
CHEKI MTU ALIVYONUSURIKA KUTEKWA ..! Tukio hili la Jaribio la utekaji limetokea katika Hotel ya Rovvenpec Resort iliyopo Kiluvya,Madukani Dar es Salaam. Jamaa aliiga mbinu zangu (Golden folk style) za kutumia nguvu na kugomea kuondoka nao hivyo kutokana na nguvu za jamaa na kelele zake za "naenda Kuuwawa" akafanikiwa kutetea uhai wake. Watekaji walishindwa kumbeba jamaa kama walivyo tarajia,na wakati wote huo hakuna mtu aliejitokeza kutoa msaada au Kuwahoji watekaji kwa lolote zaidi ya Kusimama na Kushuhudia.Inasikitisha sana. N.B 1.Somo la kujifunza ni kuwa Kuna mstari mwembamba sana kati ya Kutekwa na Kukamatwa. 2.Kama walikuwa ni askari wa Jeshi la Polisi kweli walishindwa nini Kumuonyesha Kitambulisho mkamatwaji au majirani waliokuwa wanashuhudia. 3.Walishindwa nini Kuita gari ya Polisi wenye uniforms waweze kuondoka naye. 4.kwanini wasiwe na Uniforms wote,Kwanini wasiwe na gari ya Jeshi la Polisi,kwanini wasionyeshe kitambulisho.? 5.Nimepost kuwapa mfano halisi watu wanavyotekwa,ukitoa ushirikiano tu ndiyo nitoleee hiyo. USICHOTWE KIZEMBE

















