KiPe🔰 𝕏 retweetledi

Wengi mnaiangalia hii series ya The Day of The Jackal lakini hamna kitu mnafahamu kuhusu huyu mwamba.
Hapa masela wametaka kuiba idea lakini wameiweka kisasa zaidi.
Ukiiangalia hii series, Duggan kama alivyokuwa akiitwa jeshini ama Charles kama alivyokuwa akiitwa na familia yake ama Jackal kama alivyokuwa akiitwa na watu waliokuwa wakimpa kazi.
Utagundua kwamba mchizi aliamua tu ku-fake kifo chake baada ya kutoka jeshini, yaani hakutaka kabisa kujihusisha na mambo ya kijeda.
Sasa in the real life ya The Jackal himself ilikuwa inafanana kama hivi.
Kuna mzee by then alituambia sababu kubwa ya The Jackal kutafutwa sana na Marekani ni kwa sababu alitoroka jeshini, "aliwachoma" wanajeshi halafu akaamua kuanza kufanya mauaji kwa kukodiwa, yaani kama series inavyoeleza.
Sasa Jackal alikuwa anabadilisha sana sura, yaani leo yupo na sura hii, kesho yupo na nyingine, na wengine wakasema endapo ungekutana na Jackal mara mbili, ilikuwa ni lazima akuue hata kama hukumkosea.

Indonesia




















