
GASTON SHUNDO GARUBINDI
574 posts

GASTON SHUNDO GARUBINDI
@ShundoGaston
SENIOR ADVOCATE | CHADEMA CC MEMBER 2019-2024 | CHADEMA DIRECTOR FOR LEGAL AND HUMAN RIGHT 2024-2029.
Dar es Salaam, Tanzania เข้าร่วม Şubat 2019
139 กำลังติดตาม2.8K ผู้ติดตาม

@mshana76 Anaitwa Said Mzee, Makamu mwenyekiti Zanzibar
HT

@ShundoGaston Said ISSA Tena ?mbona hapo kwenye list pamenichanganya
Filipino

KESI YA MGAWANYO WA MALI MAHAKAMA YA RUFAA DODOMA MREJESHO:
Mahakama ya Rufaa, iliyoketi jijini Dodoma jana ilipata maelezo kutoka kwa mawakili wa wadawa kuhusiana na marejeo ya shauri la madai Na. 8323/2026 shauri la msingi, pamoja na Maombi madogo namba 8960/2025 maombi ya zuio kwa Chama kufanya shughuli za kisiasa na kutumia mali za chama.
Kuhusiana na kesi ya msingi, Mahakama ya Rufaa ilitaka mawakili kutoa mawasilisho yao kuhusiana na uhalali na usahihi wa mwenendo wa shauri hilo na amri zilizotokana na shauri hilo kuhusiana na mambo yafuatayo:
Mosi, Mahakama ilitaka kusikia kutoka kwa mawakili kuhusiana na hoja ya mamlaka ya mahakama kuu kusikiliza shauri hilo.
Pili, Mahakama ilitaka kusikia kuhusiana na hoja ya ukomo wa muda,
Tatu, Mahakama ilitaka kusikia kutoka kwa mawakili kuhusiana na lini hasa mgogoro ulianza,
Nne, Mahakama ya Rufaa pia ilitaka kusikia kutoka kwa mawakili kuhusiana na hoja kama shauri hilo lilikuwa na madai yanayohusiana na uvunjwaji wa haki msingi zilizoko kwenye Katiba ya Tanzania na hivyo kutakuwa kusikilizwa na mahakama ya kikatiba.
Aidha katika shauri namba 8960/2025, ambayo ilikuwa ni Maombi ya zuio, Mahakama ya Rufaa ilitaka kusikia kutoka kwa mawakili kuhusiana na hoja zifuatazo:
Mosi, utaratibu uliotumika kusikiliza Maombi ya zuio hasa kwenye kipengele cha haki ya kusikilizwa.
Pili, Mawanda ya amri ya zuio iliyotolewa, kwa kuzingatia;
a) kama amri zilizotokana ziliendana na Amri ya XXXVII Kanuni ya 3 ya sheria ya mwenendo wa madai, sura ya 33, Marejeo ya mwaka 2023.
b) kama amri ya zuio kwa CHADEMA kufanya shughuli za kisiasa iliathiri haki za wanachama kufanya siasa.
Mahakama ya Rufaa ilichukua mwelekeo huo, kutokana na hoja kwamba, marejeo hayo yameitwa na mahakama yenyewe.
Bodi ya wadhamini wa Chama na Katibu Mkuu wa Chama waliwakilishwa na Jopo la mawakili wa Chama, kwa Mapenzi yake Allah, mawakili wametekeleza wajibu wao vizuri sana, nami kama Mkurugenzi wa sheria wa Chama, Nawashukuru na kuwapongeza mawakili wote ambao tumeshirikiana katika hatua zote za maandalizi hadi hatua ya mwisho ya mawasilisho.
Haikuwa kazi rahisi, uthubutu wa mawakili, kujitoa kwao kwa Chama kumefanikisha jambo hili.Pamoja nami, kama mratibu Mkuu wa shughuli za kila siku za kisheria kwenye Chama, Mawakili mwandamizi, Mpale Kaba Mpoki aliongoza jopo letu, pamoja nami Dr Rugemeleza Nshala, Hekima Mwasipu, Dickson Matata na Nashon Nkungu.
Nawashukuru pia mawakili wengine ambao nao walifika mahakama ya Rufaa wakipasha jalamba tusipungukiwe na chochote, hawa ni wakili Alex Massaba, Deogratius Mahinyira, Ruguna na Ikoti Lissu.
Asanteni pia wanachama mkiongozwa na @HecheJohn , Makamu mwenyekiti Bara, Mhe Said Issa Mohamed, Makamu mwenyekiti Zanzibar, Katibu Mkuu wa Chama @jjmnyika , Naibu Katibu Mkuu Bara @amanigolugwa , Mwenyekiti Bawacha Taifa, Sharifa Suleiman, viongozi wa ngazi za chama kutoka mikoa mbalimbali na marafiki wa Demokrasia ambao walifika mahakamani na kutuweka katika Maombi.
Kwa sasa, tunasubiri mahakama ya Rufaa ikamilishe kuandika uamuzi wake, Mungu akipenda tutarejea Dodoma kusikiliza maamuzi ya wazee wa Mahakama ya Rufaa, kama tutakavyo fahamishwa na Msajili wa Mahakama.
Indonesia

Tarehe 13-03-2026 kesi ya Jinai namba 21/2026 inayomkabili Yohana Kaunya (Katibu Mkuu Mstaafu wa Baraza la Vijana Chadema Taifa) itaendelea kusikilizwa, Mahakama ya wilaya Bunda kuanzia saa tatu kamili Asubuhi.
Shauri hilo litaendelea kwa upande wa Jamhuri kuendelea na mashahidi wao, ambapo hadi sasa jumla ya mashahidi 6 wameshatoa ushahidi wao.
Awali, Jamhuri walidai wataleta jumla ya mashahidi 41 kuthibitisha mashitaka yao.
Wananchi mliokaribu na Mahakama ya wilaya ya Bunda na viunga vyake, tukutane Mahakamani kesho, kama ilivyo desturi yetu!!!
Indonesia

Nimeona taarifa ya jana tarehe 11 March 2026, kutoka @Nipashedigital wakidai kwamba CCM imewaita wenye matatizo ya ndoa iwasaidie kuyatatua.
Inashangqza kwamba CCM inaendelea kuwahadaa watanzania kuwatatulia matatizo iliyotengeneza yenyewe. Matatizo ya ndoa inayoita ccm yametokana na ukosefu wa ajira unaosababishwa na Serikali ya ccm, huna uhakika wa Kulasha familia yako ndoa inakuwaje salama? Unaihudumiaje hiyo ndoa.
Wamama Vijijini wanaamka usiku wa manane kwenda kuchota Maji wanapata madhira huko njiani, wanaacha waume zao ndani, halafu aliyesabaisha hayo eti anawaita awasaidie kutatua mgogoro wa ndoa.
Nchi hii kila sehemu kuna
Migogoro ya Ardhi iwe haina wakulima na wafugaji ama haina ya wananchi na wawekezaji, ya Ngorongoro tunayafahamu, kite huko hakuna kilichotatuliwa.
Utatuzi pekee inaoweza ni kutumia Polisi kupinga mabomu wenye malalamiko.
Matatizo ya Rushwa yako kila mahali, hiyo ccm imeshindwa kutatua hizo changamoto na sasa inataka kujiingiza kwenye ndoa za watu, wanatafuta nn kwenye ndoa za watu ??
Tatueni matatizo ya kura mnazoiba kwanza, kabla hamjataka kutatua ya ndoa za watu.
Indonesia

MAREJESHO KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA BUNDA.
Shauri namba 21/2026 linalomkabili Yohana Kaunya na wenzake 20 limeendelea leo Mahakama ya Wilaya ya Bunda kwa upande wa Jamhuri kuleta shahidi mmoja.
Shahidi huyo ambaye ameiambia Mahakama kuwa ni Askari wa Jeshi la Akiba ( Mgambo) ni shahidi wa 6 Kati ya mashahidi 41 wanaotarajiwa kuitwa na Jamhuri.
Hata hivyo, pamoja na kwamba Jamhuri walidai kuleta jumla ya mashahidi 41, leo ilibidi shauri liahirishwe hadi ijumaa tarehe 13, na litaendelea tena tarehe 16 na 17 March 2026, ambayo ni Jumatatu na jumanne.
Tunawashukuru na kuwapongeza wanachama waliojitokeza, Baraza la wanawake chini ya Katibu Mkuu wake Mhandisi Pamela Maasay, Bavicha ambao wamepiga kambi Bunda.
Asanteni pia mawakili tulioshirikiana kutetea watuhumiwa leo, Wakili Dickson Matata, Alex Massaba, Deogratius Mahinyira na wakili kajinusi .
Watuhumiwa wako na afya na molari ya Hali ya juu. Tukutane Mahakamani tarehe 13,16 na 17 tukawaoneshe wanaotushitaki walivyo waongo!
Filipino
GASTON SHUNDO GARUBINDI รีทวีตแล้ว
GASTON SHUNDO GARUBINDI รีทวีตแล้ว

LHRC is closely following up on the reported news that the Tanzania Police Force has arrested several women from the CHADEMA Women’s Wing (BAWACHA) who were on transit to Musoma for the International Women’s Day celebrations.
LHRC is pursuing all necessary legal actions in relation to the matter. We urge the Tanzania Police Force to abide by human rights standards as enshrined in domestic, regional, and international human rights instruments to which Tanzania is a signatory, including respecting the right to bail and the right to a fair trial.
#FairTrialAndHumanRights

English

@MankindUwezo Uhuru wa Mahakama unaufahamu?
Nani na wapi imeandikwa kwamba Mahakama imekuwa huru kwa sababu imewaachia?
Wanaofikiri kama wewe ndiyo watu pekee wasioona janga la ccm.
Indonesia


@hataweweunaweza Tuongeze nguvu kutaka mabadiliko ya mifumo ya sheria pamoja na mfumo wa haki Jinai hapa nchini .
Filipino

@ShundoGaston Inabidi mtu akikutwa hana kosa alipwe muda aliopotezewa
Indonesia

WANACHAMA 7 WA CHADEMA MAGU WAMEACHIWA RASMI NA MAHAKAMA
Baada ya Jamhuri kushindwa kwenye kesi ya kuchoma moto hapa Magu, wameamua kuachana na kesi ya Uhaini kwa kusema Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Hana Nia ya kuendelea na kesi hiyo ya uhaini.
Sasa vijana wetu wote wa Magu wanaenda nyumbani kuungana na familia zao.
Asanteni kwa Maombi yenu, Asanteni kwa msaada wenu, !!!
Indonesia

@kiwirachief Aliyeanzisha hizo kesi ni Jamhuri, kama kuna kitu kinachoitwa hasara na au chuki aulizwe huyo Jamhuri.
HT

@ShundoGaston Aliyeanzisha hizi kesi ni nani? Kwa nini alitie taifa hasara ya mali na muda. Hawa vijana familia zao zimeyumba kiasi gani? Ni aibu kwa taifa kuwa na watu ambao Wana chuki na wakapewa madaraka.
Indonesia

MAHAKAMA YA WILAYA MAGU IMEWAACHIA WANACHAMA 7 WALIOSHITAKIWA KWA KOSA LA KUCHOMA MOTO MAJENGO YA SERIKALI:
Hakimaye, baada ya kusikiliza kesi ya Jinai namba 2037/2026 inayowakabili Peter Jackson Masulya na wenzake 6 leo Mahakama ya Wilaya MAGU imetoa hukumu na imewaachia watuhumiwa wote baada ya kutowakuta na hatia.
Washitakiwa hao, walishitakiwa kwa madai ya kuchoma moto majengo ya Serikali katika vurugu zilizotokea tarehe 29 October 2025. Awali walishitakiwa kwa kesi ya uhaini ambayo Jamhuri wanadai upelelezi Unaendelea lkn baadaye mwaka huu wakings hati nyingine ya mashitaka wakidai watuhumiwa hao pia walichoma moto Ofisi ya mtendaji kata ya Kisesa, Mahakama ya mwanzo kisesa na Ofisi ya Katibu Tarafa.
Katika uamuzi wake, Mahakama imesema, Jamhuri wameshindwa kuthibitisha tuhuma dhidi ya watuhumiwa.
Nawashukuru mawakili wenzangu ambao tumeshirikiana nao kwenye shauri hili, Nawashukuru pia kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa jitihada zao za kuhakikisha watuhumiwa wanakuwa huru.
Asanteni pia wanachi na wanachama ambao kwa namna moja au nyingine wamesaidia kwa Maombi wengine kuja mahakamani.
Tunasubiri kuona Jamhuri wanaweza nn kuhusu hati nyingine ambayo wanawatuhumu kwa kosa la uhaini!!!
Indonesia

KESI DHIDI YA Mhe LISSU & WANACHAMA, TAREHE 06-03-2026:
Kunako viwanja vya Mahakama kuu, Masijala ndogo ya Dar es salaam, Maombi namba 28922/2025 ya Mhe Tundu Lissu yatasikilizwa mbele ya Jaji Hamidu Mwanga. Mhe Lissu alisajili Maombi hayo akiomba kuunganishwa kwenye kesi ya msingi iliyofunguliwa na said issa Mohamed dhidi ya Bidi ya wadhamini wa Chama pamoja na Katibu Mkuu wa Chama, kesi maarufu kama kesi ya mgawanyo wa Mali za chama.
Mhe Lissu anadai ana maslahi katika kesi hiyo kwa sababu maamuzi yoyote yatakayotolewa yataathiri Chama ambacho yeye ni mwenyekiti wake na kwamba kwa historia yake tangu ajiunge na chama amekuwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati kuu ya Chama na hivyo anaweza kuisaidia Mahakama kufika maamuzi sahihi wakati wa kuamua mgogoro uliopo mahakamani. Wanachi wenye nafasi nawaalika kufika Mahakama kuu kusikiliza kesi hiyo.
Mkoani mwanza, Wilayani Magu, kesi ya Jinai namba 2037/2026 inayowakabili Peter Jackson Masulya na wenzake 6 inatarajiwa kutolewa hukumu na Mahakama ya wilaya Magu kuanzia saa tatu Asubuhi. Watuhumiwa katika kesi hii wanashitakiwa kuchoma moto majengo ya Serikali katika vurugu zilizotokea tarehe 29 October 2025. Watuhumiwa hao pia wanakabiliwa na kesi ya uhaini ambayo Jamhuri wanadai upelelezi Unaendelea.
Mkoani Mara, Wilayani Bunda kesi ya Jinai namba 21/2026 inayomkabili Yohana Rugembe Kaunya na wenzake 20 itaendelea kwa upande wa Jamhuri kuleta mashahidi. Hadi sasa upande wa Jamhuri umefanikiwa kuleta jumla ya mashahidi 3. Kaunya na wenzake pia wanatuhumiwa kwa makosa yanayotokana na kile kinachodaiwa kuwa vurugu za tarehe 29-10-2025.
Nirudie kuwaomba wananchi mlioko karibu na Mahakama ambako mashauri haya yanaendelea kujitokeza mahakamani kuonesha mshikamano.
Wakati Mheshimiwa Lissu anajiwakilisha mwenyewe mahakamani, Mwanasheria Mkuu wa Chama, Dr Nshallah ataongoza mawakili wengine kwa niaba ya Bodi ya wadhamini wa Chama na Katibu Mkuu wa Chama Mahakama kuu, Mkurugenzi wa sheria wa Chama atakuwa Magu wakati Wilayani Bunda jopo la mawakili wa Chama, Dickson Matata, Alex Dotto Massaba, Deogratius Mahinyira wataongoza jopo la upande wa utetezi.
Tuwatakie kheri na utetezi Mwema kwa Chama Chetu na wananchi wenzetu wenye changamoto mahakamani, tukiamini haki inacheleweshwa na kamwe haipotei!!
Indonesia
GASTON SHUNDO GARUBINDI รีทวีตแล้ว

The Tanzanian and Ugandan governments should be immediately suspended from the Commonwealth to protect the integrity of the institution. Our two applications on behalf of CHADEMA and the NUP, respectively, lay out why.
Amsterdam & Partners@amsterdamllp
Press Release: Amsterdam & Partners LLP Files Applications on Behalf of Uganda’s NUP and Tanzania’s CHADEMA, Respectively, Calls for Immediate Commonwealth Suspensions amsterdamandpartners.com/press-release-…
English

YALIYOJIKI MAHAKAMANI LEO MARCH 03, 2026
1. MAHAKAMA KUU DAR ES SALAAM
Jijini Dar es salaam, Mahakama kuu imetoa uamuzi mdogo kufuatia mapingamizi yaliyowekwa na wajibu Maombi wakipinga Maombi ya Mhe Lissu ya kuomba kuunganishwa kwenye kesi ya mgawanyo wa Mali za chama yasisikilizwe.
Jaji Mwanga ameyatupitilia mbali mapingamizi hayo na kesi imepangwa tarehe 06/03/2026 ambapo Mahakama kuu itasikiliza rasmi Maombi hayo na baadaye itapanga siku ya kuanzia ikiwa Mhe Lissu ataunganishwa kwenye kesi ya msingi au hataunganishwa.
2. MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MOROGORO:
Mkoani morogoro nako, Kesi inayomkabili mwanachama, Lucy Simon Shayo imeendelea kwa upande wa Jamhuri kubadilisha hati ya mashitaka na kusoma hoja za awali. Kwa hati mpya iliyowasilishwa sasa, Jamhuri wameachana na kosa la kusambaza taarifa za uongo mtandaoni na badala yake kosa ni “kudaiwa kutumia line ya simu iliyosajiliwa kwa kutumia kitambulisho cha mtu mwingine”
Kesi hii itaendelea tarehe 17-03-2026 ambapo Upande wa Jamhuri wanatarajiwa kuita mashahidi. Jamhuri wanatarajia kuita jumla ya mashahidi 7 na vielelezo 11 kuthibitisha madai yao.
3. MAHAKAMA YA WILAYA BUNDA - MARA.
Kesi inayomkabili, Yohana Kaunya ( Katibu mstaafu wa Bavicha Taifa) imeendelea leo kwa Upande Jamhuri kuleta shahidi 1, ambaye ni Askari wa Polisi na pia ni mwendesha mashitaka. Katika ushahidi wake amedai aliandika maelezo ya mtuhumiwa wa kwanza na kwamba alikiri kufanya makosa anayoshitakiwa nayo.
Hata hivyo, maelezo hayo hayajapokewa mahakamani kama kielelezo baada ya mawakili wa utetezi kupinga maelezo hayo kupokelewa mahakamani na Mahakama kukubaliana na pingamizi hilo.
Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea tarehe 06/03/2026 kwa Jamhuri kuendelea na mashahidi.
Indonesia

MREJESHO WA KESI ZA WANACHAMA MAGU, BUKOBA NA ILEMELA:
Leo Mahakama ya Wilaya MAGU imeahirisha kusoma hukumu dhidi ya wanachama 7 wanaotuhumiwa kuchoma moto majengo ya umma hadi tarehe 6 Machi 2026.
KUTOKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI BUKOBA.
Leo pia mahakama imemwachia aliyekuwa maya wa Manispa ya Bukoba, Mhe Chief Kalumuna na wenzake 14 waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya jinai.
KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA ILEMELA:
Jana mahakama ya wilaya ikifika kesi ya Uhaini dhidi ya viongozi 5 wa kata ya Buswelu baada ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kudai Hana nia ya kuendelea na shitaka hilo. Viongozi hao bado wanakabiliwa na kosa lingine la wizi.
Tarehe 2, Machi kesi hiyo ya tuhuma za wizi itaendelea mahakama ya wilaya ya ilemela ambapo pia tunatarajiwa watuhumiwa watapata dhamana baada ya kosa la Uhaini lisilo na dhamana kufutwa.
Indonesia



