PT

10.4K posts

PT

PT

@PaschalTemu

You can’t change people if you don’t change their environment 💭

🇺🇬 Katılım Ağustos 2022
3.6K Takip Edilen9.2K Takipçiler
PT
PT@PaschalTemu·
Utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) umefikia asilimia 81 huku ujenzi wake ukitarajiwa kukamilika Julai 2026,
PT tweet media
Indonesia
0
5
5
31
PT retweetledi
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
RAIS SAMIA ATOA PUNGUZO LA KODI KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO KUU LA KARIAKOO Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia ametoa punguzo la kodi kwa wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuwapa nafuu na kuimarisha mazingira ya biashara. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA Ashraph Abdulkarim, wafanyabiashara wa vizimba wamepatiwa punguzo la kodi la asilimia 17, huku wafanyabiashara wa biashara nyingine ikiwemo maduka wakipata punguzo la kati ya asilimia 10 hadi 16. CPA Abdulkarim ameongeza kuwa pamoja na punguzo hilo, Mhe. Rais pia ametoa msamaha wa kodi wa mwezi mmoja kwa wafanyabiashara wote wa soko hilo, kuanzia tarehe 8 Februari 2026 hadi tarehe 8 Machi 2026, tangu alipofungua rasmi Soko Kuu la Kariakoo. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, Bw. Ramadhani Kakandilo, ameishukuru Serikali kwa hatua hiyo akisema kuwa inaonesha namna inavyowajali wafanyabiashara. #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Dira Ya Samia tweet mediaDira Ya Samia tweet media
Indonesia
8
22
27
815
PT
PT@PaschalTemu·
Ujenzi wa Bwawa kubwa la Maji la Kidunda mradi wa kimkakati unaogharimu zaidi ya Sh bilioni 335 na utakuwa na uwezo wa kuzalisha hadi lita bilioni 20 za maji kwa siku na unaolenga kumaliza kabisa changamoto ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na baadhi ya maeneo ya Morogoro.
PT tweet media
Indonesia
0
5
6
54
PT
PT@PaschalTemu·
Ujenzi wa maduka 60 na vizimba 69 uliopo katika soko la Bukokwa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh milioni 577
PT tweet media
Indonesia
0
3
4
34
PT
PT@PaschalTemu·
Daraja la Mawe Karatu Kuboresha Usafiri na Uchumi wa Wananchi
PT tweet media
हिन्दी
0
2
3
72
PT
PT@PaschalTemu·
Kiwango cha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini kimefikia asilimia 88.8 mwezi Februari 2026, kikilinganishwa na wastani wa asilimia 73 mwaka 2021/22.
PT tweet mediaPT tweet media
Indonesia
0
5
6
20
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
UMEME WA GRIDI YA TAIFA KUFIKA MKOA WA RUKWA MEI 2026 Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia imejipanga kuhakikisha Mkoa wa Rukwa unaunganishwa na umeme wa gridi ya taifa ifikapo Mei 2026, kufuatia kukamilika kwa mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kV 400 kutoka mkoani Iringa. Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kuanza kunufaika na umeme wa gridi ya taifa kuanzia mwezi Mei mwaka huu (2026), hatua itakayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mkoa huo. Kupitia mradi huo wa kusafirisha umeme wa msongo wa kV 400 kutoka Iringa, Mkoa wa Rukwa utaunganishwa rasmi kwenye mfumo wa umeme wa taifa, jambo litakaloongeza uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme kwa matumizi ya majumbani, biashara na viwanda. Kwa sasa, Mkoa wa Rukwa unapata umeme kutoka nchini Zambia kupitia ushirikiano wa biashara ya umeme wa nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (SAPP), mfumo unaoruhusu nchi wanachama kuuza au kununua umeme ili kukidhi mahitaji ya wananchi wao. #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Dira Ya Samia tweet mediaDira Ya Samia tweet media
Indonesia
10
26
27
1.3K
PT
PT@PaschalTemu·
@DiraYaSamia Uwekezaji wa maana ulifanyika na sasa matunda yake yanaonekana
Indonesia
0
0
0
10
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
TANZANIA YASHIKA NAFASI YA NNE AFRIKA KWA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI Tanzania imeendelea kuimarisha nafasi yake kama moja ya vivutio vikubwa vya uwekezaji katika sekta ya madini barani Afrika, baada ya kuorodheshwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kuvutia uwekezaji duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Annual Survey of Mining Companies 2025 iliyotolewa na Taasisi ya Fraser. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania imeshika nafasi ya 34 kati ya maeneo 68 duniani yaliyotathminiwa kupitia Investment Attractiveness Index (IAI), kielezo kinachotumiwa na wawekezaji pamoja na kampuni za utafiti wa madini kuamua maeneo yenye mazingira bora ya kuwekeza katika utafiti na maendeleo ya miradi ya madini. Katika muktadha wa bara la Afrika, Tanzania imeshika nafasi ya nne kwa mvuto wa uwekezaji katika sekta ya madini, ikitanguliwa na Botswana, Morocco na Zambia. Nafasi hiyo inaonesha ushindani mkubwa wa Tanzania katika kuvutia mitaji ya kimataifa kwa ajili ya utafiti, uchimbaji na maendeleo ya rasilimali za madini. Ripoti hiyo pia inaonesha mwenendo mzuri wa kuongezeka kwa alama za Tanzania katika kigezo cha IAI. Mwaka 2025 Tanzania imepata alama 68.04, ikilinganishwa na alama 62.75 mwaka 2024 na 46.38 mwaka 2023. Ongezeko hilo linaashiria kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji pamoja na kuongezeka kwa imani ya wawekezaji wa kimataifa katika sekta ya madini nchini. #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Dira Ya Samia tweet mediaDira Ya Samia tweet media
Indonesia
10
26
24
1.3K
PT
PT@PaschalTemu·
@DiraYaSamia Serikali yenye kujali
Indonesia
0
0
0
20
PT retweetledi
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
ATCL YAWASAFIRISHA WATANZANIA WALIOKWAMA DUBAI KUREJEA NYUMBANI Kufuatia machafuko yanayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati yaliyosababisha viwanja kadhaa vya ndege kusitisha safari za ndege na hivyo kuwafanya abiria wengi kukwama, Serikali ya Tanzania imechukua hatua za haraka kwa Watanzania waliokuwa wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai wakitafuta namna ya kurejea nyumbani. Baada ya kupokea taarifa za uwepo wa Watanzania hao waliokwama, Serikali kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) iliratibu safari maalum ya ndege kwa ajili ya kuwarejesha nchini. Ndege kubwa ya ATCL aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, yenye uwezo wa kubeba abiria 262, ambayo iliondoka nchini tarehe 8 Machi 2026 majira ya saa tano usiku kuelekea Dubai. Ndege hiyo iliondoka ikiwa na abiria 113 pekee, huku safari yake ya kurejea nchini ikibeba jumla ya abiria 230 chini ya uwezo wake wa abiria 262. Abiria wengine waliotarajiwa kusafiri hawakufika uwanjani. Katika safari hiyo maalum, kipaumbele kilitolewa kwa abiria waliokuwa na tiketi za ATCL, huku nafasi zilizobaki zikitolewa pia kwa abiria wengine waliokuwa wamekwama katika uwanja wa ndege na walihitaji kurejea Tanzania. Safari hiyo ilifanyika kwa kibali maalum baada ya ATCL kuomba ruhusa ya kufanya safari ya ziada, kwa kuwa haikuwa sehemu ya ratiba ya kawaida ya safari za shirika hilo. Hatua hiyo imewezesha Watanzania waliokuwa wamekwama kurejea nyumbani salama. #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Indonesia
8
24
26
1.9K
PT
PT@PaschalTemu·
Shule 13 za msingi Wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam kuanza kutumia nishati ya umeme kupikia badala ya kuni.
PT tweet media
Indonesia
0
4
4
24
PT
PT@PaschalTemu·
Wananchi wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza wamishukuru serikali ya awamu ya sita kwa ujenzi wa daraja la Sukuma, kwani litasaidia kuimarisha shuhuli za kiuchumi, kurahisisha usafirishaji na kurahisisha huduma nyingine za kijamii.
PT tweet media
Indonesia
0
6
5
39
PT
PT@PaschalTemu·
Jumla ya vitongoji 724 vya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa vimesambaziwa umeme sawa na asilimia 89 ya vitongoji vyote wakati vilivyosalia vitakuwa vimekamilishwa nishati hiyo ifikapo mwaka 2030.
PT tweet media
Indonesia
0
5
4
27
PT
PT@PaschalTemu·
RAIS SAMIA AMUASILI MTOTO MCHANGA ALIYETELEKEZWA NZEGA Mtoto huyo aliyepewa jina la Grace Samia Suluhu, alitelekezwa mjini Nzega, mkoani Tabora, na amekabidhiwa kwa Rais Dkt. Samia na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai.
PT tweet media
Indonesia
0
3
3
54
PT
PT@PaschalTemu·
Utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa barabara ya Lusahunga – Rusumo Mkoani Kagera
PT tweet mediaPT tweet media
Indonesia
0
2
2
120
PT
PT@PaschalTemu·
Shule ya Sekondari ya Amali ya mkoa wa Rukwa imejengwa kwa gharama ya takribani Shs. Bilioni 1.6 kupitia Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
PT tweet mediaPT tweet media
Indonesia
0
2
2
16
PT
PT@PaschalTemu·
@DiraYaSamia @SuluhuSamia Dhamira ya Rais Samia iko wazi kabisa kwenye suala la mama na mtoto
Filipino
0
0
0
12
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
VITUO 36 KUTEKELEZA KITITA JUMUISHI CHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO DAR ES SALAAM Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia kupitia Wizara ya Afya imeanza utekelezaji wa Kitita Jumuishi cha Huduma za Afya ya Mama na Mtoto chenye lengo la kuimarisha ubora wa huduma za afya na kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga nchini. Mpango huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga kwa kuboresha huduma zinazotolewa katika vituo vya afya. Katika utekelezaji wa mpango huo, jumla ya vituo vya afya 36 katika Mkoa wa Dar es Salaam vimechaguliwa kuwa vituo vya mfano vitakavyoonyesha utekelezaji bora wa huduma za afya ya mama na mtoto. Aidha, mpango huo unahusisha usambazaji wa vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na utoaji wa mafunzo na mafunzo elekezi kazini kwa watoa huduma za afya ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinaendana na viwango vya kitaifa na kimataifa. Kitita hicho kinazingatia huduma muhimu zinazohusu afya ya mama na mtoto kuanzia huduma za wajawazito kabla ya kujifungua, huduma wakati wa kujifungua, huduma za watoto wachanga pamoja na huduma za mama baada ya kujifungua, hatua inayolenga kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma salama na bora kuanzia kipindi cha ujauzito hadi baada ya kujifungua. #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Dira Ya Samia tweet mediaDira Ya Samia tweet media
Indonesia
13
30
30
872
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA HUDUMA YA UMEME LINDI NA MTWARA Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia imewekeza Shilingi milioni 704 kwa ajili ya kufunga transfoma ya ziada katika Kituo cha Kupooza Umeme cha Mahumbika mkoani Lindi, hatua inayolenga kupunguza changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Kupitia uwekezaji huo, uwezo wa kituo hicho umeongezeka na kufikia takribani MVA 35, jambo litakalosaidia kuimarisha upatikanaji wa umeme na kuboresha huduma kwa wananchi pamoja na shughuli za kiuchumi katika ukanda huo. Ufungaji wa transfoma hiyo ni sehemu ya jitihada za muda mfupi za Serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara. Sambamba na hatua hizo, Serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya muda mrefu ya kuimarisha miundombinu ya umeme katika ukanda huo. Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa kusafirisha umeme kutoka Songea kupitia Tunduru hadi Masasi na hatimaye kufika Mahumbika, ambao unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Aidha, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kusafirisha umeme kutoka Mkuranga kupitia Somanga na Kilwa hadi Lindi, ambao utaunganishwa na miundombinu ya usambazaji wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara, hatua itakayosaidia kuongeza uthabiti wa huduma ya umeme katika maeneo hayo. #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Dira Ya Samia tweet mediaDira Ya Samia tweet media
Indonesia
14
33
33
1.3K
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
WANANCHI WAPONGEZA UONGOZI WA RAIS SAMIA KUPITIA PROGRAMU YA JENGA KESHO ILIYO BORA (BBT) Wananchi wamepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia kwa kuanzisha na kuendelea kutekeleza Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (Building a Better Tomorrow – BBT) kupitia Wizara ya Kilimo, inayolenga kuwahamasisha vijana na wanawake kujikita katika sekta ya kilimo. Programu hiyo inalenga kuongeza uzalishaji wa mazao na kuboresha maisha ya vijana na wanawake kwa kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kilimo biashara. Kupitia mpango huo, vijana na wanawake wanapatiwa fursa ya kupata ujuzi wa kisasa wa kilimo pamoja na matumizi ya teknolojia ili kuongeza tija katika uzalishaji. Aidha, programu ya BBT inalenga kuongeza ajira zenye staha nchini kwa kuwahamasisha vijana na wanawake kutumia kilimo kama chanzo kikuu cha kipato na maendeleo ya kiuchumi. Wananchi wameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira yanayowawezesha vijana na wanawake kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo biashara, kwa kuwapatia utaalamu wa kilimo na kuwasaidia kuongeza mavuno pamoja na kipato chao. #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Indonesia
13
28
30
966