NIMR-Amani Medical Research Centre รีทวีตแล้ว
NIMR-Amani Medical Research Centre
743 posts

NIMR-Amani Medical Research Centre
@NIMR_AMANI
National Institute for Medical Research - Amani Medical Research Centre.
Muheza, Tanga Tanzania เข้าร่วม Eylül 2016
125 กำลังติดตาม1.2K ผู้ติดตาม
NIMR-Amani Medical Research Centre รีทวีตแล้ว

FEDHA ZA MIRADI ZIKAGUSE CHANGAMOTO ZA WANANCHI VIJIJINI
Na WAF- Kagera
NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa Wadau na watendaji wote wa Serikali kuhakikisha fedha zote zinazoingia nchini na zinazotoka Serikalini kupitia ziara za nje za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan zikatatue changamoto zilizokusudiwa za wananchi katika vijiji kuliko kwenye semina na warsha.
Dkt. Mollel ametoa wito huo leo Agosti 07, 2023 wakati akizindua kampeni ya ugawaji wa vyandarua katika maeneo yote ya mikoa ya Kagera na Tabora inayoambatana na elimu itayosaidia katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria katika mikoa hiyo.
"Niwaasa taasisi zote za Serikali na zisizo za Serikali, Rais wetu anapoenda kuzunguka kwenda kwenye makampuni makubwa na mashirika makubwa duniani ili kutafuta fedha, vipaumbele vyake ni kwenda kumfikia Mtanzania mnyonge kutatua changamoto katika vijiji". Amesema Dkt. Mollel.
Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amewataka Wadau kupunguza semina, warsha na mafunzo na fedha hizo ambazo zimetumika huko zielekezwe katika kuongeza nguvu kutatua changamoto zinazowagusa Watanzania wenye uhitaji ikiwemo changamoto za afya.
Aidha, Dkt. Mollel ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera kutumia vyandarua vilivyo na dawa na kusikiliza vizuri maelekezo na ushauri kutoka kwa Wataalamu wa afya hasa kwenye afua mbalimbali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria ili kufanikisha dhamira ya Serikali ya kuutokemeza ugonjwa huo nchini.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima ameomba Serikali kupitia Wizara ya Afya kuupa Mkoa wa Kagera kipaumbele kwenye eneo la rasilimali fedha na watu ili kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa Malaria kwani Mkoa huo ni moja kati ya mikoa inayoongoza kuwa na maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria.
Pia, amewashauri wananchi kujenga tabia ya kupima ugonjwa wa Malaria kabla ya kutumia dawa ili kuondoa usugu wa dawa, huku akibainisha kama mkoa wataendelea kutekeleza juhudi za mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria ikiwemo kusafisha mazingira na kutoa elimu ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo

HT
NIMR-Amani Medical Research Centre รีทวีตแล้ว
NIMR-Amani Medical Research Centre รีทวีตแล้ว

Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,Kituo cha Nimr Amani kikitoa Huduma ya upimaji Afya BURE kwa wananchi waliofika kwenye Viwanja Vya Nimr Amani.#Umoja na Mshikamano ndio nguzo ya Uchumi wetu#




Indonesia
NIMR-Amani Medical Research Centre รีทวีตแล้ว

#Katika kuelekea siku ya Wanawake duniani (8th March, 2023), wakina mama wa NIMR vituo vya Amani na Tanga walikwenda kupeleka msaada wa mahitaji muhimu kwa wafungwa katika gereza la Maweni Tanga


Filipino

#Wafanyakazi wa Kituo cha NIMR Amani wakiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji wa Mafunzo juu ya elimu ya masuala ya UKIMWI mahala pa kazi kutoka ofisi ya Mganga Mkuu (W), Muheza.Tarehe 28/02/2023.

Indonesia

#Baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha NIMR Amani, wakifuatilia mafunzo ya elimu ya UKIMWI mahala pa kazi, tarehe 28/02/2023


Indonesia































