Julius Mtatiro

2.7K posts

Julius Mtatiro banner
Julius Mtatiro

Julius Mtatiro

@Julius_Mtatiro

Mere Servant at the URT|Shinyanga|Analyst|Author|Advocate|Translator| [email protected]|

Shinyanga, Tanzania Katılım Aralık 2010
1.1K Takip Edilen86.8K Takipçiler
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
10. Baada ya Mazishi yake, kwa mujibu wa taratibu za Kanisa Katoliki la Roma, Kanisa litatanza ratiba ya mchakato wa kumpata kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki Duniani, mchakato ambao kwa kawaida husubiriwa kwa hamu kubwa sana duniani.
Indonesia
1
0
2
652
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU PAPA FRANCIS Na. Julius Mtatiro 1. Kutoka kuwa Baunsa wa Klabu za usiku hadi kuongoza wakristo wakatoliki zaidi ya bilioni moja duniani -
Julius Mtatiro tweet media
Indonesia
15
0
13
3.3K
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
9. Wakati wa upapa wake, Papa Francis amekuwa muumini wa huruma, haki za kiraia na ushirikishwaji wa makundi yote katika michakato ya maisha ya mwanadamu. Atakumbukwa kwa kuchampioni utunzaji wa mazingira na kupambana na umasikini.
Indonesia
0
0
2
548
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
8. Hii ndiyo sababu, wakati anachaguliwa kuwa Papa, wachambuzi wengi walimtanabaisha kama "mtu wa kawaida", "mtu aliye karibu na watu wa kawaida", "mtu aliye karibu na wahitaji", na "mtu wa watu!", na katika Upapa wake, hayo ndiyo ameyadhihirisha.
Filipino
0
1
3
512
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
...asiyependa makuu, asiyependa maisha ghali na akichukulia kwa uzito wa kipekee kazi ya uchungaji. Mara nyingi katika maisha yale alichagua usafiri wa umma kuliko usafiri binafsi na akiishi kwenye nyumba za kawaida za maaskofu badala ya ya makazi aghali ya hadhi hiyo.
Indonesia
0
0
5
567
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
...na akaweka rekodi ya kuwa Papa wa Kwanza asiyetokea Ulaya kwa zaidi ya miaka 1,300, kwani Papa wa mwisho kutoka nje ya Ulaya alikuwa Papa Gregory III wa Syria ambaye alichaguliwa kuwa Papa mwaka 731. 7. Katika maisha yake yote, Papa Francis anafahamika kama mtu...
Filipino
0
0
1
398
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
...cha "Baba Mtakatifu", kufuatia kujiuzulu kwa Papa Benedicto wa 16 (XVI). Kuchaguliwa huko kukamfanya kuwa Papa wa Kwanza "Mjesuti" (Mwanachama wa Shirika la Yesu); akawa Papa wa kwanza kutokea Amerika Kusini (Amerika ya Ulatini);...
Indonesia
0
0
2
471
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
...Mwaka 2001 (akiwa na miaka 62), akapanda na kuwa Askofu wa Jimbo Kuu la Buenos Aires na Papa John Paulo wa II akamteua kuwa Kardinali.mwaka huo huo 2001. 6. Mwaka 2013 alichaguliwa  kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani na kwa hiyo akitumia cheo...
Filipino
0
0
2
409
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
...akiwa na miaka 36 (1973 - 1979). Sifa yake kubwa wakati huo ikiwa ni utoaji huduma na unyenyekevu, mambo ambayo baadaye yamekuja kujidhihirisha kwenye upapa wake. 5. Mwaka 1992, Papa John Paulo wa II alimteua "Papa Francis", kuwa Askofu (akiwa na miaka 56).
Indonesia
0
0
2
422
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
...(chemical technician) kabla ya kuamua kuwekeza muda wake wote katika masomo ya thiolojia ambayo yalikoleza wito wake wa upadre. 4. Mwaka 1969 alipadrishwa na kuwa Padre wa Shirika la Yesu, kisha akapanda vyeo na kuwa Mkuu wa Shirika la Yesu nchini Argentina na Uruguay
Indonesia
0
1
3
472
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
3. Kabla hajajiunga na utume wa upadre, alifanya kazi kama mtunza nyumba/mfanya usafi/mtunza mazingira na baadaye akafanya kazi kama BAUNSA (mlinzi) kwenye klabu ya usiku. Baadaye alijiunga na kufuzu taaluma ya kemikali...
Indonesia
0
0
6
757
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
ndivyo unaweza kuandika falsafa na historia ya maisha ya miaka 88 ya Papa Francis, mtu aliyeongoza Kanisa Katoliki kwa miaka 12 mfululizo na kufariki leo Jumatatu, 21 Aprili 2025 kama ilivyotangazwa na Vatican.
Indonesia
0
0
4
492
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
Zaire ikarudi Afrika vichwa vikiwa chini, wachawi na waganga na walozi wakarudi pia wakiwa na "tunguli" zao. JSM
Polski
0
0
3
278
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
Football ni mchezo wa wazi. We rudi kinyumenyumeeee...halafu mnatandikwa magoli ya kutosha. Katika kombe la dunia la mwaka 1974 lililofanyikia nchini Ujerumani, nchi ya Congo DRC (wakati huo Zaire), ilipangwa kundi moja na Scotland, Yugoslavia na Brazil.
Filipino
7
0
4
557
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
Hata hivyo rekodi hizi za kupigwa Zaire na Korea kusini zilivunjwa katika kombe la dunia la mwaka 1982 ambapo Hungary iliipiga El Salvador magoli 10 - 1 na rekodi hii ya 10 - 1 haijavunjwa mpaka leo. Mechi ya tatu Brazil ikaifunga Zaire magoli 3 - 0.
Indonesia
0
0
1
205
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
Mechi ya pili Zaire ikapigwa magoli 9 - 0 na Yugoslavia, idadi ya magoli ambayo inasemekana ililingana na kipigo cha magoli 9 - 0 ambacho Korea Kusini ilipigwa na Hungari katika kombe la dunia la mwaka 1954.
Filipino
0
0
1
147
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
Kwa hiyo Mobutu aliamini ndumba zitapelekea Zaire ifanye maajabu. Katika mechi ya kwanza, Waganga na Wachawi wa Mobutu na Zaire wakiwa wamejazana uwanjani na kila mmoja amefanya ndumba yake, Scotland ikaifunga Zaire goli 2 - 0.
Indonesia
0
0
1
162
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
Tena, wakati huo, miezi mitatu kabla ya kombe la dunia la mwaka 1974, Timu ya Taifa ya Zaire ilikuwa imeshinda Kombe la Mataifa ya Afrika (sasa likiitwa AFCON), na hata Klabu ya AS Vita ya Zaire ilikuwa imeshinda Ligi ya Mabingwa Afrika (sasa ikiitwa CAF Champions League).
Filipino
0
0
0
108
Julius Mtatiro
Julius Mtatiro@Julius_Mtatiro·
Rais wa Zaire wakati huo, Mobutu Sese Seko, akakodi ndege nzima ya wachawi wakubwa na waganga mashuhuri wa Zaire na kuwatuma Ujerumani ili kila mmoja wao afanye ndumba zake na mwisho wa siku Zaire ibebe Kombe la Dunia.
Filipino
0
0
1
104