@ali_naka Age is an existential phenomenon, nothing more nothing less. Being young doesn’t mean being wiser and vise versa, old is not nincompoop. This depiction of Ali not Naka but Moses is worrying though , physically incapable and mentally unaware of his surroundings 😂
Yeyote aliye nyuma ya haya matamko, asije akalaumu baadae madhara ya ufa anaotaka kuujenga kwa mgongo wa dini.
Waandamanaji hakuna hata sehemu moja wamenukuliwa wakieleza kuwa waliandamana kwa sababu ya dini zao.
Waislamu, wakristo hadi wapagani ni sehemu ya waandamanaji ambao risasi za polisi hazikuchagua wa kumkatisha uhai wake.
Let’s not be myopic to this extent and blindfold out eyes.
Tuangalie madai ya msingi ya waandamanaji na tujibu madai yao kwa busara kuepusha madhara mengine yanayoweza kuzuilika.
Binafsi nimemsamehe huyu mtoa hoja na naomba Mungu amguse kiupekee na ambadilishe misimamo yake kwa uponyaji wa Taifa.
Serikali haipingwi kwa dini yake kwani haina dini.
Serikali inapingwa kwa matendo yake yanayoibua chuki kwa jamii dhidi yake.
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.