Dr. Philip Isdor Mpango

270 posts

Dr. Philip Isdor Mpango

Dr. Philip Isdor Mpango

@dr_mpango

The official account of the Vice President of the United Republic of Tanzania🇹🇿

Dodoma, Tanzania เข้าร่วม Ekim 2021
0 กำลังติดตาม82K ผู้ติดตาม
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Nimezindua Hatifungani ya Samia ya Miundombinu (Samia Infrastucture Bond) ambayo inalenga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 150 ili kuiwezesha TARURA kuongeza mtandao wa barabara za vijijini na mijini. Hatifungani hii itaweza kuwashirikisha wawekezaji wa ndani katika ugharamiaji wa miradi ya miundombinu, kukuza ushirikiano na Sekta Binafsi na kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa barabara zinazosimamiwa na TARURA, unafanyika kwa wakati ili barabara hizo ziweze kutumika katika kipindi chote cha mwaka. Vilevile, Hatifungani hii itasaidia kukabiliana na mahitaji ya dharura ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu,unaosababishwa na uharibifu wa mvua kubwa na mafuriko. Naipongeza Ofisi ya Rais - TAMISEMI, TARURA, Kamati ya Samia Infrastructure Bond, Bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB kwa ubunifu na jitihada zao katika kufanikisha uanzishwaji wa Hatifungani hii. Kadhalika, natoa pongezi za dhati kwa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Benki Kuu ya Tanzania na Wizara ya Fedha kwa kuhakikisha Hatifungani hii inakidhi vigezo na kuiwezesha kuingia sokoni.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
111
88
389
100.7K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Umekuwa wakati mzuri kuungana na Watanzania wenzangu katika zoezi muhimu la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo tarehe 27 Novemba 2024. Nimetekeleza wajibu wangu wa Kikatiba katika kuchagua viongozi mbalimbali kwenye Kitongoji cha Kihanga, Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
67
66
393
36.1K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Ninaungana na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutoa pole kwa waathirika wote wa ajali ya kuanguka kwa ghorofa, katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Ninawaombea uponyaji wa haraka majeruhi wote. Kwa ndugu zetu waliofariki, katika ajali hiyo, tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu, awapokee na kuziweka roho zao mahali pema peponi, Amina. Aidha, Ninawaombea faraja Watanzania wote walioguswa na maafa haya.
Indonesia
194
55
700
104.4K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Mkutano wa COP29 unaoendelea nchini Azerbaijan ni fursa nyingine ya Dunia kuunganisha jitihada na kuendeleza mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Tanzania inashiriki katika Mkutano huu ikiwa miongoni mwa nchi zinazoathirika na mabadiliko ya tabianchi. Hivyo, ni fursa adhimu kwa Taifa letu kupata uzoefu na maarifa mapya, kuimarisha ushirikiano na wadau na kutafuta ufadhili wa miradi ya uhifadhi wa mazingira na ustahilivu wa mabadiliko ya tabianchi. “In Solidarity for a Green World”
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
18
40
193
12K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Nawashukuru Viongozi na Wananchi wote tulioshiriki pamoja katika Ziara yangu ya Kikazi mkoani Tabora. Hakika imekua ziara nzuri ya kujionea maendeleo ya mkoa huu pamoja na kuzifahamu vema changamoto zilizopo. Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuboresha na kusogeza jirani na wananchi huduma za kijamii ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Rai yangu kwa wananchi wa Tabora ni kuendelea kuwa Taa - Bora kama jina la mkoa huu kwa kujiepusha na vitendo vya ukatili, kuishi katika maadili mema, kulinda na kuhifadhi mazingira, kutumia vema fursa zilizopo hususani kilimo na ufugaji, kuhakikisha watoto wanapata elimu pamoja na kufuatilia wanachojifunza mashuleni.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
23
21
136
10.4K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Siku ya pili ya ziara ya kikazi mkoani Tabora. Nimeweka Mawe ya Msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wa Wilaya za Uyui na Tabora. Serikali imeendelea kuboresha huduma za kijamii katika Mkoa wa Tabora pamoja na kuinua sekta muhimu za uchumi ikiwemo kilimo cha zao la Tumbaku. Ni faraja kuona Tabora inabadilika na wananchi wanaendelea kutumia vema fursa zilizopo kujiletea maendeleo.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
7
18
108
6.7K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Ziara ya Kikazi ya siku nne Mkoani Tabora. Nimeanza kwa kuzungumza na wananchi wa Wilaya za Igunga na Nzega pamoja na kuweka Mawe ya Msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mradi mkubwa wa maji wa Bukene kutoka Ziwa Victoria unaogharimu shilingi Bilioni 29.3 ambao utaondoa changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi zaidi ya elfu 85.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
20
18
105
8.4K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Nimefungua Mkutano wa 53 wa mwaka wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha. Nimesisitiza umuhimu wa Mabunge kusimamia Serikali katika utekelezaji wa majukumu yake na kusimamia Sheria na Mikataba mbalimbali ikiwemo ya kimataifa. Ni muhimu kuhakikisha amani endelevu Barani Afrika inakuwepo pamoja na juhudi za pamoja kwa kushirikiana na wadau katika kushughulikia changamoto za uhaba wa chakula, mabadiliko ya tabianchi pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana wetu. Nimesisitiza Mkutano huo kutumika vema katika kubadilishana mbinu bora na uzoefu wa mataifa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa ufanisi zaidi sambamba na azimio la kumaliza migogoro na vita Barani Afrika.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
33
37
187
13.5K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Leo nimeshiriki kilele cha Kongamano kuhusu Uhuru wa Kidini Afrika lililofanyika mkoani Arusha. Ni matumaini yangu kuwa, limekuwa ni jukwaa zuri lililowezesha kujadili masuala muhimu yahusuyo uhuru wa kidini na kuishi pamoja kwa amani na kwamba sasa washiriki watakuwa tayari kwenda kutekeleza mapendekezo waliyokubaliana kwa kuzingatia mazingira mahsusi ya kila nchi ili kuimarisha amani na usalama katika nchi zetu za bara la Afrika. Dini zina mchango mkubwa katika kujenga familia na jamii zenye maadili mema, hivyo napenda kuwasihi viongozi wetu wa dini kusimamia kikamilifu suala la maadili mema katika jamii. Shauku yangu ni kuona jamii inayolinda, kutunza na kurithisha maadili mema kwa vizazi vijavyo na kukemea maovu kwa nguvu zote. Tunaweza kufikia azma hiyo endapo jamii yetu itakuwa na hofu ya Mungu.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
36
37
190
20.1K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Asanteni sana wananchi wa mkoa wa Dodoma kwa kuungana nami na viongozi wenzangu katika ziara ya kikazi ya siku nne. Hakika imekua ziara nzuri ambayo imeniwezesha kujionea hatua kubwa za kimaendeleo tulizopiga. Napenda kuwahakikishia kuwa ni dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kutatua changamoto zote ambazo mmenieleza katika ziara hii. Wito wangu kwenu ni kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutumia vema fursa zilizopo mkoani Dodoma kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Sandenyi sana Dodoma.
Indonesia
38
18
99
7.5K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Leo ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yangu ya kikazi mkoani Dodoma, nimefarijika kuwafikia wananchi wa Wilaya za Kondoa na Chemba. Nimezindua miradi ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi katika ujenzi unaoendelea na kuzungumza na wananchi. Wito wangu kwa Wazazi na Walezi nchi nzima ni kuacha tabia ya kuficha watoto wenye ulemavu na kuwakosesha fursa adhimu ya kupata elimu. Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia kwa watoto wenye mahitaji maalum hivyo tuwapeleke watoto hao katika vituo vya kutolea elimu. Watoto hawa wana vipaji na uwezo wa kipekee, hivyo wakiwezeshwa kupata elimu watatoa mchango mzuri kwa Taifa letu.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
62
31
190
22.2K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Ni furaha kubwa kuwa pamoja na wananchi wa Wilaya za Mpwapwa na Kongwa katika siku ya pili ya ziara yangu ya kikazi mkoani Dodoma. Kwa pamoja tumeshuhudia jitihada za serikali katika kusogeza karibu huduma za kijamii katika maeneo yao. Nimesikiliza changamoto zinazowakabili na kuwahakikishia Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kutatua changamoto hizo kwa juhudi kubwa.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Filipino
46
30
167
21.7K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Leo nimeanza ziara ya kikazi ya siku nne katika mkoa wa Dodoma. Nitakagua miradi ya maendeleo, kuzindua miradi iliyokamilika pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi wetu.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
37
27
155
9K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
East Africa, just like the rest of Africa, has a very youthful population with the highest fertility rate in the world! This population structure and dynamics can be a huge blessing. It means that we will continue to have a young and dynamic population to build our economies. If we harness our human resources fully, we will enjoy the fruits of our youthful population through what is called the Demographic Dividend. However, in order to enjoy the demographic dividend, we must significantly invest in the education and health of our children. High fertility rates in our countries imply that we must set aside more resources, both financial and human, to cater for the ever-expanding needs for quality education and health. My Remarks on The East Afrivan Community Education Conference
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
English
11
26
92
5.4K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Ziara ya kikazi katika Mkoa wa Kigoma. Kukagua Miradi ya Maendeleo pamoja na kusikiliza changamoto za Wananchi.
Indonesia
32
41
185
12K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Leo nimefungua Kongamano la Kwanza la Kitaifa kuhusu Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Pamoja na mambo mengine Dira ya 2050 inapaswa iwe ya vijana zaidi na kwa ajili ya vijana kutokana na idadi yao ya asilimia 77.5 nchini. Dira ya 2050 ni muhimu ijengwe juu ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Dira inayofikia ukomo, kwa kuyaimarisha na kuyatumia kama nyenzo ya kuongeza kasi ya mabadiliko makubwa. Itapaswa pia kubainisha kwa undani changamoto kuu za ndani na za nje, pamoja na zile za zamani na zinazoibukia ambazo ni kikwazo kikubwa kwa nchi yetu katika kupata maendeleo haraka. Na hapa itakuwa vema yakibainishwa kwa ukweli na uwazi. Ninawaalika na kuhimiza Wizara zote, Taasisi za Umma, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekta Binafsi, wananchi wote na hasa vijana, Watanzania wanaoishi Ughaibuni na Wadau wengine wote kujitokeza kutoa maoni na mikakati inayotekelezeka ya kuipaisha Tanzania kiuchumi na kijamii.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
29
41
160
9.9K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani 2024, hatuna budi kuchukua hatua za makusudi kurejesha uasili wa mazingira yetu kwa kuendeleza kampeni mbalimbali hususan za upandaji miti, kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia sambamba na uanzishaji wa Bustani za Kijani mijini ili kuongeza upatikanaji wa hewa safi, kupunguza hali ya joto, kutengeneza maeneo ya kupumzikia, kufanyia mazoezi na michezo mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kuboresha afya zetu na kupendezesha miji na majiji. Jitihada za kutunza mazingira yetu ni muhimu pia ziende sambamba na jitihada endelevu za kufanya usafi wa mazingira yetu.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
8
16
76
6.4K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Leo nimefungua Kongamano la Wadau wa Mazingira nchini. Wito wangu kwa Watendaji wote wa Wizara, Wakuu wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau wengine, kuhamasisha na kutoa elimu kwa Wananchi juu ya utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Tusaidiane kuelimisha umma kuachana na mila potofu zinazoharibu misitu, vyanzo vya maji na uoto wa asili na pia kuhimiza matumizi ya Nishati safi ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo yameendelea kuwa makubwa na kusababisha upotevu mkubwa wa misitu nchini.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Filipino
5
18
58
4.4K
Dr. Philip Isdor Mpango
Dr. Philip Isdor Mpango@dr_mpango·
Kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, nawashukuru Viongozi wote wa Dini pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa kuitikia kwa wingi katika Dua na Maombi ya kuliombea Taifa letu la Tanzania linapoadhimisha Miaka 60 ya Muungano. Tunapoliombea Taifa letu na hususani Muungano wetu, hatuna budi kuwapongeza kwa dhati Viongozi wa Awamu zote za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuendeleza na kuimarisha Muungano kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
Dr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet mediaDr. Philip Isdor Mpango tweet media
Indonesia
14
22
108
6.1K