Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Benson Kigaila amesema chama hicho kinakwenda kupambana na Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuchukua dola.
Wajumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA iliyomaliza muda wake akiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara Benson Kigaila, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, Catherine Ruge na aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano, John Mrema ambao walitangaza kujiondoa CHADEMA kuanzia May 07,2025 hatimaye wamehamia rasmi Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) wakiwa pamoja na wengine akiwemo Devotha Minja.
Mwenyekiti wa CHAUMMA, Mzee Hashim Rungwe amewapokea Wanachama hao wapya na kuwakabidhi kadi za CHAUMMA Jijini Dar es salaam leo May 19,2025 kwenye Mkutano Mkuu wa CHAUMMA.
#MillardAyoUPDATES
Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kukubali kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi nane katika mikoa mbalimbali nchini huku majimbo 12 yakibadilishwa majina.
Akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele amesema Katika mkoa wa Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Mbeya mjini limegawanywa na kuanzishwa jipya la Uyole
Katika mkoa wa Dodoma, limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Dodoma mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba
Mkoa wa Simiyu limeanzishwa Jimbo jipya la Bariadi mjini ambapo jimbo la Bariadi limegawanywa.
Mkoa wa Geita yameanzishwa majimbo mawili ambayo ni Katoro na Chato Kusini yakigawanywa majimbo ya Busanda na Chato.
Mkoa wa Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa jipya la Itwangi.
Katika Mkoa wa Dar es salaam Majimbo
mawili yamegawanywa na kuanzishwa majimbo mapya mawili ambapo Ukonga limegawanywa na kuanzishwa jipya la kivule, na jimbo la mbagala limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Chamazi.
“Nisiwaache mkaja kuniuliza maswali kwamba sasa mnaenda Chama gani kwasababu kuna fununu nyingi sana, sisi sio Wazee wakufikia kwenye kusahau, sisi bado tuna nguvu na malengo ya kisiasa, kazi ya kuwapigania Watanzania haijakamilika tutaendelea kuwapigania Watanzania waweze kufikia mahali ambapo CHADEMA ilikuwa inalenga na tutaendelea kupambana na CCM lakini tutatafuta jukwaa mwafaka”
“CCM haiwezi kuwa option yetu, tutatafuta jukwaa mwafaka ambalo tutakwenda tukahakikishe kazi ya kupigania haki, uhuru na maendeleo ya Watu inaendelea, tunaondoka leo CHADEMA tutashauriana na Vyama mbalimbali tutawaambia baadaye tunakwenda wapi?” —— Benson Kigaila akiongea Jijini Dar es salaam leo May 07,2025
#MillardAyoUPDATES
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk Juma Homera amesema tayari amelielekeza Jeshi la Polisi kuongeza jitihada za kuwatafuta wahusika waliomshambulia kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mdude Nyagali, huku akiahidi Sh5 milioni kwa atakayesaidia kumpata kada huyo alipo akiwa
hai au amekufa.
Hata hivyo, amesema pamoja na yeye kutojua tukio hilo, kwakuwa limetokea mkoani kwake akiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ameamua kulifanyia kazi kuhakikisha haki inapatikana, huku akilaani na kusikitishwa na tukio hilo.
Mdude anadaiwa kuvamiwa na kupigwa nyumbani kwake jijini Mbeya Mei 2, 2025 na watu waliojitambulisha kuwa polisi, lakini bado haijafahamika hali ya kada huyo na wapi alipo, hivyo kuibua sintofahamu kwa wafuasi wa chama hicho.
Akizungumza leo Jumatatu, Mei 5, 2025 baada ya viongozi wa Chadema mkoani humo na Kanda ya Nyasa kufika ofisini kwake kujua hatua zilizochukuliwa, Dk Homera amesema yupo pamoja na chama hicho kuhakikisha Mdude anapatikana.
Hata hivyo, amesema kufuatia matukio hayo, anatarajia kukutana na viongozi wa kimila kujadiliana namna ya kukabiliana na sintofahamu hiyo, huku akikiri kuwa hali hiyo inawatisha akitoa matumaini kwa wananchi kuwa mkoa huo utabaki kuwa wa amani.
Serikali ya Kenya kupitia Bodi ya Kudhibiti Kamari na Leseni (BCLB) imesitisha kwa muda wa siku 30 matangazo yote ya kamari, michezo ya bahati nasibu na ushuhuda wa wateja katika vyombo vyote vya habari.
Katika taarifa yake Jumanne, BCLB imeeleza kuwa kumekuwa na ongezeko la kasi la shughuli za kamari, ambapo waendeshaji wanazidi kuonesha kamari kama njia halali ya uwekezaji na njia ya mkato ya kupata utajiri.
“Miongoni mwa mambo yanayohofisha zaidi ni kuongezeka kwa matangazo ya kamari katika kipindi cha ‘watershed’ (kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa 4 usiku), hali inayowaathiri watoto na vijana wadogo wanaoingia kwenye utegemezi wa kamari,” amesema Mwenyekiti wa BCLB, Bi. Jane Makau.
Kwa mujibu wa agizo hilo, matangazo yote ya kamari kupitia runinga, redio, mitandao ya kijamii, magazeti, mabango ya barabarani, ujumbe wa maandishi (SMS), barua pepe na matangazo kwa njia ya ‘push notifications’ yamesitishwa. Hii pia inajumuisha matangazo yanayofanywa na watu maarufu na wanamitandao maarufu (influencers).
Wakati wa kipindi hicho cha marufuku, waendeshaji wa kamari wanapaswa kuwasilisha matangazo yote kwenye Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Kenya (KFCB) ili yapitiwe na kuidhinishwa kwa cheti maalum.
BCLB imeitaka pia Bunge la Taifa kuharakisha kupitishwa kwa Muswada wa Kudhibiti Kamari ili kutoa mamlaka zaidi kwa wasimamizi wa sekta hii.
Aidha, Makau ameiomba Baraza la Vyombo vya Habari (MCK) kuweka miongozo mipya ya vipindi, baada ya kanuni za awali kutangazwa kuwa hazina nguvu ya kikatiba. Pia ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano (CAK) kuzima tovuti zote za kamari zisizosajiliwa zinazofanya kazi nchini Kenya.
Agizo hili limetolewa wiki moja tu baada ya BCLB kupinga ripoti ya vyombo vya habari iliyodai kuwa Wakenya walitumia zaidi ya Ksh.766 bilioni kwa kamari mwaka jana.
Mwenyekiti wa BCLB alitetea sekta hiyo akisema inatoa ajira kwa zaidi ya Wakenya 10,000 moja kwa moja, na zaidi ya 500,000 kwa njia isiyo ya moja kwa moja, sambamba na kusaidia miradi ya jamii kupitia uwajibikaji wa kijamii (CSR).
Kampuni ya @airtel_tanzania kuna jambo gani linaendelea kwenye namba yangu ya simu?
Kwanini polisi wamezingira kwangu wakati huo huo simu yangu haiwezi kutoka wala kuingiza calls?
Mara mbili simu yangu imerekodiwa maongezi ambayo Inaonekana imetoka kwenye source…
Kuna jambo gani mnapanga?