Tanzania Plus Tv

12 posts

Tanzania Plus Tv banner
Tanzania Plus Tv

Tanzania Plus Tv

@TanzaniaPlusTv

Zaidi ya Habari, Tunajenga Taifa

Texas, USA Katılım Nisan 2026
3 Takip Edilen33 Takipçiler
Tanzania Plus Tv
Tanzania Plus Tv@TanzaniaPlusTv·
Mwanahabari wa Nigeria Atengeneza Filamu Kuhusu Vurugu za Uchaguzi Tanzania Mwanahabari mchunguzi kutoka Nigeria, @DavidHundeyin, ametangaza kutengeneza filamu maalum ya uchunguzi kuhusu vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na Graphic Online, filamu hiyo inaitwa What Happened on October 29? na inalenga kueleza kile mwandishi huyo anachodai kuwa ni ukweli uliojificha nyuma ya matukio ya vurugu yaliyotikisa Tanzania baada ya uchaguzi huo. Hundeyin alisema amefanya uchunguzi wa muda mrefu uliodumu kwa miezi kadhaa, ukihusisha mahojiano na mashahidi, uchambuzi wa taarifa mbalimbali za vyombo vya habari pamoja na kupitia ripoti ya tume ya uchunguzi iliyoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman. Akizungumza kuhusu filamu hiyo, Hundeyin alisema: “Kilichotokea Tanzania tarehe 29 Oktoba 2025 si kile ambacho dunia iliambiwa.” Alidai kuwa simulizi nyingi zilizosambazwa kimataifa kuhusu vurugu hizo hazikuonesha picha kamili ya tukio hilo. Kwa mujibu wake, vurugu hizo zilikuwa zimepangwa na kuratibiwa mapema, zikihusisha watu wa ndani pamoja na nguvu kutoka nje ya nchi. “Filamu hii ni jaribio la kuwasilisha mtazamo wa Kiafrika kuhusu simulizi la Kiafrika,” alisema Hundeyin. Kupitia ukurasa wake wa X (Twitter), Hundeyin pia alitangaza ratiba ya uzinduzi wa filamu hiyo katika miji mbalimbali barani Afrika kabla ya kutolewa rasmi mtandaoni. Katika ujumbe wake aliandika: “Filamu hiyo itaanza kuonyeshwa rasmi Mei 26 mjini Accra, Mei 29 mjini Dar es Salaam na Mei 31 mjini Nairobi kabla ya kutolewa rasmi duniani kupitia YouTube Juni 1.” Hata hivyo, matukio ya uchaguzi wa Tanzania wa 2025 bado yanaendelea kuzua mjadala mkubwa kimataifa. Wakati baadhi ya ripoti zilidai kuwa kulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu dhidi ya waandamanaji na ukiukwaji wa haki za binadamu, upande mwingine ulidai kuwa baadhi ya taarifa na picha zilizosambazwa mtandaoni zilikuwa za kupotosha au zilizotengenezwa kwa teknolojia ya AI.
Indonesia
11
16
31
5.4K
Tanzania Plus Tv
Tanzania Plus Tv@TanzaniaPlusTv·
Tanzania imeendelea kung’ara kwenye ramani ya soka la vijana barani Afrika baada ya timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, kufuzu kwa mara ya kwanza hatua ya nusu fainali ya michuano ya AFCON U17 kufuatia ushindi wa penalti dhidi ya Algeria. Katika mchezo wa robo fainali uliochezwa Mei 24, 2026, Serengeti Boys walionyesha uthubutu mkubwa kwa kupambana hadi dakika za mwisho kabla ya kuibuka washindi kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya sare ya mabao 3-3 ndani ya dakika 90. Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa huku Algeria wakianza kwa kasi na kupata bao la mapema, lakini vijana wa Tanzania walionyesha moyo wa kupambana na kurejea mara kadhaa kusawazisha mchezo huo uliokuwa na presha kubwa. Mashabiki wengi wa soka nchini wamepongeza kiwango kilichoonyeshwa na Serengeti Boys, wakieleza kuwa ni ishara ya mafanikio ya muda mrefu katika uwekezaji wa sekta ya michezo nchini. Hatua hiyo pia imeihakikishia Tanzania nafasi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika nchini Qatar mwishoni mwa mwaka huu, jambo linalozidi kuongeza heshima ya taifa katika soka la kimataifa. Wadau wa michezo wamehusisha mafanikio hayo na nguvu kubwa ya uwekezaji iliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo katika kipindi cha hivi karibuni serikali imeendelea kuboresha mazingira ya michezo, kuwekeza katika maendeleo ya vijana pamoja na kuimarisha programu za kutafuta na kukuza vipaji nchini. Kupitia mafanikio hayo, Serengeti Boys sasa wamekuwa mfano wa matumaini mapya kwa soka la Tanzania, huku macho ya Watanzania yakielekezwa katika hatua ya nusu fainali wakiamini timu hiyo inaweza kuendelea kuweka historia nyingine barani Afrika.
Indonesia
0
0
1
76
Tanzania Plus Tv
Tanzania Plus Tv@TanzaniaPlusTv·
DODOMA, Mei 24, 2026 — Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bi. Brenda Rupia, amesema kuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanahusika na mauaji. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Dodoma leo Mei 24, 2026, Bi. Rupia alisema kuwa “CCM ni chama cha viongozi wauaji.” Kauli hiyo ilitolewa mbele ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa hadhara ulioandaliwa na CHADEMA mjini humo.
Indonesia
0
0
0
39
Tanzania Plus Tv
Tanzania Plus Tv@TanzaniaPlusTv·
“TUAMKE!” — Waziri Mkuu Mwigulu Aonya Njama za Kuligawa Taifa WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, amesema kuna njama maalum zinazolenga kuwagombanisha Watanzania kupitia matukio mbalimbali ya utekaji, mashambulizi na vitendo vya vurugu vinavyoibuka nchini. Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mwigulu alisema wananchi wanapaswa kuwa makini na kutafakari kwa kina matukio hayo badala ya kuyachukulia kawaida. “Tunagombanishwa mno. Unakaa unasikia sister katekwa, padri katekwa, mwingine ameumizwa. Hii ni ajenda maalum, si mchezo wa kawaida,” alisema. Alidai kuwa matukio hayo yanafanywa kwa malengo ya kuzalisha chuki na migawanyiko ya kisiasa, kidini na kijamii. “Hizi ni ajenda za watu wenye akili wanaolitafuta taifa letu,” alisisitiza. Waziri Mkuu huyo alitoa mfano wa matukio ya mauaji yaliyowahi kutokea wilayani Kibiti, ambapo viongozi wa vijiji waliuawa katika mazingira ya kutatanisha. “Watu waliuawa mashambani lakini hata jembe hawakuchukua. Tulipaswa kujiuliza walikuwa wanatafuta nini,” alisema. Aidha, alikumbusha matukio ya mabomu yaliyowahi kurushwa makanisani, ikiwemo katika mji wa Arusha, akidai kuwa yalilenga kuchochea migogoro ya kidini nchini. “Bomu linaporushwa kanisani walikuwa wanatafuta nini? Walitaka ionekane kuna mzozo wa kidini,” alisema. Katika hotuba yake, Mwigulu pia alizungumzia mashambulizi dhidi ya viongozi wa kisiasa na mikutano ya hadhara, akisema matukio hayo yalikuwa sehemu ya njama za kuwagawa wananchi kwa misingi ya kisiasa na kiitikadi. Kadhalika, alisema kuna watu wanaoingia nchini wakiwa na silaha na mabomu kwa madai ya kujilinda, jambo alilosema ni tishio kwa usalama wa taifa. “Ni nchi gani watu wanaingia na mabomu wakidai wanajilinda? Hizi ni njama zinazolenga kuwafanya Watanzania wachukiane,” alisema. Aliwataka wananchi kuwa macho dhidi ya vitendo hivyo huku akivielekeza vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza umakini katika kukabiliana na wahusika. “Watanzania tuwe macho. Hizi ni njama za kutugawa. Vyombo vya ulinzi na usalama shughulikeni na waovu wa aina hiyo,” alisisitiza.
Indonesia
0
0
0
61
Tanzania Plus Tv
Tanzania Plus Tv@TanzaniaPlusTv·
CHADEMA WAFIKIRIA KWENDA PORINI KUPIGANIA MADARAKA. “Ni kama wanataka kutushawishi sisi badala ya kufanya mikutano ya hadhara kama hii tuanze kufikiria pori lipo wapi tuanze mapambano ya kuiondoa serikali madarakani,” alisema Adolph Mkono Mwenyekiti wa Jimbo la Sumbawanga Mjini
Indonesia
0
0
0
30
Tanzania Plus Tv
Tanzania Plus Tv@TanzaniaPlusTv·
CHADEMA WAKIRI KUWA VURUGU ZA OKTOBA 29 ZILILENGA MAPINDUZI “Tunachotakiwa sisi watanzania wote ni kuunganika kwa pamoja ili kuhakikisha kwamba tunaung’oa utawala wa CCM madarakani, tulijaribu kusimamia hilo kupitia uchaguzi wa Oktoba wakatupiga risasi za kutosha” alisema SUGU
Indonesia
0
0
0
34
Tanzania Plus Tv
Tanzania Plus Tv@TanzaniaPlusTv·
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Korogwe, Solo Mnamunga, amewapongeza wanachama wa chama hicho kwa kile alichodai kuwa ni utekelezaji wa ajenda ya “No Reforms, No Election” kupitia kujitokeza kwao katika machafuko na vurugu iliyofanyika Oktoba 29, 2025.
Indonesia
0
0
0
12
Tanzania Plus Tv
Tanzania Plus Tv@TanzaniaPlusTv·
UCHAMBUZI KUHUSU TAARIFA YA TUME YA RAIS YA KUCHUNGUZA GHASIA WAKATI WAUCHAGUZI WA OKTOBA MWAKA 2025.
Tanzania Plus Tv tweet mediaTanzania Plus Tv tweet mediaTanzania Plus Tv tweet mediaTanzania Plus Tv tweet media
Indonesia
1
0
0
21
Tanzania Plus Tv
Tanzania Plus Tv@TanzaniaPlusTv·
Baada ya kupita siku 116 tangu kutoa msimamo mkali wa kutoitambua Serikali, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche, ameonekana kubadili kauli na kuanza kuitambua Serikali iliyopo nchini. Hata hivyo, haijawekwa wazi iwapo mabadiliko hayo ya kauli yanaungwa mkono chama chake.
Indonesia
0
0
0
19
Tanzania Plus Tv
Tanzania Plus Tv@TanzaniaPlusTv·
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kwa waathirika wa ajali ya moto ulioteketeza jana sehemu ya Soko la Mawasiliano (Simu 2000) lililopo Sinza, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Tanzania Plus Tv tweet media
Indonesia
1
2
3
104
Tanzania Plus Tv
Tanzania Plus Tv@TanzaniaPlusTv·
DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkubwa wa Mamalishe na Babalishe kutoka kote nchini, utakaofanyika Aprili 11, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Convention Centre.
Tanzania Plus Tv tweet media
Indonesia
0
3
4
114