
VIDEO:
"Tukutane Kesho", ndio kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu wakati 'akiondoka' kwenye chumba Namba 1 cha Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Jumatatu Julai 20.2026
Lissu amekuwa Mahakamani hapo leo, kwaajili ya kusikiliza shauri la Kikatiba Na. 7300/2026 lililofunguliwa na Mawakili Kulwa William Maduhu, Nashon Nkung na Paul Kisabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Mkuu wa Gereza la Ukonga, Tundu Lissu na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
Shauri hilo lililofunguliwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, vikao vyake vinasikilizwa Mahakamani hapo mbele ya jopo la Majaji watatu (3) ambao ni Amir Mruma, Dkt. Angelo Rumisha na Dkt. Evaristo Longopa
Ikumbukwe kuwa, katika shauri hilo waleta maombi ambao wamejitambulisha kuwa ni Mawakili wa Tundu Lissu aliyeko gerezani kutokana na kesi ya uhaini inayomkabili, wanadai kwamba wanakosa faragha ya kuwasiliana na mteja wao wakienda gerezani kumuona jambo ambalo linakiuka misingi ya kisheria na Kikatiba.
Indonesia






