Tarehe 28/4/25, Masheikh 2, Mohamed Hasan na Rajab Ali wamehukumiwa kunyongwa, hakuna Baraza la Kiislam
lililotoa tamko. Tarehe 30/4/25 ilitolewa taarifa ya Padri Kitima kushambuliwa, siku ya pili yake, TEC walitoa tamko na wito kwa Serikali. Tunajifunza nini kati ya pande mbili.
Mwanasiasa na Mwanaharakati mashuhuri Bw. Nyagali Mdude ametekwa na huenda ameuwawa. Wanao tuhumiwa ni watu wa Usalama.
Kwa kua tuhuma hizi ni nyingi mno na haijulikani taifa linanufaika vipi, ni vema Bunge likaunda Tume ya Uchunguzi.
Kwa dhati kabisa tunalaani tukio hili zito.
TUNALAANI MASHAMBULIZI DHIDI YA PADRI KITIMA. Ajabu Tanzania ni uwepo wa watu wanao teka, kutesa na kuuwa hata viongoz wa Dini lakini hawakamatwi. (Wanamiliki magari, silaha kubwa na ndogo). Tunajiuliza ni usalama na amani ipi vinayozungumzwa Tanzania. Taifa linaelekea wapi!
MASHEIKH WALIOKAA GEREZANI MIAKA 9 wamehukumiwa kunyongwa leo. Utawala wa Magufuli uliwapa kesi ya Ugaidi. Utawala wa Samia sasa kuwanyonga. Walio hukumiwa ni Sh. Mohammed Hassan na Sh. Rajab Ali.
Sh. Kurwa Othman ameachiwa huru.
MASHEIKH wengine bado wanasota jela.
KESI YA TUNDU LISU: WAPIGANIA HAKI:
(1) Tunalaani kuzuiwa wananchi kufika Mahakamani.
(2) Tunalaani wananchi kuzuiliwa kusikiliza kesi.
(3) Tunalaani kupigwa na kumwagwa damu ya wananchi.
Yote hayo yaliyofanywa na vyombo vya Usalama ni uvunjaji wa haki za binadamu.
VIONGOZI WA DINI tumestushwa na hatua ya serikali kumpa kesi ya uhaini kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Tundu Lisu.
Aidha kwa kua Rais aliagiza vyombo vya usalama visimkamate mtu ila baada ya kukamilisha upelekezi, WITO WETU shauri lianze na kukamilika kabla ya Oktoba 2025.
JANA MAHAKAMA KUU iliwaachia huru MASHEIKH 12, waliokaa gerezani miaka 10, kwa tuhuma ya Ugaidi.
Usalama wamewakamata, wamewarudishia shtaka na wametupwa tena gerezani.
Rais Samia alipata kusema, atakuwa MTAWALA wa HAKI.
Tunatumia fursa ya tukio hili kumkumbusha AHADI yake.
RAIS SAMIA alialikwa mashindano ya QUR’AN kama mgeni rasmi akakubali. MAKKA wakamtoa IMAMU MKUU awe pamoja naye. Fadhaa imetukuta, katikati ya mashindano alipoaga kwamba anashughuli muhimu akaondoka. Tulitaraji atakaa na IMAMU mwanzo mwisho kama anavyofanya kwa “WATUKUFU” wengine
TUNALAANI UTEKAJI wa vijana 2 Kibaha 3/2/25. Watekaji walikua na bunduki na gari Land cruiser kama Usalama. Tunasoma katika IN THE NAME OF THE PRESIDENT: “Idadi kubwa ya sera za Magufuli zinaendelea…ndani ya Chama tawala na vyombo vya Usalama”. TZ hakuna tena matumaini ya UTU.
ZANZIBAR kabla ya Mapinduzi na Muungano: Picha Na.1 Umeme mitaani (uliozalishwa na kinu cha Malindi ZNZ 1870). Na.2 Treni ya mjini (1879). ZNZ haikupata kudaiwa ilikuwa na fedha za kutosha East African Currency Board. Ilipopata Uhuru 1963, ilikua Taifa Bora. WAZANZIBARI AMKENI
HONGERA CHADEMA kwa Demokrasia na Uchaguzi Huru na wa Haki.
HONGERA Mwenyekiti mpya LISU na Makamu HECHE kwa kupata ridhaa ya wana CDM.
WITO wangu ni kupatikana UMOJA (mpya 2025) wa KAMBI YA UPINZANI. MABADILIKO YATAPATIKANA.
CDM INAELEKEA HATARINI. Tusirudie makosa tunayoyaona katika vyama vyetu. Tukihubir Demokrasia basi tuitekeleze. Tukidai katiba mpya turekebishe na za kwetu. Tukipinga ukubwa wa madaraka au muda basi tuwe mfano. Viongozi CDM zingatieni maslahi ya CDM yapo kwenye UCHAGUZI WA HAKI.
UKUMBUSHO: Marais wetu Samia na Mwinyi bila shaka mmesoma kitabu IN THE NAME OF THE PRESIDENT kinachogusa kwa kina utawala wa Magufuli. Itakua si vizuri endapo nanyi mtaandikiwa vitabu kama hivyo mtakapoondoka madarakani. Ni muhimu kudhibiti vikosi vya utekaji na mauwaji ya raia.
TUKUMBUSHANE:
*Ukisimama pamoja na dhalimu nawe unakua DHALIMU.
*Ukisaidia dhulma nawe unakua DHALIMU.
* Ukiridhia au kuridhika au kukubali au kunyamazia dhulma nawe unakua DHALIMU.
Viongozi wa Dini tujipime kwa matukio ya hapa kwetu Tanzania na yale ya Palestina.
GEREZANI: Tumetembelea Wafungwa na Mahabusu Ukonga leo. Tumewapelekea Matumizi na Dawa. Mahabusu 5 (ULATULE waliokamatwa 16) wametoa wito Rais awaachie huru kwakua serikali kwa miaka 9 imeshindwa kuthibitisha makosa yao. (Wawili kati yao wamekufa gerezani na 9 hawajulikan walipo)
MARAIS WETU chukueni hatua kuzuia mauaji dhidi ya raia. Jumanne vikosi vya serikali vimeua kijana na mzee wa miaka 75, Pemba Zanzibar. Siku tano kabla tumemzika Sh. Suleiman Ulatule (99) na kabla yake tulimzika Sh. Saidi Ulatule (79), wote wamefia mikononi mwa vyombo vya dola.
SHEIKH Ulatule umri (99) amefariki jana gerezani. Mdogowake umri (79), alifariki gerezani mwaka 2023. Hiini familia moja walikamatwa 16, mwaka 2015, 7, walipewa kesi ya kuteka kituo cha polisi na 9 hawajulikani walipo. Wamebaki 5, pamoja na MASHEIKH wengine 46 bado wako MAHABUSU.