Sabitlenmiş Tweet
MAK Mringo (PhD)
22.3K posts

MAK Mringo (PhD)
@SnrDirector
PARADIGMS
Dar es Salaam, Tanzania Katılım Ağustos 2017
5.5K Takip Edilen17.9K Takipçiler

Today’s Beautiful Hadith is about the Six Fasts
It was narrated from Abu Ayyub (RA) that the Messenger of Allah (ﷺ) said:
“Whoever fasts Ramadan then follows it with six days of Shawwal, it is as if he fasted for a lifetime.
(Sunan Ibn Majah 1716, Book 7, Hadith 79)
Ramadan may be over but while you have a habit of fasting, consider planning to do the 6 fasts of Shawwal in quick succession. Coupled with the gains of Ramadan, these will put your mind, body and soul in a state ready for the year before the next Ramadan Insha'Allah.
Have you read the farewell sermon of the Prophet (SAW)? Did you know it preaches equality, justice, economic fairness, honouring and respecting women, preserving your faith and much more. Be inspired by learning more about his last sermon in this video.
Thank you for reading and have a blessed day, say Alhamdulillah before you leave and gain some rewards! 😇
English

📖 DARSA: WAJIBU WA MUISLAMU BAADA YA RAMADHANI - Abuu Hafswah
Assalaam alaykum warahmatuLLAHI wabarakaatu
🔹 Utangulizi:-
Ndugu zangu katika Uislamu, Ramadhani imeondoka, lakini Rabb wa Ramadhani yupo hai, haondoki.
Swali si “ulifanya nini Ramadhani?” bali ni:
➡️ Umebaki na nini baada ya Ramadhani?
⸻
1. Kuendelea na ibada – kwani ibada haina msimu bali ni ya wakati wote na maisha yote.
Kisa cha Salaf
Bishr al-Hafi aliwahi kusikia watu wakisema:
“Watu fulani wanafanya ibada sana Ramadhani.”
Akasema:
“Ni watu wabaya wanaomjua Allah Ramadhani tu!
Hakika watu wema ni wale wanaomwabudu Allah mwaka mzima.”
➡️ Hii ni onyo kali:
•Usimfanye Allah kuwa wa msimu
⸻
2. Alama ya kukubaliwa Ramadhani
Kisa cha Wanazuoni
Ali ibn Abi Talib amesema:
“Jali zaidi kukubaliwa kwa amali kuliko amali yenyewe.”
Na walikuwa:
➡️ Wakiomba miezi sita Allah awakubalie Ramadhani
⸻
Mfano halisi
•Mtu aliyekuwa akiswali Taraweeh kila siku
•Lakini baada ya Ramadhani haswali hata Fajr
➡️ Huyu ana hatari kubwa
➡️ Dalili ya kuwa hakunufaika ipasavyo
⸻
3. Kufunga sita za Shawwaal
Kisa cha hamasa ya wanazuoni
Sa’id ibn Jubayr alikuwa:
•Anaharakisha kufunga Shawwaal
•Kama vile anavyoharakisha fadhila za Ramadhani
➡️ Hii inaonyesha:
•Walikuwa hawapumziki baada ya ibada
⸻
Mfano wa leo
•Mtu anasema: “Ramadhani imenichosha, napumzika kwanza”
➡️ Lakini:
👉 Sahaba walikuwa wakiongeza, si kupunguza
⸻
4. Kudumisha swala
Kisa cha Salaf
Abdullah ibn Mas’ud amesema:
“Yule anayefurahia kukutana na Allah kesho, basi alinde swala hizi tano.”
⸻
Mfano halisi unaogusa
•Ramadhani: safu ya kwanza msikitini
•Baada ya Ramadhani: haonekani kabisa
➡️ Hii ni dalili ya:
•Ibada ilikuwa ya mazingira, si ya moyo
⸻
5. Kujilinda na madhambi
Kisa chenye mafunzo makubwa
Wanazuoni wanasimulia:
Mtu alikuwa:
•Analia Ramadhani
•Anafunga
•Anaswali sana
Lakini baada ya Ramadhani:
•Alirudi kwenye maasi
Mmoja wa wanazuoni akasema:
“Alivunja alichokijenga.”
⸻
Dalili
﴿وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا﴾
➡️ Usije kuwa kama:
•Unajenga Ramadhani
•Unabomoa Shawwaal
⸻
6. Kudumisha Qur-aan
Kisa cha wanazuoni
Imam Malik:
•Alikuwa anaipa Qur-aan heshima kubwa sana
•Lakini hakuihama baada ya Ramadhani
➡️ Qur-aan kwake ilikuwa:
•Maisha, si msimu
⸻
Mfano wa leo
•Ramadhani: Juzuu kila siku
•Baada ya Ramadhani: hata aya moja hakuna
➡️ Hii ni ishara ya kushuka kwa imani
⸻
7. Kuendelea na mazingira ya kheri
Kisa
Sufyan al-Thawri amesema:
“Hakuna kitu kigumu zaidi kuliko kuirekebisha nafsi yangu, kwani hubadilika kila wakati.”
➡️ Suluhisho:
•Kuwa karibu na watu wema
⸻
Mfano halisi
•Ramadhani: anakaa na watu wa msikiti
•Baada ya Ramadhani: anarudi kwa marafiki wa maasi
➡️ Matokeo:
•Imani hushuka haraka sana
⸻
8. Istiqamah (kuendelea bila kukata tamaa)
Kisa kizito sana
Mtu alimwambia Sufyan ibn Abdullah:
“Niambie neno moja katika Uislamu sitauliza tena.”
Mtume ﷺ akasema:
“Sema: Nimemuamini Allah, kisha istiqama.” (Muslim)
➡️ Hii ndiyo siri yote:
👉 Istiqamah baada ya Ramadhani
⸻
Hitimisho
Ndugu yangu:
•Kama ulikuwa unalia Ramadhani… endelea kulia
•Kama ulikuwa unaswali… endelea kuswali.
•Kama ulikuwa unamcha Allah… usimuache
➡️ Allah wa Ramadhani ndiye Allah wa Shawwaal na miezi mingine.
⸻
اللهم لا تجعل رمضان آخر عهدنا بالطاعة، واجعلنا من الذين يستمرون على الخير بعده، وثبت قلوبنا على دينك.
⸻
📌 Maneno ya Mwisho yenye uzito
Wanazuoni wamesema:
“Usiwe miongoni mwa wale wanaomjua Allah Ramadhani tu…
Bali uwe miongoni mwa wale anaowajua Allah kila wakati.”
Ni mtumishi wenu
Abuu Hafswah Haruna Jumanne Kapama Twabuuriyyu At’tanzaanii 🇹🇿
⸻
Indonesia

KUFUNGA SIKU SITA NDANI YA MWEZI HUU WA SHAWWAL
*Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh.*
Alhamdulilah! Tumehuishwa tena salama.
Kuhusu kufunga siku sita ndani ya mwezi Shawwal, baada ya funga ya Ramadhan, na fadhila zake; imepokewa kutoka kwa Abu Ayyub (رضي الله عنه) kuwa Mtume (ﷺ) amesema:
*"Mtu aliyefunga (funga ya) Mwezi wa Ramadhan, kisha akaifuatisha na (funga) ya Siku sita ktk Mwezi wa Shawwal, huwa sawa na mtu aliyefunga mwaka mzima."* (Muslim)
*Tanbih:*_Hadith inabainisha fadhila za kufunga siku sita ktk mwezi wa Shawwal._
Allah, kwa Rahmah Zake, Atujaalie tuwe ni wenye kunufaika na Hadith hii na mafunzo yake.
*Aamyin*
Indonesia

Asalaam alaykum ya ikhiwatul-muuminuuna. Natumai kwa uwezo wa Allah mmeamka salama salmini. Leo ni mwezi 30 RAMADHAN na ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa ramadhani. Nawahimiza tuyatunze tuliyoyachuma ili yatusaidie hapa duniani na kesho akhera. In sha Allah nawatakia subhi njema na aljumaa munawwara!!!!
Indonesia

Asalaqm alaykum ya ikhiwatul-muuminuuna. Natumai kwa uwezo wa Allah mmeamka salama salmini. Leo ni mwezi 23 RAMADHANI. Tuzidisheni kumcha Allah kadri tuwezavyo na tuutumie vyema mwezi huu kiibada kwani mbora miongoni mwetu ni yule anaemcha Allah. Kwa hakika huu ndio mwezi wa mavuno kwa watakaoutumia kwa kutenda mema na kuacha mabaya. In sha Allah nawatakia subhi njema na aljumaa munawwara!!!!
Indonesia

Asalaqm alaykum ya ikhiwatul-muuminuuna. Natumai kwa uwezo wa Allah mmeamka salama salmini. Leo ni mwezi 23 RAMADHANI. Tuzidisheni kumcha Allah kadri tuwezavyo na tuutumie vyema mwezi huu kiibada kwani mbora miongoni mwetu ni yule anaemcha Allah. Kwa hakika huu ndio mwezi wa mavuno kwa watakaoutumia kwa kutenda mema na kuacha mabaya. In sha Allah nawatakia subhi njema na aljumaa munawwara!!!!
Indonesia
MAK Mringo (PhD) retweetledi

Unacho kiona Pichani sio Nyota huo ni mzigo mkubwa wa makombora ya Vishada uliotumwa Israel usiku wa kuamkia leo, swala la kilicho Tokea baada ya kufika watajua wenyewe huko.
Mpaka Sasa Marekani na Israel wapo kwenye Wimbi la Aibu kubwa ya Karne, Udhibiti Upatikanaji wa Kinacho endelea huko umeongezeka kwa Asilimia 100 sasa Yani hakuna tena hata Asilimia moja ya upatikanaji wa taarifa za mashambulizi ya Iran huko Israel.
Haina maana kwamba Israel iko salama hapana bali Wanapigwa wakiwa wamejifungia Gizani, Iran kwa Sasa imepanda Mabomu nchi nzima ya Israel, Kama mnakumbuka tangazo la serikali ya Iran hapo awali lilisema "Kama unataka kuishi, hama israil"
Basi hali ni mbaya sana Israel hakuna pakukanyaga kila sehemu kwa Sasa imepandwa bomu, hata wale Raia walio Jificha mashimo Pindi wanapo hitaji kununua chakula wakitoka tu wanakutana na milipuko isio eleweka imetokea wapi.
Ngoja nikueleze haya Makombora ya Iran yalivyo 👉mabomu ya vishada yaliyo pandwa kila sehemu ya Israel ni Mabomu makubwa ambayo hubeba mabomu madogo madogo mengi ndani yake.
Yanaporushwa kutoka kwenye ndege au kombora, hufunguka angani na kusambaza mabomu madogo madogo katika eneo kubwa.
Hizi ni Hatua zake kwa ufupi
👉Ndege au kombora hurusha bomu moja kubwa.
👉Linapofika angani juu ya eneo la lengo, hufunguka.
👉Hutawanya mabomu madogo madogo mengi sana Yani Kombora moja linaweza kutawanya Mabomu madogo madogo zaidi ya elfu 80
👉Mabomu hayo huanguka ardhini na kulipuka moja moja na mengine hujichimbia Ardhi wakimsubiri Mtu au Chombo cha usafiri Kipite eneo hilo.
Mabomu ya vishada yana madhara makubwa kwa sababu yanashambulia eneo pana.
👉 Kombora moja linaweza kuzalisha mabomu madogo madogo yenye uwezo wa kufunika eneo lote la uwanja wa mpira au hata zaidi.
Kutokana na hatari hizi, mataifa mengi yalisaini makubaliano yanayoitwa Convention on Cluster Munitions ambayo yanapiga marufuku matumizi ya mabomu haya katika nchi zilizokubaliana nayo, Iran haijawahi kuingia kwenye makubaliano hayo ndiyo maana wanayatumia ili kulipa kisasi.
Mabomu hayo yametumwa Rasmi juzi na jana usiku Nchini Israel hivo hakuna mahala salama pakukanyaga, yametumwa mabomu Zaidi ya 50 nchi nzima kwa Awamu ya kwanza, Awamu ya Pili yakatumwa Pia zaidi ya 50.
Iran itaendelea kupanda mabomu hayo kila siku mpaka Vita itakapo isha.
Piga hesabu bomu moja linapanda Vishada vyenye Nafasi ya Zaidi ya ukubwa wa uwanja wa Mpira vipi Mabomu 10 unapanda ukubwa kiasi gani na vipi wakimimina Mabomu 1000 kuna eneo litakalo kanyagika kweli?
Iran iko vitani haichaguliwi silaha ya kutumia hata Nuclear ikibidi kutumika itatumika.
Nchini Israel, wakati wa vita au mashambulizi, serikali na jeshi la Israel Defense Forces (IDF) mara nyingi huweka udhibiti wa habari Yani military censorship kukwepa Fedheha.
Ikiwa mtu👇
👉Mtu atabainika Anachapisha picha au video za maeneo yaliyopigwa,
👉Anaonesha mahali kombora limepiga.
au anatoa taarifa zinazoweza kusaidia adui kujua matokeo ya shambulio.
Mtu huyo anaweza kushtakiwa kwa kuvunja sheria za usalama wa taifa.
Adhabu zinazoweza kutolewa ni
👉 Kukamatwa na kuhojiwa
👉Faini kubwa $ 60000
👉Au Kifungo jela kinaweza kufikia miaka mitano au Zaidi kulingana na uzito wa kosa
👉Kufungwa au kufutiwa akaunti zake za mitandao ya kijamii
Sababu kuu ya sheria hizi ni kwamba video au picha zinaweza kusaidia adui kurekebisha mashambulizi yao ikiwa wataona wapi makombora yamepiga.
Unacho kiona Pichani sio Nyota huo ni mzigo mkubwa wa makombora ya Vishada uliotumwa Israel usiku wa kuamkia leo, swala la kilicho Tokea baada ya kufika watajua wenyewe huko.
Cc chotara mweusi muandishi wetu akiwa Iran 🫵🏻

Filipino

Mheshimu na kumuogopa sana mtu huyu
instagram.com/reel/DT0Ye-tDd…
Filipino

*TEMBELEA HOSPITALI,*
*Tembelea hospitali,*
- Ukauone unyonge wa mwanadamu. Ukaone jinsi miili yetu iliyojaa nguvu leo inavyoweza kudhoofika na maumivu. Hata wale waliokuwa na sauti kuu, leo wanalala vitandani wakiomba msaada wa kugeuzwa upande wa pili.
-
*Tembelea hospitali,*
- Ukaione thamani ya pumzi unayoivuta bure. Utawaona ndugu zetu wanaolipia mamilioni ya pesa ili tu mashine iwasaidie kupata hewa unayoipata wewe ukiwa umelala au unatembea. Utajifunza kuwa uhai si haki yako, bali ni neema tu.
*Tembelea hospitali,*
- Ukauone ukomo wa elimu, vyeo, na madaraka. Katika korido za wodini, hakuna profesa wala fundi, hakuna bosi wala kibarua; wote wamevalishwa mavazi yanayofanana, wakisubiri kudra za Muumba na mikono ya matabibu. Hapo ndipo utajua kuwa cheo ni dhamana, lakini afya ni utajiri mkuu.
*Tembelea hospitali,*
- Ukajifunze maana ya uvumilivu na tumaini. Ukawaone wale ambao wamekaa wodini kwa miezi, wakitabasamu kwa kila hatua ndogo ya nafuu wanayoipata. Utajifunza kuacha kulalamika kuhusu chakula usichokipenda au nguo usizozitaka, maana kuna mtu anaomba tu aweze kumeza tone la maji bila maumivu.
*Tembelea hospitali,*
- Ukauone upendo wa kweli. Utawaona ndugu wanaokesha bila kulala, wakifuta jasho na kuliwaza wagonjwa wao. Utajifunza kuwa watu ni bora kuliko vitu, na kuwa na mtu wa kukushika mkono wakati wa dhiki ni baraka isiyo na mfano.
*Tembelea hospitali,*
- Ukajikumbushe kumshukuru Mungu kwa kila kiungo chako kinachofanya kazi. Utawaona waliofungwa bandeji, waliopoteza viungo, na wale ambao akili zao zimechoka. Utatoka hapo ukiwa na moyo wa shukrani, ukijua kuwa "Mzima ana matumaini, lakini mgonjwa ana hitaji moja tu—kuwa mzima."
*Tembelea hospitali,*
- Ukakumbushwe kutumia muda wako vizuri ukiwa na nguvu. Fanya kazi kwa bidii, saidia wenye uhitaji, na hubiri amani; maana siku za giza zikija, utatamani ungekuwa umefanya mengi zaidi wakati wa nuru.
*TEMBELEA HOSPITALI,*
- Ukajifunze unyenyekevu na kumpenda jirani yako. Maisha ni kama upepo, yanapita haraka sana. Jitahidi kuacha alama ya wema kila unapopita, ili hata ukidhoofika, kumbukumbu za wema wako ziwe dawa kwa waliovunjika moyo.
*TUMWOMBE MUNGU –*
Atujaalie afya ya mwili na roho, na atupe mioyo ya huruma kwa wanaoteseka, tukiwakumbuka daima katika dua zetu.
*Mwenyezi Mungu akutunze na kukulinde na maradhi.* *A'amiyn*
Indonesia

Dua-
*_Dua ya kupiga chafya (kuchenua)_*
(1)الْحَمْدُ للَّهِ(2)يَرْحَمُكَاللَّهُ(3)يَهْدِيكُمُ اللَّهُ وَيُصْلِحُ بَالَكُم
*'Akichemua mmoja wenu aseme(1) “Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.” Mwenzake amwambie:(2) “Mwenyezi Mungu akurehemu.” Kisha naye amjibu:(3) “Akuongoze Mwenyezi Mungu, na akutengenezee mambo yako.”*
Română

*Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh*
Alhamdulillah! Tumehuishwa tena salama.
Kuhusu ubora wa mwanazuoni na fadhila za kuombewa kwake *_msamaha,_* imepokewa kutoka kwa Abu Darda (رضي الله عنه) akisema kuwa Mtume (ﷺ) amesema:
*"Mwenye kufuata njia ya kutafuta ndani yake elimu, Allah Atampitisha njia ya kuelekea Peponi. Malaika nao kwa hakika, hushusha mbawa zao kumvizia mwenye kutafuta elimu. Pia walio mbinguni na ardhini humuombea _msamaha_ mwanazuoni, mpaka samaki majini. Ubora wa mwanazuoni juu ya mfanya ibada ni kama ubora wa mwezi juu ya nyota zingine. Kwa hakika, Maulamaa wao ndio warithi wa Mitume, kwani Mitume hawakurithisha Dinari wala Dirhamu, lakini wamerithisha elimu; na mwenye kuipokea, atakuwa amepata hadhi kubwa sana."*(Imam Ahmad, Muslim, Tirmidhi, Abu Daud na Ibn Majah)
*Tanbih:* _Wanazuoni ndiyo waliopewa baraka zaidi na ndio wenye kustahiki zaidi fadhila toka kwa Mola wao Mlezi, ikiwemo kuombewa msamaha. Hawa ni warithi wa Mitume._
(Taz. Tafsir Qur'an Ibn Kathir, Juzuu ya Nane, Fatir 27-35 Juzuu ya 22, Kisw, Ibn Hazm, 2021, uk.157-158).
Allah, Kwa Rahmah Zake, Atujaalie tuwe ni wenye kunufaika na Hadith hii na mafunzo yake.
*Aamyin*
Català
MAK Mringo (PhD) retweetledi

Afya ya binadamu ina uhusiano wa moja kwa moja na chakula anachokula. Pamoja na hilo, mfumo wa afya duniani umejikita zaidi kwenye tiba ya magonjwa kwa kutumia dawa badala ya kuzuia magonjwa kupitia lishe sahihi. Hali hii imechangia kuongezeka kwa magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.
Lishe ni msingi wa afya ya mwili. Mwili hujijenga, hujirekebisha na kujilinda dhidi ya magonjwa kwa kutumia virutubisho vinavyopatikana kwenye chakula. Daktari asiye na uelewa wa kina kuhusu lishe humtibu mgonjwa kwa dawa bila kushughulikia chanzo halisi cha tatizo.
Kuwajengea madaktari elimu ya lishe kutasaidia kuzuia magonjwa kabla hayajatokea, kupunguza utegemezi wa dawa, na kuboresha maisha ya wagonjwa kwa muda mrefu. Aidha, gharama za huduma za afya zingepungua kwa kiasi kikubwa iwapo kinga ingekuwa kipaumbele kuliko tiba.
Kwa hiyo, elimu ya lishe kwa madaktari si hiari bali ni hitaji la msingi. Daktari anayeelewa lishe hutibu mwili mzima, si dalili pekee, na hilo ndilo lengo halisi la tiba.
Kwa hiyo, Tanzania pia inapaswa kufikiria kwa kina kujumuisha elimu ya lishe kama sehemu ya msingi katika mafunzo ya udaktari. Hatua hii itasaidia kujenga taifa lenye afya bora, tija kazini na maendeleo endelevu.

Indonesia

*Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh*
Alhamdulillah! Tumehuishwa tena salama.
Kuhusu fadhila za kuomba msamaha, imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas (رضي الله عنه) akisema Mtume (ﷺ) amesema:
*"Mwenye kuomba msamaha, mara kwa mara, kwa Mwenyezi Mungu, basi kila penye matatizo, Mwenyezi Mungu humpatia njia ya kutoka, na kila penye dhiki Humpatia faraja, na Humruzuku pasi ya yeye mwenyewe kutazamia."*(Abu Daud)
*Tanbih:* _Hadith inabainisha fadhila za kukithirisha kuomba msamaha kwa Mola wetu Mlezi._
(Taz. Rayadh Saliheen, Uthaymeen, Juzuu 2, Kiingereza, uk. 1396)
Allah, Kwa Rehema Zake, Atujaalie tuwe ni wenye kunufaika na Hadith hii na mafunzo yake.
*Aamyin*
Català

*TEMBELEA HOSPITALI,*
*Tembelea hospitali,*
- Ukauone unyonge wa mwanadamu. Ukaone jinsi miili yetu iliyojaa nguvu leo inavyoweza kudhoofika na maumivu. Hata wale waliokuwa na sauti kuu, leo wanalala vitandani wakiomba msaada wa kugeuzwa upande wa pili.
-
*Tembelea hospitali,*
- Ukaione thamani ya pumzi unayoivuta bure. Utawaona ndugu zetu wanaolipia mamilioni ya pesa ili tu mashine iwasaidie kupata hewa unayoipata wewe ukiwa umelala au unatembea. Utajifunza kuwa uhai si haki yako, bali ni neema tu.
*Tembelea hospitali,*
- Ukauone ukomo wa elimu, vyeo, na madaraka. Katika korido za wodini, hakuna profesa wala fundi, hakuna bosi wala kibarua; wote wamevalishwa mavazi yanayofanana, wakisubiri kudra za Muumba na mikono ya matabibu. Hapo ndipo utajua kuwa cheo ni dhamana, lakini afya ni utajiri mkuu.
*Tembelea hospitali,*
- Ukajifunze maana ya uvumilivu na tumaini. Ukawaone wale ambao wamekaa wodini kwa miezi, wakitabasamu kwa kila hatua ndogo ya nafuu wanayoipata. Utajifunza kuacha kulalamika kuhusu chakula usichokipenda au nguo usizozitaka, maana kuna mtu anaomba tu aweze kumeza tone la maji bila maumivu.
*Tembelea hospitali,*
- Ukauone upendo wa kweli. Utawaona ndugu wanaokesha bila kulala, wakifuta jasho na kuliwaza wagonjwa wao. Utajifunza kuwa watu ni bora kuliko vitu, na kuwa na mtu wa kukushika mkono wakati wa dhiki ni baraka isiyo na mfano.
*Tembelea hospitali,*
- Ukajikumbushe kumshukuru Mungu kwa kila kiungo chako kinachofanya kazi. Utawaona waliofungwa bandeji, waliopoteza viungo, na wale ambao akili zao zimechoka. Utatoka hapo ukiwa na moyo wa shukrani, ukijua kuwa "Mzima ana matumaini, lakini mgonjwa ana hitaji moja tu—kuwa mzima."
*Tembelea hospitali,*
- Ukakumbushwe kutumia muda wako vizuri ukiwa na nguvu. Fanya kazi kwa bidii, saidia wenye uhitaji, na hubiri amani; maana siku za giza zikija, utatamani ungekuwa umefanya mengi zaidi wakati wa nuru.
*TEMBELEA HOSPITALI,*
- Ukajifunze unyenyekevu na kumpenda jirani yako. Maisha ni kama upepo, yanapita haraka sana. Jitahidi kuacha alama ya wema kila unapopita, ili hata ukidhoofika, kumbukumbu za wema wako ziwe dawa kwa waliovunjika moyo.
*TUMWOMBE MUNGU –*
Atujaalie afya ya mwili na roho, na atupe mioyo ya huruma kwa wanaoteseka, tukiwakumbuka daima katika dua zetu.
*Mwenyezi Mungu akutunze na kukulinde na maradhi.* *A'amiyn*
Indonesia

*KUMBUKA KUNDI LA UMRI WAKO LEO, USISAHAU KUSUDI LA MAISHA YAKO*
*Umri wa Ziada (Overtime age)*
1926 – Miaka 100
1927 – Miaka 99
1928 – Miaka 98
1929 – Miaka 97
1930 – Miaka 96
1931 – Miaka 95
1932 – Miaka 94
*Umri wa Machweo (Sunset age)*
1933 – Miaka 93
1934 – Miaka 92
1935 – Miaka 91
1936 – Miaka 90
1937 – Miaka 89
1938 – Miaka 88
1939 – Miaka 87
1940 – Miaka 86
1941 – Miaka 85
1942 – Miaka 84
1943 – Miaka 83
1944 – Miaka 82
1945 – Miaka 81
1946 – Miaka 80
1947 – Miaka 79
1948 – Miaka 78
1949 – Miaka 77
1950 – Miaka 76
1951 – Miaka 75
*Uzee (Old age)*
1952 – Miaka 74
1953 – Miaka 73
1954 – Miaka 72
1955 – Miaka 71
1956 – Miaka 70
1957 – Miaka 69
1958 – Miaka 68
1959 – Miaka 67
1960 – Miaka 66
1961 – Miaka 65
1962 – Miaka 64
1963 – Miaka 63
*Umri wa Marekebisho na Maridhiano*
1964 – Miaka 62
1965 – Miaka 61
1966 – Miaka 60
1967 – Miaka 59
1968 – Miaka 58
1969 – Miaka 57
1970 – Miaka 56
1971 – Miaka 55
1972 – Miaka 54
1973 – Miaka 53
*Umri wa Mafanikio na Utimilifu*
1974 – Miaka 52
1975 – Miaka 51
1976 – Miaka 50
1977 – Miaka 49
1978 – Miaka 48
1979 – Miaka 47
1980 – Miaka 46
1981 – Miaka 45
1982 – Miaka 44
1983 – Miaka 43
*Umri wa Kufanya Maamuzi*
1984 – Miaka 42
1985 – Miaka 41
1986 – Miaka 40
1987 – Miaka 39
1988 – Miaka 38
1989 – Miaka 37
1990 – Miaka 36
1991 – Miaka 35
1992 – Miaka 34
1993 – Miaka 33
*Umri wa Kujitoa na Dhamira*
1994 – Miaka 32
1995 – Miaka 31
1996 – Miaka 30
1997 – Miaka 29
1998 – Miaka 28
1999 – Miaka 27
2000 – Miaka 26
2001 – Miaka 25
2002 – Miaka 24
2003 – Miaka 23
*Umri wa Ujana na Masomo*
2004 – Miaka 22
2005 – Miaka 21
2006 – Miaka 20
2007 – Miaka 19
2008 – Miaka 18
2009 – Miaka 17
2010 – Miaka 16
2011 – Miaka 15
2012 – Miaka 14
2013 – Miaka 13
*Umri wa Uangalizi wa Watoto Wachanga na Wadogo*
2014 – Miaka 12
2015 – Miaka 11
2016 – Miaka 10
2017 – Miaka 9
2018 – Miaka 8
2019 – Miaka 7
2020 – Miaka 6
2021 – Miaka 5
2022 – Miaka 4
2023 – Miaka 3
2024 – Miaka 2
2025 – Mwaka 1
Epuka kujidanganya kwamba bado wewe ni kijana.
Kumbuka kila wakati kuwa muda haumsubirii mtu yeyote.
Fikiria mara mbili kuhusu umri wako. Kadri siku zinavyopita, tunakaribia mahali petu pa mwisho.
Jiulize maswali haya:
Nimefanya nini hasa kwa familia yangu, ndugu, marafiki, na Mungu tangu nilipoja duniani?
Je, bado kuna jambo ninaweza kufanya?
Basi fanya kitu sasa, kwa sababu muda unapita kwa kasi, na huenda ikawa kuchelewa.
Kila siku unapozeeka, jifanye kuwa hazina, kwa maana dunia hii ni ya kupita.
Mshukuru Bwana na endelea kusonga mbele kwa azma, bidii, maombi na uaminifu, nawe utapata uzima wa milele, yaani MBINGUNI.
*JIHADHARI NA “SIKU MOJA”*
SIKU MOJA, utastaafu kutoka utumishi wa umma na kuanza maisha ya faragha.
SIKU MOJA, mtu mwingine atakaa kwenye kiti chako na kuchukua nafasi yako.
SIKU MOJA, utafunga mlango wako, lakini hutakuwa wewe wa kuufungua.
SIKU MOJA, utaosha nguo zako nzuri, lakini hutaweza kuzivaa tena.
SIKU MOJA, chakula unachokipenda kitaandaliwa, lakini hutakuwepo kukila.
SIKU MOJA, utakula na kunywa kitu ambacho hutaweza kukitoa tena.
SIKU MOJA, wasifu wako (CV) na uzoefu wako wote hautakuwa na maana kwa mtu yeyote.
SIKU MOJA, mtu aliyekupenda zaidi hatajaribu kukukaribia.
SIKU MOJA, utawaza mambo ambayo hutaweza kuyatimiza.
SIKU MOJA, utaitwa “maiti”.
SIKU MOJA, utatengwa mahali paitwapo “kaburi”.
SIKU MOJA, vitu na watu uliowapenda sana watapita karibu nawe, lakini hutaweza kuwajali.
SIKU MOJA, utashikilia pumzi yako na hutaweza kuiachia tena.
SIKU MOJA, utasimama kama mshtakiwa mbele ya Hakimu Mkuu (MUNGU).
SIKU MOJA, nzi au mchwa watakujia, na hutaweza kuwafukuza.
SIKU MOJA, utapokea wito usioweza kuukataa.
SIKU MOJA, jina lako litaitwa, lakini hakuna atakayejibu.
SIKU MOJA, mali ulizozipenda sana zitachukuliwa na mtu mwingine.
SIKU MOJA, matendo yako duniani yatawasilishwa kwako kana kwamba ni CD.
SIKU MOJA, neno “Marehemu” litaongezwa kwenye jina lako.
SIKU MOJA, Mgawaji Mkuu atakupangia mahali panapokufaa.
SIKU MOJA, ngozi yako nzuri itarudi kwenye asili yake—mchanga/udongo.

*Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh*
Alhamdulillah! Tumehuishwa tena salama. M
Kuhusu namna Mtume (ﷺ) alivyokuwa akianza kisimamo cha usiku, huku, pamoja na mengine, akiomba msamaha na uongofu kwa Mola wake Mlezi, imepokewa kutoka kwa Aisha (رضي الله عنها) kwamba:
*"Mtume(ﷺ) alikuwa anakianza kisimamo cha usiku akitoa takbira mara kumi, na kumsifu Allah mara kumi, na anamtakasia mara kumi, na anamtaka msamaha mara kumi na anasema: _'Ewe Mola Wangu Mlezi Nisamehe mimi, Niongoze, Niruzuku na Unipe uzima'_ (Allahmma ghfir liy Wa-Ahdiniy War-zuqniy Wa-Afini). Kisha, baada ya hapo anajilinda kwa Allah na _dhiki ya kisimamo cha Siku ya Kiyama._"*(Abu Daud, An-Nasai, na Ivn Majah)
*Tanbih:* _Hadith inatupa muongozo wa kile ambacho waumini hawanabudi kukifanya kupata hifadhi ya Mola wetu tokana na dhiki ya kisimamo cha Siku hiyo ya Kiyama.Na ktk vitu hivyo, Msamaha ni moja wapo ya vitu vya kuazimia kumuomba Mola wetu Mlezi. Hadith hii imetumiwa na Ibn Kathir akisherehesha *Qur'an 83:6: 'Siku watakapo simama watu kwa Mola Mlezi wa Ulimwengu wote."*_
(Taz. Tafsir Qur'an Ibn Kathir, Juzuu ya Kumi, Al- Mutaffifin 1-17 Juzuu ya 30, Kisw, Ibn Hazm, 2021, uk.439 - 441).
Allah, Kwa Rahmah Zake, Atujaalie tuwe ni wenye kunufaika na Hadith hii na mafunzo yake.
*Aamyin*

TUSOME QURAN *-SURAT AL BAQARAH*
Aya zifuatazo;-
275 - Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.
276 - Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya na afanyae dhambi.
277 - Hakika wale walio amini na wakatenda mema na wakashika Sala na wakatoa Zaka, wao watapata ujira wao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.
278 - Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini.
279 - Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.
280 - Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkiifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua.
281 - Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi italipwa ilicho chuma. Nao hawatadhulumiwa.
282 - Enyi mlio amini! Mnapo kopeshana deni kwa muda ulio wekwa, basi andikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika. Aandike kama alivyo mfunza Mwenyezi Mungu. Na mwenye deni juu yake aandikishe; naye amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala asipunguze chochote ndani yake. Na akiwa mwenye kudaiwa ni mtu aliye pumbaa au mnyonge au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe mlinzi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika mnao waridhia kuwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine. Na mashahidi wasikatae waitwapo. Wala msipuuze kuliandika deni likiwa dogo au kubwa mpaka muda wake. Hayo ndiyo haki zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwa ushahidi, na vyema zaidi ili msiwe na shaka. Ila ikiwa ni biashara ya mkono-kwa-mkono baina yenu, basi hapo si vibaya kwenu msipo iandika. Lakini mnapo uziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hivyo basi hakika hilo ni kosa kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anakufundisheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Indonesia
MAK Mringo (PhD) retweetledi

*Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh*
Kuhusu mja, moyo wake na nafsi yake na namna ya kujihami na kujitakasa dhidi ya maovu, imepokewa kutoka kwa Zayd bin Arqam (رضي الله عنه) akisema, Mtume (ﷺ), alikuwa akiomba kwa kusema na akiwafundisha kuomba kwa kusema:
*"Ewe Mola wangu hakika mimi najilinda Kwako kutokana na kushindwa na uvivu, na ukongwe na uwoga, na ubahili na adhabu ya kaburi; Ewe Mola wangu ipe nafsi yangu uchaji wake, na Wewe Ndiye Mbora wa mwenye kuitakasa, Wewe Ndiye Msimamizi wake na Mtawala Wake; _Ewe Mola wangu najilinda Kwako na moyo usionyenyekea_ na nafsi isiyotosheka na elimu isiyo na manufaa na maombi yasiyojibiwa. "*(Imam Ahmad)
*Tanbih:*_Tunapata dua nyingine ya kumuomba Mola wetu Mlezi kulinda nyoyo na nafsi zetu.Tunapata pia somo la Sunna ya kufundisha dua hiyo._
(Taz. Tafsir Qur'an Ibn Kathir, Juzuu ya 7, Ash-Shams 1-15, Kisw, Ibn Hazm, 2021, uk.559).
Allah, Kwa Rahmah Zake, Atujaalie tuwe ni wenye kunufaika na Hadith hii na mafunzo yake.
*Aamyin*


