
Ijumaa iliyopita, pamoja na mabalozi wenzangu wa nchi za Afrika waliopo Jakarta tulisherehekea Siku ya Afrika (Africa Day 2026) ambayo huadhimishwa Mei 25 ya kila mwaka.
Katika hotuba yangu kama Amidi wa Mabalozi wa Afrika pamoja na kukumbushia kauli mbiu ya Umoja wa Afrika kwa mwaka huu kuhusu upatikanaji endelevu wa maji ili kufanikisha malengo ya Ajenda ya 2063.
Nilisisitiza pia umuhimu wa kuchagiza zaidi ushirikiano wa kiuchumi baina ya Afrika na Asia katika kutafuta uhuru wa kiuchumi kama ambavyo tulishirikiana baada ya Mkutano wa Bandung wa 1955 kuamsha fikra na hamasa za kupambania uhuru wa kisiasa kwa nchi zetu.
#africaday2026




Indonesia




































