Godbless E.J. Lema@godbless_lema
Mgodi wa makaa ya mawe wa Tancoal Energy Limited nchini Tanzania ulikuwa na ubia wa 70% Intra Energy Tanzania Limited (IETL) na 30% Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Mgodi huu ni muhimu kibiashara na kitaifa, ukiathiri sekta ya viwanda, umeme, na ajira.
Baada ya mradi kukamilika, Intra Energy Corporation (IEC) ya Australia iliorodhesha hisa zake kwenye Soko la Hisa la Australia. Bei ya hisa ilikuwa takriban AUD 0.006–0.008 na mtaji wa soko ulikuwa AUD 9.5 milioni (~TSh 16.2 bilioni). Baada ya IEC kutangaza kuondoka kwenye mradi, Rostam Aziz, kupitia kampuni yake alinunua hisa hizo. Hisa hizo zilikuwa kwenye soko la umma, Soko la Hisa la Australia (ASX) hivyo mtu yeyote angeweza kununua hisa hizo.
Sasa , ni nani anayeweza kushutumiwa? Ikiwa kuna tatizo au hoja, mdau namba moja anayepaswa kushutumiwa ni Serikali (NDC) , kwa kuwa waliweka asilimia 30 ya HISA lakini hawakuongeza HISA zao wakati zilikuwa listed ktk soko la HISA la Australia. Kama walijua mradi huu ulikuwa na maslahi makubwa kwa umma!! Kwa nini hawakuchukua nafasi ya kibiashara ya kununua HISA zaidi, na hata pale Intra Energy walipoamua kujitoa kabisa kwenye uwekezaji huu , habari hii ilikuwa ndani kwanza kwa wamiliki wote Intra Energy yenye 70% na NDC wenye 30% na ktk vyombo vya habari vya Kimataifa kwa muda sana mpaka pale Rostam alipojitokeza kununua HISA hizo. Hii inaonyesha changamoto si kwa wafanyabiashara wa nje, bali katika uwezo wa wadau ndani ya Serikali kuona na kushiriki kwenye uwekezaji kwa mtazamo wa kibiashara.
Rostam Aziz hakutenda uhalifu , aidha alitumia fursa halali ya kibiashara. Ambayo mfanyabiashara ambaye hawezi kuiona na kuipuuza ikiwa ana interest , aidha atakuwa hajui namba na mbele sana ya biashara hii , basi , kama ni kukoroga basi Intra Energy ndio wamekorogwa na changamoto zaidi ni kwa NDC na sera zao za uwekezaji na uwezo wao mdogo ktk FIKRA ya uwekezaji. Kumbukeni , Serikali imeshindwa kuendesha biashara ya dala dala hapo Dar , itakuwa haya mambo yenye Kiingreza kingi na graph mingi ? Tufikiri kibiashara kabla hatujahukumu sana.