"Si mlisema tufanye kazi?.. Tumeamua kufanya kazi"....Kibao Kipya cha familia @naythetrueboy kinakwenda kwa jina la TUPO BUSY. Twendeni zetu mjini Youtube.
Msanii wa muziki wa Hiphop Emmanuel Elibariki(Nay wa Mitego) amesema hali ya kukataliwa kwa wasanii na mashabiki nchini ni jambo ambalo litatoa somo kwa wasanii kuwa wanapaswa kuwa sauti ya mashabiki/wananchi angalau mara chache.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay amechapisha video yake aliyokuwa akitoa wito kwa wasanii kujitoa na kuwasemea wananchi huku akitolea mfano wa wasanii wa mataifa kama Kenya na Nigeria ambao wapo wamekuwa wakiungana na wananchi pindi wanapowasilisha madai yao.
Ameambatanisha video hiyo na andiko akisema "Niliwashauri wasanii wenzangu kujitoa kwa wananchi wetu ata mara moja tu kwa mwaka kuwasemea kwa sababu wao ndo maboss wetu wa kwanza na ndio wenye hatma ya nguvu thamani na ushwishi tulio nao"
Nay ameongeza "tatizo kubwa la Mastar hapa nyumbani ni ubinafsi na kusahau maboss zetu ni hawa wananchi. Sasa maboss zetu now wameamua kutuonyesha kwamba wao ndio wanaotupa jeuri na maisha mazuri tuliyonayo Ni kwa sababu yao.
Aidha amesisitiza kuwa hatua ya watanzania sio la kulaumiwa bali kuchukuliwa kama somo kwa wasanii nchini "Mimi siwalaumu watanzania wana haki ya kuendelea na walichoamua npaka hasira zao zitakapoisha. Nadhani baada ya apo somo litakua limetuingia wasanii wote na tutakua tunaongea tugha moja wananchi na wasanii wote."
Msaani wa Nigeria 🇳🇬, Akiendelea na tour yake nchini Marekani, Davido alishangaza wengi baada ya kusimamisha show kwa dakika moja huku akiwaomba mashabiki wake walio jitokeza kuiombea Tanzania kutokana na machafuko yaliyojitokeza siku chache nyuma. Show hiyo iliyoenda Kwa jina la Atlanta Concert ilihudhuriwa na mashabiki wengi, na bendera ya Tanzania ilipeperushwa muda huo.
#ThankYou@davido
Tumepoteza Ndugu Zetu Wengi Sanaaa🥹
Hakuna Damu Inaendaga Bure Malipo Yapo Na Mungu Ni Mwema Tuta shuhudia Malipo Ya umwagaji Damu Huu.
Mungu Awalaze Mahari Ndugu Zetu walio poteza Maisha🙏🙏
Wakenya Media zao zipo huru sana, sikiliza hapa wanawashauri WATANZANIA kuelekea maandamano 29.10.
Huu ujumbe wa muhimu sana. Kuna watu hawajui kazi ya cologate (DAWA YA MSWAKI) kwenye maandamano. Wanaojua waambieni hapo wenzenu wajifunze maana ni YA MUHIMU SANA.
Repost 200
#MO29#MaandamanoOktoba29#TUTAKUWEPO🫵😎
Hii Sio Tanzania yetu ya Kisiwa cha Amani tena.
Hatupo salama tena. Kuikomboa Tanzania yetu ikawa ile ya Amani Ya Kweli ni Sisi watanzania wenyewe ambao Ndo Wenye Tanzania wenyewe.
Kwani Hii Nchi Kuandamana Ni Kosa.?! Mbona Viongozi Wetu wakisikia Maandamano Wanaona Kama Watu wametangaza vita.? Awa police na wana Jeshi walio sambazwa uku mtaani ni kama kuna vita inakuja.
Wanauza Uoga Ngoja Tuone Kama kuna mtu wakununua round hii.!!
Madam President @SuluhuSamia pokea ujumbe huu mzito kwa niaba ya CCM halafu ukae chini utafakari kama unastahili kuendelea na hicho unachokiita UCHAGUZI.
Kimara Kona, Ubungo, Dar es Salaam, asubuhi ya leo.
Wananchi wanaimba “tunamtaka Tundu Lissu”. Mbogamboga mchezo wenu wa kuwalazimisha wananchi kuwapenda kwa lazima haujazaa matunda. Pamoja na kumtunza TAL gerezani siku 180 anakumbukwa na wananchi na wanaimba jina lake bila kulipwa.
Nimependa sana huyo ‘hyper’ ambaye amerekodi hili tukio, ni mwanamke ambaye mwanaume wake anatakiwa kujivunia sana – siyo mfuasi wa mbogamboga na anapenda haki kutoka moyoni.., jamii yetu inazidi kupata mwanga na kuwaona mbogamboga ni LAANA.
HYPER amefurahishwa sana na wananchi wenzake kuimba jina la Tundu A.M Lissu katikati ya barabara ya Morogoro. Kama ambavyo mimi nimefurahi zaidi kuwaona wananchi katika mateso wakilikumbuka na kuliimba jina la Tundu Antiphas Mughwai Lissu.