Stans Lascko
995 posts


Kiungo wa Manchester United, Kobbie Mainoo amesaini nyongeza ya mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitano zaidi utakaombakisha mpaka Juni 2031.
Mkataba huo mpya wa mhitimu huyo wa akademi ya Man United unaenda sambamba na ongezeko la mshahara ambapo nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kulipwa kitita cha pauni 150,000 kwa wiki.
Nyota huyo raia wa England ameichezea Manchester United mechi 98 kwenye michuano yote tangu alipocheza mechi yake ya kwanza mnamo mwaka 2023.
#KitengeSports

Filipino


@mshambuliaji Huyo sio shabiki wa mpiraa,
Na haelewi maana ya mpira
Indonesia

Shabiki wa Arsenal FC kutoka Uganda, Eric Kyama, amechukua hatua za kisheria dhidi ya klabu hiyo pamoja na meneja Mikel Arteta na wachezaji wake, akilalamikia kiwango kibovu cha timu baada ya kufungwa 2-1 na AFC Bournemouth.
Anadai kulikuwa na uzembe wa kitaaluma, ukosefu wa juhudi na mipango ya kimbinu, pamoja na kukosa uadilifu wa ushindani. Pia anamlaumu Arteta kwa kushindwa kuiongoza timu vizuri.
Kyama anasisitiza kuwa mashabiki hutumia muda, hisia na fedha nyingi kuifuatilia klabu, hivyo matokeo mabaya yanawaumiza kisaikolojia na kifedha. Anapanga kuendelea na hatua za kisheria kudai fidia hadi klabu itoe maelezo na mpango wa kuboresha kiwango chake.
#KitengeSports

Indonesia































