WAVE MEDIA
42.4K posts


"Gawio tulilolipokea leo ni kielelezo cha juhudi, uwajibikaji na uadilifu wetu katika kusimamia rasilimali za umma na ni mrejesho kwa mageuzi na maboresho ambayo tumeanza kuyafanyia kazi katika mashirika ya umma, yameanza kuleta matokeo" Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia

Indonesia

"Kote duniani, mashirika ya umma yamekuwa ni nguzo muhimu katika kuchochea maendeleo, na kwa baadhi ya nchi ndio yanayotoa mchango mkubwa katika pato la taifa." Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia

Filipino

kwa uwezo wao wa kifedha ili tupunguze mzigo kwa hazina wa deni la taifa" Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia
Indonesia

"Mwaka jana nilipokea gawio shilingi bilioni 611, mwaka wa fedha ulikuwa haujaisha. Makusanyo yaliendelea hadi kufikia Juni 30, 2024 kiasi kilichokusanywa kilifikia bilioni 767. Na leo nimepokea gawio shilingi trilioni 1.028 sawa na ongezeko la bilioni 261"Mhe. Rais @SuluhuSamia

Indonesia

"Kwa hakika tumepiga hatua kubwa katika kuongeza mchango katika mashirika ya umma, hata hivyo pamoja na mafanikio hayo tunaweza kufanya vizuri katika kufikia matarajio ya serikali juu ya mchango na taasisi katika Mfuko Mkuu wa Serikali wa mapato yasiyo ya kikodi"Rais @SuluhuSamia

Indonesia

"Lengo letu ni kuona mashirika yanachangia angalau asilimia 10 ya mapato yasiyo ya kikodi. Nina imani hili tunaliweza na inawezekana" Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia

Indonesia

"Serikali inathamini mchango wa sekta binafsi na tutaendelea kushirikiana nayo kwa mapana ya nchi yetu. Ni lazima tukubali kuwa, sekta binafsi ni kiungo muhimu katika safari ya mageuzi ya taasisi za umma na safari ya maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla" Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia

Indonesia

"Twendeni tukatumie TEHAMA ili kuongeza uwazi, ufanisi na tija katika kutekeleza majukumu yetu na kutoa huduma. Mifumo iliyopo ihuishwe ili kuwa na mlingano mzuri wa taarifa na kuongeza tija kwa taasisi zetu" Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia

Suomi

"Serikali imeongeza idadi ya kuwa na shida katika kampuni nne za madini na hadi sasa mwaka 2020 hadi kufikia kampuni 12, kote humo tuna hisa. Ni hatua muhimu katika kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali madini ambayo ipo nchini kwetu" Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia

Indonesia

"Zile zama za taasisi kuendelea kuchuma serikalini bila zenyewe kurudisha faida zimepitwa na wakati na hazipo tena. Kila Shirika lijitahidi kuzalisha ili litoe faida" Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia

Indonesia

"Hatua ya kutunga sheria mpya ya uwekezaji wa umma ikikikamilika itaimarisha usimamizi wa rasilimali zilizowekezwa. Shauku yangu na ya Watanzania ni kuona mashirika na taasisi za umma zinawajibika kwa kuleta faida na tija kwa maendeleo ya taifa letu" Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia

Indonesia

"Mashirika 8 kati ya 13 yaliyokuwa yakipata hasara mfululizo, yawetoka kwenye lindi la hasara na sasa yanapata faida. Nawapongeza wote kwa mabadiliko haya chanya na yenye kutia moyo" Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia

Indonesia

"Leo hii tumepokea zaidi ya shilingi Trilioni moja, ni fedha nyingi, zinakwenda kutufaa katika mambo mengi na pia zinakwenda kupunguza ule utegemezi tuliokuwa nao nyuma. Tukienda hivi kila mwaka tutapunguza gap la utegemezi na tunaelekea kujitegemea" Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia
Indonesia

"Tukio hili (la kupokea gawio na michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma) linaakisi dhamira yetu thabiti ya kuhakikisha kuwa uwekezaji wa umma unaendelea kuleta matokeo chanya na yenye tija katika maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa letu" Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia

Indonesia





