Kwa Nini Angela Kizigha, James Millya na Ng’waru Magembe Wanapaswa Kujiuzulu Ubunge EALA Kuepusha Kuendelea Kuvunja Mkataba wa Jumuiya
Na Maduhu William
Kwa mujibu wa ibara ya 50(1) ya Mkataba unaoanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki kila nchi mwanachama wa Jumuiya zinapashwa kuchagua wawakilishi tisa kwenda kuwa wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wa Tanzania utaratibu wa kuwapata wawakilishi hawa kwa kiasi kikubwa unafanana na ule wa kuwapata wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo vyama vya siasa kupitia michakato yake ya ndani huteua wagombea wa nafasi hizo.
Tofauti ni kwamba wawakilishi wa mwisho hupigiwa kura na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa kanuni ya 15, 16 na 17 za Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la mwaka 2025.
Kwa upande wa Tanzania wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki walichaguliwa mwaka 2022 kwa kipindi cha miaka mitano, ambapo watamaliza muda wao mwaka 2027.
Wabunge hao ni pamoja na Selema Ladislaus Gladness, James Kinyasi Millya, Ngole Khalifan Mashaka, Abdulla Hasnuu Makame, Ng’waru Jumanne Magembe, Machano Ali Machano, Angela Charles Kizigha, Ansar Kachwamba na Mohamed Juma Nadra.
Kati ya wabunge hawa tisa, watatu yaani Angela Charles Kizigha, James Kinyasi , na Dkt Ng’waru Jumanne Magembe ni wabunge wa Bunge la Tanzania. Kizigha akiwa ameteuliwa mnamo Aprili 02, 2026, huku James Kinyasi akiwa ni Mbunge wa Simanjiro na Dkt Ngwaru Jumanne Maghembe akiwa ni Mbunge wa Mwanga walioapishwa toka Novemba 2025.
Swali kubwa linalojitokeza kwa sasa ambalo ndio litakuwa kiini cha andiko langu ni: Je Tanzania inakiuka mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa wabunge wake watatu: James Millya, Ng’waru Maghembe na Anjela Kizigha kuendelea kuwa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakati huohuo wakiwa wabunge wa Bunge la Tanzania?
Ibara ya 50(1) ya Mkataba unaoanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki imeainisha kwamba kila nchi mwanachama itachagua wabunge tisa(9) wasiotokana na Bunge la nchi mwanachama kuwa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Pia ibara ya 51(2)(c) ya Mkataba huo inaeleza kuwa Mbunge atapoteza sifa za kuwa Mbunge wa Jumuiya endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa bunge la nchi mwanachama.
Kwa lugha nyingine moja ya sifa kuu na ya msingi ya Mtanzania kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ni asiwe Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii ni sifa isiyobadilika wala kuepukika.
Soma zaidi>>>thechanzo.com/2026/04/07/kwa…
The more I read about the US mission to rescue their 2nd downed airman in Iran, the more astounding it is.
Kudos to the CIA, SEAL Team 6, and all the others involved in finding their man & getting him out. And to him, for incredible guts & tenacity.
nypost.com/2026/04/05/wor…
even after life i will choose to be a woman🤣,nimekaa nimewaza swala la kumtumia mtoto wa mwingine hela na usipotuma unaachwa au kununiwa aisee🤣kwa hiki kibri totoz zingeniacha sana!!