
Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na Rais Dkt. Samia kuchunguza matukio yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu October 29,2025, Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman amesema kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa kwenye Tume matukio ya ghasia za October 29, yalikuwa na lengo la kuzuia na kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa October 29 ambapo lengo hili linadhihirishwa kupitia vitendo vya Wafanya ghasia ikiwemo kuharibu vituo vya kura. Jaji Mstaafu Chande amesema hayo wakati akiwasilisha Ripoti ya Tume hiyo mbele ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo April 23,2026 Ikulu Jijini Dar es salaam. โKwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa kwenye Tume matukio ya ghasia za October 29 yalikuwa na lengo la kuzuia na kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa October 29, lengo hili linadhihirishwa kupitia vitendo vya Wafanya ghasia ikiwemo kuharibu vituo vya kura, kuwashambulia Polisi na Wasimamizi na Wananchi, kupora mali, na waliopiga kura wakawa na alama za wino walikatwa vidole na wengi walilipwa fedha ili wajinusuru kufanyiwa hivyoโ โPili ghasia hizo zilifanywa ili kufikisha ujumbe kwa Serikali kuwa Vijana wanataka kusikilizwa na kutatuliwa changamoto zao, ilibainika kuwa Waratibu wa ghasia walitumia malalamiko ya Wananchi dhidi ya Serikali wakati wanawashawishi kufanya ghasiaโ #MillardAyoUPDATES




















