Samalen Tips🤴
33.4K posts

Samalen Tips🤴
@Samalentips
USHINDI NA MAFANIKIO |Blogger|YouTuber|Psychologist|Samalensafaries|SamalenVPN and Founder👉 @SamalenTv © President of Samalencia #SamalenTips🤴♱ Philanthropist

Mh ! Nimeona hii video nikajifunza mengi , Guys leo nawapa tu neno moja “BE HUMBLE” 🙏


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema wanaopanga njama za kudhoofisha jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kisa tamaa za kupata Urais mwaka 2030 hawatofanikiwa, ambapo amesema Watu hao wote wanaojipanga na Urais mwaka 2030 hawatoupata. Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba Jijini Arusha leo Machi 25, 2026, Makonda amesema ““Kuna Watu wengine nikikaa nasikiliza hotuba yake nasema huyu kabadilika lini?, kuna Watu wanapenda kuyatumia matatizo ya Wananchi kama vile Watetezi halafu uwezo wa kutetea hawana kwasababu hawana hiyo rekodi ya kutetea Wananchi” “Sasa tunaelekea huko 2030 wataibuka Watu wengi sana, nataka niwaambie Mtu yoyote atakayemsaliti Dkt. Samia ambaye alituona, Mimi binafsi nilipata bahati Rais Samia aliniona nikiwa Mtaani miaka mitatu na miezi sita hata simu haiiti, unakaa na Mkeo unacheza na Watoto unajifunza na muda wa kuwapeleka Shule, Mtu huyu amekuona akakupa nafasi, sasa kupitia hiyo nafasi umepata hela kidogo, umeanza kuwa na jina kidogo, unatengeneza network halafu unapambana kupambana na yule aliyekupa nafasi na heshima hiyo” “Mimi Paul Makonda sitomsaliti Dkt. Samia Suluhu Hassan na kama uongozi wangu unatakiwa kuishia 2030 utaishia hapo kwani kuna shida gani?, kwani unatakiwa utawale maisha yako yote?, na ndio maana ukiona hao Viongozi wanataka kujitenganisha hii Serikali yeye akae pembeni awe sehemu ya Wakosoaji wa Serikali” “Mimi tukiwa kwenye vita situmi Mtu, sio wale mkikutana mnachekeana aah Kamanda tuko pamoja halafu unasuka mipango huku nyuma aah Mimi nakuja mwenyewe kukushughulikia wote wanaopanga njama za kudhoofisha jitihada za Rais Samia katika uongozi wake huu kwa ndoto zako hazitotumia” “Mh. Waziri Mkuu Mimi nina bahati ya kusema kidogo ya Mungu, Watu wote wanaojipanga hawa hawawezi kushika Urais nakuhakikishia, wekeni kwenye kumbukumbu hawapati, Watanzania hawawezi kuwa wasahaulifu tutaenda rekodi kwa rekodi hauwezi kuwa Malaika dakika za mwisho, shetani ni shetani tu hata kama akizeeka” #MilardAyoUPDATES
















