G.N. Sebabi
2.1K posts








Kigali, Rwanda, 19 Mei, 2026. Nimeungana na viongozi wenzangu, mashirika ya kimataifa, wawekezaji na wataalamu wa masuala ya nishati katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA). Tanzania tumepiga hatua kubwa katika uzalishaji na umeme, na sasa Dira ya Taifa inatuelekeza tufikie uzalishaji wa megawati 70,000 ifikapo mwaka 2050. Kwa muktadha huo, tunaunga mkono uendelezaji wa nishati ya nyuklia katika kuongeza kasi ya kufikia lengo hilo, ambayo pia inaendana na lengo letu la matumizi ya nishati safi na salama. Ili kufikia malengo ya uendelezaji wa nishati ya nyuklia Afrika, nimesisitiza umuhimu wa kuimarishwa ushirikiano kati ya wadau wanaohusika ili kuwezesha upatikanaji wa fedha, rasilimali watu na teknolojia. Sambamba na hayo, ni muhimu wananchi wakapewa elimu kuhusu uendelezaji nishati ya nyuklia ili wawe sehemu ya mageuzi haya.

Pleased to announce the signing of the MOU Concerning Strategic Civil Nuclear Cooperation. This signing marks an important step forward in strengthening U.S.-Rwanda cooperation on civil nuclear energy. 🇺🇸🇷🇼 #InnovatingTogether #USAinRwanda @StateACN








































