Sam Henrq
26.8K posts


#TajiriLaKihaya KUNA MASWALI MAKUBWA YANAYOPASWA KUJIBIWA MUHIMBILI NA JKCI. Leo familia yetu imepoteza mdogo wetu. Moyo wangu umejaa huzuni, uchungu na maswali mengi ambayo hadi sasa hayajajibiwa. Siku ya kwanza nilipofanikiwa kumpeleka mdogo wangu JKCI na kupata chumba cha VIP, nilifurahi sana. Niliona kama tumepata mwanga wa matumaini. Baada ya vipimo, tuliambiwa tatizo lake la moyo lilihitaji upasuaji mdogo tu na angeweza kuendelea na maisha yake kawaida. Tukaahidiwa upasuaji ungefanyika ndani ya siku mbili au tatu. Lakini siku zikageuka wiki. Kabla hata ya kulazwa, tulikuwa tumepambana kwa zaidi ya mwezi mzima tukizungushwa kutoka leo hadi kesho. Mara daktari hayupo, mara jopo la wataalamu halijakaa, mara kipimo kirudiwe, mara tusubiri dawa zifanye kazi kwanza. Kila siku ilikuwa ni ahadi mpya na tarehe mpya. Baada ya kulazwa tuliamini safari ngumu imekwisha. Lakini ndipo mateso makubwa zaidi yalipoanza. Mdogo wangu aliingia hospitalini akiwa bado anaweza kutembea, kuongea, kula na kujitambua. Kila siku tulisubiri upasuaji ulioahidiwa, lakini haukufanyika. Badala yake hali yake ilianza kuzorota mbele ya macho yetu. Wiki moja ikapita. Wiki mbili zikapita hadi wiki tatu Hakukuwa na upasuaji. Kulikuwa na sababu mpya kila siku. Kisha tukahamishwa kutoka chumba tulichokuwa tumepewa kwa madai kuwa kingefanyiwa fumigation. Lakini usiku huo huo mgonjwa mwingine akawekwa kwenye chumba hicho. Hadi leo hatujui ukweli ulikuwa nini- lazima UFISADI ULITUMIKA HAPA! Tulihamishiwa chumba kingine JAPO kilikua VIP… ila hakikua kwenye standard sawa! Hata nakumbuka kuna Daktari wa Kihindi alikuja kusoma vipimo akasema ile MONITOR haipo sawa! Mapigo ya moyo na oxygen haisomeki kwa usahihi… Sasa kwa nn tulihamishwa chumba? Kutoka chumba kizuri kuja hiki?? Kwa nn kile tulichokuwepo alipewa mwingine usiku huo tumehamishwa? CORRUPTION! Baada ya hapo hali ya mdogo wangu ilizidi kuwa mbaya zaidi. Akapoteza nguvu, akashindwa kuzungumza, akashindwa hata kuwatambua watu waliomzunguka. Tulikuwa tunauliza maswali. Tulikuwa tunaomba msaada. Tulikuwa tunaomba hatua zichukuliwe haraka. Lakini muda uliendelea kwenda. Leo asubuhi mdogo wangu amefariki dunia. Siandiki haya kwa hasira pekee. Naandika kwa maumivu ya familia iliyokuwa na matumaini makubwa ya kumuona mpendwa wao akirudi nyumbani akiwa mzima. Kama kweli kulikuwa na uzembe, kucheleweshwa kwa huduma, ukosefu wa uwajibikaji au mifumo mibovu ya utoaji huduma, basi kuna haja ya uchunguzi wa kina na hatua kuchukuliwa. Maisha ya Watanzania yana thamani. Wagonjwa hawapaswi kupoteza maisha wakisubiri tarehe nyingine, kikao kingine au ahadi nyingine. Tunataka majibu. Tunataka uwajibikaji. Na zaidi ya yote, tunataka familia nyingine isipitie maumivu tuliyoyapitia sisi. Kama hapa ni VIP… je wagonjwa wa kawaida wanapata huduma gani??? Pumzika kwa amani mdogo wangu. Tulipambana kwa kila tulichoweza. Mungu akupokee katika makao ya milele. 💔🕊️

#TajiriLaKihaya Cc @TaasisiMoyoJKCI @MuhimbiliTaifa The first day I took my brother to the Jakaya Kikwete Cardiac Institute, I was filled with hope. I truly believed he would receive the treatment he needed and recover. Sadly, after spending nearly a month in the VIP ward, the operation we were waiting for was never performed. Every day brought another postponement, another promise, and another new date. We kept hoping, trusting, and waiting. Today, my brother is no longer with us. As a grieving family, we are deeply disappointed by the delays and the lack of urgency we experienced during such a critical time. When a patient’s life is at stake, time matters. Families place their trust in healthcare institutions, hoping their loved ones will receive timely care and a fair chance at life. Nothing can bring my brother back, but I hope our experience serves as a reminder that patients deserve better communication, better coordination, and more timely medical attention. My brother deserved that chance. May his soul rest in eternal peace. 🕊️💔








Messi in 6 World Cups: 13 goals Mbappe in 2 World Cups: 14 goals Messi is the biggest fraud in football history!





















