokea wapi?
Jibu langu kwake ni Kwamba Someni sheria mtajua hoja hiyo imetokea wapi?
Usiposoma sheria utajuaje mamlaka hewa ya mahakama ya kisutu.?
Wasome sheria wasipofanya hivyo hawataelewa hoja zinatokea wapi.
Hilo naishia hapo naenda kwenye hoja nyingine
Part 6 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Filipino
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 4
Anaendelea Wakili wa Serikali Mrema
Upande wa Jamhuri tulikuwa tunajiuliza jambo moja DPP yeye ameshajiridhisha kwa mujibu wa taratibu zake kwamba nyaraka hizi zinafaa ndio kaziwasilisha.
Sasa hatuoni kama ilikuwa ni busara kama nyaraka haijawasilishwa wewe kuiomba kwa utaratibu kama huu.
Hivyo basi principle ambayo inaambatana na haya ni kwamba the burden of proof lies to the prosecution.
Sasa huwezi kumshauri mkurugenzi wa mashitaka ushahidi gani autumie dhidi yake.
Waheshimiwa Majaji mahakama hii imepiga hatua sana. Mambo ya ufundi kwamba jambo fulani limekujaje.
Tunaikaribisha mahakama hii ireje principle ya Oxygen rule ukisoma inakuonesha kwmaba hakuna shida ambayo inaenda kwenye root ya kesi ya msingi.
Mahakama hapa tunaposema oxygen rule hapa anayepewa oxygen anayepewa hiyo oxygen ni yeye.
Alishasema kuwa amechoka kukaa ndani.
Sasa kwa tunavyoendelea akifanikiwa analotaka ataenda kisutu.
Sasa yeye avute hiyo hewa kutoka mahakamani ili shauri hili lifike mwisho kwa harakal, avute hewa.
Swali ninalojiuliza hapa. Document ambayo haijakuwa imetajwa na haikusomwa pale kwenye committal Court inaweza kutumika hapa juu bila kufuata utaratibu?
Hizo affidavit hazikusomwa wala hazikutumika.
Naomba sasa tena tuirejeshe mahakama kwa kufahamu mawanda kesi ya Michael Maige vs R criminal appeal no. 222.
Ukurasa wa 11 mahakama ya rufaa iliona na kutoa mtizamo kuwa nyaraka ambayo haikutajwa kule chini haiwezi kutumika huku juu.
Sasa hata mimi sio wakili ila Job kweli haelewi anaongea vitu tofauti.
Kuitumia wataitumia wao kwahiyo hawawezi kuitumia kama haiko kwenye orodha.
Ila mtuhumiwa anachokisema yeye ni kwamba nyaraka ambazo zinamuhusu zote na zilikuwa sehemu ya kesi yake wampatie hata kama hawatazitumia yeye anaweza zitumia kujitetea, Hili nalo linahitaji uwakili wajameni?😁😁😁
Lissu anaomba nakala wanasema hawana tena.
Wanaambiwa Kimbieni mkalete, kuweni serious kidogo.
Jamaa anaondoka na joho lake hapa.😀
Mrema anasema sasa mheshimiwa jaji naomba tu kama ndio hivyo nimalizie hapa.
Katuga anasema tumemaliza sisi.
Jaji anauliza sasa Mshitakiwa unaweza kuendelea bila hizi kesi zao kukupatia. Walizoenda kutoa copy.
Mhe. Lissu anasema niko tayari kuendelea zitanikuta mbele ya safari hakuna shida. Mimi acha nianze kupiga nondo zisitucheleweshe.
Zitakapofika nitazisoma hapa hapa na kuzijibia.
Anaanza Mhe. Lissu nawashukuru Majaji kwa nafasi hii na mimi nijibu hayo majibu yao waliyotoa kwenye hoja zangu.
Nianze na huyu Katuga na nitaenda kwa mtiririko huo huo.
Suala la kwanza alisema Katuga ni suala la mamlaka ya mahakama ni suala la kisheria. Na leo kalirudia huyu mwenzake.
Jurisdiction is created by statute and it is limited by statute.
Waheshimiwa majaji hiyo principle kama nilivyosema juzi ilitokea kwenye kesi ya Farid kwamba Jurisdiction ni creature ya sheria.
S. 262 inasema apelekwe kwenye mahakama ambayo iko mahali alipokamatiwa.
Sasa kama jurisction ni suala la kisheria basi sheria yenyewe ndio hii sasa ninayoitaja kifungu cha 262 cha CPA
Sasa ukisema Kisutu ina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mtu ambae sheria inasema kwenye mashauri ya ukabidhi mtuhumiwa anapaswa kusomewa mahali alipokamatiwa.
Na hapa wasichanganye mambo wao wanafikiri tunazunguzia kesi ya wizi wa kuku. Kwneye mashauri ya committal mambo ni tofauti kidogo. Hii ni sheria wanapaswa kuelewa na sio kukalili tu vitu.
Hoja ya msingi kwenye mahakama ya ukabidhi. Hoja sio umefanyia wapi kosa hoja ya msingi mshitakiwa amekamatiwa wapi.
Ni muhimu hawa wenzetu wakaelewa tunazungumzia jambo gani? Wasipoelewa hapo watahangaika sana.
Eti Katuga anasema Mbinga hawana tuhuma zake asingeweza somewa huko Mbinga.
Sasa na mimi namjibu kama Mbinga hawakuwa na tuhuma zangu au kesi zangu kwanini walinikamata huko Mbinga. Walimkamata mtu ambae hawajui tuhuma zake?
Part 5 itaendelea post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia
Mutashobya retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 3
Anaendelea Wakili wa Serikali Mrema
Anasema lakini shauri hili la Mahakama ya Rufaa linatofautiana na kesi hii iliyopo hapa maana lenyewe mapungufu yake ilikuwa ni kwamba hakimu hakuandika maneno kuwa namcommitt mtuhumiwa kwenda high court.
Anaikataa tena kesi yake.
Anasema zinatofautiana na kesi iliyopo hapa.
Anasoma huo uamuzi wa hiyo kesi.
Anasema nilikuwa natamani kuionesha mahakama ilivyo na uwezo na kuonesha style ambayo alitakiwa kuja nayo.
Pia kuna hoja aliomba mahakama ifute proceedings arudi nyumbani akalale.
Ni kama nilimsikia hivyo.
Mahakama hii ijue mwongozo upo kwenye hii rufaa.
Na mimi naomba kwamba kama mahakama itaona kuna shida irudishe file mahakama ya chini ili jambo hilo likafanyike vizuri.
Mheshimiwa Tundu Lissu anacheka sana wakati huyu Job Mrema anazungumza.
.
Sisi wengine hatuelewi sasa sijui anacheka nini?😀
Pengine tutajua hilo akianza kumjibu baadae ila ni kama anamuona huyu mtu mbona Kama ni mjinga mjinga.😀
Sasa anaendelea Mrema, anasema yale mambo kwamba alikamatwa Mbinga na kuletwa Dar es salaam.
Ni hoja yetu kwamba shauri lile la Kapufi aliloleta Lissu lilikuwa linahusiana na nini na lake linahusiana na nini? Ni mashauri tofauti haya.
Mhe. Jaji tunaomba kuongeza kifungu cha 187 cha CPA
Ukikisoma na kutafsiri pamoja na kesi ya Kapufi utaona kesi hiyo inaunga mkono msimamo wetu.
Wakati Lissu anasema alikuwa anaonesha kuhusu zile tarehe hiyo sip fatal ni sleep of a pen.
Haiwezi kuvitiate proceedings. Hili suala la tarehe ni dogo tu.
Jamhuri tunaomba kusema makosa ya kibinadamu yapo.
Yanatokea kwa binadamu yeyote na hicho ndio tunasema sleep of a pen.
Watu wanacheka.😂😂😂
Anasema hii sleep of a pen ina madhara gani? Imetokea Kwenye kesi nyingi sio kwenye kesi hii tu.
Shauri la Baraka Mashaka vs R CRIMINAL APPEAL No. ... ukurasa wa 5 mahakama ilipima na kuona it was mere a sleep of a pen na mahakama ilisema hicho ambacho kilitokea kwenye ukrasa wa 55 ni makosa madogo hayaathiri chochote.
Kwahiyo tunaialika mahakama hii ione. Hata kama na kama tulivyosema kwenye rekodi kuonekana makosa ya tarehe hatuoni shida.
Tundu lissu hajatuambia kama rekodi zina shida kwamba hazijaandikwa ila analalamikia tarehe.
Yeye amezungumzia tarehe na nukta.
Wakati mwingine mahakama inaweza muelewa kama ni oversight tu kwake
Lakini pia amesema kuna affidavit mbili hakuwahi kupewa ambazo ni nyaraka zinatokana na Misc. Cr application no 17059/2025.
Wapo ndege hapa wameingia mahakamani sijui wametoka wapi?
Wanatupigia kelele kidogo., wanarukaruka. Wasije kutua kwenye kipara cha Mrema bure.😀😀😀
Tuendelee na Mrema
Naomba niseme kusema kuhusu 262(4) ya CPA. Uchunguzi ukifanyika na pale inabainika ushahidi unatosha baada ya kuridhika kwa mkurugenzi wa mashtaka.
Ndipo ambapo Jamhuri inaleta taarifa mahakama kuu na taarifa hiyo kwa maana ya information ikishakuwa filed mahakamani ndio mahakama ya chini nayo inajulishwa.
Kwenye kuiweka sawa hii waheshimiwa majaji information inayofiliwa mahakama kuu inaambatanishwa na nyaraka mbalimbali kama vile maelelzo ya mashahidi.
Hoja ya msingi ni kwamba anachokiomba Bwana Lissu je hizo zilikuwa sehemu ya information iliyopandishwa?
Hizo hazikuwa nyaraka huko kwenye commital sio viambatanisho.
Part 4 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
Indonesia