Janeth Rithe Kitima
7.1K posts

Janeth Rithe Kitima
@JaneRithe
National Chairperson of the Women's Wing @ACTwazalendo

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa mkono wa Sikukuu ya Eid kwa familia mbalimbali ambazo hazina uwezo wa kifedha kusherehekea sikukuu ya Eid al-fitr, katika kila wilaya mkoani Dar es Salaam.

Ninawatakia Waislamu na Watanzania wote sikukuu njema ya Eid al-Fitr. Tumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujalia kukamilisha Ibada ya Swaumu, na tumwombe apokee funga, dua na sadaka zetu. Tuungane na ndugu, jamaa, jirani na marafiki kusherehekea sikukuu hii kwa upendo na utulivu, huku tukidumisha umoja na kulinda amani ya nchi yetu, kwani ndiyo msingi wa ustawi na maendeleo ya Taifa letu. Tuyaishi na kuyaendeleza mema yote tuliyojifunza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani: upendo, huruma na kusaidiana, tukiimarisha maadili mema na mshikamano katika jamii zetu. Eid Mubarak.






































