A.t.h Hamisi
19 posts


Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeuruhusu uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya robo fainali na nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) 2024/2025.
Uwanja huo umeruhusiwa baada ya Ukaguzi uliofanywa na Wakaguzi wa CAF hivi karibuni.
CAF inaendelea kufuatilia kwa karibu maboresho yanayoendelea kwenye uwanja huo.
#WasafiSports

Indonesia

@CloudsMediaLive Hii serikali ya kijinga sana watu wako chini ya kifusi alfu wew unasema zoezi lisitishwe wakati watu walioko chini wana hitaji hewa uhai je ukistisha uhai utawapatia wew
Indonesia

@millardayo Kama kawaida wanateteana kwhy saiv polisi amekuwa mgonjwa wa akili tuse serekali ya tz inaajili vichaa wenda hata hakimu naye anamatatizo ya akili
Indonesia

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imetupilia mbali maombi ya upande wa Mlalamikaji aliyewasilisha pendekezo kuwa ‘Afande’ Fatma Kigondo anayeshtakiwa kuwatuma Vijana kumbaka na kumuingilia kinyume na maumbile kwa kundi Binti Mkazi wa Yombo, asomewe mashtaka popote alipo badala ya kufika Mahakamani ikidaiwa ni mgonjwa.
Wakili Aron Kishai aliyemwakilisha Wakili Peter Madeleka amesema Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Nyamburi Tungaraja amesema maombi hayo hayajakidhi vigezo vya kisheria na kwamba haoni kosa la Mshtakiwa huku akitoa nafasi ya kukata rufaa kwa Walalamikaji kama hawajaridhika na uamuzi.
“October 16,2024 tulifika hapa na Hakimu wa Mahama ya Wilaya alisema leo atatoa maamuzi ya kwamba Hakimu atoe maamuzi ya kwenda kumsomea mashtaka Afande popote alipo hata Hospitali lakini leo Hakimu ametupilia mbali maamuzi hayo akisema kifungu cha 128 hakijaonesha kosa alilolifanya Mshtakiwa”
Ikumbukwe October 16, 2024, upande wa Mlalamikaji uliwasilisha ombi hilo, ambapo Hakimu Tungaraja aliahidi kupitia sheria kabla ya kutoa maamuzi ya kusaini au kutosaini hati ya mashtaka kama ilivyoombwa.
#MillardAyoUPDATES

Indonesia

#MICHEZO: Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Italia na Real Madrid ya Hispania Antonio Cassano amesemamchezaji bora wa Dunia mara 5 raia wa Ureno Cristiano Ronaldo hajui kucheza mpira licha ya kuwa na uwezo wa kufunga mabao.
Cassano ambaye alistaafu kucheza soka 2017 pia alicheza Real Madrid kwa kwa kipindi cha miaka 2 kati ya 2006 hadi 2008 alipisha mwaka mmoja na Ronaldo ambaye pia alijiunga na Madrid mwaka 2009.
Mshambuliaji huyo pia alicheza vilabu vya Inter Milan, AC Milan, Roma na Parma. Amesema anaamini wachezaji kama Sergio Aguero, Robert Lewandowski, Zlatan Ibrahimovic, Luis Suarez na Karim Benzema ni wachezaji wazuri zaidi kuliko Ronaldo kutokana na namna wanavyocheza kwa muunganiko wengine kwenye timu.
Licha ya kuwa mchezaji bora wa Dunia mara tano Ronaldo mwenye umri wa miaka 39 anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye historia ya mchezo wa soka akiwa amefunga mabao 901.
#Michezo #HainaKuchoka #EastAfricaTv

Indonesia








