Erick Wizz
914 posts



Wafanyabiashara zaidi ya 300 wa mihogo katika eneo la Coco beach Dar es salaam wamepewa siku 30 za kuondoka kwenye eneo hilo ili kupisha Mwekezaji ambaye amepewa eneo hilo na Serikali ili kupatengeneza kisasa. Baadhi ya Wafanyabiashara hao wameeleza kushtushwa na uamuzi huo na kusema waliitwa kwenye kikao na Afisa Masoko wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye kuitwa na Meya wa Manispaa hiyo na kuambiwa kuwa wana siku 30 za kuondoka ndani ya eneo hilo na kwamba kila mmoja atapewa shilingi milioni 1.5 Kwa upande wa Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule, imesema lengo la kuwaondoa Wafanyabiashara hao ni maboresho kuelekea maandalizi ya michuano ya AFCON. #MillardAyoUPDATES





Hapana wakali imebidi tusogee kwenye vibe watiiii 🤣🤣🤣🤣

Mbona Dar City wamevaa VISIT RWANDA?

@EngMapundajr Chura anafurahisha sana kama sio ndugu yako

Hapana wakali imebidi tusogee kwenye vibe watiiii 🤣🤣🤣🤣





















