Mechi iliyopita (dabi) kwenye Muungano Cup, mwamuzi alitoka Kenya,kwa hii trends na tutegemee mwamuzi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kutangazwa kuchezesha dabi au apewe nani wa ndani (mwamuzi) hii mechi?!!....
🚨Afrika Kusini hasa Mji wa Durban,kuna kundi kubwa la raia linasaka au kupita mtaa kwa mtaa kwa kuwatafuta wahamiaji haramu, yaani wakikukuta kuwa Mwafrika mwenzao na huna vitu muhimu vinavyokufanya ukae nchini humo kazi unayo,taifa kama la Ghana ndio limeathirika zaidi .
🚨Al Ahly baada ya Anguko lao hasa la michuano ya klabu Bingwa msimu huu,na wao wameanza maboresho,Zougrane kutoka MC Alger,Tougai kutoka Esperance pia anatajwa kunyatiwa na Ahly,hawa msimu ujao wakiwa mabingwa tutashangaa tena?!.
🚨MAFIA kuwarudisha tena Ulingoni Mfaume Mfaume na Iddy Pialali,pambano sasa rasmi kupigwa tarehe 27 ya mwezi wa Saba,kwenye tukio la USIKU WA VISASI,Pialali na Mfaume walitaka kuzichapa "kavukavu" kabla ya kutangazwa kwa Pambano hilo !!.
🚨Diarra mchezo dhidi ya TRA dakika za mwisho aliisaidia Yanga kupata alama MOJA muhimu,Kassali dhidi ya Pamba kama angeokoa lile shuti la Mwashinga pia angeisaidia Simba kupata ALAMA moja muhimu !...
🚨"VIBE" la TRA baada ya mechi ghafla imeleta marudio ya mafikirio mechi ya Dodoma na Simba pale Jamhuri,kuna matukio ya kupoteza muda yalikuwa na mfanano na hata TRA walivyouapproach mchezo wenyewe! Ni alama za maumivu kwa Wananchi hizi !!....
Morocco ni ving'ang'a kweli kweli! Bwana wee CAF wamewatangaza kuwa ndio Mabingwa wa AFCON! HAYA MAAMUZI UNAYAWEZA KUYAONA MARA NGAPI KWENYE ULIMWENGU WA MPIRA?!....
ZA HIVI PUNDE! Kocha wa Mpira Rhulani Mokwena amefanikiwa kuondoka Nchini Algeria,hii ni baada ya kuwa mikononi mwa Afisa Usalama waliomdaka akiwa Uwanja wa Ndege,kituo kinachofuata sasa ni Al Ittihad ya Libya kuungana na Aziz Ki !!...