
Leo tunaanza rasmi msafara maalum wa kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii zetu, unaoratibiwa na Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) kwa uongozi wa @wildaftz, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo @swissembassyintanzania @irelandintanzania @unfpatanzania @finlandintanzania @uniceftz @lsftanzania @bracmaendeleo
📍 Msafara huu unaanzia Mkoa wa Shinyanga na kuendelea katika mikoa mingine:
➡️ Singida
➡️ Morogoro
➡️ Pwani (Wilaya ya Chalinze)
➡️ Dar es Salaam
🗓️ Tarehe: 18/02/2026 – 27/02/2026
🎯 Malengo yetu ni:
✅ Kutoa elimu kwa jamii kuhusu ukatili wa kijinsia
✅ Kufanya midahalo na wananchi
✅ Kujadili mbinu za kuzuia na kupunguza vitendo vya ukatili
✅ Kutembelea masoko, nyumba za ibada, stendi za mabasi na shule
🤝 Tunawaalika wananchi wote kushiriki, kusikiliza na kuchukua hatua.




Indonesia











































