Royal Media

277.8K posts

Royal Media banner
Royal Media

Royal Media

@royalmediatz

Uhakika wa Habari, Hadhi ya Kifalme.

😎😎😎 Katılım Temmuz 2019
2.6K Takip Edilen320.1K Takipçiler
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki na Waendesha Bodaboda Mkoa wa Mbeya, Aliko Fwanda, amemwaga ukweli mzito mbele ya waandishi wa habari kufuatia vurugu zilizotokea jana Juni 21 kwenye mkutano wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge, akimtaka mbunge huyo kuacha kuingiza migogoro kwenye sekta hiyo. ​Fwanda amefunguka kuwa umoja wa bodaboda mkoani humo umepitia vipindi vigumu sana vya nyuma vilivyogharimu maisha ya madereva wengi kabla ya kufikia utulivu wa sasa, na akashangazwa na hatua ya mbunge kukurupuka kuitisha vikao vya siri bila kufuata utaratibu, jambo linalohatarisha kuwagawa na kuwasingizia vijana kupanga vurugu. ​"Inabidi mbunge zimfikie taarifa hizi kwamba kabla ya hapa, huu umoja wetu kuna muda tulikuwa tunauliwa, tunatekwa kama kuku yaani tunachinjwa shingo. Yeye saa hizi amekuta bodaboda wametulia hawana malumbano yoyote, anakuja anaingiza migogoro na kutugawanya kisiasa kwenye makundi. Sisi tunayajenga makundi haya kwa gharama kubwa," amesema Fwanda kwa uchungu. ​Mwenyekiti huyo amefafanua kuwa hakuwatuma vijana kwenda kuvuruga mkutano huo, bali madereva wenyewe walikasirishwa na kitendo cha mbunge kuitisha kikao cha "kunizia" akiwa hayupo. Alibainisha kuwa mbunge alimpigia simu na kumwamuru afike, lakini yeye alimfahamisha kuwa hakuwa na taarifa rasmi na alikuwa njiani kuelekea msibani. ​Fwanda ametoa wito kwa viongozi wa Serikali na wabunge kujifunza kuheshimu mifumo na uongozi uliopo. Amesisitiza kuwa kama Mbunge Mwalunenge ana nia ya dhati ya kusikiliza kero za sekta hiyo, anapaswa kuwasiliana na uongozi rasmi ili uitishe mkutano mkuu wa jiji zima utakaofanyika kwa amani na uwazi.
Indonesia
2
10
50
3.5K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha amesema Mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Marehemu SACP Richard Abwao utawasili Mkoani Tabora Jumatatu jioni, tayari kwa ibada ya kumuombea katika Parokia ya Mtakatifu Theresa siku ya Jumanne saa tatu asubuhi. Akizungumza na waandishi wa habari, Rc Chacha amesema shughuli hiyo itafanyika kabla ya shughuli rasmi ya kuaga mwili wa Kiongozi huyo katika viwanja vya Field Force Unity, Tabora Mjini. "Tunawaomba Wananchi wote kujitokeza kwa wingi kushiriki ibada na kutoa heshima za mwisho kwa Kamanda wetu ambaye alilitumikia Taifa kwa kujituma, uadilifu na ushirikiano mkubwa kwa wananchi katika kulinda usalama wa raia na mali zao." Amesema Mkuu wa Mkoa. Jana katika taarifa yake kwa umma, Mhe. Chacha alisema katika kipindi chake cha utumishi mkoani Tabora, Marehemu SACP Richard Abwao alikuwa kiongozi mwenye ushirikiano mkubwa, aliyesimamia kwa weledi, uzalendo na kujitoa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unalindwa wakati wote. Alikuwa karibu na wananchi, akisikiliza changamoto zao na kushirikiana na Kamati ya Ulinzi katika kudumisha amani na utulivu wa Mkoa wetu. Rc Chacha alitoa pole kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillius Wambura, familia ya marehemu, Kamati ya Ulinzi ya Mkoa, askari wote wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora pamoja na wananchi wote wa Mkoa wa Tabora kwa msiba huu mzito. "Tumeondokewa na kiongozi, mtumishi na mshiriki mkubwa wa juhudi za kulinda amani yetu." Alisema Rc Chacha.
Indonesia
3
0
6
844
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
"CCM ni ileile, haijawahi kuacha wizi wa kura lakini mimi kwa siasa zangu za miaka 20 sasa, kati ya CCM ya Kikwete na CCM hii nitasema ile ya Kikwete tulikuwa tunapata Wabunge, Madiwani, wenyeviti wa Mitaa na Vitongoji kwasababu Kikwete na CCM yake walikuwa wanatumia akili kama vile matapeli wanavyotapeli. Tapeli anakupiga maneno mpaka unaenda nyumbani kuongeza hela. CCM ile ilikuwa inatumia maneno, akili na maarifa kuiba kura." .... CCM hii inatumia mbinu za kijambazi, jambazi anakuja dukani hana stori, haitaji kukudanganya na kutumia akili, anakoki tu bunduki anasema utatoa, hutoi? Wewe unasema tu yarabi nafsi yangu, chukua." "Hawa unakuta diwani anagombea, anarudisha fomu, Ofisi ya Mtendaji ile pale CCM wanakaa kichakani, wanamvizia Diwani wa Chadema wanampora fomu wanakimbia halafu Mtendaji anasema sisi fomu tulishatoa, hatutoi mara mbili. "Hawataki kabisa kutumia akili, wote wana malengo ya kuiba kura lakini CCM ile ya zamani walikuwa wanaiba kwa ulaghai, unaibiwa mpaka mgombea ukikaa na wakala wako unamuuliza, au ulilala? Hawajatumia nguvu, unaangalia tu namba unajiuliza CCM walishindaje?"-Boniface Jacob, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Gairo, Morogoro leo Juni 21, 2026.
Filipino
2
11
61
3.2K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura pamoja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam Jumanne Muliro na waombolezaji wengine wakitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, mara baada ya Ibada iliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Polisi barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam Juni 21,2026 kabla ya kusafirishwa kuelekea Shirati Mkoani Mara kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Royal Media tweet media
Indonesia
2
1
34
3.8K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bw. John Heche amesisitiza kuwa baada ya kuhitimisha ziara za Chama hicho katika Mikoa mbalimbali, ikiwa hoja zao hazitafanyiwa kazi na serikali, Polisi na Serikali wajiandae kwa maandamano makubwa ya Chama hicho kote Tanzania bara. "Wasipotusikiliza, baada ya kikao tutarudi kwenye kikao cha ndani, tutaitisha maandamano Nchi nzima, haki ya Mungu, hakuna rangi wataacha kuona. Sijui mtawaganyikaje kwasababu Njombe kutakuwa na maandamano, Iringa maandamano, Mbeya maandamano, Tarime maandamano, Kila kona kitakuwa kinawaka. Kwahiyo tunataka watusikilize, wasipotusikiliza hakitaeleweka." Heche ameyasema hayo leo jioni Juni 21, 2026 Makambako Mjini, Mkoani Njombe, wakati wa mkutano wa hadhara chama hicho, akisema udhaifu na mapungufu ya CCM ni mengi, akisema kila mmoja anajua namna ambavyo watu wanaumizwa na kuteswa na Chama Cha Mapinduzi. "Tumesema tunaanza ziara ya kuzungumza na wananchi kwanza na tunashinikiza na kuwabana ndani ya nchi na Kimataifa, si mmesikia serikali ya Ulaya ilichokifanya? Si mmesikia Marekani inachokifanya? Tutawabana kote, yaani ndani pamoto, nje pamoto na wakisimama nchale, wakikaa nchale, wakichuchumaa nchale." Amesema Heche.
Indonesia
2
16
104
3.2K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
"Wadhalimu wamemfata Mwenyekiti wetu Tundu Lissu wanamwambia kubali utoke gerezani, urudi uraiani, uache siasa ukaishi maisha yako Ubelgiji, tutakupa fedha- amekataa amesema nipo tayari kufa kwaajili ya watu wangu." "Lissu amesema yupo tayari kufia gerezani kwasababu yenu kwasababu anataka Katiba ambayo itampa mtoto usawa wa kusoma elimu anayosoma mtoto wa Heche, akae kwenye darasa analokaa mtoto wa Samia Suluhu Hassan." "Haiwezekani kwenye Nchi hii iliyojaa matabaka, mtoto wako anasoma shule ya kidumu na fagio, mtoto wa Heche anasoma Saint Coruna halafu wanapewa mtihani wa kufanana, kila siku mtoto wako ataonekana hana akili, kumbe hakupewa fursa sawa na ya mtoto wa Heche ili washindane katika meza inayofanana."- Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bw. John Heche, akizungumza na wananchi wa Makambako Mkoani Njombe leo Jumapili Juni 21, 2026.
Indonesia
6
15
110
4.6K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao ukiwasilia katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Polisi barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam Juni 21,2026 kwaajili ya ibada ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kuelekea Shirati Mkoani Mara kwa taratibu za mazishi.
Royal Media tweet media
Indonesia
1
0
35
1.9K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema enzi za kutegemea misaada kugharamia maendeleo na huduma za kijamii zimepitwa na wakati, akisisitiza umuhimu wa Watanzania kujenga utamaduni wa kujitegemea na kuwajibika kutatua changamoto zao wenyewe. Dk Mwigulu amesema dunia ya sasa inahitaji mataifa kujenga uchumi imara unaotegemea rasilimali na mapato ya ndani badala ya kusubiri misaada. Amesema hayo kwenye harambee ya ukamilishaji wa jengo la kitega uchumi la Kanisa Anglikana Tanzania iliyofanyika kanisa kuu la Roho Mtakatifu Dayosisi ya Central Tanganyika Dodoma, leo Jumapili Juni 21, 2026. Akizungumza katika ibada hiyo, amesema ujumbe uliotolewa na askofu wakati wa mahubiri kuhusu mabadiliko ya dunia umeakisi mwelekeo wa Serikali wa kujenga uchumi unaojitegemea. "Mambo ya misaada yamekwisha kupitwa na wakati. Nadhani nchi yetu ilipata pata misaada ambapo kulikuwa na dawati linalosimamia fedha za misaada, kulikuwa na misaada ikiwamo makapu mbalimbali ya kisekta, hayo sasa kwenye bajeti yetu hayapo tena na Rais anaendelea kusisitiza kuwa na bajeti inayotegemea rasilimali za ndani ya nchi,” amesema. Amesema jambo hilo lieleweke vizuri linatakiwa iwe ni lugha na wimbo wa kila Mtanzania huku akisema mwelekeo huo unaonekana wazi katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27 ya Sh62.3 trilioni ambayo imejikita zaidi kwenye ukusanyaji wa kodi, magawio kutoka taasisi za umma na vyanzo vingine vya ndani. Akisisitiza zaidi amesema Serikali haitaki kuona huduma muhimu kwa makundi maalumu zikiendelea kutegemea misaada kutoka nje, badala yake jamii na taasisi za ndani zinapaswa kuchukua jukumu hilo. “Zamani ilizoeleka katika maeneo mbalimbali kuna vituo vya watoto wenye mahitaji maalumu, ilizoeleka kwamba, vituo hivyo vinaendeshwa kwa fedha za misaada kutoka nje na vyenyewe, kwa kuwa eneo hili ni muhimu basi ni vyema sisi serikalini lakini pia na Watanzania wote kuendelea kuachana na dhana hiyo. “Kwamba watoto wasio na wazazi watatakiwa kutunzwa na wasamaria wema wa mataifa mengine hayo mambo yanaendelea kuisha watoto wa Tanzania wenye uhitaji wanatakiwa watunzwe na Watanzania,” amesisitiza. Sambamba na hilo, Dk Mwigulu amesema Serikali imeanza kupitia baadhi ya taratibu na kanuni zinazoweza kuzuia utoaji wa misaada ya haraka kwa wahitaji. Amesema baadhi ya watu wenye ulemavu au wenye uhitaji wanapofika katika ofisi za umma kuomba msaada, wamekuwa wakipewa barua za kwenda kujichangisha badala ya kusaidiwa moja kwa moja. "Mtu mwenye ulemavu anapoenda katika ofisi ya umma kuomba msaada, hapaswi kutumwa kwenda kuchangisha. Anatakiwa kupata msaada pale pale na kuendelea na maisha yake," amesema. Kutokana na hali hiyo, amewataka viongozi wa Serikali za mitaa na halmashauri nchini kutambua vituo vya watoto yatima na makundi mengine yenye uhitaji ili viweze kupatiwa msaada kwa urahisi kupitia mifumo rasmi ya serikali. Hata hivyo, katika mahubiri ya awali mhubiri amesema Tanzania ina kila kitu na ni aibu makanisa ya Tanzania kuandika barua kuomba msaada nje ya nchi. “Kwa miaka mingi makanisa yameishi kwa kutegemea misaada Ulaya na Marekani,” amesema akiongeza kwamba watu wa huko sikuhizi hawaendi makanisani hivyo ni ngumu kutegemea misaada. Hivyo amesema kanisa la sasa la Ulaya na Marekani haliwezi kusadia kwakuwa limerudi nyuma. Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Maimbo Mndolwa amesema kanisa linakwenda kwa misingi ya enzi ya maandiko matakatifu, mapokeo ya kanisa na matumizi sahihi ya akili.
Royal Media tweet media
Indonesia
23
2
40
5.4K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
TISEZA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA UWEKEZAJI KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA DODOMA Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) inaendelea kushiriki katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma, kwa kutoa elimu kuhusu fursa za uwekezaji, huduma za uwezeshaji wa wawekezaji na nafasi mbalimbali zinazopatikana kupitia Maeneo Maalum ya Kiuchumi nchini. Maonesho hayo yanawaleta pamoja taasisi mbalimbali za umma kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na Serikali. Katika banda la TISEZA, wananchi, wafanyabiashara, wajasiriamali na wawekezaji wanapata fursa ya kujifunza kuhusu mazingira ya uwekezaji nchini, sekta zenye kipaumbele, vivutio vya uwekezaji pamoja na huduma za uwezeshaji zinazotolewa na Mamlaka kwa lengo la kurahisisha uwekezaji nchini. Akizungumza wakati wa maonesho hayo, Meneja wa Utawala wa TISEZA, Bw. Juma Mantakara, alisema ushiriki wa Mamlaka katika Wiki ya Utumishi wa Umma ni sehemu ya juhudi za kuwasogezea wananchi huduma na kuwajengea uelewa kuhusu fursa zilizopo nchini. "Wiki ya Utumishi wa Umma ni jukwaa muhimu linalotuwezesha kukutana ana kwa ana na wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji. Kupitia maonesho haya tunatoa elimu kuhusu fursa za uwekezaji, huduma zinazotolewa na TISEZA na namna tunavyorahisisha safari ya uwekezaji nchini. Tunawakaribisha wananchi wote kutembelea banda letu ili wapate taarifa sahihi na kufahamu fursa zilizopo kwa maendeleo yao na ya Taifa," alisema Bw. Mantakara. Kwa kushiriki katika maonesho hayo, TISEZA inaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha utoaji wa huduma kwa umma huku ikihamasisha uwekezaji wenye tija, unaochochea ukuaji wa uchumi, uanzishaji wa viwanda, uhamishaji wa teknolojia na ujenzi wa ajira kwa Watanzania. Wananchi wote wanaendelea kukaribishwa kutembelea banda la TISEZA katika Viwanja vya Chinangali, Dodoma, ili kupata elimu ya uwekezaji, ushauri wa kitaalamu na taarifa kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana nchini.
Royal Media tweet media
Indonesia
0
0
8
569
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bw. John Heche amewasili Njombe Mjini, Mkoani Njombe leo Jumapili Juni 21, 2026 akiambatana na Viongozi wengine wa Chama hicho kwaajili ya muendelezo wa Operesheni ya Chama hicho ya Katiba Mpya, Free Tundu Lissu, akitarajiwa kuwa na mkutano wa hadhara mchana huu na baadae kuelekea Mjini Makambako kuendelea na mkutano mwingine wa hadhara. Heche ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa, Necto Kitiga,Mkurugenzi wa Mawasiliano na uenezi Brenda Rupia pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar Said Mzee na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema Bi. Sharifa Suleiman. Saa Kumi Jioni Chadema itakuwa na mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Stendi Kuu, Makambako.
Indonesia
1
16
82
2K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Katibu wa Baraza la Habari la Waislamu nchini Tanzania (BAHAKITA) Sheikh Said Mwaipopo amewatahadharisha wale wote wanaoratibu na kuandaa maandamano ya Julai 07, 2026, akiyaita maandamano haramu na kuwataka wale wote watakaoandamana wasithubutu kukanyaga Magomeni, Kinondoni, Sinza na Kariakoo kwani kipo kikosi kazi kilichojizatiti kuhakikisha wanadhibiti maandamano hayo. Sheikh Mwaipopo amebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam, akiambatana na baadhi ya Vijana waliokuwa wamemzungumza na kutoa tahadhari ya maandamano hayo aliyoyaita kuwa haramu yaliyoandaliwa na wanaojiita wanaharakati, akisema wao kama Watanzania na watu wanaojitambua hawayatambui na hawayaungi mkono maandamano hayo. "Tunasema maeneo haya ya Magomeni, Kinondoni, Sinza na Kariakoo tunawaonya wasithubutu kukanyaga hiyo tarehe saba kwani tuna watu hatari sana ambao wanaweza kutembea juu ya kamba kwa zaidi ya kilomita moja, miongoni mwao ni hiki kikosi unachokiona hapa nyuma. Wallah, tumejipanga sana, tunawatahadharisha hayo maeneo msiguse, tuna vijana wanaitwa mbwa mwitu, tukiwaambia kamata wanakamata, kula wanakula, hawa vijana ni hatari wanatisha na ni watoto wa Mjini." "Kama kuna kijana wa Kitanzania anajihusisha na maandamano haya, sisi tunamnasihi kabisa aache, litakalokukuta usije ukamlaumu Mungu, mwanadamu au ukamlaumu mwanasiasa." "Maandamano haya kiuwazi kabisa, kama serikali itatumia nguvu, sisi tutatumia nguvu maradufu na tumemwaga watoa taarifa (informer) kila kijiwe cha kahawa, maskani zote, vituo vya bodaboda, ka bar, hoteli, guest house, kanisani na misikitini. Tuna vijana wazalendo huo kwahiyo sisi tukishakuwa na uthibitisho tu kuwa ulipanga njama hizo za maandamano, tutakuja kukuchomoa chumbani au kwenye andaki, hatutakuacha." Amesema Sheikh Mwaipopo.
Indonesia
16
8
25
3.9K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejibu kwa msimamo mkali na wa kujiamini mapendekezo ya rasimu ya hoja ya Bunge la Ulaya kuhusu Mpango wa Utekelezaji wa Mwaka 2026, ikisisitiza kuwa baadhi ya tuhuma zilizomo zinapotosha hali halisi ya nchi na zinaonyesha uelewa usio kamili wa matukio ya baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025. Tanzania imesema inaheshimu haki ya Bunge la Ulaya kujadili masuala ya ushirikiano wa nje wa Umoja wa Ulaya, lakini imekosoa kile ilichokiita “hitimisho za haraka” na taarifa zisizo sahihi kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali kufuatia vurugu za uchaguzi, ikisisitiza kuwa tayari imeanzisha hatua pana za kitaifa za uwajibikaji. Katika taarifa yake, serikali imeeleza kuwa haijakaa kimya kama inavyodaiwa, bali imeanzisha Tume ya Uchunguzi huru na baadaye Tume ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kuchunguza mauaji, uharibifu na madai yote ya uhalifu, huku ikisisitiza kuwa mchakato huo unaendeshwa kwa mujibu wa sheria na misingi ya haki, hivyo madai ya “kutotambua waliohusika” hayana msingi. Tanzania pia imeweka wazi kuwa mchakato wa maridhiano na mageuzi ya kitaasisi unaendelea, ukilenga kuimarisha umoja wa kitaifa na kuandaa mabadiliko yatakayofikia katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2030, hatua ambayo serikali imesisitiza kuwa ni ushahidi wa dhamira yake ya kuimarisha demokrasia badala ya kudhoofisha. Kuhusu ripoti ya Tume ya Uchunguzi, serikali imefafanua kuwa kutokuitangaza kwa umma hakumaanishi ukosefu wa uwazi, bali ni uamuzi wa kisheria unaolenga kulinda ushahidi, usalama wa mashahidi na uadilifu wa uchunguzi unaoendelea, huku ikieleza kuwa nchi nyingi za Jumuiya ya Madola hufuata utaratibu huo. Katika suala la kiongozi wa upinzani Tundu Lissu, Tanzania imesisitiza kuwa si “mfungwa wa kisiasa” kama inavyodaiwa, bali ni mtu anayekabiliwa na mashauri ya jinai mahakamani, na kwamba ni mahakama pekee ndizo zenye mamlaka ya kuamua hatia au kutokuwa na hatia bila kuingiliwa na siasa za ndani au nje. Aidha, serikali imekanusha madai kwamba ilikataa ziara ya Kamati ya Haki za Binadamu ya Bunge la Ulaya, ikieleza kuwa hakukuwa na kukataa ushirikiano bali kulikuwa na mazungumzo ya kubadilisha ratiba, huku ikisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika misingi ya kuheshimiana, ukweli na uhuru wa kila upande.
Royal Media tweet media
Indonesia
29
2
58
8.2K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bw. John Heche, ameonesha kushangazwa na kiwango kikubwa cha bajeti kilichotengwa na serikali kwaajili ya safari za Viongozi (Trilioni Moja), akisema licha ya kutengwa kiasi hicho cha fedha, ziara na safari za Viongozi zimekuwa hazina tija kwa wananchi. "Wametenga Shilingi trilioni moja kwaajili ya safari za viongozi. Yaani unapitisha bajeti ya Trilioni moja kwa safari ambazo kiongozi kama Waziri Mkuu anaenda analetewa matatizo eti 'mimi nimefukuzwa na mume wangu', 'Mhe. Waziri Mkuu nilikuja na mbuzi hapa kukupa zawadi, mbuzi kaibiwa lakini nilipewa mimba na mwanaume kanitelekeza." Amesema Heche. Heche amebainisha hayo Jumamosi Juni 20, 2026, katika mkutano wa hadhara wa operesheni Katiba Mpya, Free Tundu Lissu uliofanyika Songea Mjini, ukiwa ni Mkutano wa mwisho kwa Kanda hiyo katika awamu hii ya pili ya mwendelezo wa operesheni hiyo inayoendelea kote Nchini ikisisitiza kuhusu Katiba mpya na kupaza sauti za kuachiwa kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Tundu Lissu. "Tuna watu wanaitwa ustawi wa jamii, wapo kila Wilaya, hao wanafanya nini? Kuna Wakurugenzi, wanafanya nini? Waziri Mkuu anatembea na magari zaidi ya 30, shughuli hazifanyiki, barabara zinafungwa, magari yanawekwa mafuta, watu wanalipwa posho- Ukiona msafara wa Waziri Mkuu ni zaidi ya Milioni 300-400 imetumika kwa siku moja katika eneo moja. Halafu eti anaenda kutatua matatizo ya ndoa." Ameeendelea kusema @HecheJohn
Indonesia
2
12
50
2K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Serikali ya Tanzania imesema imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha ukweli, uwajibikaji na maridhiano vinapatikana kufuatia vurugu zilizotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, huku ikisisitiza kuwa suala la Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, linaendelea kushughulikiwa na vyombo vya sheria bila kuingiliwa na mamlaka za kisiasa. Kauli hiyo imetolewa katika ufafanuzi rasmi wa Serikali kuhusu rasimu ya Azimio la Bunge la Ulaya kuhusu Mpango wa Utekelezaji wa Mwaka 2026 kwa Tanzania, ambapo baadhi ya madai yaliyomo kwenye rasimu hiyo yameelezwa kuwa yanategemea taarifa zisizo kamili na hitimisho lisiloakisi hali halisi ya Tanzania. Kuhusu vurugu za uchaguzi wa Oktoba 2025, Serikali imesema inatambua uzito wa matukio hayo yaliyosababisha vifo, majeruhi, uharibifu wa mali na madhara kwa familia nyingi, huku ikibainisha kuwa hayo ni masuala yanayogusa mustakabali wa mshikamano wa taifa, utulivu wa kisiasa na maendeleo ya demokrasia nchini. Serikali imeeleza kuwa kutokana na uzito wa matukio hayo, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliunda Tume Huru ya Uchunguzi iliyochunguza chanzo, mazingira na athari za vurugu hizo pamoja na kutoa mapendekezo ya namna ya kuzuia matukio kama hayo kujirudia. Aidha, Mei 18, 2026 Rais Samia aliunda Tume ya Uchunguzi wa Jinai kuhusu Matukio ya Vurugu Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, chini ya Jaji wa Mahakama ya Rufani, Shaban Ally Lila. Tume hiyo imepewa jukumu la kufanya uchunguzi wa kina kuhusu vifo, majeruhi, watu waliopotea, uharibifu wa mali na makosa mengine ya jinai yanayodaiwa kufanyika katika kipindi hicho. Kwa mujibu wa Serikali, madai kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa kuwabaini waliohusika na vurugu hizo hayazingatii ukweli kwamba uchunguzi wa kubaini wahusika binafsi bado unaendelea kupitia tume hiyo ya jinai. “Uwajibikaji utawahusu wote watakaobainika kufanya vitendo visivyo halali bila kujali nafasi zao, taasisi wanazotoka au mwelekeo wao wa kisiasa,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo. Serikali pia imebainisha kuwa pamoja na uwajibikaji, inaandaa mchakato wa maridhiano ya kitaifa utakaojumuisha vyama vya siasa, taasisi za umma, asasi za kiraia na viongozi wa dini kwa lengo la kuimarisha umoja wa taifa baada ya mgawanyiko uliojitokeza katika kipindi cha uchaguzi. Katika hatua nyingine, Serikali imeeleza kuwa ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa Rais haijachapishwa hadharani kwa sasa kutokana na sababu za kisheria, kiusalama na kulinda mashahidi pamoja na waathirika waliotoa ushahidi kwa masharti ya usiri. Kwa upande wa kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Serikali imepinga maelezo yaliyotolewa katika rasimu ya azimio la Bunge la Ulaya yanayomtaja kama “kiongozi wa upinzani aliyefungwa jela”. Kwa mujibu wa Serikali, Lissu hajafungwa baada ya kuhukumiwa na mahakama yoyote, bali anakabiliwa na mashtaka ya jinai ambayo bado yako mahakamani na yanasikilizwa na vyombo husika vya sheria. Serikali imesisitiza kuwa hatma ya kesi hiyo itaamuliwa na mahakama kwa kuzingatia ushahidi na sheria zilizopo, huku ikieleza kuwa Lissu anaendelea kunufaika na haki zote za kikatiba ikiwemo haki ya kudhaniwa hana hatia hadi itakapothibitishwa vinginevyo, haki ya kupata uwakilishi wa kisheria na haki ya kusikilizwa kwa haki mbele ya mahakama huru. “Serikali haiamui matokeo ya mashauri yaliyopo mahakamani wala kuelekeza mahakama namna ya kutoa maamuzi. Kufanya hivyo kungekuwa ni kukiuka misingi ya utawala wa sheria,” imeeleza taarifa hiyo. Katika ufafanuzi huo, Serikali imeonya dhidi ya hitimisho la kisiasa kuhusu kesi ya Lissu kabla ya mchakato wa mahakama kukamilika, ikisema hatua hiyo inaweza kuathiri uhuru wa mahakama na misingi ya haki. Pamoja na hayo, Serikali imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika masuala mbalimbali ya maendeleo, demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria kupitia mazungumzo na mifumo rasmi ya ushirikiano iliyopo kati ya pande hizo mbili.
Royal Media tweet media
Indonesia
20
5
66
13.4K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amewataka wanasiasa wanaojiunga na chama hicho kutokuwa na matarajio ya kupata vyeo mara moja, akisisitiza kuwa nafasi za uongozi hutolewa kwa kuzingatia katiba, kanuni, taratibu na sifa zilizowekwa. Kihongosi ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Mwembe Togwa, mkoani Iringa, alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa na maendeleo ya taifa. Amesema kujiunga na CCM kunapaswa kuongozwa na dhamira ya kuitumikia nchi, wananchi na chama, badala ya kutanguliza matarajio ya kushika nafasi za uongozi. Aidha, amewahimiza wanachama wapya kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama, kuzingatia maadili na kuheshimu taratibu zilizowekwa katika mchakato wa kupata viongozi.
Indonesia
2
1
27
4.2K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Chama cha ACT Wazalendo kimezindua mashambulizi dhidi ya mapendekezo ya hivi karibuni ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikidai kuwa viongozi hao wamepoteza uhalali wa kusimamia sheria na sasa wanageuza nchi kuwa "urithi wa familia zao." Akitupa makombora hayo jana, Juni 20, 2026, Waziri Kivuli wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Janeth Rithe, amesema Ngome ya Wanawake haitafunga mdomo kuona makundi ya chini yakikandamizwa. Kauli hiyo inakuja kujibu pendekezo la Mbunge wa Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge (CCM), aliyetaka madereva bodaboda na machinga watozwe shilingi 1,000 kila siku kwa ajili ya miundombinu. Rithe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo, amesema kuwa kundi la machinga na bodaboda linajumuisha vijana na wananchi maskini wanaopambana kutafuta ajira, hivyo kujaribu kuwanyonya na kuwakandamiza ni kuchokoza kundi kubwa linaloweza kuivuruga amani ya nchi ambayo bado haijatulia vizuri. Kiongozi huyo amemalizia kwa kutoa rai nzito kwa viongozi wa CCM akisema: "Ukiona juu ya chungu kuna kifaranga, jua chini yuko mama yake. Wabunge wa CCM wasijisahau kwa sababu wameshakaa kwenye kokasi zao wakapanga ajenda hii. Hatunyamazi kimya; atakayetokeza kichwa tunakigonga, na kila atakayesimama lazima tumgonge"
Indonesia
2
12
82
7.1K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Ombi la mchango wa maendeleo limegeuka shubiri kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge, baada ya kuwasha moto wa hasira na kuzomewa na mamia ya madereva bodaboda na wafanyabiashara wadogo (machinga) katika kikao cha majumuisho kilichofanyika leo Juni 20, 2026. ​Zomeazomea hiyo imezuka kufuatia kauli ya mbunge huyo iliyotafsiriwa na wengi kama kejeli kwa hali ngumu ya kiuchumi,.pale alipowataka wadau hao kuanza kuchangia shilingi 1,000 kila mmoja kila siku kwa ajili ya kufadhili ujenzi wa miundombinu ya barabara mkoani humo. ​Mwalunenge, akijitetea jukwaani kuhusu mchango wa sekta isiyo rasmi, alishikilia hoja kuwa kipato cha makundi hayo kimeshakua na hakipaswi kuchukuliwa kama cha kimaskini, jambo lililoamsha zogo ukumbini.
Filipino
44
22
170
29.4K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali inaendelea kuweka nguvu kubwa katika sekta ya michezo kwa lengo la kuibua vipaji, kuongeza ajira na kuiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa mataifa yanayotambulika kimataifa kupitia michezo. Akizungumza Zanzibar wakati wa ufunguzi wa Ngao ya Jamii katika mashindano ya PBZ Bank Yamle Cup 2026, Makonda alisema michezo ni sekta yenye mchango mkubwa katika uchumi kutokana na mnyororo mpana wa ajira unaozalishwa na shughuli zake. Alieleza kuwa pamoja na kutoa ajira kwa wanamichezo, sekta hiyo pia inanufaisha makundi mbalimbali ikiwemo waandishi wa habari, sekta ya usafirishaji, hoteli, biashara ndogo ndogo na huduma nyingine zinazohusiana na matukio ya michezo. “Michezo ni fursa kubwa kwa vijana wetu. Tunahitaji kuitumia vizuri ili kuzalisha ajira nyingi zaidi na kukuza uchumi wa nchi. Faida zake haziishii kwa wachezaji pekee bali zinagusa sekta nyingi za huduma na biashara,” alisema Makonda. Waziri huyo alisema Serikali inaendelea kutekeleza maelekezo ya viongozi wa nchi kwa kuhakikisha ndoto za vijana wenye vipaji zinatimia kupitia uwekezaji katika miundombinu ya michezo, mafunzo ya makocha na programu za kuendeleza vipaji. Aidha, alibainisha kuwa mwezi ujao anatarajia kufanya mazungumzo nchini Ufaransa kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya soka, ikiwemo namna ya kuwapatia fursa vijana wa Tanzania kwenda kuendeleza vipaji vyao katika klabu na akademi za kimataifa. Makonda alisema Ufaransa imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya soka barani Afrika, hivyo Tanzania inalenga kujifunza na kushirikiana nayo ili kuinua kiwango cha mchezo huo nchini. Alisisitiza umuhimu wa kuibua vipaji kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania badala ya kutegemea vilabu vikubwa pekee, akitaja haja ya kuona wachezaji wakitokea Zanzibar, Mwanza, Arusha, Mbeya, Mtwara, Kigoma, Geita na mikoa mingine wakipata nafasi ya kusajiliwa na vilabu vikubwa duniani. Kwa mujibu wa Waziri huyo, Serikali inaendelea kujenga vituo vya kisasa vya mafunzo ya michezo Zanzibar na Tanzania Bara ili kuweka mazingira bora ya kuandaa wanamichezo wa ngazi za kimataifa. Aliongeza kuwa lengo la muda mrefu ni kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wa Tanzania wanaocheza katika ligi mbalimbali duniani na kurejea kuitumikia timu ya taifa, jambo litakalosaidia kuimarisha ushindani wa soka la Tanzania na kuitangaza nchi kimataifa. Makonda alihitimisha kwa kusisitiza kuwa michezo ni chombo muhimu cha kuimarisha umoja, amani, upendo na mshikamano wa Watanzania, huku akiwasihi wadau wote kuendelea kushirikiana katika kuendeleza sekta hiyo kwa manufaa ya taifa.
Indonesia
2
2
39
4.8K
Royal Media
Royal Media@royalmediatz·
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, amewataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha kuzunguka katika maelezo yao na badala yake kutoa majibu ya moja kwa moja kuhusu fedha wanazodai kupokea kutoka kwa wafadhiri wa nje. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Kahama, Hapi anasema viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuweka wazi ni chama gani rafiki au taasisi gani kutoka nje ya nchi imekuwa ikiwapatia fedha, kiasi gani wamepokea na fedha hizo zimetumika kwa shughuli zipi. Anasema wananchi na wanachama wa chama hicho wana haki ya kufahamu vyanzo vya fedha vinavyotumika kuendesha shughuli za kisiasa za chama hicho, akidai kuwa kumekuwa na maswali mengi ambayo hayajajibiwa kuhusu ufadhili huo. Hapi anaendelea kueleza kuwa zipo taasisi mbalimbali ambazo kwa nyakati tofauti zimehusishwa na shughuli za chama hicho katika upokeaji wa fedha kutoka kwa wafadhiri, akisisitiza kuwa ni muhimu kwa viongozi wa CHADEMA kuweka wazi taarifa zote ili kuondoa mashaka yaliyopo kwa umma. Katika hotuba yake, Hapi anahoji sababu za chama hicho kuendelea kuendesha kampeni za kuchangisha fedha kwa wanachama na wafuasi wake kupitia mfumo wa “tonetone”, huku akidai kuwa chama hicho kimekuwa kikipokea fedha kutoka nje ambazo hazijawekwa wazi kwa wanachama wake. “Wanapaswa kueleza fedha wanazopata zinatoka wapi, ni kiasi gani na zinatumika kwa shughuli zipi. Wananchi wanahitaji ukweli na uwazi kuhusu masuala haya,” alisema Hapi. Aidha, amewataka Watanzania kuwa makini wanapofuatilia shughuli za vyama vya siasa, akidai kuwa baadhi ya vyama vinaendeshwa kwa maslahi ya watu wachache badala ya maslahi mapana ya wananchi.
Royal Media tweet media
Indonesia
23
2
46
7K